Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Ujenzi wa Miundombinu Watajwa Kuchochea Ukuaji wa Uchumi

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akisisitiza kuhusu mafanikio yaliyofikiwa na Serikali katika utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2019/20 na hali ya uchumi wa Taifa leo Jijini Dodoma

Na Mwandishi Wetu

Uwekezaji katika sekta za miundombinu umetajwa kuchochea ukuaji wa uchumi na ustawi wa wananchi mijini na vijijini kufikia asilimia 7.0 mwaka 2018.

Akizungumza leo Jijini Dodoma  kuhusu hali ya uchumi wa Taifa kwa mwaka 2019 na tathmini ya utekelezaji wa Bajeti kwa nusu ya kwanza ya mwaka wa fedha 2019/20, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango amesema kuwa sekta zilizokua kwa kasi katika kipindi cha nusu ya kwanza ya mwaka 2019 ni pamoja  na ujenzi asilimia 16.5, uchimbaji wa madini na mawe asilimia 13.7,habari na mawasiliano asilimia 10.7, maji asilimia 9.1 na usafirishaji na uhifadhi wa mizigo asilimia 9.0 Read more

Tanzania Yapokea Msaada wa Shilingi Bilioni 4.2 kutoka Japan

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (kulia), na Naibu na Kaimu Balozi wa Japan nchini Tanzania, Bw. Katsutoshi Takeda, wakisaini mkataba wa Msaada wa Sh. 4.2 kwa ajili ya kufufua Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO), hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (kulia), na Naibu na Kaimu Balozi wa Japan nchini Tanzania, Bw. Katsutoshi Takeda, wakibadilishana mkataba wa Msaada wa Sh. 4.2 kwa ajili ya kufufua Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO) ambapo TAFICO itaweza itaweza kuwa na Meli ya Uvuvi, hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam

Na. Peter Haule, WFM, Dar es Salaam

Tanzania imepokea msaada wa Yen za Japan milioni 200 sawa na Shilingi Bilioni 4.2 kutoka Serikali ya Japan kwa ajili ya kufufua Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO)

Mkataba wa msaada huo umesainiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James, kwa niaba ya Serikali ya Tanzania na Naibu na Kaimu Balozi wa Japan, Bw. Katsutoshi Takeda, kwa niaba ya Serikali ya Japan.

Katibu Mkuu, Bw. Doto James, alisema kuwa msaada huo utatumika kununua Meli ya Uvuvi yenye vifaa vya kisasa, mashine ya kutengeneza barafu, ghala la baridi la kuhifadhia samaki, Vifaa mbalimbali vya kuvulia samaki na vya karakana, gari lenye mitambo maalum ya barafu na Gari kwa ajili ya kusambazia samaki.

Alisema kuwa utekelezaji wa Mradi huu utachangia kwa kiasi kikubwa katika kufikia malengo ya Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano Awamu ya Pili (FYDP II), ambayo pamoja na mengine unalenga kuboresha Sekta ya Uvuvi na hatimaye kuvutia Watanzania zaidi kujihusisha katika Sekta ya Uvuvi kama shughuli kuu ya kujipatia kipato.

“Mradi huu utaongeza uuzaji wa samaki nje ya nchi, kuongeza uhakika wa chakula nchini, na pia utaboresha usindikaji wa samaki, kuongeza thamani na masoko na kupunguza upotevu wa mazao ya samaki baada ya kuvua”, alieleza Bw. James.

Alisema kuwa Kiwango cha ukuaji kwa shughuli ndogo za kiuchumi za uvuvi kilifikia asilimia 9.2 mwaka 2018 ikilinganishwa na ukuaji wa asilimia 8.4 mwaka 2017 ambapo kiwango kikubwa cha ukuaji kilitokana na utunzaji mzuri wa mazalia ya samaki yakiwemo mabwawa ya watu binafsi sambamba na kuongezeka kwa mahitaji katika soko la ndani na nje.

Bw. James alisema kuwa, shughuli za uvuvi zilichangia asilimia 1.7 katika Pato la Taifa mwaka 2018, ambayo inadhihirisha umuhimu wa uvuvi katika uchumi, hivyo msaada uliotolewa utachangia jitihada za Serikali katika kufikia Dira ya Maendeleo ya mwaka 2025, Malengo Endelevu ya mwaka 2030 na Agenda ya Maendeleo ya Afrika ya mwaka 2063.

Alisema kuwa Serikali ya Japan imekuwa ikiisaidia Tanzania kupitia misaada na mikopo nafuu katika Sekta mbalimbali ikiwemo Kilimo, Miundombinu ya barabara, Maji, Nishati Utawala Bora na Uwajibikaji ambapo mpaka sasa Jumla ya Sh. Trilioni 1. 3 zimetolewa na Serikali hiyo tangu mwaka 2012.

Read more

Rais Dkt. Magufuli Asajili Laini ya Simu, Atoa Pole kwa Familia ya Bw. Atanasi Mnaku

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wanafamilia pamoja na waombolezaji wengine nyumbani kwa marehemu Mzee Atanasi Masansa Mnaku aliyefariki Dunia Desemba 25, 2019 Wilayani Chato Mkoa wa Geita wakati alipokwenda kuwapa pole wafiwa kwa kuondokewa na Mpendwa wao leo Disemba 27, 2019.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiweka alama ya kidole gumba alipokwenda kusajili Laini yake ya simu kwa njia ya alama ya Vidole katika kampuni ya simu ya Airtel Mjini Chato Mkoani Geita. Desemba 27, 2019.Kushoto ni Msajili wa laini za Simu wa Airtel tawi la Chato Michael Martin.

Mhe. Rais Magufuli amefanya usajili huo Chato Mjini katika Mkoa wa Geita.

Hata hivyo, Mhe. Rais Magufuli ameongeza siku 20 kuanzia tarehe 01 Januari, 2020 hadi tarehe 20 Januari, 2020 kwa wote ambao watashindwa kusajili laini zao katika kipindi cha kuishia tarehe 31 Desemba, 2019 kama ilivyotangazwa na TCRA kutokana sababu mbalimbali zikiwemo kuugua na kukamilisha upataji wa namba ama Vitambulisho vya Taifa.

Mhe. Rais Magufuli amesisitiza kuwa baada ya muda huo hakuna kisingizio chochote kitakachokubalika na ameagiza TCRA kuhakikisha laini ambazo hazijasajiliwa zinazimwa

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akielekea kusajili Laini ya simu kwa njia ya alama ya Vidole Mjini Chato Mkoani Geita Desemba 27,2019.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi kitambulisho chake cha Taifa Msajili wa laini za Simu wa kampuni ya simu ya Airtel Michael Martin aliokwenda kusajili Laini ya simu kwa njia ya alama ya Vidole Mjini Chato Mkoani Geita. Desemba 27, 2019.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akionyesha simu yake ambayo ametoka kusajili laini yake ya simu kwa njia ya alama ya Vidole na kisha kuzungumza na Wananchi wa Mjini Chato Mkoani Geita na Watanzania wote ambapo ameongeza muda wa usajili siku ishirini (20) kuanzia Januari 01 hadi Januari 20, 2019 ndio utakuwa mwisho wa zoezi hilo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wananchi wa Mjini Chato Mkoani Geita na Watanzania wote mara baada ya kusajili laini yake ya simu kwa njia ya alama ya Vidole ambapo Mhe. Rais ameongeza muda wa usajili siku ishirini (20) kuanzia Januari 01 hadi Januari 20, 2019 ndio utakuwa mwisho wa zoezi hilo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Mjasiliamali wa Chipsi Joseph Wandwi wa Mjini Chato Mkoani Geita mara baada ya kusajili laini yake ya simu kwa njia ya alama ya Vidole na kuzungumza na Wananchi hao, ambapo Mhe. Rais ameongeza muda wa usajili siku ishirini (20) kuanzia Januari 01 hadi Januari 20, 2019 ndio utakuwa mwisho wa zoezi hilo.

Amefafanua kuwa usajili wa laini za simu kwa alama za vidole ni muhimu kwa usalama wa nchi ikiwemo kuepusha vitendo vya utapeli na ujambazi vinavyofanywa na wahalifu, ambao licha ya wengi wao kukamatwa na vyombo vya dola wameendelea kusababisha usumbufu na upotevu mali za wananchi hususani fedha.

Pamoja na kuwasalimu wananchi wa Chato Mjini waliojitokeza kushuhudia wakati akisajili laini yake kwa alama za vidole, Mhe. Rais Magufuli amewasalimu na kusikiliza maoni yao kuhusu zoezi hili na pia mwananchi Steven Joseph Wandwi anayefanya biashara ya kuuza chipsi na mishikaki akawaongoza wenzake kumuombea Mhe. Rais Magufuli na kumshukuru kwa utumishi wake mzuri ulioongeza kasi ya maendeleo kwa Taifa hasa vijana ambao sasa wanachapa kazi bila bughudha.

Kabla ya kwenda kusajili laini yake ya simu, Mhe. Rais Magufuli ametembelea Mtaa wa Chato Kati na ametoa pole kwa familia ya Marehemu Atanasi Masansa Mnaku aliyefariki dunia juzi tarehe 25 Desemba, 2019 na mazishi yake yamepangwa kufanyika kesho.

Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Chato

27 Desemba, 2019

Lindi Waaswa Kujiunga na Vifurushi vya Bima ya Afya

 

Mkuu wa mkoa wa Lindi Mhe. Godfrey Zambi akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya kuhamasisha wananchi kujiunga na vifurushi vya bima ya afya kupitia mfuko wa Taifa wa Bima ya AFya (NHIF) mkoani humo Desemba 20, 2019.

Na Mwandishi wetu- Lindi

Mkuu wa Mkoa wa Lindi Godfrey Zambi amesema mpango wa vifurushi vya bima ya afya una lengo la kuhakikisha kuwa tunakuwa na Taifa lenye afya na lenye nia ya kuzalisha mali kuelekea uchumi wa kati kwa kuwa tutakuwa na  nguvu kazi yenye afya. Read more

Sekta ya Umma Kushindanishwa Tuzo za Mwaajiri Bora

Na Mwandishi Wetu

Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu  kwa kushirikiana na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) pamoja na Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA) imedhamiria  kuishindanisha sekta ya Umma katika tuzo za mwaka 2020 ili ushindani huo unaofanywa katika sekta binafsi uyashirikishe mashirika ya umma  kwa kiwango kikubwa kwa ajili ya  kuweza kuboresha mazingira ya kazi na ajira  na kuongeza  tija hapa nchini.

Akiongea katika hafla ya tuzo ya mwaajiri bora wa mwaka 2019 iliyoandaliwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), jijini Dar es salaam, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,Bunge,Kazi,Vijana, na watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama, aliye mwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, amefafanua kuwa ustawi wa wafanyakazi sio kwa sekta binafsi peke yake ni pamoja na sekta ya umma, hivyo ili sekta binafsi iiwe injini ya kuendesha uchumi wa Taifa,  ni lazima pia sekta ya Umma nayo iwekeze rasilimali watu ili kuweza kuongeza tija katika maeneo ya kazi.

“Niipongeze ATE kwa kuwa na tuzo hizi, tungependa kuona ni mashirika gani ya Umma yanafanya vizuri katika kuangalia ustawi wa wafanyakazi na kuleta tija nchini. Maamuzi ya kuwa na washindi wa jumla  katika makundi ya kisekta yataongeza chachu mpya ya mashindano amabayo itakuza sekta mbalimbali na hatimaye yataboresha na kuleta tija katika ukuaji wa uchumi wa Taifa letu”, amesisitiza, Mhe. Mhagama.

Waziri Mhagama ameitaka ATE kuendelea kutoa mafunzo katika maeneo ya kazi na juu ya sheria za kazi na usimamizi wa rasilimali watu ambapo kutokana na mafunzo hayo yatasaidia kupunguza migogoro mahala pa kazi na hivyo kujenga mazingira tulivu ya kibiashara ndani ya maeneo ya kazi. lakini pia mafunzo hayo huwasaidia wafanyakazi kukidhi ushindani wa mazingira ya kibiashara  kwa sasa.

“Takwimu zinaonesha mafunzo ambayo yameratibiwa na kuandaliwa na ATE kuwa vijana  1, 437, waliidhinishwa na kupata nafasi kwa waajiri huku kwenye tovuti ya serikali wapo vijana 6,919,  walijiandikisha hadi Julai mwaka huu, hivyo nitoe rai kwa waajiri wapeni fursa  vijanaili waweze kujifunza kwa vitendo,  niipongeze Kampuni ya TCC kwa kuwa mstari wa mbele kutoa nafasi kwa vijana kujifunza kwa vitendo hapa nchini.” Amesema, Mhe. Mhagama.

Aidha. Amewataka waajiri kuendelea  kushirikiana na serikali katika kutekeleza mpango wa kitaifa wa miaka 5 wa kukuza ujuzi ambao hufadhiliwa na serikali kupitia tozo ya kukuza ujuzi mahala pa kazi ili kuweza kuongeza ujuzi kwa vijana na kutatua tatizo la ajira nchini huku akiwasisitiza kuzingatia sheria za kazi zinazo onya ajira kwa watoto.

Mhe. Mhagama amewataka waajiri kuendelea kuchangia katika mfuko wa fidia kwa wafanyakazi ili kuweza kuwakinga wafanyakazi dhidi ya majanga yatokanayo na kazi. Pia amewasisitiza waajiri kuzingatia haki, usawa mahala  pa kazi ili kuondoa unyanyasaji wa kijinsia katika maeneo ya kazi hivyo katika kuhakikisha hilo linafanikiwa serikali tayari imeshazindua mkakati wa Kitaifa wa usawa wa kijinsia mahala pa kazi.

Naye, Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye ulemavu) Mhe.  Stella Ikupa amewapongeza ATE kwa juhudi zao za kuunga juhudi za serikali za kuwawezesha watu wenye Ulemavu hivyo amewasihi waendelee kujenga mazingira rafiki mahala pa kazi ili watu wenye ulemavu na watu wenye mahitaji maalum waweze kufanya kazi  na kuchangia kwenye maendeleo ya Taifa.

Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya ATE, Jayne Nyimbo amefafanua kuwa ushirikiano wanaoupata serikalini wa kushirikiana na sekta binafsi umesaidia kuboresha kwa tuzo hizo ambazo zimekuwa zikiboresha mazingira ya kazi na ajira hapa nchini.

Awali akiongea katika Hafla hiyo, Afisa Mtendaji Mkuu wa ATE, Dkt Aggrey Mlimuka amesema tuzo ya Mwajiri Bora wa Mwaka mwaka huu imefanyia kazi ushauri uliotolewa na seriikali mwakk na  Waziri Mhagama kuwa katika tuzo za mwaka huu ziongeze vipengele vipya vitatu (3) ambavyo viezifanya tuzo za mwaka huu kuwa na Jumla ya vipengele 38 kutoka vipengele 35.

“Vipengele vilivyoongezeka ni Mwajiri Bora anayeendeleza Mafunzo ya Ujuzi wa Kazi kwa wahitimu (Internship), Mwajiri Bora anayetoa mafunzo ya Uanagenzi (Apprentiship), Mwajiri Bora anayezingatia Haki Rasilimali ijulikanavyo kama “Local Content”, ” Alisema, Dkt.  Mlimuka.

Tangu mwaka 2015 Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) kilianzisha Tuzo ya Mwajiri Bora kwa kila mwaka,   lengo la tuzo hizo ni kutathmini na kutambua  waajiri wenye mikakati bora ya usimamizi wa rasilimali watu kwa ajili ya kuongeza uzalishaji kibiashara na kuwahamasisha waajiri kufuata taratibu za kitaifa na kimataifa katika uendeshaji wa biashara zao ambapo makampuni wanachama kutoka sekta binafsi hushindanishwa kwa kila mwaka.

Taarifa kwa Umma

Wizara ya Fedha na Mipango inapenda kutoa ufafanuzi kuhusu taarifa iliyoandikwa kwenye gazeti la Mtanzania toleo la tarehe 18/12/2019 yenye kichwa cha habari “Wastaafu EAC waibuka na mafao yao” ambapo taarifa hiyo ilieleza kuwa wastaafu wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki hawajalipwa mafao yao kwa miaka 40 iliyopita.

Read more