Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Rais Magufuli Mgeni Rasmi Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 58 ya Uhuru Jijini Mwanza

Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania leo Novemba 27, 2019 Jijini Mwanza, maadhimisho hayo yanafanyika mkoani humo kwa mara ya kwanza.

Na Mwandishi Wetu- Mwanza

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya sherehe za miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara na miaka 57 ya Jamhuri  zinazotarajiwa kufanyika Kitaifa mkoani Mwanza.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkuu wa Mkoa huo Mhe. John Mongella amesema kuwa maadhimisho hayo yatafanyika Disemba 9, 2019 kwa mara ya kwanza katika mkoa huo katika uwanja wa CCM Kirumba.

Kauli mbiu ya sherehe hizo ni “ Miaka 58 ya Uhuru na miaka57 ya Jamhuri:Uzalendo, Uwajibikaji na Ubunifu ni Msingi wa Ujenzi wa Uchumi wa Taifa Letu,” Alisistiza Mhe. Mongella. Read more

Simbachawene Azitaka Halmashauri Kutoa Elimu ya Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu waRais (Muungano na Mazingira) Mhe. George Simbachawene akifungua Mkutano wa mwaka wa wadau wa kilimo kuhusu athari za mabadiliko ya tabianchi na fursa zilizopo katika sekta ya kilimo na utayari wa nchi katika kukabiliana na changamoto hiyo iliyoandaliwa na Jukwaa Lisilo la Kiserikali la Wadau wa Kilimo (ANSAF) jijini Dodoma.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu waRais (Muungano na Mazingira) Mhe. George Simbachawene ametoa wito kwa halmashauri zote kuwa na mipango kabambe inayotekelezeka kwa ajili ya kuhakikisha elimu ya kilimo kinachohimili mabadiliko ya tabianchi inawafikia wakulima katika maeneo yao.

Pia amezitaka kuwajengea uwezo maafisa ugani kutekeleza jukumu hili muhimu pamoja na kuboresha mawasiliano na Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) na kuboresha ufikishaji wa taarifa hizi kwa wakulima na maelekezo ya nini wafanye kulingana na hali ya wakati husika. Read more

Miaka Minne ya JPM: Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali imeimarisha Miundombinu

Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko akizungumza na Waandishi wa Habari (Hawapo Pichani), kuhusu mafanikio ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali ikiwemo ununuzi wa vifaa vya TZS Bilioni 6.5 na Ujenzi wa Maabara za kanda kwa miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Tano, Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Idara ya Habari-MAELEZO, Jijini Dar es Salaam.

Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko akizungumza na Waandishi wa Habari (Pichani), kuhusu mafanikio ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali ikiwemo ununuzi wa vifaa vya TZS Bilioni 6.5 na Ujenzi wa Maabara za kanda kwa miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Tano, Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Idara ya Habari-MAELEZO, Jijini Dar es Salaam.

Kaimu Mkurugenzi Idara ya Usimamizi wa Kemikali kutoka Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Daniel Ndiyo, akizungumza na Waandishi wa Habari (Hawapo Pichani), Kuhusu Mafanikio ya Ofisi hiyo, ikiwemo ununuzi wa vifaa vya TZS Bilioni 6.5 na Ujenzi wa Maabara za kanda, Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Idara ya Habari-MAELEZO, Jijini Dar es Salaam.

Kaimu Mkurugenzi Idara ya Usimamizi wa Kemikali kutoka Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Daniel Ndiyo, akisisitiza jambo kwa A Waandishi wa Habari (Hawapo Pichani), Kuhusu Mafanikio ya Ofisi hiyo, ikiwemo ununuzi wa vifaa vya TZS Bilioni 6.5 na Ujenzi wa Maabara za kanda, Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Idara ya Habari-MAELEZO, Jijini Dar es Salaam.

TANTRADE YASAIDIA KAMPUNI 31,891 KUPATA TAARIFA ZA BEI YA MASOKO NA BIDHAA

Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara (TanTrade), Bi. Latiffa Mohammed, akizungumza na Waandishi wa Habari (Hawapo Pichani), kuhusu Mafanikio ya TANTRADE kwa maiaka minne ya Serikali ya Awamu ya Tano, Mkutano uliofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Idara ya Habari-MAELEZO, Jijini Dar es Salaam.

Na Mwandishi Wetu

MAMLAKA ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) katika kipindi cha miaka minne ya Uongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano imefanikiwa kuziunganisha kampuni 31,891 kuweza kupata taarifa za bei na  masoko ya bidhaa za ndani na nje ya nchi.

Hayo yamebainishwa leo Jumatano (Novemba 27, 2019) Jijini Dar es Salaam na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TANTRADE, Latifa Khamis wakati alipokuwa akitoa taarifa ya mafanikio ya Taasisi hiyo katika Kipindi cha miaka minne ya Uongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano kuanzia Novemba 2015 hadi Novemba 2019.

Alisema kuwa ya wafanyabiashara hao, TANTRADE iliweza kuunganisha katika masoko wafanyabiashara  405 na kuuza tani 102,000 za mahindi, tani 2,000 za karanga, tani 5,000 za soya, tani 50 za ufuta, tani 7 za majani ya papai, kilogramu 200 za unga wa ubuyu, tani 2 za iliki, tani 5,000 za muhogo na tani 3.2 za tangawizi ya unga.

Aliongeza kuwa miongoni mwa bidhaa zilizoonesha uhitaji mkubwa katika masoko ya nje ni pamoja na matunda, samaki na mazao ya bahari, jamii ya mikunde, asali, kahawa, chai, korosho, viungo na vyakula, ambapo maulizo ya bidhaa hizo yalitoka katika nchi za India, Nchi za Kiarabu, Misri, Marekani, Vietnam na Ulaya.

‘’Mbali na kusambaza taarifa za uhitaji wa bidhaa mbalimbali TANTRADE kwa kushirikiana na wanunuzi kutoka nchi zao tumewezesha kupatikana kwa muendelezo wa kimkakati wa kupenya katika masoko yao, semina mbalimbali ziliratibiwa ambapo wafanyabiashara na wadau 425 walishiriki ili kutambua fursa za masoko ya nje na taratibu za kuyafikia’’  alisema Latifa.

Kuhusu ukuzaji na uendelezaji wa masoko ya nje ya nchi, Latifa alisema TANTRADE imeendelea kuratibu maonesho ya biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF) kwa lengo la kutoa fursa za kutangaza bidhaa zilizoongezewa thamani na upatikanaji wa teknolojia ili kupanua wigo wa masoko ya nje ya nchi.

Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara (TanTrade), Bi. Latiffa Mohammed, akizungumza na Waandishi wa Habari (Hawapo Pichani), kuhusu Mafanikio ya TANTRADE kwa maiaka minne ya Serikali ya Awamu ya Tano, Mkutano uliofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Idara ya Habari-MAELEZO, Jijini Dar es Salaam

Latifa alisema kupitia DITF kila mwaka Tanzania hupokea wastani wa kampuni 500  kutoka zaidi ya nchi 35 zinazoshiriki maonesho hayo na hivyo kuwasaidia wafanyabiashara katika upatikanaji wa teknolojia na kusaidia kutatua changamoto za uzalishaji hafifu wa bidhaa za kilimo, uchenjuaji wa madini na hivyo kuleta matokeo chanya yaliyokusudiwa.

Akifafanua zaidi Latifa alisema kwa mwaka 2019 pekee kupitia DITF, mafanikio mbalimbali yaliweza kupatikana ikiwemo kampuni 437 kupata oda ya kufanya biashara zenye thamani ya Tsh Bilioni 7.93, kufanyika kwa mauzo ya papo kwa papo yenye thamani ya wastani wa Tsh. Milioni 209, pamoja na kutengeneza ajira za muda mfupi zipatazo 14,912 zilizotokana na kazi mbalimbali za maonesho ikiwemo ujenzi, ulinzi na usafi.

Akizungumzia kuhusu ushiriki wa Tanzania katika maonesho ya nje ya nchi, Latifa alisema Tanzania imefanikiwa kushiriki katika maonesho katika nchi zilizo na utengamano ikiwemo Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) ambapo wastani wa kampuni 200 zimeweza kushiriki na kutambua bidhaa zao kwenye nchi hizo na kuingia mikataba ya kibiashara ili kupata masoko endelevu.

Akitoa mfano Latifa alisema katika mwaka 2018/19, Tanzania ilishiriki maonesho ya 15 ya Biashara China ambapo kampuni 20 zilishiriki na kuweza kutafutiwa masoko ya bidhaa na kutangaza vivutio mbalimbali vya uwekezaji ikiwemo vivutio vya utalii, mazao ya kilimo hususani kahawa, chai, karafuu, asali, korosho, mazao ya jamii ya kunde na bidhaa za mikono ikiwemo vikoi.

‘’Katika maonesho ya chakula ya Gulfood-Dubai kampuni tatu zaTanzania zilifanikiwa kutembelea maonesho hayo yaliyofanyika Dubai kwa lengo la kutambua fursa mbalimbali kutoka kwa washiriki, ambapo wanunuzi wa bidhaa mbalimbali kama asali kontena 30, kahawa tani 50, ukwaju tani 10 walipatikana’’ alisema Latifa.

Aidha Latifa alisema TANTRADE katika kutekeleza adhima ya Tanzania ya Viwanda ilianzisha maonesho ya bidhaa za Viwanda vya Tanzania yanayofanyika kila mwezi Desemba, ambapo tangu kuanza kwake mwaka 2007 wastani wa makampuni 497 hushiriki na kuwafanya wazalishaji wa bidhaa nchini kupata fursa ya kutambulisha bidhaa zao na kuhamasisha matumizi ya bidhaa za Tanzania.

 

Benki ya Biashara na Maendeleo Mashariki na Kusini mwa Afrika Yaahidi Kutoa Fedha Ujenzi wa Reli ya Kisasa

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Bw. Masanja Kadogosa, akimpokea Rais wa Benki ya Biashara na Maendeleo Mashariki na Kusini mwa Afrika (TDB), Dkt. Admassu Tadesse alipotembelea Mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR), kipande cha Dar es Salaam hadi Morogoro, jijini Dar es Salaam.

Na Benny Mwaipaja, Dar es Salaam

Rais na Mtendaji Mkuu wa Benki ya Biashara na Maendeleo Mashariki na Kusini mwa Afrika (TDB) Dkt. Admassu Tadesse ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa kutekeleza mradi mkubwa wa ujenzi wa Reli ya Kati kwa Kiwango cha Kimataifa (SGR) kwa kutumia fedha zake za ndani na kuahidi kuwa Benki yake itafanya kila linalowezekana kuhakikisha inatafuta fedha za kujenga reli hiyo

Dkt. Tadesse ametoa kauli hiyo alipotembelea sehemu ya ujenzi wa miundombinu ya reli hiyo, kipande cha Dar es Salaam hadi Morogoro na kujionea kazi kubwa iliyofanyika ambapo amesema mradi huo hautainufaisha Tanzania peke yake bali pia nchi za ukanda wa Afrika hususan ambazo hazipakani na Bahari. Read more

Waziri Ummy awapa Maagizo Maafisa Maendeleo ya Jamii

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza katika uzinduzi wa Kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia iliyofanyika kitaifa jijini Dodoma.

Na Mwandishi Wetu Dodoma

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amewaagiza Maafisa Maendeleo ya Jamii kusimamia uanzishwaji na uendeshwaji wa Kamati za ulinzi wa wanawake na watoto katika mikoa na Halmashauri ambazo hazijaanzishwa ili kuzuia vitendo vya ukatili wa kijinsia hadi ngazi ya Kata na Vijiji.

Akizungumza katika uzinduzi wa Kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsi leo Jijini Dodoma, Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu amesema kuwa dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe. Dkt John Pombe Magufuli imetekeleza kwa vitendo azma ya kukomesha vitendo hivyo. Read more

Waliokamatwa na Viza za Kughushi Washughulikiwe- Rais Magufuli

Na Jonas Kamaleki- MAELEZO, Dodoma

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ameagiza waliokamatwa na viza za kughushi washughulikiwe bila kujali cheo, umaarufu wala majina yao.

Agizo hilo Raisi amelitoa wakati akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya Uhamiaji leo jijini Dodoma.

Rais ameipongeza Uhamiaji kwa kujenga jingo zuri la kisasa ambalo liboresha utoaji wa pasipoti hasa mikoani na kuwa litpendezesha Jiji la Dodoma.

Aidha, Rais Magufuli ameonyesha kukerwa na Jeshi la Magereza kutowatumia wafungwa kwenye miradi ya maendeleo ikiwemo ya ujenzi.

“Ni aibu nyumba za askari magereza kujengwa na Jeshi la Wananchi wakati wafungwa wapo,” alisema Rais Magufuli. Read more

Agizo la Rais Magufuli Latekelezwa ndani ya saa 24

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akisisitiza kuhusu umuhimu wa Taasisi na Mashirika ya umma kutekeleza agizo la Rais Dkt. John Pombe Magufuli la kuhakikisha kuwa zinawakilisha gawio lao ndani ya siku 60 zilizotolewa.

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akipokea mfano wa hundi kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania Bw. Masanja Kadogosa ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais Dkt. John Pombe Magufuli alilotoa wakati akipokea gawio kutoka kwa Taasisi na Mashirika ya Umma Novemba 24, 2019 Jijini Dodoma.

Na. Immaculate Makilika Read more