Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

WANA HABARI MTAKUWA VIBARUA MPAKA LINI- WAZIRI MWAKYEMBE

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Haarrison Mwakyembe akizungumza na washiriki wa Jukwaa la Waandishi wa Habari Wanawake kuhusu unyanyasaji wa Kijinsia kwenye vyombo vya habari, lilifanyika Jijini Dar es Salaam leo Novemba 29, 2019.

Na Judith Mhina

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt Harrisom Mwakyembe amezindua kitabu  cha  Gender and Media  Handbook in Tanzania wakati wa  maadhimisho  ya miaka miwili ya  Mtandao  wa  Wanahabari Wananawake Tanzania  na Maafisa Uhusiano.

Akizindua kitabu hicho katika ukumbi wa Kibo ndani ya  hoteli i  ya  Kimataifa ya  Hyatt Regence  – The Kilimanjaro  leo  Jijini Dar-es-salaam Waziri Dkt Mwakyembe amesema  “Wana habari mtakuwa vibarua mpaka lini”.

Hebu tujaribu kutekeleza sheria mbili ya Habari na ile ya haki ya kupata taarifa, ambapo Tanzania ni kati ya nchi chache ambazo  zimeiga kiila kitu kilichoandikwa  kwenye sheria husika  ya kimataifa,  badala yake wanaleta  mada yao pendwa ya jinsia moja, hatuwezi kukubali. Amesema Waziri Mwakyembe.

Akijibu risala iliyosomwa  na Mwenyekiti wa  Mtandao  wa  Wanahabari Wananawake Tanzania  na Maafisa Uhusiano- Tanzania Women Media and Public  Relation Networ,. Bevin Bhoke Chacha Mwita ambaye amesema kuwa  waandishi wa habari wanawalke  wananyanyaswa  kijinsia katika vyumba vya habari . Hii ikiwa ni  pamoja na kutolipwa mshahara stahiki kulingana na sifa walizonazo, kutopandishwa madaraja, lugha chafu na kubaguliwa katika majukumu ya kazi  kama waandishi wa kiume  na kujikuta wengi wao wakiwa  waadhirika  wa  kunyanyaswa kijinsia.

Waziri mwakyembe aliongeza kwa kusema “Tunaomba wahisani watenge nusu ya fedha wanazotoa ili kuangalia  masilahi ya waandishi wa habari na kuboresha mazingira ya kazi kutokana na kuwa na vitendea kazi duni  katika vyombo vyao vya Habari.

Ninashangaa waandishi wa Habari ambao wanashangilia kuwa na taaluma isiyo na mpangilio, sheria wala kanuni, katika kuimarisha  taaluma yao na ndio maana leo hii mnalalamika masilahi madogo  yasiyolingana na kazi mnayofanya  au hatopata  mishahara kabisa .

Mwakilishi wa UN Women Nchini, Bi. Hodan Addou akizungumza na washiriki wa Jukwaa la Waandishi wa Habari Wanawake kuhusu unyanyasaji wa Kijinsia kwenye vyombo vya habari, lilifanyika Jijini Dar es Salaam leo Novemba 29, 2019.

Read more

Madaktari na Wauguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Wajifunza Jinsi ya Kuokoa Maisha ya Mtu Aliyepata Tatizo la Dharula la Kiafya

Madaktari na wauguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakijifunza jinsi ya kuokoa maisha ya mtoto aliyepata tatizo la dharula la kiafya wakati wa mafunzo ya siku tatu yanayofanyika katika ukumbi wa mikutano Taasisi hiyo jijii Dar es Salaam. Mafunzo hayo yanatolewa na wataalamu kutoka kituo cha Emergency Medical Services Academy kilichopo Mikocheni jijini Dar es Salaam.

Sylivester Fanya kutoka kituo cha Emergency Medical Services Academy kilichopo Mkocheni jijini Dar es Salaam akiwafundisha madaktari na wauguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) jinsi ya kuokoa maisha ya mtu aliyepata tatizo la dharula la kiafya wakati wa mafunzo ya siku tatu yanayofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akielezea umuhimu wa mafunzo ya jinsi ya kuokoa maisha ya mtu aliyepata tatizo la dharula la kiafya kwa washiriki wa mafunzo hayo ya siku tatu yaliyoandaliwa na kituo cha Emergency Medical Services Academy kilichopo mikocheni jijini Dar es Salaam.
Picha na JKCI

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Dar es salaam(UDSM), Jaji Mstaafu, Damian Lubuva , wakati alipotembelea Chuo cha Uvuvi Kunduchi, jijini Dar es Salaam Novemba 28, 2019.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Mifugo na Uvivu, Luhaga Mpina, wakati alipotembelea Chuo cha Uvuvi Kunduchi, jijini Dar es Salaam Novemba 28, 2019. Katikati ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu, Jenista Mhagama.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akielekeza jambo, wakati alipotembelea Chuo cha Uvuvi Kunduchi, jijini Dar es Salaam Novemba 28, 2019.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapa chakula samaki wanaofugwa kwa adili ya utafiti, kwenye Chuo cha Uvuvi Kunduchi, jijini Dar es Salaam Novemba 28, 2019.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiangalia nyanya zilizopandwa katika kitalu nyumba, kwenye Chuo cha Uvuvi Kunduchi, jijini Dar es Salaam Novemba 28, 2019.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifafanuliwa jambo na Mwanafunzi wa Shahada ya Uzamivu, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Aulath Mustafa, wakati akiangalia nyanya zilizopandwa katika kitalu nyumba, kwenye Chuo cha Uvuvi Kunduchi, jijini Dar es Salaam Novemba 28, 2019.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiangalia samaki wanaofugwa kwa adili ya utafiti, kwenye maabara ya Chuo cha Uvuvi Kunduchi, jijini Dar es Salaam, wakati alipotembelea Chuo hicho, Novemba 28, 2019. Kulia ni Waziri wa Mifugo na Uvivu, Luhaga Mpina. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

DPP Afuta Kesi 59 Zaidi Jijini Mbeya

Waziri wa Katiba na Sheria Mh. Balozi Dkt Augustine Mahiga (Mb) akisalimiana na afisa wa magereza wakati wa ziara ya kikazi katika gereza la Tukuyu Wilaya ya Rungwe Jijini Mbeya. Kushoto ni Mkuu wa Gereza la Tukuyu ASP. Samwel J. Kaluwa akiwatambulisha Staff wa gereza hilo mbele ya Waziri.

Na: Mwandishi Wetu

Katika mwendelezo wa ziara ya kikazi ya Waziri wa Katiba na Sheria Mh. Balozi Dkt Augustine Mahiga (Mb) kwenye mikoa ya kusini, Mkurugenzi Mkuu wa Mashitaka Tanzania (DPP) Biswalo Mganga amefuta jumla ya kesi 59 katika mahakama za Mkoa wa Mbeya.

Mkurugenzi Biswalo ameyafanya hayo katika gereza la Ruanda mjini Mbeya na gereza la Tukuyu Wilaya ya Rungwe alipoambatana na Waziri wa Katiba na Sheria Balozi Mahiga ili kujionea hali halisi ya mazingira ya utoaji haki jinai katika magereza hayo na taasisi mbalimbali za haki jinai ikiwemo Ofisi ya Taifa ya Mashitaka, Polisi, Mahakama na Magereza yenyewe. Read more

Uyui Yajivunia Mafanikio ya Miaka 4 ya Serikali ya Awamu Tano

Mkuu wa Wilaya ya Uyui Mkoani Tabora Mhe. Gift Msuya akisisitiza kuhusu mikakati yake ya kuhakikisha wanafikia maendeleo endelevu kupitia miradi inayotekelezwa kwa manufaa ya wananchi.

Na mwandishi Wetu

Serikali ya Awamu ya Tano imefanikiwa kuleta mageuzi katika sekta ya Afya, Maji, Elimu na sekta nyingine zinazolenga kuwainua wananchi kiuchumi katika Wilaya ya Uyui, Mkoani Tabora.

Akizungumza katika mahojiano maalum kuhusu utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa kipindi cha miaka 4 ya Serikali ya Awamu ya Tano, Mkuu wa Wilaya hiyo, Mhe. Gift Msuya amesema kuwa moja ya miradi hiyo ni ujenzi wa Hospitali ya wilaya  uliogharimu shilingi bilioni 1.6 na ujenzi umefikia asilimia 95 na inatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Novemba, 2019. Read more

Matukio Katika Picha: Waziri Dkt.Mpango katika Siku ya Takwimu Afrika, 2019.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt.Philip Mpango akizungumza na Washiriki wa Mkutano wa Siku ya Takwimu Afrika uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, Waziri amatoa maagizo kwa Ofisi ya Takwimu (NBS), na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) kufanya kazi kwa kushirikiana.

Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Dkt. Albina Chuwa akizungumza katika na Washiriki wa Mkutano wa Siku ya Takwimu Afrika uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, ambapo kauli mbiu ilikuwa ni ‘Kila mmoja wetu ana umuhimu kwa takwimu bora, kwa usimamizi bora wa watu wanaolazimika kuyakimbia makazi yao barani Afrika’

Wanafunzi kutoka Shule mbalimbali za Jijini la Dar es Salaam wakifuatilia Mkutano wa Siku ya Takwimu Afrika uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam leo Novemba 28, 2019. Read more

Naibu Waziri Shonza: Wafundisheni Vijana Mila na Desturi za Makabila

Naibu Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza akicheza ngoma ya asili na vijana wa jamii ya Kiiraiqw waliyoshiriki shindano la Mr.Mayo na Miss Imbori ambao wanahistoria katika jamii hiyo katika masuala ya mila na desturi leo katika Uwanja wa Michezo wa Mwl.Julius Kambarage Nyerere Wilayani Mbulu wakati wa sherehe za kufunga Tamasha la nne la Utamaduni na Michezo la jamii hiyo lililoandaliwa na uongozi wa Kanisa Katoliki Jimbo la Mbulu.

Na Anitha Jonas – WHUSM,Mbulu Manyara.

Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza ametoa wito kwa wadau mbalimbali katika jamii kujitokeza kuandaa matamasha ya kufundisha vijana katika kuhusu maadili, mila na desturi nzuri.

Mheshimiwa Shonza ametoa wito huo leo Wilayani Mbulu alipokuwa akifunga Tamasha la Nne la Utamaduni na Michezo la Jamii ya Wairaiq lilolenga kutoa piga vita mila potofu na kutoa kuwafundisha vijana wa jamii hiyo maadili,mila na desturi za jamii hiyo ili waweze kuzitunza na kuzienzi . Read more

Rais Magufuli Ampa Tano Waziri Biteko

Na Tito Mselem Bukombe,

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jonh Pombe Magufuli amempongeza Waziri wa Madini ambae pia ni Mbunge wa Jimbo la Bukombe kwa kazi nzuri za maendeleo anazozifanya katika kuleta maendeleo jimboni humo.

Kauli hiyo aliitoa alipokuwa kwenye ziara yake ya kikazi akielekea mapumzikoni Wilayani Chato ambapo alisimamisha msafala wake ili awasalimie wananchi wa Jimbo la Bukombe.

Rais Magufuli amesema anawashukuru sana wananchi wa Bukombe kwa kumchagua Mbunge wa Jimbo hilo ambapo ameeleza kuwa anamsaidia sana katika kutekeleza majukumu yake. Read more

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Akagua Miradi wa Nyumba za NSSF, Zilizopo Tuangoma Kigamboni, Jijini Dar es Salaam

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi wa NSSF, Balozi Alli Siwa, wakati alipokagua Miradi ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa Taifa na Shirika la Nyumba la Taifa ya Ujenzi wa nyumba Tuangoma, Mtoni Kijichi na Dungu, Novemba 27, 2019.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua mradi wa nyumba za Watumishi Housing, uliyopo Dege wilayani Kigamboni, jijini Dar es Salaam, Novemba 27, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua mradi wa nyumba za NSSF, zilizopo Tuangoma katika Wilaya ya Kigamboni, jijini Dar es Salaam, Novemba 27, 2019.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua mradi wa nyumba za NSSF, zilizopo Tuangoma katika Wilaya ya Kigamboni, jijini Dar es Salaam, Novemba 27, 2019.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua mradi wa nyumba za NSSF, zilizopo Tuangoma katika Wilaya ya Kigamboni, jijini Dar es Salaam, Novemba 27, 2019.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akizungumza na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, wakati alipotembelea mradi wa nyumba za NHC, zilizopo Mtoni Kijichi katika Wilaya ya Kigamboni, jijini Dar es Salaam, Novemba 27, 2019.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifafanuliwa jambo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira, Vijana, Kazi na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, wakati akikagua mradi wa nyumba za NSSF, zilizopo Tuangoma katika Wilaya ya Kigamboni, jijini Dar es Salaam, Novemba 27, 2019.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua mradi wa nyumba za NSSF, zilizopo Tuangoma katika Wilaya ya Kigamboni, jijini Dar es Salaam, Novemba 27, 2019.

 

Waziri Biteko Akagua Miradi ya Maendeleo Wilayani Bukombe

Waziri wa Madini Mhe. DOto Biteko akizungumza na wananchi wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya miradi inayotekelezwa na Serikali wilayani Bukombe.

Na: Tito Mselem Bukombe,

Waziri wa Madini Doto Biteko, amekagua miradi ya maendeleo katika wilaya ya Bukombe mkoani Geita na kuwataka madiwani wilayai humo kutoa ushirikiano kwa watalamu ili kukamilisha miradi hiyo kwa wakati.

Waziri Biteko alitoa wito huo wakati alipotembelea miradi ya ujenzi wa madarasa katika shule ya sekondari Iguwa na shule ya msingi Mwalo zilizopo wilayani Bukombe.

Katika kutekeleza hayo Waziri Biteko alichangia vifaa vya ujenzi kwenye shule ya msingi Segwe, Mwalo pamoja na shule ya Sekondari ya Iguwa zilizopo wilayani humo ili kuharakisha ukamilishwaji wa shule hizo. Read more