Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

TBS Yatoa Elimu kwa Wajasiriamali juu ya Uzalishaji kwa Kufuata Mifumo Sahihi

Na Mwandishi Wetu

SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limetumia Maadhimisho ya Siku ya Viwango Duniani kwa kutoa elimu, kusikiliza changamoto za wenye viwanda, wazalishaji na wajasiriamali na kuzipatia ufumbuzi ili kuhakikisha wanaendelea kufanya uzalishaji kwa kufuata mifumo sahihi.

Maofisa hao walikutana na wadau hao mwishoni mwa wiki katika ofisi za SIDO, Vingunguti jijini Dar es Salaam ambapo pia waliwahamasisha kushiriki katika uandaaji viwango.

Shirika la Viwango la Kimataifa (ISO) ambalo TBS ni mwanachama, huadhimisha Siku ya Viwango Duniani kila mwaka Oktoba 14, lakini kwa Tanzania kutokana na siku hiyo kuangukia tarehe ya kumbukizi ya kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, TBS ilisogeza mbele maadhimisho hayo hadi kuanzia Oktoba 21 na yanatarajiwa kufikia kilele chake Oktoba 31, mwaka huu.

Ofisa Viwango Mwandamizi wa TBS, Joseph Mwaipaja, alisema wanatumia fursa hiyo kumbusha wadau umuhimu wa viwango, lengo likiwa ni kupunguza bidhaa zisizofaa katika masoko ya Tanzania na kuwajengea wananchi, wenye viwanda na wazalishaji uelewa wa pamoja kuhusiana na masuala ya viwango.

Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Rais Magufuli: Watanzania Tutembee Kifua Mbele, Tunaweza

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.John Pombe Magufuli, akihutubia wananchi mara baada ya kupokea Ndege mpya Aina ya Dreamliner 787-8, yenye uwezo wa kubeba Abiria 262, hafla hiyo ilifanyika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, Kulia ni Spika wa Bunge Job Ndugai, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof.Palamagamba Kabudi na Kaimu Balozi wa Marekani, Dkt.Inmi Patterson..

Ndege Mpya Aina ya Dreamliner 787-8, yenye uwezo wa kubeba Abiria 262, ikimwagiwa maji (water salute) ikiwa ni ishara ya ndege mpya inapokuwa inapokelewa, hafla ya kuipokea ndege hiyo, ilifanyika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Julius Nyerere Terminal 1Jijini Dar es Salaam .

Na Mwandishi Wetu-MAELEZO, Dar es Salaam

RAIS Dkt. John Magufuli amesema Tanzania itaendelea kutekeleza kwa kasi kubwa miradi ya maendeleo nchini kwa kuwa Serikali imeimarisha nidhamu katika usimamizi na matumizi ya rasilimali zilizopo pamoja na ukusanyaji wa kodi.

Akizungumza katika hafla ya upokeaji wa ndege mpya ya Serikali ya Boeing 787-8 Dreamliner katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere leo Jumamosi (Oktoba 26, 2019) Jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli aliwataka Watanzania kujivunia na kuendelea kuiunga mkono Serikali yao kwa kuwa imedhamiria kuwaletea maendeleo ya kweli na ya haraka. Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Majaliwa Aitetea Zimbabwe Mkutano wa NAM

Na Mwandishi wetu-MAELEZO

Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa Majaliwa amehimiza mjadala wenye tija kutoka Jumuiya ya Kimataifa ili kuiondolea vikwazo vya kiuchumi nchi ya Zimbambwe.

Waziri Mkuu Majaliwa ameyasema hayo katika Mkutano wa 18 wa Wakuu wa nchi na Serikali wa nchi zisizofungamana na upande wowote (NAM) kutoka Afrika na kwingineko duniani uliofanyika Baku, Azerbaijan.

“Uwekwaji wa vikwazo vya kiuchumi kwa nchi ya Zimbambwe unalemaza ukuaji wa uchumi,ufanyaji wa biashara,uwekezaji na ustawi wa watu”Aliongeza Waziri Mkuu Majaliwa.

Hatua hiyo imekuja wakati China ikiunga mkono wazo la Rais Dkt. Magufuli la kuitaka Jumuiya ya Kimataifa kuindolea Zimbabwe vikwazo vya kiuchumi ambapo kupitia Balozi wake hapa nchini Wan Ke aliitaka jumuiya ya kimataifa kuondoa vikwazo hivyo katika kongamano maalum kuhusu vikwazo vya kiuchumi na hatma ya maendeleo ya Afrika lililofanyika Chuo kikuu cha Dar es salaam.


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Nchi za SADC Kuendeleza Mikakati ya Itifaki za Pamoja Kukuza Maendeleo ya Sekta za Mazingira , Maliasili na Utalii

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akifungua Mkutano wa pamoja wa Mawaziri wanaosimamia Sekta ya Mazingira, Maliasili na Utalii kwa Nchi 16 za Jumuiya ya Wanachama wa Maendeleo Kusini mwa Afrika SADC Unaojadili kuhusu mkakati wa kukabiliana na mabadiliko ya Tabia Nchi, Uchumi wa Bluu, Misitu, Utalii, Wanyamapori pamoja na Hifadhi ya Utunzaji wa Mazingira kwa Nchi Wanachama wa SADC. Mkutano huo umefunguliwa leo Oktoba 25,2019 Katika Ukumbi wa Mikutano wa AICC Jijini Arusha.

Na Prisca Libaga- MAELEZO Arusha

Waziri wa maliasili na utalii Dkt.Khamis Kigwangalla mikutano yote ya wataalamu na maktibu wakuu wa jumuiya ya maendeleo kusini mwa Afrika ililenga kujadili na kutoa mapendekezo ya juu ya masuala mbali mbali yanahusu sekta za mazingira maliasili na utali kwa lengo la kuhakikisha zinaendelea kuchangia maendeleo ya sekta hiyo kwenye ukanda huo wa SADC.

Dkt.Kigwangalla ameyasema hayo wakati akimkaribisha makamu wa Raisi Samia Suluhu Hassan kufungua mkutano wa pamoja wa mawaziri wanaosimamia  sekta za Mazingira maliasili na Utalii kwa nchi za jumuiya ya maendeleo kusini mwa Afrika SADC unaoendelea jijini hapa. Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Tanzania Yakabidhiwa Urais wa AALCO

Waziri wa Katiba na Sheria wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Balozi, Dkt.Augustine Mahiga akiongoza Mkutano wa Shirika la Mashauriano ya Kisheria kwa nchi za Asia na Afrika(AALCO) Uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, Katika Mkutano huo Waziri Mahiga alikabidhiwa kuwa Rais wa AALCO

Katibu Mkuu kutoka Wazira ya Katiba na Sheria, Prof. Sifuni Mchome akizunguma na wageni wa Mkutano wa Shirika la Mashauriano ya Kisheria kwa nchi za Asia na Afrika(AALCO) kuhusu kutembelea vivutio vya utalii vilivyoko tanzania bara na Zanzibar mara baada ya kumaliza Mkutano huo katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Na. Paschal Dotto-MAELEZO

Shirika la Mashauriano ya Kisheria kwa Nchi za Asia na Afrika (AALCO) ambalo kikao chake cha 58 kimemalizika hapa Jijini Dar es Salaam safari hii kimeteua Tanzania kuwa Rais wa Shirika hilo na kwa maana hiyo Waziri wa Katiba na Sheria Tanzania, Balozi Augustine Mahiga anashika nafasi hiyo.

Kikao hicho kilichoanza jumatatu, wiki hii kimemalizika leo naajenda mbalimbali zilijadiliwa huku Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Epukeni Matumizi ya Dawa zinazotangazwa Mitandaoni : Ummy Mwalimu

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akisisitiza jambo wakati wa Kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii leo Oktoba 23, 2019 Bungeni Jijini Dodoma.

Na Mwandishi Wetu

Serikali imewataka wananchi kuepuka matumizi ya dawa zinazotangazwa kupitia mitandao ya kijamii kwa kuwa hazijadhibitishwa ubora wake na Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA). Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Rais Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli Akutana na Kufanya Mazungumzo na Viongozi wa AALCO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Viongozi wa Taasisi ya Mashauriano ya Kisheria kwa Nchi za Asia na Afrika (AALCO) ambao wanahudhuria mkutano wa 58 unaofanyika hapa nchini kwa siku 5 ukiwakutanisha wajumbe kutoka nchi wanachama 49 na mashirika mbalimbali walipomtembelea ikulu jijini Dar es Salaam. Oktoba 23, 2019.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa AALCO aliyechaguliwa katika mkutano huu Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga (Waziri wa Sheria na Katiba, Tanzania), Makamu wa Rais wa AALCO aliyechaguliwa katika mkutano huu Prof. Mohamad Shalaldeh (Waziri wa Sheria wa Palestina), Katibu Mkuu wa AALCO Prof. Kennedy Gastorn (Tanzania) na Naibu Makatibu Wakuu wa AALCO watatu ambao ni Bw. Yukihiro Takeya (Japan), Bi. Wang Liyu (China) na Dr. Ali Garshasbi (Iran) pamoja na Amon Mpanju Naibu katibu mkuu Wizara ya Katiba na Sheria (Tanzania), ambao wanahudhuria mkutano wa 58 unaofanyika hapa nchini kwa siku 5 ukiwakutanisha wajumbe kutoka nchi wanachama 49 na mashirika mbalimbali walipomtembelea ikulu jijini Dar es Salaam. Oktoba 23, 2019

Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Ziarani Urusi

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mwakilishi wa Kampuni ya Sinara Transport Machinary kwenye hoteli ya Marriot, Sochi nchini Urusi, Oktoba 22, 2019.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mwakilishi wa Kampuni ya Sinara Transport Machinary kwenye hoteli ya Marriot, Sochi nchini Urusi, Oktoba 22, 2019.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Russian Railways, Alexander Misharin kabla ya mazungumzo yao kwenye hoteli ya Marriot ya Sochi nchini Urusi, Oktoba 22, 2019.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na Wakurugenzi wa kampuni ya kutengeneza matrekta ya BTP, Alexsey Pankov (kushoto) na Ignat Dydyshko baada ya mazungumzo kwenye hoteli ya Marriot ya Sochi nchini Urusi, Oktoba 22, 2019.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Wakurugenzi wa kampuni ya kutengeneza matrekta ya BTP, Alexsey Pankov (kuatikati) na Ignat Dydyshko kwenye hoteli ya Marriot ya Sochi nchini Urusi, Oktoba 22, 2019.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Wakurugenzi wa kampuni ya kutengeneza matrekta ya BTP, Alexsey Pankov (kuatikati) na Ignat Dydyshko kwenye hoteli ya Marriot ya Sochi nchini Urusi, Oktoba 22, 2019.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Wakurugenzi wa kampuni ya kutengeneza matrekta ya BTP , Alexsey Pankov (kushoto) na Ignat Dydyshko baada ya mazungumzo kwenye hoteli ya Marriot ya Sochi nchini Urusi, Oktoba 22, 2019. Kulia ni Balozi wa Tanzania nchini Urusi, Meja Jenerali Mstaafu, Simon Mumwi.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mafuta na Gesi ya ya Zarubezhnefe, Bw. Sergey Kundryashov kwenye hoteli ya Marriot iliyopo Sochi nchini Urusi, Oktoba 22, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


FacebooktwittermailFacebooktwittermail