Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Tanzania Kuanzisha Kituo cha Kimataifa cha Usuluhishi wa Migogoro ya Kibiashara

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi akizungumza na Afisa Mtendaji Mkuu na Mkurugenzi wa Taasisi ya ushauri wa kisheria ya Afrika (ALSF) iliyoko chini ya Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Bwana Stephen Karangizi mazungumzo hayo yamefanyika katika makao makuu ya Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) Abidjan Nchini Ivory Coast.

Na Mwandishi wetu, Abidjan,Ivory Coast.

Tanzania na Taasisi ya ushauri wa kisheria ya Afrika (ALSF) iliyoko chini ya Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) zimekubaliana kuandaa mkakati maalum kwa ajili ya kutoa mafunzo maalum na ya haraka ya msaada wa kisheria kwa Ofisi ya mwendesha mashtaka mkuu wa serikali (DPP) hususani katika kusimamia mashauri katika mahakama na mabaraza ya usuluhishi ya Tanzania na ya Kimataifa katika maeneo ya madini, biashara na usuluhishi na makampuni ya Kimataifa pamoja na mafuta na gesi.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi ameyasema hayo mara baada ya majadiliano na Afisa Mtendaji Mkuu na Mkurugenzi wa Taasisi hiyo ya ushauri wa kisheria ya Afrika (ALSF) Bwana Stephen Karangizi mazungumzo yaliyofanyika katika makao makuu ya Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) Abidjan Nchini Ivory Coast. Read more

Wazazi/ Walezi Waasawa Kupambana na Changamoto za Malezi ya Watoto Nchini

Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Mtoto kutoka Wizara ya Afya, Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Bi. Mwajuma Magwiza akizungumza na wadau na waandishi wa habari za Watoto na Malezi wakati wa Kongamano kuhusu Ajenda ya kitaifa ya wajibu wa wazazi na walezi katika malezi na matunzo ya familia liliwahusisha wahariri na waandishi wa habari za Watoto na Familia lililofanyika jijini Dar es Salaam.

Na Mwandishi Wetu

Wazazi na Walezi nchini wameaswa kuzingatia suala la malezi kwa watoto katika familia kwani bado ni changamoto na limekuwa likileta matatizo mbalimbali kwa watoto nchini ikiwemo kukosa malezi bora kutoka kwa wazazi wao na wengi wao kukimbilia kuishi mitaani.

Hayo yamebainika leo jijini Dar e salaam katika kongamano la kitaifa la waandishi wa habari kuhusu Agenda ya Kitaifa kuhusu wajibu wa wazazi/ walezi katika malezi na matunzo ya Familia liliwakutanisha wahariri na waandishi wa habari zinazohusu Watoto, Malezi na Matunzo ya Familia. Read more

RC Mtwara Atoa Neno kwa Sekta Binafsi Kuhusu Miradi ya REA

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa akizungumza na Ujumbe wa Bodi ya Nishati Vijijini (hawapo pichani), walipomtembelea ofisini kwake, Oktoba 30, 2019 wakiwa katika ziara ya kazi kukagua maendeleo ya utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini mkoani humo.

Na: Veronica Simba – Mtwara

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa ametoa wito kwa sekta binafsi nchini kujitathmini na kufanya kazi kwa uadilifu ili kuonesha mchango wao katika kujenga nchi, hususan kupitia utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini.

Byakanwa alitoa wito huo, Oktoba 30, 2019 wakati akizungumza na Ujumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Nishati Vijijini (REB), uliomtembelea ofisini kwake, ukiwa katika ziara ya kukagua maendeleo ya utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini mkoani humo.

Mkuu huyo wa Mkoa amelazimika kutoa wito huo kutokana na kutoridhishwa kwake na kasi ya mkandarasi anayetekeleza mradi husika mkoani Mtwara, ambaye ni muunganiko (JV) wa kampuni za Radi Services Ltd, Njarita Contractors Ltd & Aguila Contractors Ltd. Read more

Dkt. Abbasi, Bosi PSSSF Watatua Kero ya Walimu Papo kwa Papo Simiyu

Mkurugenzi wa Idara ya Habari -MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali akizungumza katika mkutano ulioandaliwa na Chama cha Walimu Tanzania (CWT) jana mkoani Simiyu. Mkutano huo umewakutanisha walimu kutoka mikoa ya Kagera, Mwanza, Kigoma, Mara, Tabora, Shinyanga, Geita na wenyeji Simiyu.

Na: Immaculate Makilika- MAELEZO

Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali,  Dkt. Hassan Abbasi, jana jioni alilazimika  kumpigia simu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bw. Hoseah Kashimba ili kutatua kero za walimu waliodai kuna wenzao wamestaafu hawajalipwa mafao yao.

Tukio hilo lilijitokeza wakati Dkt. Abbasi akijibu hoja za walimu mara baaya ya kuwasilisha mada wakati wa Mkutano ulioandaliwa  na Chama cha Walimu Tanzania (CWT) mkoani Simiyu na kuhudhuriwa na walimu kutoka mikoa ya Kigoma, Simiyu, Shinyanga, Mwanza, Geita, Mara, Tabora na Kagera  Read more

Serikali Yapongeza Juwanata kwa Kuanzisha Jumuiya ya Wasindikaji Nafaka

Na: Mwandishi Wetu

Serikali imeupongeza uongozi wa muda wa Jumuiya ya Wasindikaji Nafaka Tanzania (JUWANATA) kwa kukamilisha rasimu ya katiba ya umoja  wao

Pongezi hizo za serikali zimetolewa leo na Mkurugenzi Msaidizi wa Kitengo cha Masoko toka Wizara ya Kilimo Benito Kavenuka wakati wa mkutano maalum wa Juwanata uliofanyika Jijini Dar es Salaam .

Kavenuke amesema kuundwa kwa jumuiya ya wasindikaji mazao ya nafaka ni utekelezaji wa azimio la mkutano wa wafanyabiashara ya mazao ya nafaka uliofanyika mwezi Agosti mwaka huu chini ya  Waziri wa Kilimo. Read more

Waziri Dkt. Mwakyembe Azindua Jukwaa la Utengenezaji Maudhui na Usambazaji wa Kazi za Sanaa (BDF).

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe akifafanua jambo Waandishi wa Habari (hawapo pichani), kuhusu Jukwaa la utengenezaji maudhui mbalimbali ya filamu na Muziki na kusambaza (BDF) lililozinduliwa leo katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, Wengine ni Mtangazaji kutoka Clouds Media Group (Clouds Plus), Gift Swai (kushoto) na Isaya Kandonga (Kulia).

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe akifafanua jambo kwa Mtangazaji wa Clouds Media Group(Clouds Plus), Isaya Kandonga kuhusu Jukwaa la utengenezaji maudhui mbalimbali ya filamu na Muziki na kusambaza (BDF) lililozinduliwa leo katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe akifafanua jambo kwa Waandishi wa Habari (hawapo pichani), kuhusu Jukwaa la utengenezaji maudhui mbalimbali ya filamu na Muziki na kusambaza (BDF) lililozinduliwa leo katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu, Dkt. Kiagho Kilonzo Akifafanua Jambo kwa Waandishi wa Habari (hawapo pichani), kuhusu Jukwaa la utengenezaji maudhui mbalimbali ya filamu na Muziki na kusambaza (BDF) lililozinduliwa leo katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, kulia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe

Msanii wa Mashairi ya Kughani, Mrisho Mpoto akieleza jambo Waandishi wa Habari (hawapo pichani), kuhusu Jukwaa la utengenezaji maudhui mbalimbali ya filamu na Muziki na kusambaza (BDF) lililozinduliwa leo katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.

MKUTANO WA MAWAZIRI WA AFYA NA UKIMWI, SADC KUJADILI NAMNA YA KUIMARISHA SEKTA YA AFYA

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akifafanua jambo kwa Waandishi wa Habari (Hawapo pichani) kuhusu Mkutano wa Mawaziri wa Afya na Ukimwi kwa nchi za SADC, utakaofanyika kuanzia Novemba 04 hadi 08, 2019 katika ukumbi wa Banki Kuu ya Tanzania Jijini Dar es Salaam.

Na.Paschal Dotto

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatarajiwa kuwa mwenyeji wa Mkutano wa Mawaziri wa Sekta ya Afya na UKIMWI kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) unaotarajiwa kufanyika nchini kuanzia Novemba  04 hadi 08, 2019, katika  Ukumbi wa Mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika Mkutano na Waandishi wa Habari, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe.Ummy Mwalimu amesema kuwa Mkutano huo utafunguliwa rasmi na  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, huku kauli mbiu yake ikiwa ni “Ushirikiano wa nchi za SADC ni nguzo kuu kufikia Maendeleo Endelevu ya Sekta ya Afya na Mapambano dhidi ya UKIMWI.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu, kwa Waandisahi wa Habari na Wataalmu wa Afya Kutoka Wizara ya Afya (Hawapo pichani) kuhusu Mkutano wa Mawaziri wa Afya na Ukimwi kwa nchi za SADC, utakaofanyika kuanzia Novemba 04 hadi 08, 2019 katika ukumbi wa Banki Kuu ya Tanzania Jijini Dar es Salaam, kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari-MAELEZO(Uratibu-Mawasiliano Serikalini) Bi. Zamaradi Kawawa wa (kwanza) na Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Dkt. Zainabu Chaula.

Read more

Dkt. Mwakyembe: Ni heshima Kutembelewa na Miss World 2018

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akiongea na wanafunzi wa shule ya sekondari Moshono leo jijini Arusha.

Na Eleuteri Mangi, WHUSM, Arusha

Ni heshima kubwa kwa Tanzania kutembelewa na Mwenyekiti na Mwendeshaji wa Shindano la Miss World Bi Julia Morley pamoja na Mshindi wa Miss World 2018 Vanessa Ponce.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe wakati wa uzinduzi wa taulo za kike zinazojulikana kama Uhurupads uliofanyika leo katika shule ya sekondari Moshono iliyopo jijini Arusha.

“Ujio wao leo hapa Arusha, ni heshima kwa taifa. Katika mataifa yote duniani, wameichagua Tanzania, hii ni heshima kubwa na wametuletea zawadi ya Uhurupads ambazo zitawaweka huru watoto wetu katika kutimiza ndoto zao hasa wanapokuwa shuleni” amesema Waziri Dkt. Mwakyembe.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Miss World 2018 Vanessa Ponce kutoka Mexico (kushoto) na Miss Tanzania 2019 Sylivia Sebastian (kulia).

Aidha, Waziri Dkt. Mwakyembe amesema kuwa bidhaa ya taulo hizo alizozindulia leo ni rafiki kwa mazingira kwa kuwa zinaweza kutunzwa mahali popote na zisiwe na madhara kwenye mazingira kwa kuwa haina  mchanganyiko wowote wa plastiki. Taulo hizo zinazotengenezwa na kikundi cha wanawake 12 kiachojulikana kama timu ya Uhuru Kit Ltd ambao wanaunga mkono juhudi za Serikali katika kutunza mazingira kwa marufuku ya matumizi ya mifuko ya plastiki nchini Julai, 2019. Read more

Rais Dkt. Magufuli Apokea Hati za Utambulisho Toka kwa Mabalozi Wapya wa Finland, Umoja wa Ulaya na Rwanda Ikulu Jijini Dar es Salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea hati ya utambulisho toka kwa Balozi mteule wa Jamhuri ya Rwanda nchini Meja Jenerali Charles Karamba kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaa leo Jumatatu Oktoba 28, 2019

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea hati ya utambulisho toka kwa Balozi mteule wa Jamhuri ya Rwanda nchini Meja Jenerali Charles Karamba kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaa leo Jumatatu Oktoba 28, 2019

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na Balozi mteule wa Jamhuri ya Rwanda nchini Meja Jenerali Charles Karamba baada ya kupokea hati yake ya utambulisho kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaa leo Jumatatu Oktoba 28, 2019

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuliakipokea hati ya utambulisho toka kwa Balozi mteule wa Jamhuri ya Finland nchini Mhe. Riita Swan kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaa leo Jumatatu Oktoba 28, 2019

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Balozi wa Jamhuri ya Finland nchini Mhe. Riita Swan baada ya kupokea hati yake ya utambulisho kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaa leo Jumatatu Oktoba 28, 2019

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea hati ya utambulisho toka kwa Balozi mteule wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini Mhe. Manfredo Fanti kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaa leo Jumatatu Oktoba 28, 2019

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifanya mazungumzo na Balozi mteule wa Umoja wa Ulaya (EU) Mhe. Manfredo Fanti baada ya kupokea hati yake ya utambulisho kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaa leo Jumatatu Oktoba 28, 2019