Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Imarisheni Mahusiano na Wadau-Majaliwa

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema mahusiano kati ya Serikali na wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa kidini, kimila ni muhimu yakaimarishwa.

Ameyasema hayo jana (Jumanne, Septemba 24, 2019) wakati akipokea taarifa ya mkoa wa Iringa alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Iringa kwa ajili ya ziara ya kikazi.

Waziri Mkuu alisema ni lazima mahusiano hayo yakadumishwa katika ngazi zote kwa sababu Serikali ipo kwa ajili ya wananchi wote na inawahudumia bila ya ubaguzi.

Aliwataka viongozi waliopewa dhamana ya kusimamia maeneo mbalimbali nchini wahakikishe wanatekeleza majukumu yao ipasavyo na uwajibikaji wao uwe na tija.

 Waziri Mkuu amesisitiza kuwa watendaji wahakikishe suala la ukusanyaji wa mapato linapewa kipaumbele katika maeneo yao.

“Ukusanyaji wa mapato ni muhimu kwa ajili ya maendeleo ya Taifa kwa sababu miradi ya maendeleo kama ujenzi wa shule haiwezi kutekelezeka bila ya kukusanya mapato.”

Awali, Akisoma taarifa ya mkoa, Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Hapi alisema mkoa huo umepewa zaidi ya sh. bilioni saba kwa ajili ya ujenzi wa hospitali za wilaya.

Alisema fedha hizo zimetumika kwa ajili ya ujenzi wa hospitali kwenye Manispaa ya Iringa (98%), Halmashauri ya wilaya ya Iringa (90%), Kilolo(99%), Mufindi (89%).

Mkuu huyo wa mkoa alisema mbali na fedha hizo za ujenzi wa hospitali pia Serikali imetoa zaidi ya sh. bilioni tatu kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa vituo vya afya.

Akizungumzia kuhusu uchaguzi wa Serikali za mitaa, kiongozi huyo alisema wanaendelea na maandalizi.Mkoa una vijiji 360, mitaa 222 na vitongoji 2,216


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Dkt. Shein na Ujumbe Wake Watembelea Kiwanda Cha Uchimbaji Wa Mafuta na Gesi (Rak Ges)

Mwangalizi Mkuu wa Uzalishaji wa kiwanda cha Kampuni ya Kimataifa ya Uchimbaji wa Mafuta na Gesi Asilia cha Ras Al Khaimah (RAK GAS) Deepu Thomas (kulia)akimueleza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein jinsi ya kiwanda hicho kinavyoendesha shughuli zake za uzalishaji wa Gesi wakati Mh.Rais alipofanya ziara katika kiwanda katika ziara Nchi za Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mh.Dk Ali Mohamed Shein (katikati) akipata maelezo kutoka kwa Meneja Mkuu wa Kiwanda cha Kampuni ya Kimataifa ya Uchimbaji wa Mafuta na Gesi Asilia cha Ras Al Khaimah (RAK GAS) Peter Deibel (kushoto) wakati alipotembelea kiwanda hicho katika ziara Nchi za Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).

Baadhi ya viongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibra walioambatana na  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein wakisikiliza kwa makini maelezo kutoka kwa mèneja uzalishaji wa kampuni ya Rak Gas (hayupo pichani) wakati ujumbe huo ulipofanya ziara katika kiwanda hicho wakiwa katika ziara ya Nchi za Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Serikali Kuvuna Mabilioni Kupitia Usambazaji Gesi Asilia Viwandani

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa matumizi ya gesi asilia katika kiwanda cha Lodhia, kilichopo Mkuranga, Mkoa wa Pwani,

Wizara ya Nishati kupitia Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), inatarajia kukusanya kati ya shilingi milioni 85 hadi 120 kwa mwezi, sawa na shilingi bilioni 1.02 hadi 1.4 kwa mwaka kutokana na matumizi ya gesi asilia katika kiwanda cha Lodhia kilichopo Mkuranga, ambayo hadi sasa ni futi za ujazo laki mbili kwa siku.

Hayo yamebainishwa Septemba 24, 2019 wakati Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani, alipozindua matumizi ya gesi asilia katika kiwanda hicho cha kufua vyuma ambacho awali kilikuwa kikitumia mafuta mazito.

Mbali na makusanyo hayo kwa serikali; kwa upande wa kiwanda, kupitia matumizi ya gesi asilia, kimeweza kupunguza gharama za uzalishaji wa bidhaa zake kwa zaidi ya asilimia 40 ikilinganishwa na gharama zilizokuwa zikitumika kwa ajili ya mafuta mazito.

Akizungumza baada ya kukagua shughuli za kiwanda hicho pamoja na kufanya uzinduzi husika, Waziri alitoa mwezi mmoja kwa uongozi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA), Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) pamoja na wataalamu wa Wizara, kufanya mapitio ya bei za gesi viwandani ili ziwawezeshe wawekezaji kuzalisha kwa tija.

“Mje na bei muafaka ambazo haziathiri uwekezaji wa TPDC na haziathiri uwekezaji wa wenye viwanda lakini pia zisiathiri mapato ya serikali,” alisisitiza.

Waziri wa Nishati, Dkt, Medard Kalemani (katikati), akisikiliza maelezo kutoka kwa wamiliki wa kiwanda cha kufua vyuma cha Lodhia, kilichopo Mkuranga, Pwani, kabla ya kuzindua rasmi matumizi ya gesi asilia katika kiwanda hicho

Akifafanua zaidi, Waziri alisema bei ya sasa inaanzia Dola 4.7 hadi 7.72 kwa uniti moja, ambayo imekuwa kikwazo kwa wawekezaji.

Aidha, Waziri aliiagiza TPDC na kampuni yake tanzu ya GASCO, kukamilisha zoezi la ukusanyaji takwimu kwa ajili ya usambazaji wa gesi wilayani Mkuranga ndani ya kipindi cha miezi miwili ili ziwezeshe kubaini mahitaji ya gesi viwandani katika wilaya hiyo na kuvisambazia nishati hiyo kwani manufaa yake ni makubwa.

Waziri pia alieleza kuwa serikali inafanya mapitio ya bei za umeme ili kuzirekebisha na kwamba bei hizo zitapungua, hususan baada ya kukamilika kwa miradi mikubwa ya uzalishaji umeme, ukiwemo wa Julius Nyerere, Rufiji.

Aidha, aliwataka wadau wa sekta za gesi na mafuta, kutoa ushirikiano wakati wa zoezi la kupitisha mabomba ya gesi katika maeneo yao. “Msidai fidia kwakuwa nasi hatutozi gharama za kuunganisha. Hivyo nanyi, msilete vikwazo.”

Katika hatua nyingine, Waziri aliuagiza uongozi wa TANESCO wa Wilaya, Mkoa na Makao Makuu, kukipatia kiwanda cha Lodhia megawati nane zaidi za umeme kama kilivyoomba ili zifike 14 kufikia mwisho wa mwezi huu.

Alisema hakuna sababu ya kushindwa kutekeleza agizo hilo maana kuna umeme wa kutosha. Sambamba na hilo, aliagiza pia kusiwe na mgao wa umeme wilayani humo kwani kuna umeme wa ziada.


Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani na Ujumbe wake, wakikagua kiwanda cha kufua vyuma cha Lodhia, kilichopo Mkuranga, Mkoa wa Pwani, kabla ya kuzindua matumizi ya gesi asilia kiwandani hapo, Septemba 24, 2019.

Kuhusu usambazaji umeme katika mitaa na vijiji vya wilaya hiyo, Waziri aliitaka TANESCO kuhakikisha vijiji vyote 88 vya wilaya hiyo vinaunganishiwa umeme kupitia miradi mbalimbali inayoendelea kutekelezwa.

Akizungumza kwa niaba ya wananchi wa Mkuranga, Mkuu wa Wilaya hiyo, Filberto Sanga aliishukuru serikali na kupongeza jitihada za wizara ya nishati katika kusambaza nishati ya umeme na gesi kwa wananchi. Aliomba wilaya yake ipewe kipaumbele kwa kupatiwa umeme zaidi kutokana na uwepo wa viwanda vingi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Lodhia, Sailesh Pandit, alisema Wizara ya Nishati, kupitia TPDC na TANESCO imekuwa ikiwapa ushirikiano mkubwa katika kuongeza tija ya uzalishaji wao kwa kuwapatia nishati wanayoihitaji pasipo vikwazo. Aliwaasa wamiliki wengine wa viwanda, kutumia gesi asilia kwani inapunguza kwa kiasi kikubwa gharama za uzalishaji.

Kiwanda kingine ambacho kimeunganishiwa gesi asilia wilayani humo ni cha Goodwill Ceramics kilichopo kijiji cha Njopeka. Zoezi la kuunganisha wateja wengine linaendelea.


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Wahariri wa Habari Waaswa Kuzingatia Matumizi ya Takwimu Rasmi

Mtakwimu Mkuu wa Serikali toka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Dkt. Albina Chuwa akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku mbili kwa Wahariri wa Vyombo vya Habari kuhusu Marekebisho ya Sheria ya Takwimu ya mwaka 2015 yaliyofanyika mwaka 2018 na 2019 leo jijini Dodoma.

Na Mwandishi Wetu- Dodoma

Wahariri wa Vyombo vya Habari nchini wameaswa kuendelea kuzingatia matumizi ya takwimu rasmi katika kuelimisha umma  kuhusu miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali.

Akizungumza  wakati akifungua warsha kwa wahariri hao leo Jijini Dodoma, Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Dkt Albina Chuwa amesema kuwa dhamira ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) ni kuendelea kuhakikisha kuwa wananchi wanapata taarifa sahihi katika nyanja mbalimbali ikiwemo katika matumizi ya takwimu zinazozalishwa hapa nchini. Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Mbunge wa Kwimba Aimwagia Sifa Serikali Baada ya Kukamilisha Mradi wa Maji

Mbunge wa Jimbo la Kwimba Mhe. Shanif Mansoor (CCM) (katikati) akinawa mikono wakati wa sherehe za kupokea mradi wa maji wa Kijiji cha Shilima, Kata ya Kikubiji, Wilaya ya Kwimba, Mkoani Mwanza. Kulia ni Diwani wa Kata ya Kikubiji, Alfred Luteja.

Mbunge wa Jimbo la Kwimba Mhe. Shanif Mansoor (CCM) ameipongeza Serikali kupitia Wizara ya Maji kwa kukamilisha mradi wa maji wa Kijiji cha Shilima, Kata ya Kikubiji Wilaya ya Kwimba, Mkoani Mwanza.

Ametoa pongezi hizo jana alipojumuika na wapiga kura wake wa Kijiji cha Shilima kusherehekea kukamilika kwa mradi huo ambao ulipaswa kukamilika tangu mwaka 2013 lakini kutokana na udhaifu wa Mkandarasi haukuweza kukamilika kwa wakati. Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Taarifa Muhimu kwa Waombaji Mikopo kwa 2019/2020

Waombaji Mikopo Kurekebisha Taarifa

Jumatatu, Septemba 23, 2019

 

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) inapenda kuwajulisha waombaji wote wa mikopo kwa mwaka wa masomo 2019/2020 kuwa kwa sasa HESLB inaendelea na kazi ya uhakiki (verification of online-submitted applications) wa maombi yaliyowasilishwa ambayo itakamilika Jumapili, Septemba 29, 2019. 

Baada ya kukamilika kwa kazi ya uhakiki, HESLB itatoa fursa ya siku nne, kuanzia Jumatatu, Septemba 30 hadi Alhamisi, Oktoba 3, 2019 kwa waombaji mikopo ambao maombi yao yatakuwa yamebainika kuwa na upungufu kufanya marekebisho.

Taarifa hii inatolewa kufuatia HESLB kupokea maoni na maswali kupitia barua pepe na simu kuhusu hatua iliyofikiwa katika uhakiki na uchambuzi wa maombi ya mikopo ya elimu ya juu yaliyowasilishwa HESLB.

Waombaji mikopo wote wanashauriwa kutembelea tovuti yetu (www.heslb.go.tz) au kuingia katika akaunti zao waliozoombea mkopo kupitia mfumo wa uombaji mkopo (www.olas.heslb.go.tz) kuanzia Septemba 30, 2019 ili kupata mwongozo wa kufanya marekebisho kwa njia ya mtandao. Baada ya kuingia, watapata ujumbe iwapo maombi yao yamekamilika au yanahitaji marekebisho.

HESLB imejipanga kuhakikisha kazi yote ya uhakiki na uchambuzi wa maombi yote ya mikopo inakamilika ifikapo Oktoba 6, 2019 ili wanafunzi wahitaji wapangiwe mikopo, wapate taarifa na fedha za mikopo zitumwe vyuoni kabla ya vyuo kufunguliwa katika wiki ya kwanza ya mwezi Novemba, 2019.

Taarifa hii pia inapatikana katika tovuti ya HESLB (www.hesl.go.tz).

Imetolewa na:

Abdul-Razaq Badru,

Mkurugenzi Mtendaji,

Bodi ya Mikopo ya Wa-nafunzi wa Elimu ya Juu

 


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Matukio Mbalimbali Kwenye Ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Katika Maonesho ya Teknolojia na Uwekezaji wa Madini Geita

Mtaalam kutoka Tume ya Madini, Monica Mkumbo (kulia) akielezea majukumu ya Tume ya Madini kwa mchimbaji wa madini ya dhahabu katika eneo la Kakola mkoani Geita, Yohana James (kushoto) kwenye Maonesho ya Teknolojia na Uwekezaji wa Madini yanayoendelea mjini Geita tarehe 23 Septemba, 2019.

Fundi Sanifu Migodi Mwandamizi, Msafiri Kussa na Mjiolojia Asimwe Kafrika kutoka Tume ya Madini wakitoa elimu kwa umma kwa wanafunzi wa shule za msingi za Kalangala na Nyasa waliotembelea banda la Tume ya Madini kwenye Maonesho ya Teknolojia na Uwekezaji wa Madini yanayoendelea mjini Geita tarehe 23 Septemba, 2019

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (kulia) akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika banda la Tume ya Madini, kwenye Maonesho ya Teknolojia na Uwekezaji wa Madini yanayoendelea mjini Geita tarehe 23 Septemba, 2019

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Dustan Kitandula na Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo wakisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika banda la Wizara ya Madini kwenye Maonesho ya Teknolojia na Uwekezaji wa Madini yanayoendelea mjini Geita tarehe 23 Septemba, 2019.

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo akisaini kitabu cha wageni kwenye banda la Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) kwenye Maonesho ya Teknolojia na Uwekezaji wa Madini yanayoendelea mjini Geita tarehe 23 Septemba, 2019.


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Majaliwa Afungua Maonyesho ya Pili ya Tekinolojia ya Dhahabu Mjini Geita

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kuhusu noti bandia na noti halali kutoka kwa Angela Kashanga (kulia) wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) wakati alipotembelea banda la BOT katika Maonyesho ya Tekinolojia ya Dhahabu yaliyofunguliwa na Waziri Mkuu, kwenye uwanja wa CCM Kahangalala mjini Geita, Septemba 22, 2019. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Gabriel na katikati ni Mkurugenzi wa BOT tawi la Mwanza, Florence Kazimoto. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kuhusu noti bandia na noti halali kutoka kwa Angela Kashanga wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) wakati alipotembelea banda la BOT katika Maonyesho ya Tekinolojia ya Dhahabu yaliyofunguliwa na Waziri Mkuu, kwenye uwanja wa CCM Kahangalala mjini Geita, Septemba 22, 2019.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mtalaam wa Uchenjuaji madini, John Ngenda ( wa pili kulia) kuhusu mtambo wa kuchenjua madini wakati alipofungua Maonyesho ya Pili ya Tekinolojia ya Dhahabu kwenye uwanja wa CCM, Kahangalala mjini Geita, Septemba 22, 2019. Watatu kulia ni Waziri wa Madini, Doto Biteko na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Gabriel.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipozindua Maonyesho ya Pili ya Tekinolojia ya Dhahabu kwenye uwanja wa CCM Kahangalala mjini Geita, Septemba 22, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe kuzindua Mwongozo wa Unaoonyesha Fursa za Uwekezaji wakati alipofungua Maonyesho ya Tekinolojia ya Dhahabu kwenye uwanja wa Kahangalala mjini Geita, Septemba 22, 2019. Wengine pichani kutoka kushoto ni Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, Waziri wa Madini, Doto Biteko, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi, Robert Gabriel na kulia ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Geita, Alhaj Said Kalidushi.


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Uzinduzi wa Jamafest

Makamu wa Rais wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akipiga ngoma kama isha ya Uzinduzi Rasmi wa Tamasha la Jumuiya ya Afrika Mashariki (Jamafest) pamoja na Tamasha la Urithi Wetu.

Kikundi cha Ngoma kutoka Burundi kikitumbuiza katika Tamasha la Jamafest lililozinduliwa leo na Makamu wa Rais wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam

Kikundi cha Ngoma kutoka Rwanda kikitumbuiza

Kikundi cha Ngoma kutoka Uganda kikitumbuiza Uwanja wa Uhuru Dar es salaam kwenye Tamasha la Jamafest

Kikundi cha Kenya kikitoa burudani kwa watazamaji waliofurika kwenye uwanja wa Taifa kushuhudia uzinduzi wa Tamasha la Jamafest.


FacebooktwittermailFacebooktwittermail