Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Makamu wa Rais Mhe. Samia Akutana na Kufanya Mazungumzo na Balozi wa Denmark, Ufaranza na Qatar Hapa Nchini

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Balozi wa Denmark hapa Nchini Bibi. Mette Norgaard Dissing Spandet wakati Balozi Spandet alipofika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikuklu Jijini Dar Es salaam leo Sept 30,2019 kwa ajili ya kujitambulisha.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Denmark hapa Nchini Bibi. Mette Norgaard Dissing Spandet wakati Balozi Spandet alipofika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikuklu Jijini Dar Es salaam leo Sept 30,2019. kwa ajili ya kujitambulisha.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Ufaransa hapa Nchini Bw. Frederic Clavier wakati Balozi Clavier alipofika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikuklu Jijini Dar Es salaam leo Sept 30,2019 kwa ajili ya kuelezea Mipango na Mlengo ya maendeleo ya Nchi yake kwa Tanzania.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Balozi wa Ufaransa hapa Nchini Bw. Frederic Clavier wakati Balozi Clavier alipofika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikuklu Jijini Dar Es salaam leo Sept 30,2019 kwa ajili ya kuelezea Mipango na Mlengo ya maendeleo ya Nchi yake kwa Tanzania.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Qatar hapa Nchini Bw. Abdulla Jassim Al-Maadadi wakati Balozi Al-Maadadi alipofika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikuklu Jijini Dar Es salaam leo Sept 30,2019 kwa ajili kuaga baada ya kumaliza kipindi chake cha kazi hapa Nchini..(Picha na Ofisi ya Makamu ya Rais)

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Balozi wa Qatar hapa Nchini Bw. Abdulla Jassim Al-Maadadi wakati Balozi Al-Maadadi alipofika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu Jijini Dar Es salaam leo Sept 30,2019 kwa ajili kuaga baada ya kumaliza kipindi chake cha kazi hapa Nchini.

Rais Dkt. John Pombe Magufuli Apokea Taarifa ya Utekelezaji wa Ushauri Wake wa Kuwasamehe Watuhumiwa wa Uhujumu Uchumi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono na Mwendesha Mashataka Mkuu wa Serikali (DPP) Bw. Biswalo Mganga baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa ushauri alioutoa wa kuwasamehe watuhumiwa wa uhujumu uchumi walio tayari kutubu na kurejesha fedha na mali kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatatu Septemba 30, 2019. Kushoto ni Katibu Mkuu Ikulu Mhe. Dkt. Moses Kusiluka

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea baada ya Mwendesha Mashataka Mkuu wa Serikali (DPP) Bw. Biswalo Mganga kumkabidhi taarifa ya utekelezaji wa ushauri alioutoa wa kuwasamehe watuhumiwa wa uhujumu uchumi walio tayari kutubu na kurejesha fedha na mali kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatatu Septemba 30, 2019

Read more

Balozi Sokoine Azindua Mfumo wa Ukusanyaji Takwimu za Gesi Joto

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Balozi Joseph Sokoine akizundua Mfumo wa Kitaifa wa Ukusanyaji Takwimu za Gesijoto, Ufuatiliaji, Uandaaji Taarifa na Uhakiki katika Ukumbi wa Kituo cha Kuratibu Hewa Ukaa Chuo Kikuu cha Kilinmo Sokoine (SUA) mkoani Morogoro. Wanaoshuhudia ni Mkurugenzi wa Misitu na Nyuki Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Ezekiel Mwakalukwa na Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Profesa William Mwegoha

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Balozi Joseph Sokoine amezindua Mfumo wa Kitaifa wa Ukusanyaji Takwimu za Gesijoto, Ufuatiliaji, Uandaaji Taarifa na Uhakiki katika Ukumbi wa Kituo cha Kuratibu Hewa Ukaa Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA) mkoani Morogoro.

Akizindua mfumo huo kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa ais (Muungano na Mazingira) Mhe. George Simbachawene, Balozi Sokoine alisema kuwa utawezesha nchi kukusanya takwimu za gesijoto kutoka sekta mbalimbali kwa ajili ya kuchukua hatua stahiki na maamuzi.

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Balozi Joseph Sokoine akitoa hotuba ya ufunguzi kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa ais (Muungano na Mazingira) Mhe. George Simbachawene.

Naibu Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Sergio Valdini akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mfumo wa Kitaifa wa Ukusanyaji Takwimu za Gesijoto, Ufuatiliaji, Uandaaji Taarifa na Uhakiki.

Pamoja na mambo mengine alisema pia utasaidia kuandaa taarifa mbalimbali ambazo nchi inatakiwa kuandaa kama Mwanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi ambazo zinabainisha kiasi cha uzalishaji wa gesijoto kutoka sekta mbalimbali husika na uondoshaji wake kupitia misitu.

Balozi Sokoine aklibainisha kuwa hadi sasa Tanzania imeandaa taarifa mara mbili na kuwasilisha Sekretareti ya Mkataba mwaka 2003 na ya pili mwaka 2015 na kwa muda wote Tanzania kama ilivyokuwa kwa nchi nyingine.

Aliongeza kuwa Tanzania imetumia wataalamu elekezi kufanya kazi hii chini ya Mradi uliokuwa unatekelezwa na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) kuratibiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais Idara ya Mazingira hivyo kuleta ugumu katika kuthibiti ubora na kulinganisha takwimu za nchi mbalimbali kwani hakukuwa na mfumo au njia iliyokubalika kimataifa kufanya kazi na haikujenga uwezo wa sekta husika.

Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Profesa William Mwegoha akizungumza kumkaribisha mgeni rasmi kuzindua rasmi mfumo huo.

Mratibu wa Kituo cha Kitaifa cha Kuratibu Hewa Ukaa, Prof. Eliakim Zahabu akitoa maelezo kuhusu namna mfumo unavyofanya kazi kwa wageni waalikwa wa hafla hiyo.

“Mfumo wa Kitaifa wa ukusanyaji na usimamizi wa Takwimu za gesijoto, unaozinduliwa leo utawezesha nchi kutoa  takwimu sahihi na za kutosheleza kuhusu uzalishaji wa gesijoto kutoka sekta mbalimbali husika na uondoshaji kwa njia ya misitu, kwa hatua sahihi za uamuzi na kutoa taarifa,” alisema.

Aidha Balozi Sokoine alisema kuwa uzinduzi wa Mfumo huu umekuja wakati muafaka ambapo tunajipanga kuanza utekelezaji wa Makubaliano ya Paris ambayo yalipitishwa na Mkutano wa 21 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabinchi na Tanzania kuridhia Mei 2018.

Aliongeza kuwa kwa sasa Tanzania inakamilisha maandalizi ya Mchango wake katika juhudi za kupambana na Mabadiliko ya Tabianchi hivyo Mfumo huo utasadia katika upatikanaji wa takwimu na taarifa kuhusu utekelezaji wa NDCs na uandaaji wa Taarifa ya Tatu ya Mawasiliano.

Sehemu ya wageni waalikwa wakifuatilia matukio wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mfumo wa Kitaifa wa Ukusanyaji Takwimu za Gesijoto, Ufuatiliaji, Uandaaji Taarifa na Uhakiki.

Mkurugenzi wa Misitu na Nyuki Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Ezekiel Mwakalukwa akitoa neno wakati wa hafla hiyo.

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Balozi Joseph Sokoine akitumia mfumo huo mara baada ya kuuzindua rasmi.

Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Balozi Joseph Sokoine (mbele katikati) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wengine kuanzia kushoto ni Mkurugenzi wa Misitu na Nyuki Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Ezekiel Mwakalukwa, Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Profesa William Mwegoha, Naibu Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Sergio Valdini na Mkuu wa Ndaki ya Misitu, Wanyama Pori na Utalii Prof. John F. Kessy pamoja na washiriki. (Picha Zote na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Utekelezaji wa Mfumo huu utahitaji kila mdau kubaini majukumu yake na kuyatekeleza na hivyo kila mdau anatakiwa kubaini majukumu yake kama yalivyobainishwa katika Mfumo ili  kuhakikisha kuwa Mfumo huu unatekelezwa na hivyo kutuwezesha kufikia malengo tarajiwa,” alisisitiza Balozi Sokoine.

Naibu Katibu Mkuu aliagiza Kituo Cha Kitaifa cha Kuratibu Hewa Ukaa (NCMC) kuratibu na kusimamia mfumo wa Kitaifa wa Ukusanyaji Takwimu za Gesijoto, Ufuatiliaji, Uandaaji Taarifa na Uhakiki.

Aliagiza Wizara za Kisekta ziteue Wataalamu watakaohusika na usimamizi na uandaaji wa takwimu za uzalishaji wa gesijoto katika sekta zao na kuwasilisha kwenye Kituo cha Kitaifa cha Kuratibu Hewa Ukaa.

Pia aliagiza Wizara za Kisekta kwa kushirikiana na Kituo cha Kitaifa cha Kuratibu Hewa Ukaa ziweke Utaratibu wa kuwasilisha taarifa katika Kituo cha Kitaifa cha Kuratibu Hewa Ukaa kila mwaka.na kubainisha watoaji takwimu chini ya sekta zao za uzalishaji wa gesijoto na kuweka utaratibu wa kupata takwimu hizo.

Majaliwa Akagua Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Kilolo

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Ally Happy na Mkuu wa wilaya ya Kilolo, Asia Abdallah (wa pili kushoto) kukagua ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Kilolo , Septemba 27, 2019.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Kilolo, Septemba 27, 2019.

Muonekano wa sehemu ya Hospitali ya Wilaya ya Kilolo ambayo ujenzi wake uko katika hatua za mwisho. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amekagua ujenzi huo Septemba 27, 2019 na kusema kuwa amefurahishwa.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi baada kukagua na kufurahishwa na ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Kilolo, Septemba 27, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Majaliwa Atembelea Kiwanda cha Nguzo za Umeme cha Qwihaya Mjini Mafinga

Nguzo za umeme zikiwa kwenye mtambo wa kuziwekea dawa maalum ya kuzifanya zisishambuliwe na wadudu au kuungua moto zikiwa katika kiwanda cha Qwihaya General Enterprises Company Limited cha mjini Mafinga ambacho kilitembelewa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, September 26, 2019.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua nguzo za umeme zilizorundikana kwenye kiwanda cha Qwihaya General Enterprises Company LTD cha Mafinga zikisubiri wanunuzi. Kiwanda hicho cha nguzo kilitembelewa na Waziri Mkuu, Septemba 26, 2019. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa kiwanda hicho, Leonard Mahenda, wa tatu kushoto ni Meneja Uzalishaji wa kiwanda hicho, Fred Ngwega na wa nne kusho ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Happy. (

Baadhi ya nguzo za umeme zilizorundikana zikisubiri wanunuzi kwenye kiwanda cha Qwihaya General Enterprises Limited cha mjini Mafinga ambacho kilitembelewa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Septemba 26, 2019. {Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

RC Fuatilia Utendaji Kazi Ofisi ya DC Kilolo-Majaliwa

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Iringa, Septemba 27, 2019. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Happy na kulia ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Iringa, Dkt. Abel Nyamahanga.

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemwagiza Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Happi afuatilie utendaji kazi kwenye ofisi ya mkuu wa wilaya ya Kilolo kufuatia watumishi 14 wa ofisi hiyo wakiwemo madereva 10 kuhamishwa baada ya Mkuu wa Wilaya hiyo Asia Abdallah kudai kuwa hawafanyi kazi ipasavyo.

Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema ni mhuimu kwa viongozi wakatambua dhamana zao katika utekelezaji wa shughuli zao pamoja na kuwatambua, kuwajali na kuwathamini watumishi wa kada zote wakiwemo madereva, hivyo ni vizuri wawaandae kwa kuwapa maelekezo kwa wakati kwa kuwa nao ni binadamu na wanafamilia. Read more

TBS Yashiriki Mikutano Ya Mashauriano Kati ya Serikali, Wafanyabiashara na Wawekezaji

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania akiongea wakati wa Mkutano wa Mashauriano kati ya Serikali, Wafanyabiashara na Wawekezaji Uliofanyika Mkoani Ruvuma

Na Neema Mtemvu

SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limetoa elimu kuhusu fursa wanazopata wafanyabiashara na wazalishaji ambao bidhaa zao zimethibitishwa  ubora wake hivyo kuhamasisha wajasiriamali kuthibitisha ubora wa bidhaa zao bure pamoja na kuzipatia majibu changamoto wanazokumbana nazo wadau wake mbalimbali.

Shirika hilo limetoa elimu hiyo wakati wa mikutano ya mashauriano kati ya Serikali, wafanyabiashara na wawekezaji kwa ajili ya kusikiliza changamoto zinazowakabili kwenye mikoa ya Kusini ambayo ni Ruvuma, Mtwara na Lindi kuanzia Septemba 24, mwaka huu. Mikutano hiyo ilimalizika  mkoani Lindi.

Mikutano hii imehudhuriwa na Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa, Naibu Waziri wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Anjelina Mabula, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya  Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira),  Mussa Sima, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Anjellah Kairuki  wabunge na wakuu wa wilaya zote.

Akitoa mada kwa nyakati tofauti kwenye mikutano hiyo, Mkurugenzi wa TBS, Dkt. Yusuf Ngenya, aliwaeleza washiriki hao kuhusiana na mabadiliko ya sheria ya fedha ya mwaka 2019 ambayo yameleta mabadiliko katika Sheria ya Viwango Na: 2 ya mwaka 2009.

Read more

Dkt.Ndungulile: JAMAFEST Iwe Kichocheo Ulaji Vyakula vya Asili, Kulinda Afya

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndungulile, akiwekewa mafuta ya kulainisha ngozi yaliyotengenezwa kutokana na matunda alipotembelea Banda la Chuo cha VETA katika Tamasha la Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki (JAMAFEST) linaloendelea Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. (Picha na Idara ya Habari-MAELEZO)

Na. Paschal Dotto – MAELEZO, Dar es Salaam.

25.09.2019

Naibu wa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dkt. Faustine Ndungulie ametembelea Maonesho ya Tamasha kubwa la Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki (JAMAFEST) na kusisitiza wananchi kutumia zaidi vyakula vya asili ili kupunguza uwezekano wa kupata magionjwa yasisyo ya kuambukiza.

Dkt. Ndungulie amesisitiza utumiaji wa vyakula vya asili baada ya kutembelea Tamasha hilo jana Septemba 25, 2019 ambapo pamoja na mambo mengine alijionea vitu mbalimbali vikiwemo vyakula vya asili na kuwataka Watanzania kujifunza jinsi ya kutumia kuandaa na kutumia vyakula hivyo ambavyo havina madhara katika mwili.

“Katika Tamasha hili Watanzania wanapaswa kujifunza njia za asili katika kuandaa chakula ambacho kinaweza kuwasaidia kulinda afya zao”, alieleza Naibu Waziri

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndungulile, akiangalia moja ya Batiki kutoka kwa Mjasiriamali ambaye anashiriki Maonesho ya Tamasha la Utamaduni la Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (JAMFEST) linaloendelea katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam. (Picha na Idara ya Habari-MAELEZO)

Amesema kuwa masuala ya michezo, sanaa na utamaduni yana uhusiano mkubwa na afya na kuwashauri wasanii kutumia Sanaa kuongelea masuala ya kuimarisha afya kkwa kuwasisitiza wananchi kula chakula bora na kufanya mazoezi ili kufikisha ujumbe kwa Jamii kuhusiana na ulaji bora wa chakula.

Kwa mujibu wa Dkt. Ndungulile, asilimia 30 ya watoto chini ya miaka mitano wana utapiamlo na wamedumaa huku asilimia 10 ya watu wazima wakiwa na lishe iliyopitiliza (vitambi) na asilimia 30 wanapatwa na magonjwa yasiyo ambukizwa ambayo mengi yanatokana na vyakula visivyo bora.

Kwa upande mwingine Naibu Waziri Ndungulile ameipongeza Wizara ya Habari, UtamaDUNI, Sanaa na Michezo kwa kushirikiana na Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kuandaa Tamasha hilo kwa mafanikio ambapo washiriki kutoka nchi tano za Jumuiya ya Afrika Mashariki zimeshiriki. Nchi hizo ni wenyeji Tanzania, Burundi, Kenya, Rwanda na Uganda.

JAMAFEST ni Tamasha la Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki ambalo lilipitishwa katika kikao cha 20 na 23 cha Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kilichofanyika mwezi Machi na Septemba 2012.

Tamasha hili hufanyika mara moja kila baada ya miaka miwili na huzunguka katika nchi wanachama wa EAC. Mpaka sasa Tamasha limekwishafanyika katika nchi za Rwanda (2013) na kuhudhuriwa na washiriki 17,500, Kenya (2015) washiriki 21,000 na Uganda (2017) washiriki 42,600 na sasa linafanyika nchini kuanzia Septemba 21 – 28, 2019.

Naibu Waziri Ikupa Atembelea Tamasha la Jamafest

 

Naibu Waziri Stella akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kutembelea mabanda mbalimbali kwenye Tamasha hilo.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Anayeshughulikia Watu Wenye Ulemavu Mhe. Stella Ikupa, leo ametembelea  Tamasha la JAMAFEST na kuwa moja ya viongozi ambao wamepata Fursa za kuja kutembelea Maonesho haya makubwa ya tamasha la  Utamaduni kwa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki JAMAFEST

Mbali na kutembelea mabanda kwenye Tamasha hilo kubwa la Afrika Mashariki linaloendelea Jijini Dar es Salaam Naibu Waziri Stella amekabidhi viti maalumu kwa watu wenye ulemavu.

Mbali na kutembelea mabanda kwenye Tamasha hilo kubwa la Afrika Mashariki linaloendelea Jijini Dar es Salaam Naibu Waziri Stella amekabidhi viti maalumu kwa watu wenye ulemavu.