Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Ni Wajibu wa Watanzania Kulinda na Kudumisha Utamaduni Wetu;- Mhe.Shonza.

Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe,Juliana Shonza akikimbia leo Agost 31 kuashiria ufunguzi wa mbio za riadha ya Kondoa Irangi Marathon mwaka 2019 zitakazofanyika Jijini Dodoma.

Na Shamimu Nyaki –WHUSM  DODOMA

Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza amesema kuwa watanzania wanao wajibu wa kulinda,kuthamini na kuendeleza Utamaduni wa nchi katika shughuli zote za uzalishaji pamoja na za kijamii.

Mhe.Shonza ameyasema hayo  leo Jijini Dodoma wakati wa maonyesho ya  Utalii wa Utamaduni, mambo kale  na bidhaa za asili za hapa nchini yaliyoongozwa na kauli mbiu  “Utamaduni mambo kale na bidhaa za asili yetu ni fursa ya kibiashara katika utalii” ambayo yalikuwa na lengo la kutangaza utalii wa utamaduni  . Read more

Zabuni  Ununuzi wa Treni 5 Za Umeme, Mabehewa na  Vichwa Waiva

: Mkurugenzi wa Idara ya Habari –MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi akisisitiza jambo wakati akiongea na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) leo tarehe 31 Agosti 2019 jijini Dodoma kuhusu utekelezaji wa Serikali katika kuwaletea wananchi maendeleo kupitia miradi mbalimbali.

Na Mwandishi Wetu

Serikali imesema kuwa zabuni ya ununuzi wa treni 5 za umeme zilizokamilika za abiria utawezesha kuanza kwa huduma ya usafirishaji kati ya Jiji la Dar es Salaam na Morogoro na baadae Dodoma.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi wakati akizungumza na Waandishi wa Habari leo jijini Dodoma kuhusu utekelezaji wa Serikali hadi kufikia Agosti 2019.

Dkt. Abbasi amesema kuwa Serikali imeanza zabuni hiyo ambayo itawezesha kununuliwa kwa  vichwa 22 vya Treni (vitano vya mafuta yaani Diesel Locomotive na 17 vya umeme yaani Electrical Locomotive), pamoja na mabehewa ya abiria 60 na 1430 ya mizigo.

“Treni tano (5) zilizokamilika (Electrical Multiple Unit) za abiria zenye mabehewa nane (8) kila moja na vichwa viwili kwa ajili ya uendeshaji wa treni za abiria kwa kipande cha Dar es Salaam hadi Morogoro na kisha Dodoma zitawezesha watanzania kuanza kutumia usafiri wa kisasa na wa gharama nafuu hivyo kuchochea shughuli za kiuchumi.” Alisisitiza Dkt. Abbasi

Akifanua amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imeweka mkazo katika kuimarisha miundombinu ikiwemo ya reli ndio maana imeweka mkazo katika ujenzi wa mradi huo wa reli ya kiwango cha kimataifa (SGR)

Kuanza kwa huduma ya usafirishaji kati ya Morogoro na Dar es Salaam na baadae Dodoma kunatajwa kuwa kichocheo kikubwa cha maendeleo hapa nchini.

Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt John Pombe Magufuli imeweka mkazo katika kuimarisha miundombinu ili kukuza na kujenga uchumi jumuishi unaowawezesha wananchi kuondokana na umasikini kwa kujikwamua kiuchumi.

 

 

Bilioni 30 Zatumika Ujenzi wa Hospitali za Kanda

Mkurugenzi wa Idara ya Habari –MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) leo jijini Dodoma kuhusu utekelezaji wa Serikali katika kuwaletea wananchi maendeleo kupitia miradi mbalimbali.

Na; Mwandishi Wetu

Takribani Shilingi Bilioni 30 zimetumiwa na Serikali kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali za Kanda ili kuimarisha huduma za Afya hapa nchini ikiwa ni kusogeza zaidi huduma kwa wananchi.

Akizungumzia utekelezaji wa Serikali katika sekta ya Afya hadi kufikia mwezi Agosti mwaka huu Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali,  Dkt. Hassan Abbasi amesema kuwa, Serikali imeshatoa shilingi bilioni 30 kwa ajili ya Ujenzi wa Hospitali za Rufaa za Mikoa (RHH) na sehemu kubwa ya ujenzi umekamilika.

“Niwathibitishie Watanzania kuwa azma yetu ya kuiendeleza nchi kwa kasi chini ya Jemedari Dkt. John Pombe Magufuli inaendelea kushika kasi na katika hili hakuna atakayetuzuia wala kuturudisha nyuma,” Amesisitiza Dkt Abbasi.

Alifafanua kuwa Hospitali hizi za Kanda zinajengwa katika mikoa ya Mwanza, Simiyu, Njombe, Songwe, Katavi, Geita na Dar es Salaam (Mwananyamala) nakuongeza kuwa SShilingi Bilioni 3 zimetolewa kujenga Hospitali ya Kanda ya Wazazi Mbeya na shilingi bilioni 6.32 kujenga Hospitali ya Kanda Mtwara.

Dkt. Abbasi aliongeza kuwa, katika kuwekeza kwenye maisha ya watu wa ngazi ya chini, Serikali mapema mwaka huu ilitoa shilingi Bilioni 105 kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali za Wilaya 67 ambapo katika miaka zaidi ya 50 ya Uhuru tumekuwa na Hospitali katika Wilaya 77 tu; ndani ya mwaka huu mmoja zinajengwa 67 ambapo ujenzi umekamilika kwa zaidi ya asilimia 90.

Serikali ya Awamu ya Tano imejipambanua katika kuimarisha huduma za afya hapa nchini kwa kuimarisha huduma katika vituo vya afya, Zahanati, Hospitali za Wilaya na Kanda.

 

Ujenzi Njia Sita Kimara Kibaha Wafikia Asilimia 40

Mkurugenzi wa Idara ya Habari –MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) leo jijini Dodoma kuhusu utekelezaji wa Serikali katika kuwaletea wananchi maendeleo kupitia miradi mbalimbali.

Na Mwandishi Wetu

Ujenzi wa Barabara ya Njia Sita pamoja na barabara za waenda kwa miguu ya Kimara-Kibaha (Km19.2) wenye thamani ya TZS Bilioni 140.44  unaojumuisha madaraja ya Kibamba, Kiluvya na Mpiji umefikia 40%.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dodoma kuhusu utekelezaji wa Serikali, Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi amesema kuwa mradi huo unagharamiwa na Serikali ya Tanzania kwa asilimia100 unaendelea kama ilivyopangwa na utakamilika kwa wakati.

Mradi huo unatarajiwa kuondoa changamoto ya foleni katika Jiji la Dar es Salaam hivyo kuchochea maendeleo na ukuaji wa uchumi.

“Serikali pia imesaini mkataba wa shilingi bilioni 699.9 kwa ajili ya ujenzi wa Daraja refu zaidi Afrika Mashariki na Kati la Kilometa 3.2 kuunganisha mikoa ya Mwanza na Geita kwenye eneo la Kigongo-Busisi katika Ziwa Victoria”. Alisisitiza Dkt. Abbasi

Aliongeza kuwa Serikali kupitia Mamlaka ya Babaraba Vijijini na Mijini (TARURA) imejenga madaraja madogo madogo katika wilaya 7 nchini ambayo ni; Kondoa (Kisese, urefu mita 38, Bilioni 2.08); Kishapu (Manonga, urefu mita 45,Bilioni 2.436); Bahi (Chipanga Bridge, urefu mita 45, Bilioni 2.11; Iringa (M) (Tagamenda Bridge, urefu mita 30, Bilioni 4.5).

Madaraja mengine yamejengwa katika mikoa ya Songwe (W) (Kikamba Bridge, urefu mita 60, Bilioni 1.2); Iramba  (Mtoa Bridge, urefu mita 60, gharama Bilioni 2.676 ); na Kilombero (Kihansi Bridge, Urefu mita 40, Gharama Milioni 972) “ Aliongeza Dkt Abbasi

Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi wa Rais wa Jamahuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe magufuli imeweka mkazo katika kuimarisha miundombinu ili kuchochea ukuaji wa uchumi kupitia sekta mbalimabli ikiwemo uchukuzi, viwanda na kilimo.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Tanzania Yaendelea Kunga’ra Kimataifa

Mkurugenzi wa Idara ya Habari –MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) leo jijini Dodoma kuhusu utekelezaji wa Serikali katika kuwaletea wananchi maendeleo kupitia miradi mbalimbali.

Na Mwandishi Wetu- MAELEZO, Dodoma

Heshima na hadhi ya Tanzania Kimataifa imeendelea kupanda kutokana na nia njema na kazi kubwa inayofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais wa Jamahuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari leo (Agosti 31, 2019) Jijini Dodoma kuhusu utekelezaji wa Serikali kwa mwezi Agosti 2019. Read more

TACAIDS Yajidhatiti Kuzuia Maambukizi Mapya ya VVU

 

Na; Mwandishi Wetu

Tume ya Taifa ya Kudhibiti UKIMWI (TACAIDS) imejidhatiti kukabiliana na maambukizi mapya ya ugonjwa huo kwa kuanzisha vituo vya kutoa huduma za ushauri nasaha na upimaji katika maeneo yote ya barabara kuu za kwenda nchi jirani.

Akizungumza katika kipindi cha “TUNATEKELEAZA” Mkurugenzi Mtendaji wa Tume hiyo Dkt. Leonard Maboko amesema mpaka sasa vituo 20 vimeanza kutoa huduma katika barabara kuu za kuelekea nchi jirani ili kuyafikia makundi maalum kama madereva na vijana wanaoishi katika maeneo ambayo yana mikusanyiko mikubwa ya watu kutokana na shughuli za kibiashara. Read more

Tanzania Yatoa Rai kwa Japan na Jumuiya za Kimataifa

Tanzania imetoa rai kwa Jumuiya ya Kimataifa na Japan kuendelea kutafuta suluhu ya kudumu kwenye changamoto mbalimbalii ambazo bado zinajitokeza kwenye baadhi ya nchi za Afrika ikiwemo ugaidi wa kimataifa, uhalifu, mabadiliko ya tabianchi, ukame, njaa na magonjwa sambamba na kujitolea kuchangia na kuwekeza kwenye miradi iliyobuniwa na Serikali ya Tanzania kwa ajili ya kuboresha mazingira yaliyoharibiwa kutokana na uwepo wa kambi za Wakimbizi kwenye maeneo mbalimbali nchini.

Rai hiyo imetolewa na Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa kwenye Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali kuhusu kuimarisha amani na usalama barani Afrika uliofanyika wakati wa Mkutano wa Saba wa Kimataifa wa Tokyo kuhusu Maendeleo ya Afrika (TICAD 7) uliomalizika leo tarehe 30 Agosti 2019 jijiji Yokohama, Japan.

Mhe. Waziri Mkuu amesema kuwa, miradi hiyo ambayo ni pamoja na kubadilishana teknolojia hususan kwenye maeneo ya mipakani na mifumo ya kutoa taarifa mapema kwa ajili ya kujikinga na majanga mbalimbali yanayoweza kujitokeza itasaidia kuboresha mazingira ambayo kwa kiasi kikubwa yameharibiwa na wakimbizi na watu wanaotafuta makazi.

“Uwepo wa wakimbizi na watu wanaotafuta makazi kwa namna moja au nyingine huathiri mazingira, jamii usalama na uchumi wan chi inayowapokea. Hivyo ni ombi letu kwenu kushirikiana nasi kwenye miradi mbalimbali katika kuboresha mazingira” alisema Mhe. Waziri Mkuu.

Aliongeza kusema kuwa, kwa miaka mingi Tanzania imekuwa kimbilio kwa wakimbizi kutoka nchi jirani wanaokimbia nchi zao kutokana na migogoro ya kisisasa, kikabila na kuibuka kwa vikundi vya uasi. Alieleza kuwa hadi kufikia tarehe 1 Agosti 2019, Tanzania inahifadhi wakimbizi wapatao 305,983.

Vilevile, Mhe. Waziri Mkuu aliongeza kuwa, katika kuhakikisha amani inapatikana pote dunaiani, Tanzania ina mchango mkubwa katika amani, utulivu na utatuzi wa migogoro barani Afrika na kwamba ni miongoni mwa nchi zinazochangia misheni za ulinzi wa amani katika nchini mbalimbali Afrika na duniani.

Wakati huo huo, Mhe. Waziri Mkuu amefanya mazungumzo na Kamishna Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Bw. Fillipo Grandi walipokutana pembezoni mwa Mkutano wa Saba wa Tokyo kuhusu Maendeleo ya Afrika.

Wakati wa mazungumzo hayo, Mhe. Waziri Mkuu na Bw. Grandi wamekubaliana kuimarisha ushirikiano katika kuhakikisha usalama kwenye makambi ya wakimbizi, kuimarisha mipaka pamoja na kukabiliana na changamoto ya uharibifu wa mazingira unaofanywa na Wakimbizi.

Akizungumzia Mkutano wa Saba wa Kimataifa kuhusu Maendeleo ya Afrika (TICAD 7) uliofanyika kwa siku tatu jijini Yokohama, Japan. Mhe. Waziri Mkuu amesema Mkutano huo umemalizika kwa mafanikio huku Wakuu wa Nchi a Serikali wakikubaliana kuteleleza Azimio la Yokohama linalolenga kuleta mapinduzi barani Afrika kwa kuimarisha  masuala ya usalama, elimu, sayansi na teknolojia na kukuza sekta binafsi.

Amesema kuwa, Tanzania itajipanga kikamilifu kutekeleza maazimio yaliyofikiwa kwenye mkutano huo ambayo ni ya manufaa makubwa kwa nchi za Afrika.

Mhe. Waziri Mkuu alieleza kuwa, maazimio hayo ambayo kwa kiasi kikubwa yamegusa sekta zote muhimu zikiwemo afya, elimu, maendeleo ya miundombinu, sayansi na teknolojia na amani na usalama yanalenga kuzikwamua kiuchumi nchi za Afrika kupitia ushirikiano  na Serikali ya Japan.

“Tumemaliza kikao cha TICAD leo ambacho kimejadili mambo mengi yakiwemo ya usalama, maendeleo ya elimu, sayansi na teknolojia na namna nzuri ya kuendesha nchi zetu kupitia miradi ya maendeleo kama ujenzi wa miundombinu. Kikao hiki kwetu Tanzania ni chachu ya kuendeleza jitihada zetu za kufikia uchumi wa kati na mapinduzi ya viwanda ifikapo mwaka 2025”  alifafanua Waziri Mkuu.

Mhe. Waziri Mkuu aliongeza kuwa, Japan imetenga kiasi cha fedha kwa ajili ya kuzisaidia nchi za Afrika kupitia fursa ya mikopo na ufadhili. Aliongeza kuwa, Tanzania itajipanga vizuri ikiwa ni pamoja na kuandaa maandiko mazuri ya miradi ya kipaumbele ili kupata fedha hizo.

Amesema kuwa, nchi za Afrika ambazo kwa kiasi kikubwa zimejaliwa kuwa na maliasili na malighafi za kutosha kwa ajili ya kujenga uchumi, zimesisitizwa kuimarisha mahusiano na sekta binafsi katika ujenzi wa uchumi wa nchi hizo.

Imetolewa na:

Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki

Yokohama, Japan

30 Agosti 2019

 

Rais Dkt. Magufuli Apokea Hati za Utambulisho za Mabalozi 5

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati ya Utambulisho kutoka kwa Mhe. Sanjiv Kohli Balozi wa India hapa nchini Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati ya Utambulisho kutoka kwa Balozi mteule wa Denmark hapa nchini Mhe. Mette Norgaard Dissing Spandet Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 29 Agosti, 2019 amepokea hati za utambulisho za Mabalozi 5 walioteuliwa kuziwakilisha nchi zao hapa nchini.

Mabalozi hao ni Mhe. Mahayub Buyema Mahafud (Balozi wa Jamhuri ya Saharawi hapa nchini), Mhe. Sanjiv Kohli (Balozi wa India hapa nchini), Mhe. Mej. Jen. Anselem Nhamo Sanyatwe (Balozi wa Jamhuri ya Zimbabwe hapa nchini), Mhe. Sandro Renato Agostinho De Oloveira (Balozi wa Jamhuri ya Angola hapa nchini) na Mhe. Mette Nørgaard Dissing Spandet (Balozi wa Denmark hapa nchini).

Katika mazungumzo, Mhe. Rais Magufuli amewapongeza na kuwakaribisha Mabalozi hao hapa nchini Tanzania, na kuwahakikishia kuwa Tanzania inatambua uhusiano na ushirikiano mzuri na wa kihistoria na nchi zao na kwamba ipo tayari kuukuza na kuuimarisha zaidi uhusiano huo.

Read more

Rais Magufuli Ayataka Mataifa ya Afrika Kujiepusha na Masalia ya Fikra za Kikoloni

Rais Dkt. John Pombe Magufuli akilakiwa na Mtendaji Mkuu wa
Taasisi ya Uongozi, Profesa Joseph Semboja, alipowasili kuhutubia
Mkutano wa sita Jukwaa la Uongozi Afrika katika Ukumbi wa Jakaya
Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 20, 2019

Rais Dkt. John Pombe Magufuli akijiunga na viongozi
wastaafu kukiliza majadiliano wakati wa Mkutano wa Sita Jukwaa la
Uongozi la Afrika katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es
salaam leo Agosti 20, 2019

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ametoa wito kwa Mataifa ya Afrika kutafsiri vizuri dhana ya uhuru na kujiepusha na masalia ya fikra za kikoloni za kuamini kuwa watawala wa zamani wa Mataifa ya Afrika ndio wenye uwezo wa kusaidia kusimamia na kuendeleza rasilimali zilipo katika Bara la Afrika.

Mhe. Rais Magufuli ametoa wito huo leo tarehe 29 Agosti, 2019 Ikulu Jijini Dar es Salaam alipohutubia Mkutano wa 6 wa Jukwaa la Uongozi Afrika unaohudhuriwa na Marais Wastaafu Mhe. Benjamin William Mkapa (Tanzania), Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (Tanzania), Mhe. Thabo Mbeki (Afrika Kusini), Mhe. Hassan Mohamud (Somalia), Mhe. Hery Rajaonarimampianina (Madagascar), Mabalozi, Wawakilishi wa Kimataifa na washiriki wa Jukwaa la Uongozi Afrika.

Read more