Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Mkataba Ujenzi Daraja la Kigongo Busisi Wasainiwa

Mtendaji Mkuu Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Mhandisi Patrick Mfugale akisaini Mkataba wa ujenzi wa Daraja la Kigongo-Busisi mkoani Mwanza na Mwakilishi kutoka kampuni ya ujenzi ya China Civil Engeering Construction Coorporation, Zhang Jang, katika hafla iliyofanyika Makao makuu ya Mamlaka ya Bandari Tanzania TPA, Jijini Dar es Salaam, wanaoshuhudia ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe na Waziri wa TAMISEMI, Selemani Jaffo.

: Mtendaji Mkuu Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Mhandisi Patrick Mfugale na Mwakilishi kutoka kampuni ya ujenzi ya China Civil Engeering Construction Coorporation, Zhang Jang, wakionesha nakala za mkataba wa ujenzi wa Daraja la Kigongo- Busisi mara baada ya kusainiwa, ujenzi wake utagharimu TZS. Bilioni 592.

Na.Mwandishi Wetu –MAELEZO.

Hatimaye historia imeandikwa nchini Tanzania kwa kusainiwa kwa mkataba wa ujenzi wa daraja la Kigongo Busisi katika Ziwa Victoria mkoani Mwanza lenye urefu wa kilometa 3.2, ambao utagharimu jumla ya fedha za kitanzania Bilioni 592.

Akizungumza Jijini Dar es Salaam katika hafla ya utiaji saini mkataba wa ujenzi wa daraja hilo, Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isaac Kamwelwe, amesema mradi huo utatekelezwa kwa fedha za walipa kodi wa Tanzania bila kutegemea fedha za wafadhili.

Waziri Kamwelwe alisema mradi wa Kigongo Busisi kama ilivyo miradi mingine ya kimkakati ulipigwa vita sana na baadhi ya watanzania na hata wahisani, amesema hata baadhi ya wanasiasa waliupinga wakidai ni mradi mkubwa sana kwa taifa na hauna tija kwa wakazi wa maeneo hayo na nchi kwa ujumla.

Read more

Balozi Kijazi Aridhishwa na Maandalizi ya Mkutano wa SADC

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hatua iliyofikiwa katika maandalizi ya mkutano wa 39 wa wakuu wa nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) utakaofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Mwalimu Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam Agosti 17 na 18 mwaka huu ambapo ameridhishwa na hatua iliyofikiwa katika maandalizi, Mkutano huo utatanguliwa na wiki ya viwanda kuanzia Agosti 5 hadi 8, 2019 na mikutano ya wataalamu wa kisekta . Kulia ni Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dkt Abdulhamid Yahya Mzee.

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi akisistiza jambo kwa Makatibu Wakuu wakati akikagua hatua iliyofikiwa katika maandalizi ya mkutano wa 39 wa wakuu wa nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) utakaofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Mwalimu Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam Agosti 17 na 18 mwaka huu ambapo ameridhishwa na hatua iliyofikiwa katika maandalizi, Mkutano huo utatanguliwa na wiki ya viwanda kuanzia Agosti 5 hadi 8, 2019 na mikutano ya wataalamu wa kisekta .

Na Mwandishi Wetu- MAELEZO

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi amesema maandalizi ya Mkutano wa 39 wa Wakuu wa nchi na Serikali wa nchi wananchama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika(SADC) unaotarajiwa kufanyika hapa nchini mwezi ujao yanaridhisha.

Ameyasema hayo wakati akikagua hatua iliyofikiwa katika maandalizi hayo katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam amesema kuwa maandalizi yaliyobaki ni madogo na yako katika hatua za mwisho kukamilika ili kuwezesha mkutano huo kufanyika kwa ufanisi kama ilivyopangwa.

“Mkutano huo ni fursa kwa kila mwananchi na hasa kwa kuzingatia kuwa mikutano yote ya SADC itafanyika hapa nchini kwa kipindi chote cha mwaka mmoja ambapo Tanzania itakuwa Mwenyekiti wa Jumiya hii hivyo kila sekta itanufaika ikiwemo utalii, usafirishaji na mahoteli” Alisisitiza Balozi Kijazi

Read more

Naibu Waziri wa Afya wa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China Mhe. Lin Bin Atembelea JKCI Kuona Huduma za Matibabu ya Moyo Wanazozitoa

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu na Naibu Waziri wa Afya wa Serikali ya Jamhuri ya watu wa China Mhe. Lin Bin wakimsikiliza mtoto anayetibiwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa ziara iliyofanywa na Naibu waziri huyo ya kuona huduma za matibabu ya moyo wanazozitoa. Serikali ya Jamhuri ya watu wa China kupitia Hospitali kuu ya Jimbo la Shanding imetuma timu ya wataalamu ambao wanashirikiana na wenzao wa JKCI kufanya kambi maalum ya upasuaji wa moyo.

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akimwelezea Naibu Waziri wa Afya wa Serikali ya Jamhuri ya watu wa China Mhe. Lin Bin namna ambavyo chumba cha uangalizi maalum (ICU) kwa watoto wenye magonjwa ya moyo kitakavyorahisisha huduma za matibabu katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete Jijini Dar es Salaam. Naibu Waziri huyo alitembelea JKCI leo kwa ajili ya kuona huduma mbalimbali za matibabu ya moyo zinazotolewa na Taasisi hiyo.

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu pamoja na Naibu Waziri wa Afya wa Serikali ya Jamhuri ya watu wa China Mhe. Lin Bin wakizungumza na wagonjwa wanaotibiwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa ziara fupi ya kuangalia huduma za matibabu ya moyo zinayotolewa na Taasisi hiyo. Naibu Waziri huyo alitembelea kambi maalum ya upasuaji wa moyo inayofanywa na madaktari wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao wa China na kushuhudia utiaji saini wa makubaliano ya kushirikiana katika mafunzo na matibabu ya moyo baina ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete na Hospitali kuu ya jimbo la Shandong.

Daktari bingwa wa wagonjwa wa moyo waliolazwa katika chumba cha uangalizi maalum (ICU) wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Vivian Mlawi akiwaelezea Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu na Naibu Waziri wa Afya wa Serikali ya Jamhuri ya watu wa China Mhe. Lin Bin jinsi wauguzi wa chumba hicho wanavyowahudumia wagonjwa waliofanyiwa upasuaji wa moyo.

Naibu Waziri wa Afya wa Serikali ya Jamhuri ya watu wa China Mhe. Lin Bin akimpa pole mgonjwa aliyefanyiwa upasuaji wa moyo wa kufungua kifua katika kambi maalum ya matibabu ya moyo inayofanywa na wataalamu kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao wa nchini China. Hii ni mara ya kwanza kwa Serikali ya Jamhuri ya watu wa China kuleta madaktari katika Taasisi ya Moyo kwa ajili ya kufanya kambi maalum ya upasuaji wa moyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi na Makamu Rais wa Hospitali ya Jimbo kuu la Shandong la nchini China Li Leping wakisaini mkataba wa makubaliano ya kushirikiana katika mafunzo na matibabu ya moyo baina ya hospitali hizo mbili leo jijini Dar es Salaam. Moja ya makubaliano hayo ni wataalamu wa afya kutoka JKCI kwenda katika hospitali hiyo kujifunza matibabu ya moyo kwa kutumia vifaa vya kisasa.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi na Makamu Rais wa Hospitali ya Jimbo kuu la Shandong la nchini China Li Leping wakibadilishana mkataba wa makubaliano ya kushirikiana katika mafunzo na matibabu ya moyo baina ya hospitali hizo mbili leo jijini Dar es Salaam. Hii ni mara ya kwanza kwa Serikali ya Jamhuri ya watu wa China kuleta madaktari katika Taasisi ya Moyo kwa ajili ya kufanya kambi maalum ya upasuaji wa moyo.

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akimkabidhi zawadi ya ngao Naibu Waziri wa Afya wa Serikali ya Jamhuri ya watu wa China Mhe. Lin Bin mara baada ya kumaliza ziara yake ya kutembelea Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ajili ya kuona huduma za matibabu ya moyo wanazozitoa. Serikali ya Jamhuri ya watu wa China kupitia Hospitali kuu ya Jimbo la Shanding imetuma timu ya wataalamu ambao wanashirikiana na wenzao wa JKCI kufanya upasuaji wa moyo nchini.

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu na Naibu Waziri wa Afya wa Serikali ya Jamhuri ya watu wa China Mhe. Lin Bin wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), hospitali ya jimbo kuu la Shandong na Ubalozi wa China nchini wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea Taasisi hiyo leo kwa ajili ya kuona huduma za matibabu ya moyo zinazotolewa.(Picha na Genofeva Matemu – JKCI)

 

Hifadhi Mpya ya Mwl.Nyerere Kukuza Utalii Selous

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia michoro ya ujenzi huo mkubwa wa kufua umeme.

Na. Mwandishi Wetu-MAELEZO

Rais Dkt. John Pombe Magufuli ameitaka wizara ya Maliasili na Utalii kutenganisha eneo la uwindaji Selou (Hunting block) kwa kutengeneza Hifadhi ya Taifa ambayo itaitwa Hifadhi ya taifa ya Mwalimu Julius Nyerere.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa mradi wa kufua umeme wa mto Rufiji mkoani Pwani utakaozalisha megawatt 2,115, Rais Magufuli amesema kuwa eneo la uwindaji la Selou ni eneo ambalo limezunguka mradi huo mkubwa wa umeme na lina urefu wa  kilomita za mraba elfu 57. Read more

Mchakato wa Tathmini Mchango wa Sekta ya Usafiri wa Anga Katika Uchumi Waiva

Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Sekta kuu ya Uchukuzi, Mhandisi. Aron Kisaka akizungumza wakati wa kikao cha kujadiliana hatua zilizofikiwa katika mchakato wa kuanza matumizi ya mfumo wa kutathmini mchango wa Sekta ya Usafiri wa Anga katika ukuaji wa uchumi nchini. Kutoka kushoto ni Mtakwimu Mkuu wa Serikali toka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Dkt. Albina Chuwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ua Usafiri wa Angaa (TCAA), Hamza Johari.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA), Hamza Johari. akizungumza wakati wa kikao cha kujadiliana hatua zilizofikiwa katika mchakato wa kuanza matumizi ya mfumo wa kutathmini mchango wa Sekta ya Usafiri wa Anga katika ukuaji wa uchumi wa Taifa leo jijini Dodoma. Kutoka kushoto ni Mtakwimu Mkuu wa Serikali toka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Dkt. Albina Chuwa na Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Sekta kuu ya Uchukuzi, Mhandisi. Aron Kisaka na Mtakwimu Mkuu, Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Zanzibar, Mayasa Mahfoudh Mwinyi.

Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya kubaini mchango wa Sekta ya Usafiri wa Anga katika uchumi wa Taifa wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi(hayupo pichani) alipokuwa akifungua kikao cha kujadiliana hatua zilizofikiwa kabla ya kuanza matumizi ya mfumo wa kutathmini mchango wa Sekta ya Usafiri wa Anga katika ukuaji wa uchumi wa Taifa leo jijini Dodoma.

Katibu wa Kamati ya Kubaini mchango wa Sekta ya Usafiri wa Anga katika Uchumi wa Taifa ambaye pia ni Mkurugenzi wa Udhibiti Uchumu toka Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA), Danieli Malanga akiwasilisha taarifa fupi ya hatua zilizofikiwa katika mchakato wa kuelekea kuanza matumizi ya mfumo rasmi wa tathmini ya mchango wa Sekta ya Usafiri wa Anga katika uchumi wa Taifa wakati wa kikao cha kamati hiyo leo jijini Dodoma.

Katibu wa Kamati ya Kubaini mchango wa Sekta ya Usafiri wa Anga ambaye pia ni Kaimu Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi toka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Daniel Masolwa akichangia hoja wakati wa kikao cha kujadili hatua zilizofikiwa katika mchakato wa kuelekea kuanza matumizi ya mfumo rasmi wa tathmini ya mchango wa Sekta ya Usafiri wa Anga katika uchumi wa Taifa wakati wa kikao cha kamati hiyo leo jijini Dodoma. Kulia ni Katibu Mwenza wa Kamati ya Kubaini mchango wa Sekta ya Usafiri wa Anga katika Uchumi wa Taifa ambaye pia ni Mkurugenzi wa Udhibiti Uchumu toka Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA), Danieli Malanga

Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta Kuu ya Uchukuzi), Mhandisi. Aron Kisaka (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati ya Kubaini mchango wa Sekta ya Usafiri wa Anga katika Uchumi wa Taifa wakati wa kikao cha kujadiliana hatua zilizofikiwa katika mchakato wa kuanza matumizi ya mfumo wa kutathmini mchango wa Sekta ya Usafiri wa Anga katika ukuaji wa uchumi nchini. (Picha na: Idara ya Habari MAELEZO)

Rais Mhe. Dkt. Magufuli Aweka Jiwe la Msingi Ujenzi wa Mradi wa Kufua Umeme wa Maji Katika Mto Rufiji

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Waziri wa Nishati wa Misri Dkt. Mohamed Shaker wakivuta utepe kuashiria uwekaji wa Jiwe la Msingi mradi wa Ujenzi wa Kuzalisha umeme Megawati 2115 katika eneo la mto Rufiji katikati ya Morogoro na Pwani.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Waziri wa Nishati wa Misri Dkt. Mohamed Shaker mara baada ya kuweka Jiwe la Msingi mradi wa Ujenzi wa Kuzalisha umeme Megawati 2115 katika eneo la mto Rufiji katikati ya Morogoro na Pwani.

Read more