Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Hospitali ya Benjamin Mkapa Yapongezwa kwa Kuunda Baraza la Wafanyakazi

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Zainabu Chaula akizungumza na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Hospitali ya Benjamin Mkapa alipokuwa mgeni rasmi katika hafla ya uzinduzi wa Baraza hilo mapema hivi karibuni jijini Dodoma. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH), Dkt. Alphonce Chandika.

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH), Dkt. Alphonce Chandika akizungumza na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Hospitali hiyo wakati wa hafla ya uzinduzi wa Baraza hilo mapema hivi karibuni jijini Dodoma. Kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Zainabu Chaula.

Read more

Serikali Yashirikiana na Kampuni ya Simu Kusaidia Watoto na Wanawake

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Joseph Kandege akihutubia kwenye hafla ya uzinduzi wa Ripoti ya Jamii kutoka vodacom ( Social Impact Report and new strategy to deliver inclusive growth) inayohusu kazi zinazofanywa na Taasisi hiyo, uliofanyika Juni 27, 2019, Jijini Dar es Salaam.

Na Lailat Abeid MAELEZO

Serikali imesema itaendelea kushirikiana na kampuni za simu ili kuwasaidia wananchi katika mambo mbalimbali ya kijamii yakiwemo ya Afya, Elimu  na Miundombinu.

Akizungumza  katika hafla ya uzinduzi wa Vodacom Tanzania Foundation, Naibu  Waziri wa  Tamisemi,  Joseph Kandege amesema Serikali itaendelea kuimarisha miundombinu ili kuwawezesha Vodacom kuwafikia watanzania wote wenye mahitaji .

 Waziri kandege Amesema Vodacom wanafanya   kazi ambazo zinagusa jamii kama afya   na kuwasaidia watoto wa kike kwenda shule kwa kuwapatia vitaulo vya kujihifadhia katika hedhi, pia wameendelea kuwasaidia kina mama juu ya ugonjwa wa fistula ambayo inawapelekea wamama wengi kutengwa na jamii. Read more

Walimu wa Masomo ya Hisabati na Sayansi Kukuza Ufaulu Nchini

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Uratibu na Uwekezaji ) Bi Dorothy Mwaluko akifungua mkutano wa kwanza wa chama cha Walimu wa Hisabati na Masomo ya Sayansi June 29, 2019 Jijini Dodoma.

Na Frank Mvungi- Dodoma

Walimu wa masomo ya  Hisabati  na Sayansi nchini wametajwa kuwa chachu ya kuendelea kukuza kiwango cha ufaulu katika masomo hayo na hivyo kuchochea ujenzi wa dhana ya uchumi wa viwanda.

Akizungumza wakati akifungua mkutano wa mwaka wa chama cha walimu wa Hisabati na Sayansi  June 29, 2019 Jijini Dodoma Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia (Sera Uratibu na Uwekezaji) Bi Dorothy Mwaluko amesema kuwa walimu wa masomo hayo wamekuwa wakifanya kazi kubwa yakuwaandaa vyema wanafunzi wanaochukua michepuo ya sayansi na hivyo kuchochea ufaulu kuongezeka.

“ Nawapongeza na kuwataka muongeze juhudi katika kuhakikisha kuwa tunasaidia katika ujenzi wa uchumi wa viwanda kwani unategekea wataalamu wa Hisabati na Sayansi ili azma hii ya Serikali ya Awamu ya Tano iweze kutimia kwa wakati” Alisisitiza Bi Mwaluko. Read more

Matukio Katika Picha Uzinduzi wa Matokeo ya Viashiria vya Mapato na Matumizi kwa Kaya Binafsi

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Dkt. Albina Chuwa alipo wasili katik hafla ya uzinduzi wa Matokeo ya Viashiria Muhimu vya Utafiti wa Mapato na Matumizi kwa Kaya Binafsi kwa Tanzania Bara mwaka 2017/18 pamoja na uzinduzi wa jingo la Ofisi ya Taifa ya Takwimu(NBS) leo jijini Dodoma.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Matokeo ya Viashiria Muhimu vya Utafiti wa Mapato na Matumizi kwa Kaya Binafsi Tanzania Bara mwaka 2017/18 pamoja na uzinduzi wa jengo la Ofisi ya Taifa ya Takwimu(NBS) leo jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango. Dkt. Ashatu Kijaji akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Matokeo ya Viashiria Muhimu vya Utafiti wa Mapato na Matumizi kwa Kaya Binafsi Tanzania Bara mwaka 2017/18 pamoja na uzinduzi wa jengo la Ofisi ya Taifa ya Takwimu(NBS) leo jijini Dodoma.

Mtakwimu Mkuu wa Serikali toka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Dkt. Albina Chuwa akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Matokeo ya Viashiria Muhimu vya Utafiti wa Mapato na Matumizi kwa Kaya Binafsi Tanzania Bara mwaka 2017/18 pamoja na uzinduzi wa jengo la Ofisi ya Taifa ya Takwimu(NBS) leo jijini Dodoma.

Mkuu wa Wilaya ya Bahi ambaye pia ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Bi. Mwanahamisi Mukunda akitoa salamu za mkoa wakati wa hafla ya uzinduzi wa Matokeo ya Viashiria Muhimu vya Utafiti wa Mapato na Matumizi kwa Kaya Binafsi Tanzania Bara mwaka 2017/18 pamoja na uzinduzi wa jengo la Ofisi ya Taifa ya Takwimu(NBS) leo jijini Dodoma.

Mwakilishi wa Benki ya Dunia, Denis Biseko akitoa salamu wakati wa hafla ya uzinduzi wa Matokeo ya Viashiria Muhimu vya Utafiti wa Mapato na Matumizi kwa Kaya Binafsi Tanzania Bara mwaka 2017/18 pamoja na uzinduzi wa jengo la Ofisi ya Taifa ya Takwimu(NBS) leo jijini Dodoma.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango. Dkt. Ashatu Kijaji wakifurahia baada ya kufunua kitamba kuashiria kuweka jiwe la msingi la uzinduzi wa jengo la Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) leo jijini Dodoma.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa na akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa jengo la Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) leo jijini Dodoma.

Muonekano wa nje wa jengo la Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) lililozinduliwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa leo jijini Dodoma.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa na akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Matokeo ya Viashiria Muhimu vya Utafiti wa Mapato na Matumizi kwa Kaya Binafsi Tanzania Bara mwaka 2017/18 leo jijini Dodoma.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa akimkabidhi Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Mhe. George Simbachawene Kitabu cha Matokeo ya Viashiria Muhimu vya Utafiti wa Mapato na Matumizi kwa Kaya Binafsi Tanzania Bara mwaka 2017/18 mara baada ya kuzinduliwa leo jijini Dodoma. Kushoto ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango. Dkt. Ashatu Kijaji.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa akimkabidhi Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Bibi. Mayasa Sadala Kitabu cha Matokeo ya Viashiria Muhimu vya Utafiti wa Mapato na Matumizi kwa Kaya Binafsi Tanzania Bara mwaka 2017/18 mara baada ya kuzinduliwa leo jijini Dodoma. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Bahi ambaye pia ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Bi. Mwanahamisi Mukunda.

Baadhi ya washiriki wa hafla ya uzinduzi wa Matokeo ya Viashiria Muhimu vya Utafiti wa Mapato na Matumizi kwa Kaya Binafsi Tanzania Bara mwaka 2017/18 pamoja na uzinduzi wa jengo la Ofisi ya Taifa ya Takwimu(NBS) wakifuatilia hotuba mbalimbali za viongozi leo jijini Dodoma.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Kamati ya Maandandilizi ya hafla ya uzinduzi wa Matokeo ya Viashiria Muhimu vya Utafiti wa Mapato na Matumizi kwa Kaya Binafsi Tanzania Bara mwaka 2017/18 pamoja na uzinduzi wa jengo la Ofisi ya Taifa ya Takwimu(NBS) leo jijini Dodoma. (Picha na Frank Shija – MAELEZO).

TAGCO na Idara ya Habari- MAELEZO Zawezesha Utatuzi wa Changamoto Kada ya Mawasiliano Serikalini

 

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA) Mhandisi Victor Seif akisisitiza kuhusu umuhimu wa hatua zinazochukuliwa na dara ya Habari- MAELEZO na Chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO) katika kuimarisha mawasiliano ya Serikali kwa Umma hasa katika kipindi hiki miradi mikubwa inayolenga kuwakwamua wananchi kiuchumi inapotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Tano.

Na Frank Mvungi- Dodoma

Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini wa Taasisi na Mashirika ya Umma  Jijini Dodoma wamekipongeza Chama Cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini TAGCO kwa kushirikiana na Idara ya Habari MAELEZO kwa kuendelea kusimamia vyema kada ya Mawasiliano Serikalini.

Wakizungumza wakati wa ziara  ya ujumbe wa Chama hicho na Idara ya Habari  MAELEZO  kutembelea na kujionea changamoto zinazowakabili  ili kuzitafutia ufumbuzi changamoto zinazowakabili, Maafisa hao akiwemo Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania Bw. Ntambi Bunyanzu amesema kuwa utaratibu huo unapaswa kuendelezwa ili kusaidia kuimarisha utendaji wa vitengo vya mawasiliano Serikalini. Read more

Maafisa Habari Waaswa Kuongeza Kasi Kutangaza Mafanikio ya Serikali

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO) Bi Sarah Kibonde akisisitiza umuhimu wa maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini kutumia mbinu za kisasa katika kutangaza mafanikio ya Serikali , hayo yamejiri June 25, 2019 Jijini Dodoma wakati wa ziara ya ujumbe wa TAGCO na Idara ya Habari- MAELEZO walipotembelea Tume ya Maendeleo ya Ushirika kwa lengo la kujionea utendaji wa Kitengo Cha mawasiliano Serikalini cha Tume hiyo ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuimarisha mawasiliano ya Serikali kwa Umma.

Na Frank Mvungi-  Dodoma

Kada ya Mawasiliano Serikalini imetajwa kuwa chachu ya kujenga uelewa kwa wananchi kuhusu miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Tano .

Akizungumza wakati wa ziara yakuwatembelea na kuona utendaji wa maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini wa Mashirika na Taasisi zilizopo Dodoma, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano  (TAGCO) Bi Sarah Kibonde  amesema kuwa  kuna umuhimu mkubwa kwa maafisa hao kutumia mbinu za kisasa kutangaza mafanikio ya Serikali. Read more

Mpango wa Blueprint Kuanza Julai Mosi Mwaka Huu – Majaliwa

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisoma hotuba yake ya kuahirisha Bunge, jijini Dodoma Juni 28, 2019 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema kuanzia Julai Mosi mwaka huu Serikali itaanza kutekeleza Mpango Kazi wa Utekelezaji wa Mpango wa Kuboresha Mfumo wa Udhibiti wa Biashara nchini (Blueprint) kwa lengo la kurahisisha mazingira ya kufanya biashara.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Ijumaa, Juni 28) wakati akiahirisha mkutano wa 15 wa Bunge, jijini Dodoma. Amesema wakati kazi hiyo inaendelea Serikali itafanya ufutialiaji kuhusu utekelezaji wa mpango huo na kutathmini kama lengo limefikiwa.

Read more

Lindi Watakiwa Kushiriki Katika Zoezi la Umezaji Kingatiba

Na WAMJW-Lindi

Wakazi wa Lindi na vitongoji vyake wametakiwa kushiriki katika kampeni ya kutokomeza magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele kwa kumeza kingatiba za kutokomeza magonjwa hayo pamoja na kutunza mazingira kwa kuondoa mazalia ya mbu waenezao magonjwa hayo.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile wakati wa uzinduzi wa kambi ya upasuaji wa Mabusha na Ngirikokoto (Henia) unaofanyika mkoani Lindi.

Read more

Wananchi Zanzibar Waaswa Kutumia Hati za Kumiliki Ardhi Kujikwamua Kiuchumi

Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Maji Nishati na Mazingira Ali Khalil Mirza akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Uongozi ya MKURABITA walipomtembelea Katibu huyo Ofisini kwake Forodhani mjini Zanzibar.

Na Mwandishi wetu- MAELEZO Zanzibar

Mwenyekiti wa Kamati  ya uongozi ya Ofisi ya Mpango wa kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge (MKURABITA )  Balozi mstaafu  Daniel Ole Njolay  amewataka Wananchi waliokabidhiwa Hati za Ardhi kuzitumia vyema kwa ajili ya kuombea Mikopo itakayowasaidia kupambana na umasikini wa kipato.

Balozi Njolay ametoa wito huo katika hafla ya kuwakabidhi Wananchi 54 wa Mpendae mjini Zanzibar Hati hizo mara baada ya kukamilisha masharti ya usajili. Read more

Serikali Inawathamini Wawekezaji Sekta ya Michezo

Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe (Katikati) akizungumza na wanafunzi (hawapo katika picha) ambao pia ni wanamichezo wa Shule ya Sekondari ya Foutain Gate Academy leo Juni 28,2019 alipofanya ziara kituoni hapo kuona namna vijana hao wanavyofundishwa michezo mbalimbali.Kushoto ni Meneja wa kituo hicho Bw.Wendo Makau, na kulia ni Mkuu wa Shule ya Msingi Bw.William Tumshabe.

Na Shamimu Nyaki -WHUSM

Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe amesema kuwa Serikali inatambua na kuthamini mchango mkubwa unaofanywa na Taasisi pamoja na vituo vya kukuza vipaji katika sekta ya michezo hapa nchini kwakua imechangia kwa kiasi kikubwa kupatikana kwa wachezaji wengi walioliwakilisha Taifa vizuri katika mashindano mbalimbali.

Waziri Mwakyembe ameyasema hayo leo, Jijini Dododma alipotembelea kituo cha mafunzo ya Michezo cha Foutain Gate Academy ambapo mbali na kuupongeza uongozi wa kituo hicho na kuahidi kutafuta wafadhili mbalimbali watakaowezesha kituo hicho kufanya vizuri zaidi.

Read more