Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Naibu Waziri Mhe. Kanyasu Aahidi Mageuzi Kwenye Jumuiya za Hifadhi za Wanyamapori

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akipewa zawadi ya fimbo mara baada ya kuvishwa vazi aina ya kikoi ikiwa ni ishara ya kumpongeza kwa utendaji kazi wake mzuri katika masuala ya Uhifadhi wa Wanyamapori wakati wa mkutano kati ya Wenyeviti wa Muungano wa Jumuiya za Hifadhi za Wanyamapori nchini (WMAs) na Wizara ya Maliasili na Utalii uliofanyika leo jijini Dodoma.

Serikali imewahakikishia Wenyeviti wa Muungano wa Jumuiya za  Hifadhi za Wanyamapori nchini (WMAs) kuwa itaendelea kufanya mageuzi pamoja na kuwapa ushirikiano kwa kuendeleza dhana halisi  ya uhifadhi wa wanyamapori shirikishi katika jamii.
Hayo yamebainishwa leo jijini Dodoma  na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Constantine Kanyasu wakati akizungumza na wenyeviti hao kwenye mkutano wa siku moja uliolenga kuimarisha ushirikiano kati ya wizara na wadau hao wa uhifadhi nchini.
Amesema Wizara itaendelea kutatua changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo kwa kuwa inatambua mchango mkubwa wanaoutoa katika shughuli za uhifadhi wa wanyamapori nchini.
Aidha,  Mhe. Kanyasu ameziagiza WMAs zinazotegemea kufanya uchaguzi hivi karibuni  ziendelee na utaratibu wa zamani wa kutumia kigezo cha elimu ya kuanzia darasa la 7 na kuendelea.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akizungumza na Wenyeviti wa Muungano wa Jumuiya za Hifadhi za Wanyamapori nchini (WMAs) kwenye mkutano wa siku moja uliolenga kuimarisha ushirikiano kati ya Wizara ya Maliasili na Utalii na Wadau wa uhifadhi wa Wanyamapori nchini uliofanyika leo jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akisalimiana na Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na nNyuki, Dkt. Ezekiel Mwakalukwa mara baada ya kuwasili kwenye mkutano wa Wenyeviti wa Muungano wa Jumuiya za Hifadhi za Wanyamapori nchini (WMAs) wa siku moja uliolenga kuimarisha ushirikiano kati ya Wizara ya Maliasili na Utalii na Wadau wa uhifadhi wa Wanyamapori nchini uliofanyika leo jijini Dodoma. SWengine ni watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii pamoja na Wafanyakazi wa WWF.

Mkurugenzi Mtendaji wa Jumuiya za Hufadhi za Wanyamapori, George Wambura akizungumza na Wenyeviti wa Muungano wa Jumuiya za Hifadhi za Wanyamapori nchini (WMAs) kwenye mkutano wa siku moja uliolenga kuimarisha ushirikiano kati ya Wizara ya Maliasili na Utalii na Wadau wa uhifadhi wa Wanyamapori nchini uliofanyika leo jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu (katikati) akiwa na baadhi ya watendaji wa Wizara ya Maliasili na Utalii wa mkutano wa Wenyeviti wa Muungano wa Jumuiya za Hifadhi za Wanyamapori nchini (WMAs).

 Amesema lengo la  kuruhusu kutumika kwa kigezo hicho cha elimu  ya darasa la saba na kuendelea ni kutoa fursa kwa  wagombea wengi wenye uwezo kuweza kujitokeza.
 Amezitaka WMAs hizo  kuchagua viongozi watakaokua na uwezo wa  kutekeleza  mipango mbalimbali kwa ufanisi.
Hata hivyo, amesema kuwa yapo baadhi ya mambo ya msingi ambayo Wizara imeanza kuyaboresha kwenye kanuni za WMAs  likiwemo suala la kiwango cha elimu kwa viongozi wa WMAs nchini ili kupunguza migogoro isiyo ya lazima inayojitokeza mara kwa mara ndani ya WMAs hizo.
Kwa upande Mwenyekiti wa Muungano huo, Bw. Christopher Mademula amemueleza Mhe.Kanyasu kuwa suala la kigezo cha elimu liangaliwe kwa mapana yake kwa kigezo kuwa ikiwa wagombea wa darasa la saba hawataruhusiwa kugombea nafasi za uongozi kwenye WMAs, kitendo hicho kitachochea ujangili kwa kuwa wao wamekuwa mstari wa mbele katika kutoa taarifa za kiinteligensia za ujangili kwenye maeneo yao.

Maonesho ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo Yafanyika kwa Mara ya Kwanza.

 

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha akiwasili aktika Viwanja vya Jamhuri jijini Dodoma leo kwa ajili ya hafla ya kufunga Maonesho ya Kwanza ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo yaliyoratibiwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE).Kutoka kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Avemaria Semakafu na Mwenyekiti wa Bodi ya NACTE, Profesa John Kondoro (kulia).

Na Lilian Lundo – Dodoma.

Baraza la Taifa la Elimu na Ufundi (NACTE) kwa kushirikiana na Vyuo na Taasisi za Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa mara ya kwanza limeandaa Maonesho ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo ambayo yamefanyika Jijini Dodoma tarehe 27 hadi 30 Mei, katika uwanja wa Jamhuri.

Maonesho hayo yaliyofanyika kwa takribani siku tano na kufungwa leo na Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha ambapo kabla ya hotuba ya kufunga maonesho hayo, Ole Nasha aliweza kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na Vyuo na Taasisi za Elimu na Mafunzo. Read more

Waziri Jafo Atoa Maelekezo Maalumu kwa Ma-RC, Ma DC na Wakurugenzi.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Suleiman Jafo amewaagiza Wakuu wa Mikoa minne iliyopo kwenye mradi wa “lishe Endelevu” kuhakikisha kuwa mikataba hiyo ya utekelezaji wa afua za lishe inawashukie wakuu wa Wilaya, nao wasainiane na wakurugenzi wa halmashauri, nao pia waishushe kwa watendaji wa kata na watendaji hao  wasainiane na watendjai wa vijiji na mitaa ili utekelezaji wa mikataba hiyo kuwa shirikishi bila ya kubagua eneo lolote la utawala.

Read more

Thamani ya Mfuko wa Pensheni Kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) Yafikia Trilioni 5.8

 

Na Frank  Mvungi

Thamani ya Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) imefikia Trilioni 5.8 hali inayoonesha kuwa mfuko huo unaendelea kuimarika na hivyo kuendelea kutoa huduma bora kwa wanachama wake.

Akizungumza katika kipindi cha ‘TUNATEKELEZA’ Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo  Bw. Hosea  Kashimba  amesema kuwa  kuunganishwa kwa mifuko ya GEPF, LAPF, PSPF na PPF kunatoa  fursa ya kuimarisha zaidi sekta ya hifadhi ya Jamii hali iliyochangia thamani ya mfuko mpya wa PSSSF kuendelea kukua hata katika kipindi kifupi tangu kuanzishwa kwake. Read more

Serikali Kuja Na Mbinu za Ziada Kukabiliana na Ugonjwa wa Mnyauko wa Migomba – Mhe Bashungwa

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Innocent Bashungwa (Mb) akijibu swali Bungeni leo tarehe 31 Mei 2019 wakati wa mkutano wa kumi na tano wa Bunge la Bajeti Jijini Dodoma. 

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma

Kwa kipindi cha Mwaka 2006 – 2014, Wizara ya Kilimo kwa kushirikiana na Uongozi wa Mkoa wa Kagera umetoa mafunzo ya kutokomeza ugonjwa wa mnyauko wa migomba kwa wakulima na maafisa ugani kwenye wilaya zote zilizoathirika.

Serikali imekuwa ikiendesha kampeni ya kung’oa migomba yote iliyoathirika, kukata Ua Dume na kuiteketeza. Halmashauri zote za Wilaya za Mkoa wa Kagera ziliweka sheria ndogo ndogo za kuwataka wakulima kung’oa na kuchoma au kuzika migomba yote iliyoathirika. Zoezi hilo lilipunguza ueneaji wa ugonjwa huo kwa asilimia 70.

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Innocent Bashungwa (Mb) ameyasema hayo leo tarehe 31 Mei 2019 Bungeni Jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mhe Jasson Samson Rweikiza Mbunge wa Bukoba vijijini aliyetaka kufahamu Serikali ina mpango gani kuchukua hatua za makusudi za kupambana na ugonjwa huo na kutokomeza kabisa.

Read more

Vyama na Mashirikisho ya Michezo Vyaelekezwa Kusimamia Utaratibu wa Upimaji Afya za Wanamichezo

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Juliana Shonza akijibu swali wakati wa kikao cha 40 cha Bunge leo jijini Dodoma.

Na Shamimu Nyaki -WHUSM

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza amevielekeza Vyama na Mashirikisho ya Michezo nchini kuwa na utaratibu wa kutoa elimu ya afya  na kinga  kwa wanamichezo  ili kulinda afya za wanamichezo hao kabla, wakati na baada ya michezo.

Mhe. Shonza ameyasema hayo leo Bungeni Jijini Dodoma alipokua akijibu swali la msingi la Mhe. Haji Khamis Mbunge wa Nugwi aliyetaka kufahamu Serikali kupitia Vyama vya Michezo imeweka utaratibu gani wa kuhakikisha upimaji wa afya za wanamichezo linalopewa kipaumbele.

Read more

Mageuzi ya Kisayansi Yazaa Matunda Sekta ya Madini, Mapato

Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt.Hassan Abbasi akifafanua jambo kwa Waandishi wa Habari (hawapo pichani), kuhusu utekelezaji wa Serikali kwenye sekta mbalimbali, katika Mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika Jijini Dar es Salaam, leo Alhamisi 30. Mei. 2019.

Na Mwandishi Wetu

Hatua za serikali kuhakikisha Watanzania wananufaika na rasilimali za nchi yao na kuongeza mapato zimeanza kuzaa matunda licha ya kupingwa vikali hapo awali. Read more