Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Asilimia 71 ya Wasichana Ruvuma Wapatiwa Chanjo ya Kuzuia Saratani ya Mlango wa Kizazi

Revocatus Kasimba – Songea

Mkoa wa Ruvuma umefanikiwa kutoa chanjo ya kuzuia saratani ya mlango wa kizazi kwa wasichana wenye umri wa miaka 14 kwa asilimia 71 ya lengo kwa mwaka 2018

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Wilaya ya Songea, Pololet Mgema  kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma alisema chanjo hiyo ilianza kutolewa mwezi Aprili mwaka 2018 katika Halmashauri nane za mkoa wa Ruvuma.

Alitoa taarifa hiyo jana mjini Songea wakati wa kikao cha kamati ya Afya ya Msingi mkoa kutathamini zoezi la utoaji chanjo hii kwa viongozi wa mkoa na halmashauri zote Read more

Waziri Mkuu Awataka Viongozi wa UCSAF Kubaini Maeneo Yenye Changamoto za Mawasiliano Nchini.

 

 

Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa akipata maelezo juu ya huduma zinazotolewa na Shirika la Mawasiliano Nchini (TTCL) wakati wa maadhimisho miaka kumi ya Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) yaliyofanyika katika viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma.

Na Beatrice Lyimo -MAELEZO

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania – Mhe. Kassim Majaliwa amewataka viongozi wa “Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote” kuendelea kubaini maeneo ambayo bado yana changamoto za mawasiliano nchini, ili Serikali iweze kupeleka huduma hiyo kwa walengwa mapema iwezekanavyo kabla ya 2020. Read more

Maboresho Miundombinu Mawasiliano ya Simu Mji wa Serikali Yaanza

Katibu wa Kikosi Kazi cha Taifa cha Kuratibu Serikali kuhamia Dodoma na Mratibu wa Ujenzi wa Mji wa Serikali, Bw. Meshach Bandawe akielezea jambo kwa wawakilishi wa Kampuni za Simu za TTCL, Airtel, Tigo na Vodacom wakati wa ziara ya kukagua maeneo yatajayojengwa Minara ya Mawasiliano ya Simu katika Mji wa Serikali ikiwa ni mkakati wa kuboresha miundombinu ya Mawasiliano ya Simu katika mji huo na maeneo jirani.

Katibu wa Kikosi Kazi cha Taifa cha Kuratibu Serikali kuhamia Dodoma na Mratibu wa Ujenzi wa Mji wa Serikali, Bw. Meshach Bandawe akielezea jambo kwa wawakilishi wa Kampuni za Simu za TTCL, Airtel, Tigo na Vodacom wakati wa ziara ya kukagua maeneo yatajayojengwa Minara ya Mawasiliano ya Simu katika Mji wa Serikali ikiwa ni mkakati wa kuboresha miundombinu ya Mawasiliano ya Simu katika mji huo na maeneo jirani.

Katibu wa Kikosi Kazi cha Taifa cha Kuratibu Serikali kuhamia Dodoma na Mratibu wa Ujenzi wa Mji wa Serikali,, Bw. Meshach Bandawe akiteta jambo na Mkuu wa Uendeshaji wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Mhandisi. Albert Richard wakati wa ziara ya kukagua maeneo yatajayojengwa Minara ya Mawasiliano ya Simu katika Mji wa Serikali ikiwa ni mkakati wa kuboresha miundombinu ya Mawasiliano ya Simu katika mji huo na maeneo jirani. Ziara hiyo imehusisha wawakilishi kutoka Kampuni za Simu za TTCL, Airtel, Tigo na Vodacom ambapo Kampuni zote zitakuwa zinatumia mnara moja. Katikati ni Fundi Sanifu wa Kampuni Ujenzi ya Gopa iliyopewa Kandarasi ya ujenzi wa Mnara wa Awali unaojengwa katika eneo hilo, Bw. Charles Mndilila.

Katibu wa Kikosi Kazi cha Taifa cha Kuratibu Serikali kuhamia Dodoma na Mratibu wa Ujenzi wa Mji wa Serikali, Bw. Meshach Bandawe akielekeza jambo kwa wawakilishi wa Kampuni za Simu za TTCL, Airtel, Tigo na Vodacom wakati wa ziara ya kukagua maeneo yatajayojengwa Minara ya Mawasiliano ya Simu katika Mji wa Serikali ikiwa ni mkakati wa kuboresha miundombinu ya Mawasiliano ya Simu katika mji huo na maeneo jirani.

Katibu wa Kikosi Kazi cha Taifa cha Kuratibu Serikali kuhamia Dodoma na Mratibu wa Ujenzi wa Mji wa Serikali, Bw. Meshach Bandawe akisisitiza jambo kwa wawakilishi wa Kampuni za Simu za TTCL, Airtel, Tigo na Vodacom wakati wa ziara ya kukagua maeneo yatajayojengwa Minara ya Mawasiliano ya Simu katika Mji wa Serikali ikiwa ni mkakati wa kuboresha miundombinu ya Mawasiliano ya Simu katika mji huo na maeneo jirani.

Mwakilishi wa Kampuni ya Simu ya Airtel, Mhandisi. Swaleh Bajber akifafanua jambo wakati wa ziara ya kukagua maeneo yatajayojengwa Minara ya Mawasiliano ya Simu katika Mji wa Serikali ikiwa ni mkakati wa kuboresha miundombinu ya Mawasiliano ya Simu katika mji huo na maeneo jirani. Kutoka kulia ni : Katibu wa Kikosi Kazi cha Taifa cha Kuratibu Serikali kuhamia Dodoma na Mratibu wa Ujenzi wa Mji wa Serikali, Bw. Meshach Bandawe, Meneja Msaidizi wa Mtandao wa TTCL Mkoa wa Dodoma, Abbas Buge, Mwakilishi wa Vodacom Tanzania, Mhandisi, David Mbogela na Mwakilishi wa Tigo, Mhandisi. Simpilicius Komba. (Picha zote na: Idara ya Habari –MAELEZO).

Mmiliki Kiwanda cha Parachichi Atakiwa Kuwaongezea Bei Wakulima

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Uyole nje kidogo ya jiji la Mbeya wakati akiwa njiani kuelekea Wilayani Rungwe.

Na. Paschal Dotto-MAELEZO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemtaka mmiliki wa kiwanda cha kupaki maparachichi cha Rungwe overcado Company, kuongeza bei na maslahi kwa wafanyakazi na wakulima wa zao hilo.

Akizungumza kiwandani hapo, katika mwendelezo wa ziara yake ya siku nane Mkoani Mbeya, Rasi Magufuli amesema kuwa Serikali iko tayari kuwasikiliza wawekezaji ili kuwawezesha wakulima kupata faida kubwa kutoka katika uwekezaji pia  makampuni kuongeaza bei kwa wakulima ili waongeze kipato. Read more

Waziri Mkuu Aagiza Taec, Tbs na Tfda Ziharakishe Kutoa Majibu Kwa Wadau Wake

*Azindua maabara ya Tume ya Nguvu za Atomiki

*Aagiza watumishi watatu wapandoshwe vyeo kwa kukataa rushwa

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amezitaka taasisi zinazofanya uhakiki na upimaji bidhaa nchini zijirekebishe na ziongeze kasi ya utoaji matokeo kwa wateja.

 “Kumekuwa na malalamiko kutoka mipakani juu ya bidhaa zinazochukuliwa ili zikapimwe kwamba zinachukua muda mrefu. Tume ya mionzi, TBS na TFDA ni mioyo mwa taasisi zinazolalamikiwa. Tumieni fursa hii kujirekebisha na kuharakisha utoaji wa matokeo,” amesema.

 Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Jumatatu, Aprili 29, 2019) wakati akizindua maabara ya Maabara ya kisasa ya Teknolojia ya Nyuklia ya Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (Tanzania Atomic Energy Commission -TAEC) iliyopo Njiro, jijini Arusha. Read more

Rais Dkt. Magufuli Azungumza na Wananchi wa Kiwira Pamoja na Kufungua Kiwanda cha Maparachichi Kilichopo Rungwe Mkoani Mbeya

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Uyole nje kidogo ya jiji la Mbeya wakati akiwa njiani kuelekea Wilayani Rungwe.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Uyole nje kidogo ya jiji la Mbeya wakati akiwa njiani kuelekea Wilayani Rungwe.

Read more

Matukio Katika Picha Siku Ya Usalama Na Afya Mahali Pa Kazi-Mbeya.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akipokelewa na watumishi wa OSHA alipowasili katika viwanja vya bustani ya Jiji Mkoani Mbeya kwa ajili ya maadhimisho ya sherehe Usalama na Afya Mahali Pa Kazi yaliyofanyika mkoani hapo kitaifa.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Wenye Ulemavu) Mhe. Stella Ikupa akiweka sahihi kwenye kitabu cha wageni katika banda la maonesho la Wakala wa Afya na Usalama mahala pa Kazi (OSHA) wakati wa maadhimisho hayo.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akipewa maelezo ya vifaa saidizi kazini kutoka kwa Mtaalamu kutoka Wakala wa Afya na Usalama Mahala Pa Kazi (OSHA) wakati wa maadhimisho hayo.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista pamoja na naibu wake Mhe. Anthony Mavunde wakiangalia mfano wa namna ya kuokoa mtu aliyepata madhara awapo kazini walipotembelea banda la MUST (Mbeya University of Science and Technology) wakati wa kilele cha maadhimisho ya Siku ya Usalama na Afya Mahali Pa Kazi Jijini Mbeya.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista akifurahia pamoja na watumishi wa Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) baada ya kuibuka washindi wa kwanza kwa kupokea tuzo nyingi kuliko washiriki wengine wa maonesho ya Siku Usalama na Afya Mahali Pa Kazi yaliyofanyika Jijini Mbeya. (PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

Mradi wa umeme wa Kinyerezi I Extension kukamilika mwezi Agosti mwaka huu

Meneja Miradi kutoka TANESCO, Mhandisi Stephen Manda (wa pili kushoto) akitoa maelezo kwa Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (katikati) kuhusu utekelezaji mradi wa Kinyerezi I Extension utakaozalisha megawati 185. Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt. Tito Mwinuka.

Na Teresia Mhagama

Imeelezwa kuwa mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia gesi wa Kinyerezi I extension utakamilika mwezi Agosti mwaka huu ambapo utazalisha umeme wa kiasi cha megawati 185.

Hayo yalisemwa jijini Dar es Salaam tarehe 28 Aprili, 2019 na Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani wakati alipofanya ziara ya ukaguzi wa miradi mbalimbali ya umeme ambapo aliambatana na Kaimu Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Innocent Luoga, Kaimu Kamishna wa Petroli na Gesi, Mwanamani Kidaya, Kamishna Msaidizi anayeshughulikia Maendeleo ya Nishati, Mhandisi Juma Mkobya  na Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Tito Mwinuka. Read more

Picha za Matukio Mbalimbali Fainali za AFCON U17

Mgeni Rasmi, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Juliana Shonza (kulia) akisalimiana na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bi. Susan Mlawi wakati Naibu Waziri alipowasili kushuhudia fainali za mashindano ya kombe la mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17, jana jijini Dar es Salaam.

: Mgeni Rasmi, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Juliana Shonza (kulia) akisalimiana na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika (CAF), Bw. Ahmad Ahmad wakati Naibu Waziri alipowasili kushuhudia fainali za mashindano ya kombe la mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17, kati ya Guinea na Cameroon jana jijini Dar es Salaam.

Kikundi cha Mpoto Theatre kikitoa burudani kwa watazamaji wa fainali za mashindano ya kombe la mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 yaliyokutanisha Cameroon na Guinea hapo jana na Cameroon kutwaa ubingwa kwa mikwaju ya penati 5 dhidi ya penati 3 za Guinea.

Vikosi vya timu za vijana chini ya miaka 17 toka Guinea na Cameroon wakiimba nyimbo za mataifa yao kabla ya kuanza kwa mchezo wa fainali hapo jana ambapo Cameroon waliibuka mabingwa kwa mikwaju ya penati 5 dhidi penati 3 za Guinea.

Mgeni Rasmi, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Juliana Shonza akimkabidhi zawadi ya kombe mchezaji ambayealiibuka kuwa mfungaji bora katika mashindano ya kombe la mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 jana jijini Dar es Salaam.

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika (CAF), Bw. Ahmad Ahmad (katikati) akimkabidhi bendera ya CAF Balozi wa Morocco Nchini Tanzania Mhe. Abdelilah Benryane ikiwa ishara ya kuwa muandaaji wa mashindano hayo, kushoto ni Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Bw. Wallace Karia.

Washindi wa mashindano ya kombe la mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17, timu ya Cameroon wakivalishwa medali mara baada ya kuibuka na ushindi wa magoli ya penati tano dhidi ya penati tatu za Guinea jana jijini Dar es Salaam.

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika (CAF), Bw. Ahmad Ahmad akimkabidhi nahodha wa timu ya Taifa ya vijana ya Cameroon chini ya miaka 17 mara baada ya kuibuka mabingwa kwa ushindi wa magoli ya penati tano dhidi ya penati tatu za Guinea jana jijini Dar es Salaam.

Wachezaji wa timu ya Taifa ya vijana ya Cameroon chini ya miaka 17 wakishangilia mara baada ya kuibuka mabungwa wa mashindano ya kombe la mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 baada ya kuifunga Guinea kwa mikwaju ya penati tano dhidi ya penati tatu za Guinea jana jijini Dar es Salaam.
Picha na WHUSM – Dar es Salaam