Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Tanzania Yang’ara Suala la Amani Duniani

Yaongoza Afrika Mashariki, Yawa 10 Bora Barani Afrika

Na Mwandishi Wetu

Taswira ya Tanzania kimataifa imeendelea kupaa baada ya Taasisi ya Global Peace Index (GPI) kuitangaza Tanzania kushika nafasi ya 51 miongoni mwa nchi zenye amani zaidi duniani katika kipindi cha mwaka 2018.

Tanzania imeshika nafasi hiyo ikiwa ni ya juu zaidikufikiwa tangu mwaka 2010 na kuzishinda nchi kubwa duniani kama Marekani, China, Uingereza na Ajentina ambapo kwa Afrika ipo katika nafasi 10 bora na kuwa kinara katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Read more

DC Ruangwa Awataka Wachimbaji Namungo Kuzingatia Sheria

Kaimu Mkurugenzi wa Sayansi Jinai na Huduma za Vinasaba, Bw. David Elias (kushoto), akiongea kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa, Mhe. Hashim Mgandilwa (wa pili kushoto), kufungua mafunzo kwa wachimbaji wadogo wadogo wa dhahabu wa Namungo. Wengine kutoka kulia ni Katibu wa Mkuu wa Wilaya na Kaimu Meneja wa Maabara ya Kanda ya Kusini, Bw. Eliamini Mkenga.

Na Sylvester Omary – GCLA

Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa, Hashim Mgandilwa amewataka wachimbaji wadogo wadogo wa dhahabu wa mgodi wa Namungo kuzingatia Sheria ya Usimamizi na Udhibiti wa Kemikali wanapokuwa wanatekeleza shughuli za uchimbaji kwa lengo la kulinda afya zao na mazingira.

Mgandilwa ameyasema hayo leo wakati akifungua mafunzo ya siku mbili ya Matumizi Salama ya Kemikali kwa wachimbaji hao yanayotolewa na Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Kanda ya Kusini na kufanyika kwenye kijiji cha Namungo wilayani Ruangwa.

Read more

Wananchi 62 Wafanyiwa Vipimo vya Kuangalia Moyo Unavyofanya Kazi JKCI

Na Mwandishi Maalum – JKCI

 Jumla ya watu 62 wamefanywa vipimo vya kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (Echo Cardiogram)  na umeme wa moyo (ECG) wakati wa punguzo la gharama za matibabu kwa wagonjwa wa kulipia lililotolewa na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI).

Punguzo hilo lilitolewa hivi karibuni na Taasisi hiyo ikiwa ni sehemu ya  kusherehekea ushindi wa timu ya Taifa ya mpira wa miguu  kwa kuifunga timu ya Uganda mabao 3-0 na  kuweza kushiriki katika mashindano ya  Taifa Bingwa Barani Afrika AFCON. 2019.

Akiongea na mwandishi wa habari hizi jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Tiba Shirikishi ambaye pia ni daktari bingwa wa magonjwa ya moyo  Dkt. Delila Kimambo alisema  kati ya wagonjwa 62 waliopima afya zao nane walikuwa ni watoto. Read more

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan Azindua Mashine za Mionzi Ocean Road

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa hafla ya uzinduzi wa Jengo na mashine za tiba ya saratani.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema tatizo la saratani kwa Watanzania linaweza kupungua ama kuondokana nalo endapo kutakuwa na tabia ya kupima afya zetu mara kwa mara.

Makamu wa Rais ameyasema hayo leo kwenye uzinduzi wa jengo na mashine mpya za tiba ya mionzi LINAC ambazo ni za kisasa kabisa na kwa Afrika, Tanzania inakuwa nchi ya kwanza kuwa nazo.

tunaweza kujikinga kwa kufuata kanuni za afya zinavyotuelekeza kula chakula bora, kufanya mazoezi mara kwa mara, na kuepuka kunywa pombe kupita kiasi na kuepuka matumizi ya tumbaku”alisema Makamu wa Rais. Read more

Naibu Waziri Nishati Awaonya Wakandarasi wa Miradi ya Umeme Vijijini

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (mwenye kilemba) akikata utepe kuashiria uwashaji rasmi wa umeme katika kijiji cha Ngazi, wilayani Lushoto, Machi 28, 2019 akiwa katika ziara ya kazi. Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Handeni, January Lugangika.

Na Veronica Simba – Lushoto

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu amewaonya wakandarasi wanaotekeleza miradi ya umeme vijijini kuzingatia masharti yaliyowekwa na serikali hususani kutumia vifaa vya ndani ya nchi, na kwamba atakayeona hawezi kutekeleza masharti hayo, arudishe kazi hiyo kwa Serikali ili apewe mkandarasi mwingine.

Alitoa onyo hilo jana, Machi 28, 2019 katika kijiji cha Ngazi, wilayani Lushoto, Mkoa wa Tanga, wakati akizungumza na wananchi, kabla ya kuwasha rasmi umeme katika kijiji hicho.

“Kwanini muagize vifaa kama nguzo nje ya nchi wakati sisi bado miti tunayo na mingine imepandwa kwa makusudio hayo?”

Read more