Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

BOT yaanza kufuta Maduka ya Kubadilishia Fedha Yasio na Leseni

Tarehe 27 Februari 2019 Benki Kuu ya Tanzania ilifanya ukaguzi wa kawaida wa maduka ya kubadilisha fedha za kigeni jijini Dar es Salaam na kubaini kwamba maduka mengi yanaendesha biashara hiyo pasipo kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za utoaji wa huduma ya kubadilisha fedha za kigeni.

Kufuatia ukaguzi huo, Benki Kuu ya Tanzania imeanza utaratibu wa kufuta leseni za maduka yote yaliyokutwa yanaendesha biashara hiyo bila kuzingatia masharti ya leseni. Zoezi hili linaendelea.

Read more

NBS na Sheria Mpya ya Utoaji Takwimu

Na. Msafiri Ulimali, Fatma Athumani

Ofisi ya Taifa ya Takwimu –NBS imetoa maelezo ya marekebisho ya Sheria ya Takwimu Namba 9 ya mwaka 2015 katika ofisi za takwimu zilizopo barabara ya Sokoine jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Waandishi wa Habari katika mkutano jana, Mkurugenzi Mtendaji wa NBS Dkt. Albinas Chuwa amesema kuwa sheria ya takwimu ya Mwaka 2015 imerekebishwa kupitia Sheria Namba 8 ya mwaka 2018.

Dkt Chuwa amesema “Lengo la marekebisho hayo, ni kuimarisha utaratibu wa usambazaji takwimu nchini, kwa nia ya kuepusha kutoa takwimu zinazokinzana kwa jamii, pia, marekebisho hayo yanalenga kuimarisha mijadala ya kisera pamoja na matokeo yake’.

Read more

Taarifa kwa Umma

MADUKA YA KUBADILISHA FEDHA ZA KIGENI

Tarehe 27 Februari 2019 Benki Kuu ya Tanzania ilifanya ukaguzi wa kawaida wa maduka ya kubadilisha fedha za kigeni jijini Dar es Salaam na kubaini kwamba maduka mengi yanaendesha biashara hiyo pasipo kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za utoaji wa huduma ya kubadilisha fedha za kigeni.

Read more

Taarifa kwa Umma

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 28 Februari, 2019 amekutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA) Bw. Kazuhiko Koshikawa.

Mazungumzo hayo yamefanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damas Ndumbaro na Balozi wa Japan hapa nchini Mhe. Shinichi Goto.

Read more

Rais Dkt. Magufuli Akutana na Makamu wa Rais Mtendaji Mwandamizi wa JICA Ikulu Leo

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Makamu wa Rais Mtendaji Mwandamizi wa Shirika la Kimataifa la Ushirikiano la Japan (JICA) Bw. Kazuhiko Koshikawa (wa tatu Kushoto) na ujumbe wake walipokutana Ikulu jijini Dar es salaa leo Februari 28, 2019. Wa pili kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt Damas Ndumbaro

Read more

Mipango ya Serikali Kuhusu Gesi ya Kusini Iko Palepale – Mgalu

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akizungumza wakati wa hafla ya uwashaji rasmi wa umeme katika kijiji cha Ntauna, Kata ya Rondo, Lindi Vijijini, akiwa katika ziara ya kazi, Februari 27, 2019.

Na Veronica Simba – Lindi

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu amewataka watanzania kuondoa shaka kuhusu mipango ya serikali kufuatia gesi iliyogunduliwa mikoa ya kusini, kwani haijabadilika na inaendelea kutekelezwa.

Aliyasema hayo jana Februari 27, 2019 kijijini Ntauna, Kata ya Rondo, Lindi Vijijini, alipokuwa akihitimisha ziara yake ya siku nne mkoani Lindi ambapo alikagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya umeme, kuwasha umeme katika vijiji mbalimbali na kuzungumza na wananchi.

Read more

Wamiliki wa Leseni za Uchimbaji Madini Zisizotumika Morogoro Wakalia Kuti Kavu

Na Peter Haule, WFM, Morogoro

Serikali imeahidi kulifanyia kazi suala la Leseni mfu za uchimbaji madini mkoani Morogoro, ili kutoa fursa ya wachimbaji wadogo  kuchimba madini hayo na kulipa kodi stahiki kwa manufaa mapana ya Taifa.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji alipofanya Mkutano na Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi na Watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Mkoani Morogoro na wadau wengine.

Maelekezo hayo yanafuatia maelezo ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Steven Kebwe, ambaye pamoja na kuishukuru Serikali kwa  kutoa fedha zenye lengo la kuzisaidia Mamlaka za Serikali za Mitaa kujitegemea kimapato na akaiomba Serikali kuhakikisha inafuta Leseni mfu za wachimba madini takribani 174 ambao wanazuia wachimbaji wadogo kufanya shughuli za kujipatia kipato kutokana na  madini na kulipa kodi.

Read more

Ruge Alikuwa Mstari wa Mbele Kuwasaidia Vijana-Majaliwa

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Taifa limepoteza kijana aliyekuwa mstari wa mbele kuwahamasisha vijana wajitambue wawe wazalendo kwa nchi yao na watambue fursa za maendeleo zilizopo na wasiwe walalamikaji.

Ameyasema hayo leo (Jumatano, Februari 27, alipokwenda kuhani msiba wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba kwa niaba ya Serikali, nyumbani kwa wazazi wa marehemu Mikocheni jijini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu amesema vijana nchini walikuwa na kiongozi aliyekuwa akiwaongoza kwa kuwafungua kimawazo na kuwaonesha fursa mbalimbali zitakazowawezesha kuwakwamua kifikra na kiuchumi ili waweze kujitegemea.

Waziri Mkuu amesema msiba huo ni wa wote kwani marehemu amefanya kazi kubwa ya kushirikiana na Serikali kuhamasisha vijana kujitambua na kutambua fursa zilizopo na kuzifanyia kazi. “Ruge ametoa mchango mkubwa kwa Taifa

Amesema marehemu Ruge katika kipindi cha uhai wake amefanya kazi kubwa kwa upande wa Serikali, kuanzia awamu ya nne hadi ya tano hususani katika suala la kuhamasisha vijana kujikwamua na kutokuwa wategemezi.

Pia, Waziri Mkuu amesema historia yake inaeleza namna alivyozunguka nchi nzima na kukutana na makundi ya vijana mbalimbali na kuwaelimisha namna ya kutambua fursa zilizopo nchini huku akiwahamasisha wawe wazalendo.

“Marehemu alikuwa akitoa hadi fedha zake binafsi kwa ajili ya kuwawezesha vijana hasa wale ambao hawakuwa na uwezo wa kiuchumi ili nao washiriki katika shughuli mbalimbali za ujasiriamali na hatimaye waondokane na utegemezi.”

Kadhalika, Waziri Mkuu ametoa wito kwa wazazi, watoto wa marehemu pamoja na wananchi kwa ujumla waendelee kuwa na subira na watulivu katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa wao.

IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU,

JUMATANO, FEBRUARI 27, 2019

 

Taarifa kwa Umma

BODI YA WAKURUGENZI YA MAMLAKA YA USIMAMIZI WA WANYAMAPORI TANZANIA – (TAWA)

Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Hamisi A. Kigwangalla (Mb.), amekamilisha uteuzi wa safu ya wajumbe wa bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania – (TAWA), kulingana na mamlaka aliyonayo kwa mujibu wa kifungu cha 3.1.1 cha amri ya uanzishwaji wa Mamlaka ya TAWA ( GN na. 135 ya mwaka 2014)  kwa kuwateua wajumbe wengine wawili.

Read more

Fanyeni Kazi kwa Umoja na Kuwatendea Haki Wagonjwa-Dkt. Chaula

Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Godfrey Mbawala akimwelezea Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Idara kuu ya Afya Dkt. Zainab Chaula jinsi wanavyofanya upasuaji wa moyo wa bila kufungua kifua kwa watoto kutumia mtambo wa Cathlab wakati katibu mkuu huyo alipotembelea Taasisi hiyo leo kwa ajili ya kuona huduma za matibabu ya moyo zinazotolewa.

Na Mwandishi Maalum

Wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete wametakiwa kufanya kazi zao kwa umoja, kuwasaidia wahitaji na kuwatendea haki wagonjwa wanaotibiwa katika Taasisi hiyo.

Rai hiyo imetolewa leo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Idara Kuu ya Afya Dkt. Zainab Chaula alipokuwa akizungumza  na wafanyakazi wa Taasisi hiyo jijini Dar es Salaam.

Read more