Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Korosho Yaingiza Serikali fedha za Kigeni Zaidi ya Tsh. Trilioni Moja

Na Jonas Kamaleki- MAELEZO, Dodoma

Zao la Korosho katika kipindi kilichoishia Januari 2018 liliingizia Taifa fedha za kigeni shilingi 1,136,609,586,722 ikilinganishwa na mazo mengine ya biashara.

Akijibu swali la Mbunge wa Mtwara Mjini, Mhe. Maftaha Abdallah Nachuma, Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Omari Mgumba, amesema licha mchango huo katika uchumi wa Taifa, zao la korosho limekuwa likikabiliwa na changamoto mbalimbali ambazo Serikali imekuwa ikizitafutia ufumbuzi ikiwemo kuongeza bei ya korosho na kutafuta masoko ya uhakika. Read more

Matukio Katika Picha Bungeni Leo

Spika wa Bunge Job Ndugai  (kulia) akimwapisha Mbunge wa Temeke, Abdallah Mtolea , Bungeni jijini Dodoma

 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira, Vijana  na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama akiwasilisha Muswada wa Sheria ya Marekebisho  ya Sheria ya Vyama vya Siasa wa Mwaka 2018, Bungeni jijini Dodoma

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Kiembe Samaki, Ibrahim Raza kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wananchi kutoka jimbo la Kilwa Kusini waliotembelea Bunge kwa mwaliko wa Mbunge wao  Selemani Bungara, kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akizungumza na mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma

Majaliwa Awataka Viongozi wa Serikali Kutekeleza Maagizo ya Rais Magufuli Katika Sekta ya Madini.

Na Beatrice LyimoMAELEZO, Dodoma

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amewataka Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa na Maafisa Madini wakazi wa Mikoa kuhakikisha wanatekeleza kwa haraka  maagizo yaliyotolewa na Rais John Pombe Magufuli ikiwemo kuanzisha masoko ya madini kwa lengo la kukabiliana na  changamoto za utoroshwaji  wa madini na migogoro kwa wachimbaji wadogo.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo Jijini Dodoma wakati akifungua mkutano kuhusu uanzishwaji wa masoko ya madini kwa lengo la kukabiliana na  changamoto hizo ili kuongeza tija katika sekta ya madini.

Read more

Majaliwa Aongoza Kikao Cha Kujadili Uwekezaji Wa Kiwanda Cha Mponde Wilayani Lushoto

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika Kikao alichokiitisha cha kujadili Uwekezaji wa Kiwanda cha Chai cha Mponde katika Halmashauri ya Bumbuli mkoani Tanga kilichowajumuisha Naibu Mawaziri wa Kilimo, Viwanda na Biashara, Makatibu Wakuu wa Wizara hizo, Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF na Msajili wa Hazina. Kikao hicho kilifanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma

Read more

Majaliwa Akutana na Wajumbe wa Bodi ya Mishahara na Maslahi katika Utumishi wa Umma

 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Wajumbe wa Bodi ya Mishahara na Maslahi katika Utumishi wa Umma, kwenye Makazi ya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa  amekutana na kufanya mazungumzo wa wajumbe wa Bodi ya Mishahara na Maslahi katika Utumishi wa Umma na ameitaka ifanye kazi kwa weledi.

Ameiagiza ifanye marekebisho ya maslahi kulingana na mazingira ya mtumishi, akitolea mfano kada za elimu, afya, kilimo na mifugo ili yalingane na kazi wanazozifanya. Read more