Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

DC Chongolo, Msuya Waaga Mwaka 2018 kwa Kueleza Mafanikio ya Serikali

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam Mhe. Daniel Chongolo

Na. Frank Mvungi

Wakuu wa Wilaya za Kinondoni, Daniel Chongolo na Wilaya ya Uyui, Gift Msuya kwa pamoja wamepongeza Juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano katika kipindi cha mwaka 2018 ambazo zilizolenga kuboresha huduma za jamii na kuinua maisha ya wananchi.

Akizungumza leo katika mahojiano maalum na Idara ya Habari-MAELEZO, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Daniel Chongolo, amesema kuwa katika kipindi cha mwaka 2018, wananchi wameshuhudia uboreshaji wa miundombinu ya barabara, madaraja, vituo vya afya, Elimu, ujenzi Reli ya kisasa, Zahanati na ujenzi wa Hospitali mpya za Wilaya zipatazo 67.

“Ujenzi wa reli ya kisasa kwa Kiwango cha Kimataifa (SGR) hapa nchini utawezesha kufungua sekta mbalimbali ikiwemo uchukuzi, kukuza biashara kati ya Tanzania na mataifa ya jirani, kufungua uwekezaji ambao utachochea kwa kiwango kikubwa kukuza uchumi na ustawi wa wananchi”, ameeleza Chongolo. Read more

Watanzania Waaga Mwaka 2018, Wataja Mambo Saba Yaliyowagusa

: Bibi. Daniella Massinga Mkazi wa jiji la Dodoma akizungumzia mambo makubwa yaliyofanywa na Serikali katika kipindi cha mwaka 2018 leo.

Na. Jacquiline Mrisho – MAELEZO

Wakati dunia nzima ikisubiri kwa hamu kubwa ifike saa sita kamili za usiku ili kuuaga mwaka 2018 na kuukaribisha mwaka 2019, kwa upande wa Tanzania, wananchi wameeleza na kuoa maoni yao juu ya mambo mbalimbali yaliyotekelezwa na kuufanya mwaka 2018 kuwa ni wa kipekee.

Mosi: Katika mahojiano hayo maalumu, Mkazi wa Dodoma, Bi. Daniella Masenga, ameeleza kufurahishwa na hatua ya Rais Magufuli kumaliza utata wa suala la Kikokotoo cha mafao ya wastaafu kwa kuagiza vikokotoo vya zamani viendelee kutumika mpaka mwaka 2023. Read more

Waziri Kalemani Awataka Wakandarasi Miradi ya Umeme Kueleza Mipango Kazi Yao kwa Viongozi

Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani, akimweleza dhamira ya ziara yake, Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe, Colonel Magembe (kushoto) pamoja na wajumbe wengine wa Kamati ya Ulinzi na Usalama, alipowasili wilayani humo Desemba 30, mwaka huu, kukagua utekelezaji wa miradi ya umeme.

Na Veronica Simba – Ukerewe

Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani amewataka wakandarasi wanaotekeleza miradi ya umeme vijijini nchini kote, kuwasilisha mipango-kazi yao kwa viongozi na wawakilishi wa wananchi wa maeneo wanakofanyia kazi ili waweze kuielewa hivyo kusimamia utekelezaji wake.

Read more

.Kanyasu Awataka Wananchi Wanaoishi Ndani ya Hifadhi ya Misitu Kulipa Tozo Bila Shuruti

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu (katikati) akiwa na baadhi ya viongozi wa kijiji cha Buhama wakati akiwasili katika Hifadhi ya msitu ya Kisiwa cha Kome Mchangani ambayo ni Kambi ya wavuvi kwa ajili ya kutatua kero zinazowakabili wananchi wa maeneo hayo.

Na Lusungu Helela-Mwanza

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Costantine Kanyasu amewataka wananchi wanaoishi na kufanya shughuli za uzalishaji mali ndani  ya Hifadhi ya misitu ya Visiwa vya  Kome  na Maisome vilivyoko wilayani Sengerema mkoa wa Mwanza kulipa tozo za serikali bila kulazimishwa.

Read more

Stempu za Kielektroniki za Ushuru wa Bidhaa Kuanza Kutumika Januari, 2019

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere (kulia) akisaini kitabu cha wageni katika kiwanda cha kutengeneza vinywaji vikali cha Nyati Spirit Tanzania cha jijini Dar es Salaam wakati alipotembelea kiwanda hicho kukagua ufungaji wa mfumo wa stempu za kielektroniki ambapo Januari, 2019 bidhaa zote zinazozalishwa kiwandani hapo zinatakiwa kutumia Stempu za Kielektroniki za Ushuru wa Bidhaa.

Na Veronica Kazimoto

Bidhaa zinazostahili kutozwa ushuru wa bidhaa kama vile sigara, mvinyo, pombe kali pamoja na bia zitaanza kutumia rasmi stempu za kielektroniki Januari, 2019 katika Mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, Kilimanjaro, Mwanza, Shinyanga na Mbeya ambapo mfumo wa stempu hizo umeshafungwa kwenye mitambo ya uzalishaji.

Akizungumza mara baada ya kumaliza kukagua ufungaji wa mfumo huo katika Kampuni ya Sigara Tanzania (TCC) na Kiwanda cha kutengeneza vinywaji vikali cha Nyati Spirit Tanzania jijini Dar es Salaam, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere alisema kuwa mfumo huo mpya unaondoa mfumo wa zamani wa stempu za karatasi.

“Nimekuja kufanya ziara katika viwanda hivi ili kujiridhisha kama kweli mfumo huu wa stepu za kielektroniki umefungwa na nimejionea mwenyewe mfumo tayari umefungwa katika viwanda vyote nilivyotembelea. Hivyo, tunaachana na mfumo wa zamani wa stempu za karatasi na kwa sasa tunaendelea kufunga mfumo huu mpya wa stempu za kielektroniki kwenye mikoa mingine ambayo haitaanza katika awamu hii”, alisema Kichere.

Kichere alisema kuwa lengo la kuweka stempu za kielektroniki kwenye bidhaa hizo ni kupata idadi halisi ya uzalishaji wa bidhaa ili kutoza kodi stahiki na kuondoa dhana ya kusema kwamba TRA inawaonea wafanyabiashara wanaozalisha bidhaa hizo kwa kutoza kodi isiyoendana na uzalishaji.

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere (katikati) akizungumza na watendaji wakuu wa kiwanda cha kutengeneza vinywaji vikali cha Nyati Spirit Tanzania cha jijini Dar es Salaam wakati alipotembelea kiwanda hicho kukagua ufungaji wa mfumo wa stempu za kielektroniki ambapo Januari, 2019 bidhaa zote zinazozalishwa kiwandani hapo zinatakiwa kutumia Stempu za Kielektroniki za Ushuru wa Bidhaa.

“Lengo la kuweka stempu hizi za kielektroniki ni kupata kiasi halisi cha uzalishaji wa bidhaa hizi ili kila upande uridhike yaani mzalishaji alipe kodi sahihi na sisi TRA tutoze kodi stahiki bila kupingana wala kugombana na wateja wetu”, alisema Kichere.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa kiwanda cha kutengeneza vinywaji vikali cha Nyati Spirit Tanzania Rupa Suchak amesema kuwa amefurahishwa na kitendo cha serikali kufunga mfumo huo wa stempu za kielektroniki kwa sababu serikali itaongeza mapato na wafanyabiashara wataongeza uhiari wa kulipa kodi.

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere akikagua bidhaa katika kiwanda cha kutengeneza vinywaji vikali cha Nyati Spirit Tanzania cha jijini Dar es Salaam ambapo Januari, 2019 Stempu za Kielektroniki za Ushuru wa Bidhaa zitaanza kutumika rasmi katika bidhaa hizo. Kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa kiwanda hicho Bi. Rupa Suchak.

“Ninaishukuru sana serikali yetu kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania kwa kuleta mfumo huu mpya ambao utaongeza mapato na kupanua wigo wa kodi lakini pia kwetu sisi wafanyabiashara tutaongeza uhiari wa kulipa kodi”, alisema Rupa.

Uwekwaji wa stempu za kielektroniki katika bidhaa nyingine kama vile juisi, maji ya chupa, bidhaa za muziki na filamu (CD\DVD\Tape) zitafuata kwa tarehe ambayo itatangazwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania hapo badae.

 

Waziri Mkuu: Serikali Imeshalipa Bilioni 222, Itanunua Korosho Yote Itakayohakikiwa

Na Mwandishi Wetu

WAZIRI MKUU wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa amesema jumla ya shilingi bilioni 222 zimelipwa na Serikali kwa wakulima wa zao la korosho na kuwataka wakulima wawe na subira.

Waziri Mkuu Majaliwa ameyasema hayo leo alipozungumza na wananchi wa kijiji cha Nandagala ‘A’ baada ya kufungua ofisi ya CCM kata ya Nandagala Mkoani Lindi.

Amesema kuwa wakulima walioanza kulipwa ni wale wenye kilo zisizozidi kilo 1,500 na wale wenye kilo zaidi ya 1,500 na kuendelea Serikali inaendelea na uhakiki kisha watalipwa.

Read more

Tanzania Miongoni mwa Nchi Tano Bora Kwa Ukuaji wa Uchumi Afrika

 

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango (Mb) akizungumza na Waandishi wa habari leo Jijini Dodoma kuhusu hali ya uchumi wa Taifa na utekelezaji wa bajeti ya Serikali ambapo uchumi wa Tanzania umetajwa kuwa miongoni mwa nchi Tano bora kwa kasi ya ukuaji wa uchumi katika bara la Afrika katika kipindi cha nusu ya kwanza ya mwaka 2018.

Na; Mwandishi Wetu

Tanzania imetajwa kuwa miongoni mwa nchi Tano bora kwa kasi ya ukuaji wa uchumi katika bara la Afrika hali inayoonesha jinsi Serikali ya Awamu ya Tano ilivyojidhatiti kuwainua wananchi wake.

Akizungumza leo Jijini Dodoma kuhusu hali ya Uchumi wa Taifa na Utekelezaji wa Bajeti ya Serikali kwa kipindi cha miezi 6 iliyopita, Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango (Mb) amesema kuwa nchi hizo ni Ethiopia asilimia (8.5) Ivory Coast (7.4) Rwanda (7.2) Tanzania(7.0) na Senegal (7.0). Read more

Majaliwa Atembelea Mradi wa Uendelezaji Miji ya Kimkakati Katika Jiji La Dodoma

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua uboreshaji wa Mandhari ya eneo la kupumzikia la Chinangali jijini Dodoma, wakati alipokagua Mradi wa Uendelezaji wa Miji ya Kimkakati katika Jiji hilo, Desemba 29, 2018. Wapili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Bilinith Mahenge na kulia ni Mkurugenzi wa jiji la Dodoma, Gowin Kunambi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ujenzi wa Maegesho ya Malori Makubwa katika eneo la Nala jijini Dodoma, wakati alipotembelea Mradi wa Uendelezaji wa Miji ya Kimkakati katika jiji la Dodoma, Desemba 29, 2018. Watatu kushoto ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde na wapili kushoto ni Mkurugenzi wa jiji la Dodoma, Godwin Kunambi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ujenzi wa Maegesho ya Malori Makubwa katika eneo la Nala jijini Dodoma wakati alipotembelea Mradi wa Uendelezaji wa Miji ya Kimkakati katika jiji hilo, Desemba 29, 2018. Watatu kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Bilinith Mahenge na kulia ni Mkurugenzi wa jiji la Dodoma, Godwin Kunambi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua utekelezaji wa agizo alilolitoa Oktoba 21, 2018 kwa uongozi wa jiji la Dodoma la kubomoa uzio wa mabati uliojengwa kwenye eneo la wazi lililotengwa kwa ajili ya kuchezea watoto na kuziba barabara ya tisa katika Mtaa wa Mji Mpya Kata ya Madukani jijijini Dodoma. Mheshimiwa Majaliwa alikuwa katika ziara ya kukagua Mradi wa Uendelezaji Miji ya Kimkakati katika jiji la Dodoma, Desemba 29, 2018. Wengine pichani kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa jiji la Dodoma, Godwin Kunambi, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Bilinith Mahenge na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)