Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Miaka 3 ya JPM Imechagiza Mageuzi Katika Sekta ya Anga

 

Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akifanya mahojiano maalum katika kipindi cha MORNING TALK cha Ebony Fm Mkoani Iringa kuhusu Utekelezaji wa Serikali katika Kipindi cha Miaka mitatu ya Uongozi wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Na Mwandishi Wetu

Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dkt. John Magufuli ndani ya miaka mitatu imeweza kuleta ukombozi katika sekta ya anga kwa lengo la kuchagiza mageuzi katika sekta hiyo.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi wakati wa kipindi cha Morning Talk cha redio Ebony Fm Mjini Iringa.

Dkt. Abbasi amesema kuwa Rais Dkt. Magufuli amekuwa akitekeleza yale yote aliyoyaahidi ambapo mpaka sasa anaendelea kutekeleza aliyoyaahidi katika sekta ya anga.

Read more

Serikali Kuendelea Kushirikiana na TPSF Kuimarisha Mazingira ya Ufanyaji Biashara Nchini

Muwezeshaji wa Masuala ya Biashara kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Bw. Patrokil Kanje akizungumzia umuhimu wa kuibua changamoto na kuziwekea mkakati wa kuzitatua ili kuchochea ukuaji wa sekta binafsi hapa nchini.

Na; Mwandishi Wetu

Serikali imesema itaendelea Kushirikiana na Sekta  Binafsi hapa Nchini ili kuimarisha mazingira ya Biashara hivyo kuchochea ukuaji wa sekta hiyo.

Akizungumza leo Jijini Dodoma kwa niaba ya Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji  Mhe. Joseph  Kakunda, Mkurugenzi wa Masoko wa Wizara hiyo Bw. Wilson Malosha  amesema kuwa sekta Binafsi  na sekta ya Umma  zinajukumu kubwa la kuendelea kushirikiana ili kuimarisha na kukuza Biashara hapa nchini.

“Ukiwa na taarifa sahihi na zenye takwimu zitakusaidia kufanya maamuzi sahihi na kwa wakati muafaka hali itakayochangia katika ustawi wa sekta  Binafsi na pia  kujenga utamaduni wa kubadilishana taarifa zinazokusanywa katika sekta husika ni jambo muhimu kwa ustawi wa sekta hii na ukuaji wa uchumi;” Alisisitiza Malosha

Akifafanua  Bw. Malosha amesema kuwa wanachama wa sekta binafsi wanazo taarifa muhimu katika kukuza sekta hiyo hivyo kuna umuhimu mkubwa wa kubadilishana taarifa za kisekta ili kuwasadia wawekezaji mbalimbali ambao wanataka kuwekeza hapa nchini.

Mkurugenzi wa Masoko kutoka Wizara ya Viwanda Biashara na Uwekezaji Bw. Wilson Malosha akizungumza wakati akifungua warsha ya wanachama wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF) kwa niaba ya Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Mhe. Josephat Kakunda leo Jijini Dodoma.

Read more

Majaliwa Afungua Mkutano wa Baraza la Mawaziri la Nchi za Bonde la Mto Nile

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa wakati alipowasili kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es salaam kufungua Mkutano wa Baraza la Mawaziri la Nchi za Bonde la Mto Nile za Ukanda wa Maziwa Makuu kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es salaam Novemba 22, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Bw. George Lugomela (kulia) kuhusu mashine ya kutambua uwepo wa maji ardhini kabla ya kufungua Mkutano wa Baraza la Mawaziri la Nchi za Bonde la Mto Nile za Ukanda wa Maziwa Makuu kwenye hoteli ya Serena, Novemba 22, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama burudani ya ngoma wakati alipowasili kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es salaam kufungua Mkutano wa Baraza la Mawaziri la Nchi za Bonde la Mto Nile za Ukanda wa Maziwa Makuu, Novemba 22, 2018. Wapili kulia ni Waziri wa Maji, Profesa Mbarawa Makame na watatu kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipofungua Mkutano wa Baraza la Mawaziri la Nchi za Bonde la Mto Nile za Ukanda wa Maziwa Makuu kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es salam, Novemba 22, 2018.

TPSF Yadhamiria Kuendelea Kuwezesha Wajasiriamali Nchini

Mkurugenzi wa Uendeshaji kutoka Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF) Bw. Valency Mutakyamirwa akizungumza na washiriki wa warsha ya siku mbili kuhusu uwezeshaji wa wanachama wa Taasisi hiyo leo Jijini Dodoma ikilenga kuibua changamoto na kuweka mikakati ya pamoja yakuzitatua.

Meneja Mradi kutoka Taasisi ya  Sekta  Binafsi  (TPSF)  Bi.  Veneranda   Sumila akisisitiza  kuhusu  umuhimu wa semina ya kuwajengea uwezo   wanachama  wa TPSF leo Jijini Dodoma wakati wa hafla yakufungua warsha hiyo.

Mratibu kutoka Taasisi ya Best Dialogue  Bi. Manka  Kway akizungumzia umuhimu wa Maktaba ya Mtandaoni inayoleta pamoja taarifa za wajasiriamali wa Tanzania ikiwemo tafifi mbalimbali zinazofanyika zikilenga kuchangia katika kukuza biashara hapa nchini.

Muwezeshaji  wa masuala ya Biashara kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Bw. Patrokil Kanje akizungumzia namna wajasiriamali wa Tanzania wanavyoweza kukuza na kuendeleza biashara zao  kwa kutumia mbinu za kisasa wakati wa warsha ya wanachama wa Taasisi ya Sekta Binafsi.

Katibu Mtendaji wa Umoja wa Wachimbaji wa Madini na Nishati  Tanzania (TCME) Bw. Gerald Mturi akizungumzia umuhimu wa semina hiyo kwa wanachama wa Taasisi ya Sekta Binafsi.

                          Na; Mwandishi Wetu

 Taasisi ya Sekta Binafsi Nchini imedhamiria kuendelea kuwajengea uwezo wajasiriamali nchini ili waweze kuzalisha na kukuza biashara zao na kuchangia katika ujenzi wa uchumi wa viwanda.

Akizungumza leo Jijini Dodoma, Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF) Bw. Valley Mutakyamirwa amesema kuwa  dhamira yao ni kuendelea kujenga uwezo kwa wajasiriamali hao  ili waweze kuchangika katika kutatua changamoto zinazowakabili  kwa kuweka mikakati ya pamoja kati ya wanachama wa Taasisi hiyo.

“ Wajasiriamali hawa ni wanachama wetu hivyo jukumu letu ni kuhakikisha kuwa tunashirikiana nao katika kuibua changamoto na kuweka mikakati ya pamoja ambayo tunashirikiana na Serikali katika kuona namna bora yakuzitatua “; Alisisistiza  Mutakyamirwa Read more

Fanyeni Kazi Kwa Bidii Huku Mkimtanguliza Mungu-Prof. Janabi

Na: Mwandishi Wetu

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi amewataka wafanyakazi wa Taasisi hiyo kufanya kazi kwa bidii huku wakimtanguliza Mungu mbele kwani huduma wanayoitoa inagusa uhai wa  watu.

Prof. Janabi ambaye pia ni daktari bingwa wa magonjwa ya moyo ameyasema hayo leo wakati wa hafla fupi ya kuwaaga maafisa uuguzi wawili ambao wamestaafu kwa mujibu wa sheria ya utumishi wa umma na kumpongeza mfanyakazi bora wa robo ya kwanza ya mwaka wa fedha wa Julai-Septemba 2018.

Alisema kazi ya kuwahudumia wagonjwa siyo kazi rahisi sana kuna wakati wagonjwa wanakuwa wakali wao na  ndugu zao jambo la muhimu ni kuwa wavumilivu na kuwahudumia kwa moyo wa upendo. Read more

Majaliwa Akagua Kiwanda cha Korosho cha Buko na Kiwanja cha Michezo cha Ilulu Mjini Lindi

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua uwanja wa michezo wa Ilulu uliopo mjini Lindi, Novemba 21, 2018. Kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua kiwanda cha korosho BUKO cha mjini Lindi ambacho kimesimamisha uzalishaji, Novemba 21, 2018. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akishuhudia wakati , Afisa anayesimamia Ubora wa Korosho, Dastan Milazi alipokuwa akipima korosho zilizopokelewa kwenye ghala la kiwanda cha korosho cha BUKO cha mjini Lindi wakati alipotembelea kiwanda hicho kilichosimamisha uzalishaji, Novemba 21, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Madaraja ya Korosho Yatambuliwe Kuanzia Ngazi AMCOS – Majaliwa

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwaamewaagiza Warajisi Wasaidizi wa Ushirika katika Mikoa yote inayolima korosho nchini waandae semina kwa Maafisa Ushirika, viongozi wa vyama vya msingi (AMCOS), maafisa ugani na wakulima ili kuwawezesha kubaini na kupanga korosho katika madaraja kuanzia ngazi ya vyama vya msingi.

Amesema jambo hilo litasaidia mkulima aweze kujua korosho aliyoipeleka ina ubora gani akiwa huko kijijini na wanapoifikisha kwenye ghala kuu wafanye kazi ya kuthibitisha , kwa hatua hiyo itasaidia kuondoa malalamiko kuhusu madaraja .

“Zoezi hili licha ya kuthibitisha ubora itasaidia kuboresha uzalishaji kwani wakulima wataelimishwa namna ya kuimarisha na kuboresha uzalishaji wa korosho nchini ikiwa ni pamoja na matumizi bora ya viatilifu ’’ Read more

Waziri Mkuu Azindua Jukwaa La Biashara Na Uwekezaji Tabora

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipozindua Jukwaa la Fursa za Biashara na Uwekezaji Mkoani Tabora kwenye ukumbi wa Mkuu wa Mkoa huo, Novemba 21, 2018.

Awaagiza viongozi wa mikoa nchini wabaini fursa walizonazo na wazitangaze.

Waziri Mkuu amewaagiza viongozi wote wa mikoa nchini wahakikishe wanashirikiana na makundi yote kuzibaini fursa zilipo katika maeneo yao, kuziorodhesha na kuzitangaza kwenye vyombo vya habari na majukwaa ya biashara na uwekezaji ili zipate wawekezaji haraka.

Waziri Mkuu ametoa maagizo hayo leo (Jumatano, Novemba 21, 2018) wakati akizindua Jukwaa la Fursa za Biashara na Uwekezaji la Mkoa wa Tabora, ambapo ameagiza fursa zote ziandaliwe na kuandikwa vizuri ili wenye mitaji kutoka ndani na nje waweze kuziona na kuja kuwekeza.

Pia Waziri Mkuu amewataka Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri mkoani Tabora na watendaji wote wa Serikali wawajibike kwa wananchi kwa kusikiliza kero zao na kizitatua kero zote zinazochelewesha biashara na uwekezaji katika maeneo yao. Read more

Waziri Kairuki Aagiza Rita Kuvunja Bodi ya Uongozi wa Mfuko wa Udhamini wa North Mara

1. Waziri wa Madini Angellah Kairuki akieleza jambo. Kulia ni Mkuu wa MKoa wa Mara, Adam Malima na kushoto ni Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko

Na Asteria Muhozya, Mara

Waziri wa Madini Angellah Kairuki ameuagiza Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) kuvunja uongozi wa Mfuko wa Udhamini wa North Mara ( Bodi ya Wadhamini na Menejimenti) kwa kuwa umeshindwa  kusimamia  uendeshaji wa Mfuko kwa tija na kuandaa utaratibu mzuri  wa usimamizi  wa Mfuko huo ambao utakuwa na  manufaa kwa Taifa .

Aidha, Waziri Kairuki amemwagiza Mkuu wa Wilaya ya Tarime kuruhusu fedha za Keng’anya Enterprises Ltd ( KEL) kuendelea kulipwa  hadi hapo vyombo vya uchunguzi vitakakapobaini na kuelekeza vinginevyo, huku Mkuu wa Mkoa wa Mara akitakiwa kusimamia utekelezaji wa agizo hilo

“Kwa kuwa Keng’anya Enterprises iliomba kupata PL 303/95 kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu zinazosimamia Sekta ya Madini, hivyo malipo ya mrabaha wa asilimia moja yanayopokelewa kutoka kwenye mgodi kwa mujibu wa mkataba wake ni halali,” alisisitiza Kairuki. Read more

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Azindua Kamati ya Uratibu wa VVU/UKIMWI na Magonjwa Yasiyoambukiza Mahali pa Kazi

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Joseph Malongo akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Kamati ya uratibu VVU/UKIMWI na magonjwa yasiyoambukizwa mahali pa kazi, mara baada ya kuzindua kamati hiyo yenye wajumbe kutoka Idara na Vitengo mbalimbali. Uzinduzi huo umefanyika hii leo katika Ofisi ya Makamu wa Rais Jengo la Mtaa wa Makole, Dodoma.

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Joseph Malongo akimsikiliza Bi. Bi. Everada Ndugumchana kutoa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora mara baada ya kuzindua Kamati hiyo leo. Wengine katika picha ni wajumbe wanaowakilisha Idara na Vitengo vya Ofisi ya Makamu wa Rais.

Mjumbe kutoka Kamati ya kuratibu VVU/UKIMWI mahali pa kazi kutoa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora Bi. Everada Ndugumchana (katikati) akifafanua jambo katika kikao cha uzinduzi wa Kamati hiyo. Kulia ni Bi. MwanaAmani Mtoo kutoka ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora na Bw. Samuel Mwashambwa Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu kutoka Ofisi ya Makamu.