Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Taarifa kwa Umma

Rais Magufuli apokea hati za utambulisho za Mabalozi wawili wa Japan na Georgia

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 19 Oktoba, 2018 amepokea hati za utambulisho za Mabalozi 2 walioteuliwa kuziwakilisha nchi za Japan na Georgia hapa nchini.

Mabalozi waliokabidhi hati zao za utambulisho ni Mhe. Shinichi Goto – Balozi wa Japan hapa nchini mwenye makazi Dar es Salaam Tanzania, na Mhe. Zurab Dvalishivili – Balozi wa Georgia hapa nchini mwenye makazi yake Addis Ababa Ethiopia.

Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Ziara ya Majaliwa Wilayani Bahi, Azungumza na Watumishi

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Bahi kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa wilaya hiyo, Oktoba 19, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe kuzindua daraja la Chipanga wilayani Bahi, Oktoba 19, 2018. Wa pili kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo, Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhandisi Bilinith Mahenge, Wanne kushoto ni Mbunge wa Bahi, Omary Badwel na wapili kulia ni Mkuu wa wilaya ya Bahi, Mwanahamisi Athumani. Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Rais Magufuli aichangia Taifa Stars mil. 50

Na. Immaculate Makilika

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameichangia timu ya Taifa ya   mpira wa miguu (Taifa stars)  kiasi cha fedha  shilingi milioni 50, ambazo zitatumika katika maandalizi ya wachezaji hao ambao wanatarajia kuwa na mechi dhidi ya timu ya Lesotho.

Akizungumza  leo Ikulu Jijini Dar es salaam, ambapo aliwaalika wachezaji wa timu ya Taifa ya mpira wa miguu , viongozi  wa mchezo wa mpira wa miguu pamoja na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe, Rais Magufuli amesema kuwa anaichangia fedha timu hiyo ili ifanye maandalizi mazuri yatakayosaidia timu hiyo kushinda dhidi ya timu ya Lesotho.

Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Serikali Kuongeza Mawasiliano Eneo la Uwekezaji Mkuranga

Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye amefanya ziara ya kukagua upatikanaji wa mawasiliano kwenye Wilaya ya Mkuranga iliyopo mkoa wa Pwani na kuahidi wananchi kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itaongeza mawasiliano kwenye Wilaya hiyo ambayo ina viwanda vingi vyenye uwekezaji wa aina mbali mbali

Amesema kuwa katika ziara yake amebaini kuwa yapo baadhi ya maeneo ambayo yanahitaji kuongezewa nguvu ili mawasiliano yaweze kufika eneo kubwa zaidi na kupeleka mawasiliano kwenye baadhi ya maeneo ambayo yana ukosefu wa mawasiliano kwenye Wilaya hiyo kwa kuwa mawasiliano ni maendeleo, uchumi na ulinzi na usalama.

Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Serikali Inatekeleza Miradi ya Maji yenye Thamani ya Shilingi Trilioni 5

Na; Frank   Mvungi

Waziri wa Maji, mheshimiwa Profesa Makame Mbarawa, amesema serikali ya awamu ya tano inatekeleza miradi ya maji yenye thamani ya shilingi trilioni tano kote nchini.

Akizungumza katika kipindi cha Tunatekeleza kinachorushwa na runinga ya TBC1, Profesa Mbarawa amesema kiasi hicho cha fedha kilichotengwa kwa ajili ya miradi hiyo inaonyesha nia ya serikali kuhakikisha Watanzania walio wengi wanapata maji safi na salama ifikapo mwaka 2020. Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Dkt Kalemani Afanya Mazungumzo na Waziri wa Mafuta wa DRC

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (katikati) akiwa na Waziri wa Mafuta wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Profesa Aime Ngoi-Mukena (kulia) na Mwakilishi kutoka Ubalozi wa Tanzania nchini DRC, Michael Sereki.

Na Teresia Mhagama

Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani amekutana na Waziri wa Mafuta wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Profesa  Aime Ngoi-Mukena ambapo wamejadiliana kuhusu utekelezaji wa makubaliano yaliyoingiwa siku za nyuma ya ushirikiano katika kuendeleza sekta ya mafuta na gesi kati ya nchi hizi mbili.

Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Milioni 500 zatumika kuleta neema ya maji Charambe na Kibondemaji

Naibu Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso akizungumza na wananchi wakati wa kukabidhi miradi ya maji ya Charambe na Kibonde maji Jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya hatua zinazochukuliwa katika kuimarisha huduma hiyo kwa wananchi.

Na; Mwandishi wetu

Naibu Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso ameikabidhi DAWASA miradi miwili ya majisafi na usafi wa mazingira yenye thamani ya milioni 500 na inahudumia wananchi wasiopungua 160,133 lengo likiwa kuwafikia wananchi 280,000 katika Wilaya ya Temeke.

Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Maji Prof. Makame Mbarawa, Naibu Waziri Mhe. Aweso amesema kuwa Serikali inaendelea na jitihada za kuimarisha huduma za maji katika Jiji la Dar es Salaam na maeneo mbalimbali hapa nchini ili kufikia malengo yaliyowekwa kufikia mwaka 2020. Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail