Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

TEWW yawezesha wasichana kupata stadi za maisha

Mkufunzi Mkazi wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima mkoa wa Dodoma Bw. Habibu Muyula akisisitiza jambo wakati wa ziara ya ujumbe wa Taasisi hiyo Wilayani Kongwa mkoani Dodoma ikiwa ni sehemu ya kuhitimisha mafunzo ya elimu juu ya kuzuia ndoa za kulazimishwa za utotoni katika Wilaya hiyo leo, ambapo mradi huo unatekelezwa katika Wilaya hiyo na ile ya Bahi kupitia Taasisi ya Elimu ya Watu wazima.

Na; Mwandishi Wetu

Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima kwa kushirikiana na Shirika la Elimu ya Jumuiya ya Madola kuendelea kuwawezesha wasichana waliokosa elimu katika mfumo rasmi kutokana na ndoa za kulazimishwa za utotoni kupata stadi za maisha ili waweze kujitegemea.

Akizungumza wakati wa kuhitimisha mafunzo ya mradi wa GIRLS Inspire katika Wilaya ya Kongwa, Mkufunzi mkazi wa Taasisi hiyo mkoani Dodoma Bw. Habibu Muyula amesem kuwa dhamira yao ni kuona kundi hilo la wasichana waliokosa elimu katika mfumo rasmi linajikwamua kielimu na kiuchumi kupitia mafunzo waliyopata,  yakielenga kuwajengea uwezo wa kujitambua, stadi za uzalishaji na ubunifu kwa lengo la kuwakumboa kifikra na kiuchumi.

“Tumewajengea uwezo mabinti hawa ambao kutokana na  mimba za utotoni walishindwa kuendelea na masomo, hapa Kongwa tayari wameshawezeshwa kuanza uzalishaji wa bidhaa mbalimbali ikiwemo batiki,sabuni na kusindika bidhaa”; Alisisitiza Muyula. Read more

Serikali Yarahisisha Ukusanyaji wa Takwimu za Vifo Vinavyotokea Katika Ngazi ya Jamii Nchini

Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendelo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto (Idara Kuu ya Afya) Dkt. Mpoki Ulisubisya akiongea na baadhi ya Wakurugenzi wa halmashauri mbalimbali na Maafisa Afya mkoani Iringa wakati wa kukabidhi Kompyuta Kibao ( Tablets) zanye mfumo maalum wa kukusanyia takwimu za vifo ngazi ya jamii kwa Maafisa Afya mkoani humo.

Na: WAMJW-Iringa

SERIKALI kupitia Wizara ya afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto imerahisisha ukusanyaji wa takwimu za vifo vinavyotokea kwenye ngazi ya jamii nchini kwa kugawa vifaa maalumu vya kukusanyia takwimu hizo kwa Maafisa afya katika kata za mkoa wa Iringa.

Hayo yamezungumzwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendelo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto (Idara Kuu ya Afya) Dkt. Mpoki  Ulisubisya wakati akikabidhi Kompyuta Kibao ( Tablets) zanye mfumo maalum wa kukusanyia takwimu hizo  kwa Maafisa Afya leo  Mkoani Iringa.

“Takwimu zitakazokusanywa kuhusu vifo na  Maafisa hawa wa afya  kutokana na Mifumo hii zitawasaidia madaktari kujadili changamoto pamoja na sababu za vifo hivyo ili kupata ufumbuzi wa matatizo hayo na kuweza kupunguza idadi ya vifo nchini” alisema Dkt. Ulisubisya. Read more

Serikali Imedhamiria Kuboresha Huduma za Afya – Majaliwa

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali imedhamiria kuboresha huduma za afya kwenye maeneo mbalimbali nchini yakiwemo ya halmashauri ya wilaya ya Lushoto.

Amesema lengo ni kuhakikisha kila kata inakuwa na kituo cha afya chenye uwezo wa kutoa huduma mbalimbali muhimu zikiwemo za maabara, upasuaji na mama na mtoto.

Ametoa kauli hiyo leo (Jumatano, Oktoba 31, 2018) wakati akizungumza na wakananchi katika kata ya Malindi, baada ya kutembelea jengo la soko mbogamboga la Malindi.

Waziri Mkuu amesema Serikali imejipanga vizuri katika sekta ya afya baada ya bajeti ya kununulia dawa kuongezeka kutoka sh. bilioni 31 kwa mwaka na kufikia bilioni 269.

“Hatutaki tena kusikia mgonjwa anaenda hospitali na kukosa dawa biashara hiyo tumeimaliza, Rais Dkt. John Magufuli ametoa fedha nyingi kwa ajili ya ununuzi wa dawa.”

Amesema katika wilaya ya Lushoto Serikali imetenga sh. bilioni 1.4 kwa ajili ujenzi na ukarabati wa majengo ya vituo vya afya vya kata za Kangagai. Mnazi na Mlola. Read more

Ziara ya Majaliwa Wilayani Lushoto

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe wakati alipozindua Jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto akiwa katika ziara ya Mkoa wa Tanga Oktoba 31, 2018. Kulia ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu na wapili kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba. Wapili kulia ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Tanga, Henry Shekifu, watatu kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigela. na kushoto ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Lushoto, Ikupa Harrison Mwasyoge.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto, Ikupa Harrison Mwasyoge wakati alipotembelea ofisi mpya za Halmshauri hiyo baada ya kuzindua jengo la utawala, Oktoba 31, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ujenzi wa Soko la Kisasa la mbogamboga na matunda linalojengwa na Serikali katika kijiji cha Malindi wilayani Lushoto, Oktoba 31, 2018. Alikuwa katika ziara ya Mkoa wa Tanga. Wapili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigela.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi wa kijiji cha Lukozi wilayani Lushoto wakati alipowasili kijijini hapo akiwa katika ziara ya Mkoa wa Tanga, Oktoba 31, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasalimia wananchi wa kijiji cha Lukozi katika Jimbo la Mlalo wilayani Lushoto akiwa katika ziara ya Mkoa wa Tanga, Oktoba 31, 2018.

Serikali ya Tanzania Haitambui Uhalali wa Airtel Afrika Limited

Msajili wa Hazina Bw. Athuman Muttuka akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Serikali kutotambua mchakato wa Kampuni ya Bharti Airtel kuuza hisa zake leo jijini Dodoma. Kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO, Bibi. Zamaradi Kawawa na Mkurugenzi Msaidizi anayeshughulikia Uwekezaji toka Ofisi ya Msajili wa Hazina, Bw. Joseph Mwaisembe. (Picha na: Frank Shija)

Msajili wa Hazina Bw. Athuman Muttuka akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Serikali kutotambua mchakato wa Kampuni ya Bharti Airtel kuuza hisa zake leo jijini Dodoma.

Na. Gerogina Misama

Serikali ya Jamuhuri ya Muugano waTanzania haitambui mchakato uliotangazwa na Kampuni ya Bharti Airtel wa kukaribisha wanahisa wapya ndani ya Kampuni walioiita kwa jina la Airtel Africa Limited.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dodoma Msajili wa Hazina Bw. Athumani Mbuttuka amesema kwamba Kampuni ya Airtel Tanzania Plc inamilikiwa kwa ubia kati ya Serikali ya Tanzania na Bharti Airtel. Read more

Waziri Mkuu Aagiza Eneo la Kiomoni Litathminiwe

*Ni baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wanancho juu ya kutoridhishwa na fidia

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema atamuagizaMthamini Mkuu wa Serikali Bibi. Evelyne Mugasha kwenda katika Kata ya Kiomoni kufanya tathmini ya ardhi ya wananchi ili kubaini thamani halisi ya maeneo hayo ili wananchi waweze kufidiwa.

Hatua hiyo inakuja baada ya wananchi hao kumlalamikia Waziri Mkuu kuhusu kutoridhishwa na fidia ya maeneo yao yaliyochukuliwa na kampuni ya Neelkanthinayomiliki kiwanda hicho cha kuzalisha chokaa.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo jana jioni (Jumanne, Oktoba 30, 2018) wakati akizungumza na wananchi wa kata ya Kiomoni katika mtaa wa Kiomoni wilayani Tanga akiwa katika siku ya kwanza ya ziara yake ya kikazi ya siku tatu mkoani Tanga. Read more

Polisi,TRA Kilimanjaro Wanasa Kiwanda Feki cha Kutengeneza Pombe Kali.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Kamishna Msaidizi wa Polisi ,Hamisi Issah (anayeongea na Simu ) akiongozana na Meneja Msaidizi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Kilimanjaro ,Godfrey Kitundu walifika kwenye nyumba inayoaminika kuwa kiwanda cha kutengeneza Pombe kali.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini.
JESHI la Polisi mkoa wa Kilimanjaro kwa kushirikiana na
Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) wamefanikiwa
kukamata kiwanda  cha kutengeneza Pombe
kali ambacho kimekuwa kikizalisha bidhaa hiyo bila ya usajili.

Moja ya dira za serikali ya awamu ya tano ni kufikia uchumi
wa kati kupitia Viwanda ,hata hivyo baadhi ya wafanyabiahara watafsiri Dira hii
tofauti kwa kuamua kuanzisha Viwanda bila ya kufuata matakwa ya Sheria na
taratibu za nchi.

Read more