Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Jeshi la Polisi Lawashikilia Mgambo Waliompiga Raia Dar

Na Fatma Salum-MAELEZO

Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni linawashikilia watuhumiwa watatu kwa tuhuma za kumshambulia na kumsababishia maumivu makali mtu anaetambulika kwa jina la Robson Orotho ambaye ni mfanyabiashara na mkazi wa Bunju A Jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, ACP Murilo Jumanne Murilo, imebainishwa kuwa sababu ya kushambuliwa kwa mfanyabiashara huyo ni kutokulipa faini ya usafi kiasi cha shilingi elfu 50.

Read more

Taarifa kwa Umma

WAZIRI MKUU KUHUDHURIA MKUTANO WA FOCAC

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa ameondoka nchini leo (Ijumaa, Oktoba 31, 2018) kuelekea nchini China kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC).

Mkutano huo wa siku mbili unatarajiwa kuanza Jumatatu, Septemba 03, 2018 jijini Beijing nchini China, ambapo utafunguliwa na Rais wa China, Xi Jinping. Katika mkutano huo Waziri Mkuu anamuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli.

Mbali na kuhudhuria mkutano huo pia, Waziri Mkuu anatarajia kukutana na kufanya mazungumzo na viongozi wakuu wa kampuni mbalimbali akiwemo Rais wa Kampuni ya CCECC, Rais wa Shirika la NORINCO, Rais wa Kampuni ya Zijin Gold Mine pamoja na Mwenyekiti wa Kampuni ya saruji ya HEGNYA.

IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU, 

IJUMAA, OKTOBA 31, 2018.

 

 

 

TADB Yajitosheleza Kimtaji – Kaimu Mkurugenzi

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Japhet Justine (kushoto) akitoa ufafanuzi kuhusu masuala mbalimbali ya Benki hiyo mara baada ya Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TADB, Bibi Rosebud Kurwijila kuwasilisha taarifa ya utendaji ya Benki hiyo mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji jijini Dodoma.

Na Mwandishi wetu,

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Japhet Justine amesema kuwa TADB ina mtaji wa kutosha kwa sasa kwa ajili ya kuwahudumia wakulima.

Read more

Taarifa kwa Umma

MAANDALIZI YA MICHEZO YA SHIMIWI 2018

         Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) limeandaa Michezo kwa Watumishi wa Seriali kutoka katika Wizara, Idara Zinazjitegemea, Wakala wa Serikali na Ofisi za Wakuu wa Mikoa itakayofanyika Jijini Dodoma kuanzia tarehe 25 Septemba  hadi 06 Oktoba, 2018  katika Viwanja vya Jamhuri na Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM).

Michezo hiyo itakayoshindaniwa ni  Mpira wa Miguu (Wanaume), Netiboli (Wanawake), Kuvuta Kamba (Wanaume na Wanawake), Riadha (Wanaume na Wanawake), Baiskeli (Wanaume na Wanawake),  Karata (Wanaume na Wanawake), Bao (Wanaume na Wanawake), Drafti (Wanaume na Wanawake) na Darts (Wanaume).        Read more

Posta Yaeleza Matarajio Yake Mwaka 2018/2019

Baadhi ya Waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari, wakichukua taarifa iliyokuwa ikitolewa na  Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania, Kanali Mstaafu, Dk. Haruni Kondo.

Mwenyekiti wa Bodi, Kanali Mstaafu, Dk. Haruni Kondo (katikati), akizungumza na waandishi katika mkutano huo.  

Postamasta Mkuu, Hassan Mwang’ombe, akizungumza katika mkutano huo, wakati alipoelezea kuhusu duka la Shirika la kwenye mtandao kwamba sasa tayari linafanya kazi na kuwataka wananchi kulitumia kwa kuweka bidhaa zao ili kuweza kuuza ndani na nje ya nchi. Kulia Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika, Kanali Mstaafu, Dk. Haruni Kondo.

Maofisa wa Kitengo cha Mawasiliano cha Shirika la Posta Tanzania (TPC),wakiwa katika mkutano huo, wakimsikiliza Postamasta Mkuu wa shirika hilo, Hassan Mwang’ombe, alipokuwa akizungumza katika mkutano huo, jijini Dar es Salaam leo.


Taarifa kwa Umma

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amewataka viongozi wote nchini kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia sheria sambamba na kuhakikisha wanasimamia ipasavyo matumizi ya rasilimali za umma kwa maslahi ya wananchi.

Mhe. Rais Magufuli ametoa maagizo hayo leo tarehe 30 Agosti, 2018 katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato mkoani Geita, wakati akizungumza na viongozi na wafanyakazi wa wilaya hiyo, ambapo amesisitiza kuwa viongozi wote wajenge utaratibu wa kusoma sheria na kujiepusha kutumiwa kwa maslahi ya watu binafsi.

Read more

Sekta ya Mifugo Kuchochea Ujenzi wa Uchumi wa Viwanda

 

Frank Mvungi- MAELEZO, Dodoma

Serikali imepanga  kuzalisha mitamba zaidi ya milioni 1  kwa mwaka ili kukuza sekta ya mifugo hapa nchini ili  kuchochea ujenzi wa uchumi wa  viwanda.

Akizungumza  katika kipindi maalum cha TUNATEKELEZA kinachorushwa na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) na kuratibiwa na Idara ya Habari- MAELEZO, Waziri wa Mifugo na Uvuvi  Mhe. Luhaga Mpina amesema kuwa Serikali imejipanga kuhakikisha kuwa sekta hiyo inatoa mchango mkubwa katika ujenzi wa uchumi na ustawi wa wananchi.

“Vituo vya uhaulishaji vilivyopo Arusha na Sao Hill Iringa vimeboreshwa ili viweze kutoa mbegu bora za kutosha kwa kufanya maboresho makubwa katika vituo  vya kanda vya uzalishaji mbegu za mifugo” alisisitiza Mpina Read more

Halmashauri Nchini Zatakiwa Kuwa na Mikakati ya Mawasiliano

Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida, Dkt. Angelina Lutambi akizungumza na ujumbe kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Chamacha Mawasiliano Serikali (TAGCO) walipomtembelea ofisini kwake leo. Ujumbe huo upo katika ziara ya kutembelea Maafisa Habari wa Mikoa ya Kanda ya Kati inayohusisha Tabora, Singida na Dodoma ikiwa ni jutekelezaji wa maazimio ya Kikao Kazi cha Maafisa Mawasiliano Serikali kilichofanyika mapema mwezi machi mwaka 2018. Katikati ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari –MAELEZO, Bibi. Zamaradi Kawawa, anayemfuati ni Makamu Mwenyekiti wa TAGCO, Sarah Kibonde Msika, mjumbe wa Kamati tendaji wa chama hicho Innocent Byarugaba na Mweka Hazina Msaidizi Gerald Chami.

Na: Frank Shija – Idara ya Habari –MAELEZO, Singida

Halmashauri zote nchini zimetatikiwa kuwa na mkakati wa mawasiliano utakaotumikakufikisha taarifa za utekelezaji wa sshughuli za maendeleo kwa wananchi.

Wito huo umetolewa leo Wilayani Mkalama mkoani Singida na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari MAELEZO, Bibi. Zainabu Kawawa  wakati wa ziara ya kutembelea na kujionea changamoto zinazowakabili Maafisa Habari wa Mikoa ya Kanda ya Kati  inayohusisha mikoa ya Tabora, Singida na Dodoma. Read more

Taarifa kwa Umma

Adhabu kwa Wanafunzi Bila Kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu

Katibu Ofisi ya Rais, Tume ya Utumishi wa Walimu, Bibi Winifrida Rutaindurwa ametoa onyo kwa Walimu wanaowaadhibu wanafunzi bila kuzingatia Sheria Kanuni na Taratibu zinazotoa mwongozo wa aina, kiwango na namna  adhabu inavyotakiwa kutolewa kwa wanafunzi.

Amesema kuwa, kutoa adhabu ya viboko kwa wanafunzi bila kuzingatia taratibu zinazohusika sio tu kwamba inaleta athari kwa wanafunzi wanaoadhibiwa bali inaweza kusababisha chuki kati ya wazazi na walimu.

Read more