Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

MKURABITA Yasogeza Huduma za Urasimishaji kwa Wananchi

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Simiyu ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Bw. Festo Kiswaga akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo wakati wa hafla ya uzinduzi wa Vituo Vya Kurasimisha na Kuendeleza Biashara kwa Kanda ya Ziwa Mashariki jana Mjini Bariadi. Vituo hivyo vitakuwa vikitoa huduma za urasimishaji biashara kwa kuwepo wataalamu wote wanaohusika na usajili na utoaji huduma za uanzzishaji na uendelezaji wa biashara kama vile Brella, TRA, Afisa Biashara, Wakala wa Vipimo, taasisi za kibenki na sekta binafsi inayowakilishwa na Kampuni ya GODTEC.

Na: Mwandishi Wetu, Bariadi

Waziri wa Nchi  Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora Kapteni Mstaafu George Mkuchika ameziagiza  halmashauri zote nchini  kutenga maeneo ya uanzishwaji vituo vya urasimishaji biashara kwa wananchi ili waweze kuondokana na umasikini.

Agizo hilo limetolewa na kwa naiba yake na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Festo Kiswaga  katika uzinduzi wa kituo kimoja cha urasimishaji na uendelezaji biashara katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi.

Amesema MKURABITA ndio nyenzo muhimu ya kuwawezesha, kuibua na kuendeleza uwezo wa wananchi kuwa wawekezaji wa ndani wanaowajibika kutengeneza mtaji, soko, ajira na kujenga uchumi wa viwanda ndani ya mfumo rasmi, hivyo ipo haja kwa halmashauri kutenga maeneo kwa ajili ya vituo vya urasimishaji biashara  ili kuwasaidia wananchi. Read more

Wachimbaji Wadogo wadogo Watakiwa Kulipa Maduhuli ya Serikali

Na Jonas Kamaleki, Dodoma

Serikali imewataka wachimbaji wadogo wadogo Mkoani Dodoma kulipa maduhuli yake ili kuiwezesha kutekeleza mipango yake ya maendeleo ikiwemo kutatua changamoto zinazowakabili wachimbaji hao.

Rai hiyo imetolewa leo na Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Prof. Idris Kikula wakati wa ziara ya kukagua shughuli za uchimbaji madini Mkoani Dodoma.

“Utakuta leseni moja inatumiwa na watu kama kumi ambao hawalipi kodi ya Serikali, hii haivumiliki, ulipaji wa maduhuli hayo uanze mara moja”, alisema Prof. Kikula.

Akiongea kuhusu uchenjuaji wa dhahabu baada ya kutembela kiwanda hicho, Prof. Kikula amesema kuwa kuna changamoto katika uchenjuaji, hivyo imeundwa timu ndogo ya kufuzifuatilia ili utatuzi wake uweze kupatikana.

Changamoto zilizobainishwa na wachenjuaji ni pamoja na kutokuwa na umeme wa uhakika katika viwanda vyao, hivyo kuiomba Serikali kuingilia kati. Read more

TAGCO, Idara ya Habari-MAELEZO Zapongezwa Kwa Utendaji

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru Bw. Chiza Marando akisisitiza jambo kwa ujumbe wa chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO) na Idara ya Habari MAELEZO wakati wa ziara ya ujumbe huo katika Halmashauri hiyo kukagua na kujionea jinsi maafisa Habari wanavyotekeleza jukumu la kuisemea Serikali katika Mikoa na Halmashuri zao.

Kiongozi wa Ujumbe wa Viongozi wa Chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO) na Idara ya Habari (MAELEZO) Bi. Gaudensia Simwanza akisisitiza jambo kwa Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru Bw. Chiza Marando wakati wa ziara ya ujumbe huo katika Halmashuri hiyo uliolenga kukagua na kuweka mikakati ya pamoja katika kuimarisha mawasiliano ya Serikali kwa umma.

Frank Mvungi- MAELEZO, Tunduru

Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO) na Idara ya Habari (MAELEZO) vimepongezwa kwa kubuni na kuweka utaratibu wa kufuatilia utendaji wa Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini hadi katika ngazi ya Halmashuri.

Akizungumza na Ujumbe wa chama hicho uliofika Ofisini kwake mapema wiki hii, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo Bw.  Chiza Marando  amesema kuwa hili ni jambo la kihistoria ambapo ufuatiliaji wa utendaji wa Maafisa Habari unafanyika katika ngazi zote.

“Tangu nimeanza kazi sijawahi kushuhudia ufuatiliaji wa namna hii na sisi tuko tayari wakati wote kutoa ushirikiano utakaosaidia Afisa Habari katika Halmashauri yetu atekeleze majukumu yake vizuri hasa katika kutangaza miradi ya maendeleo” Alisisitiza Marando

Read more

Maafisa Habari Watakiwa Kuwa na Mawasiliano ya Kimkakati

Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara Bw. Alfred Luanda akisisitiza jambo kwa Mwakililishi wa Idara ya Habari MAELEZO Bw. Casmir Ndambalilo wakati wa ziara iliyoandaliwa na Chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO) kwa kushirikiana na Idara ya Habari MAELEZO katika Mkoa wa Mtwara leo kuona utendaji wa Vitengo vya Mawasiliano Serikalini pamoja na changamoto zilizopo ili kuweka mikakati ya pamoja ya kuzitatua hali itakayoimarisha Mawasiliano Serikali kwa umma katika mkoa huo.

 

Mwakilishi wa Idara ya Habari MAELEZO Bw. Casmir Ndambalilo akisisitiza jambo Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara Mikindani ambaye pia ni Afisa Mipango Mji Bi. Mariam Kimolo wakati wa ziara ya Ujumbe kutoka Chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO) na Idara ya Habari MAELEZO wakati wa ziara yakutembelea vitengo vya mawasiliano Serikalini katika Mkoa huo hivi karibuni.

Frank Mvungi- MAELEZO

Maafisa Habari Katika Mkoa wa Mtwara wametakiwa kutekeleza majukumu yao kwa weledi ili kuimarisha mawasiliano ya Serikali kwa umma.

Akizungumza na Ujumbe wa chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini  (TAGCO) na Idara ya Habari MAELEZO uliomtembelea ofisini kwake , Katibu Tawala wa Mkoa huo Bw. Alfred Luanda amesema kuwa jukumu la Maafisa Habari ni kuhakikisha kuwa masiliano kati ya Serikali na wananchi yanakuwa yakimkakati  na yanayoendana na kasi ya Serikali katika kuwahudumia wananchi.

“ Baadhi ya  Maafisa  Habari wanajiweka nyuma na kusahau kuwa wanalo jukumu kubwa la kuuhabarisha umma kuhusu miradi ya maendeleo inayoteklezwa katika maeneo yao hasa kwenye Mikoa na Halmashauri” Alisisitiza Luanda

Read more

Masasi Yajidhatiti Kuimarisha Mawasiliano na Wananchi

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara Bi. Changwa Mkwazu akisisitiza jambo viongozi wa Chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO) na Idara ya Habari-MAELEZO walipotembelea Manispaa hiyo ikiwa ni ya juhudi za kuhamasisha Maafisa Habari na Mawasiliano kutekeleza majukumu yao kwa weledi na pia kuweka mikakati ya pamoja ya kutatua changamoto zinazowakabili katika Halmashauri zao na Mikoa.

Kiongozi Mwenza wa msafara kutoka Chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO) na Idara ya Habari–MAELEZO, Bi. Gaudensia Simwanza akisisistiza jambo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara Bi. Changwa Mkwazu walipofanya ziara katika Halamashauri hiyo kuona utendaji kazi wa Maafisa Habari na Mawasiliano na namna wanavyokabiliana na changamoto mbalimbali katika kuisemea Serikali.

Na Frank Mvungi- MAELEZO

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashuri ya Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara Bi. Changwa Mkwazu, amesema kuwa dhamira ya Halmashauri hiyo ni kuendelea kuimarisha mawasiliano na wananchi ili waweze kufahamu miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali.

Akizungumza na ujumbe wa viongozi kutoka Chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO) na Idara ya Habari MAELEZO, uliomtembelea Ofisini kwake Bi. Mkwazu amesema kuwa halmashuri hiyo inatambua umuhimu wa wananchi kupata taarifa za miradi ya maendeleo kwa wakati kupitia vyombo vya habari.

“Afisa Habari wetu anashiriki kikamilifu katika jukumu hili la kuwajulisha wananchi kuhusu miradi ya maendeleo inayoteklezwa na mikakati yetu ni kumuwezesha zaidi kadiri rasilimali zitakavyopatikana kwa kumpatia vitendea kazi bora ili atekeleze jukumu hili kwa ufanisi, “alisisitiza Bi. Mkwazu

Read more

Mafunzo Mkurabita Yaibua Kampuni Sita Mkoani Simiyu

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka (kushoto) akiteta jambo na Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA), Balozi Daniel Ole Njolay alipomtembelea Ofisini kwake leo Mkoani Simiyu. Mwenyekiti huyo pamoja na wajumbe wake wapo ziarani mkoani humo kwa ajili ya kukagua utekelezaji wa shughuli za urasimishaji na uzinduzi wa Kituo cha pamoja cha urasimishaji Kanda ya Ziwa Mashariki.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka akiteta jambo na Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA), Balozi Daniel Ole Njolay (kulia) alipomtembelea Ofisini kwake leo Mkoani Simiyu. Mwenyekiti huyo pamoja na wajumbe wake wapo ziarani mkoani humo kwa ajili ya kukagua utekelezaji wa shughuli za urasimishaji na uzinduzi wa Kituo cha pamoja cha urasimishaji Kanda ya Ziwa Mashariki.Kushoto ni Mratibu wa MKURABITA, Bibi. Seraphia Mgembe.

Read more

Serikali Yatekeleza Miradi 1,498 ya Maji Nchini

Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi akiongea na Wanahabari leo Mjini Dodoma

Na: Lilian Lundo – MAELEZO, Dodoma.

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya uongozi wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli imetekeleza jumla ya miradi 1,493 ya maji vijijini kufikia Desemba, 2017 na ujenzi wa miradi 366 unaendelea kutekelezwa sehemu mbalimbali nchini.

Hayo yameelezwa leo, Jijini Dodoma na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa ahadi za Serikali.

“Mwaka 2017, Serikali iliendelea kutekeleza miradi ya maji vijijini kupitia programu ya kuendeleza sekta ya maji kwa lengo la kuongeza kiwango cha upatikanaji wa maji vijijini,” amesema Dkt. Abbasi.

Read more