Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Serikali Yatenga bilioni 4.3 Kujenga Vituo vya Kuhifadhi Damu Salama

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imetenga sh. bilioni 4.3 ili kujenga vituo vya kuhifadhi damu (satellite blood banks) kwenye mikoa 12.

Ameitaja mikoa hiyo kuwa ni Manyara, Katavi, Rukwa, Ruvuma na Njombe. Mingine ni Tanga, Arusha, Pwani, Singida, Songwe, Geita na Simiyu.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Ijumaa, Juni 29, 2018) bungeni jijini Dodoma katika hotuba yake aliyoitoa wakati wa kuahirisha Mkutano wa 11 wa Bunge. Bunge limeahirishwa hadi Septemba 4, mwaka huu.

Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Taarifa kwa Umma

Rais wa Jamhuri ya Zimbabwe Mhe. Emmerson Dambudzo Mnangagwa leo tarehe 29 Juni, 2018 amemaliza ziara yake rasmi ya kiserikali hapa nchini na kurejea nchini kwake Zimbabwe.

Katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam Mhe. Rais Mnangagwa ameagwa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.

Kabla ya kuondoka nchini Mhe. Rais Mnangagwa ametembelea chuo cha kilimo na mifugo cha Kaole kilichopo Bagamoyo Mkoani Pwani ambacho mwaka 1963 kilikuwa kambi ya wapigania uhuru wa chama cha FRELIMO, na yeye akiwa mmoja wa waanzilishi wa kambi hiyo.

Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Dar es Salaam

29 Juni, 2018

 


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Wanawake Milioni 2.6 Kunufaika na Mradi wa ‘50 Million Women Speak Project’

Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jinsia kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Bw. Julius Mbilinyi akifungua kikao cha wadau wa Kitaifa wa masuala ya maendeleo ya wanawake nchini kilichofanyika jijini Dodoma.Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Sekta ya Jamii kutoka Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mary Makoffu na Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Vijana na Uwezeshaji Kiuchumi, Esther Riwa.

Na Jacquiline Mrisho.

Takribani wanawake milioni 2.6 wanategemea kunufaika na mradi ujulikanao kama 50 Million Women Speak Project’ unaolenga kuwawezesha wanawake kupata taarifa za kiuchumi kupitia mtandao wa mawasiliano.

Takwimu hizo zimetolewa leo jijini Dodoma na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jinsia kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Bw. Julius Mbilinyi alipokuwa akifungua kikao cha wadau wa Kitaifa wa masuala ya maendeleo ya wanawake nchini.

Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Taarifa kwa Umma

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa Jamhuri ya Zimbabwe Mhe. Emmerson Dambudzo Mnangagwa wamekubaliana kuimarisha biashara na uwekezaji baina ya mataifa hayo mawili yenye udugu wa kihistoria ulioasisiwa na Baba wa Taifa la Tanzania Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere na Baba wa Taifa la Zimbabwe Mzee Robert Mugabe.

Viongozi hao wamefikia makubaliana hayo baada ya kufanya mazungumzo rasmi na baadaye kuzungumza na wananchi kupitia vyombo vya habari, Ikulu Jijini Dar es Salaam katika siku ya kwanza ya ziara rasmi ya kiserikali ya Rais wa Jamhuri ya Zimbabwe Mhe. Mnangagwa iliyoanza leo tarehe 28 Juni, 2018 hapa nchini.

Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Taarifa kwa Umma

TANZANIA NI KIMBILIO KWA WALIOKOSA AMANI-MAJALIWA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema kuvumiliana na kustahamiliana ndiko kunakolifanya Taifa la Tanzania kuwa mfano wa kuigwa na kimbilio la wale waliovurugikiwa na amani katika nchi zao.

Kadhalika, uwepo wa amani nchini si tu unatoa fursa ya kutekeleza majukumu ya kiuchumi na kijamii bila hofu bali pia ni sababu muhimu ya wenzetu wengine kutoka nje kuona fursa ya kuwekeza na kushirikiana nasi katika kujenga maendeleo ya nchini.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Alhamisi, Juni 28, 2018) wakati akizindua Umoja wa Kimataifa wa  Wabunge Wapenda Amani tawi la Tanzania (IAPP), kwenye mkutano uliyofanyika katika ukumbi wa Msekwa Bungeni, jijini Dodoma.

Amesema amani na utulivu ni tunu kubwa sana katika jamii yoyote ile Duniani na Tanzania muda wote imeendelea kuenzi tunu hiyo iliyojengwa kwenye misingi imara kupitia waasisi wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere na Sheikh Abeid Amani Karume.

Kadhalika, Waziri Mkuu amezungumzia kuhusu Shirikisho la Amani kwa Wote  (Universal Peace Federation (UPF), ambalo lilianzishwa kwa lengo la kumkomboa binadamu kutoka katika udhalili wa kukosa mahitaji muhimu.

“Hili linadhihirika kupitia mipango ya shirikisho hilo ya kushirikiana na jamii nyingine katika kuimarisha sekta zenye kugusa maisha ya watu wengi kama vile kilimo, mazingira, afya, elimu, miundombinu na nyinginezo,” amesema.

Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema utekelezaji wa mipango hiyo utategemea kwa kiasi kikubwa uwepo wa amani na utulivu katika jamii husika, ambapo amewahakikishia kwamba Serikali ipo tayari na itaendelea kushirikiana nao katika nyanja hizo za kijamii na maeneo mengine kwa ajili ya kulinda maslahi ya pande zote mbili na kuwaletea maendeleo wananchi.

“Nitoe rai kwa Waheshimiwa Mawaziri wa sekta husika kwamba hakikisheni mnaanzisha mazungumzo na wawakilishi wa UFP nchini kwa lengo la kuona namna nzuri ya kuchangamkia fursa zinazopatikana kupitia shirikisho hilo hususan katika sekta za kilimo, elimu, afya, mazingira na miundombinu,” amesema.

Awali, Mwenyekiti Mwanzilishi wa IAPP, Bw. Mussa Ntimizi amesema Shirikisho la Amani kwa Wote  litasaidia nchi kuboresha miradi mbalimbali ya maendeleo kama ya kilimo, afya kwa sababu hakuwezi kuwa na amani bila maendeleo.

Naye, Makamu Mwenyekiti wa umoja huo, Bw. William Ngeleja amesema Shirikisho la Amani kwa wote  limetenga dola bilioni tatu kwa ajili ya kusaidia sekta ya afya katika nchi 10 za Bara la Afrika na Tanzania ikiwemo.

Katika hafla hiyo Waziri Mkuu amepewa tuzo ya Balozi wa Amani na Mwenyekiti wa Shirikisho la Amani kwa Wote (UPF), Dkt. Thomas Walsh. Viongozi wengine walipewa tuzo hiyo ni pamoja na Spika wa Bunge, Job Ndugai, Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson, Makamu Mwenyekiti wa umoja huo,Bw. William Ngeleja Katibu Msaidizi wa umoja huo Bibi Anna Lupembe, Mweka hazina Bibi Ritta Kabati.

Baada ya kukabidhi tuzo hizo, Dkt. Walsh shirikisho lao linahitaji kufanya kazi nna Serikali, sekta binafsi, asasi za kiraia kwa ajili ya kuboresha maendeleo na amani. Amesema katika Taifa kukiwa na maendeleo amani lazima itakuwepo.

Hafla hiyo imehudhuriwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai, Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson, Mwenyekiti wa Shirikisho la Amani kwa Wote (UPF), Dkt. Thomas Walsh, Katibu wa Shirikisho la Amani kwa Wote Kanda ya Afrika (UPF_Afrika), Bw. Adama Doumbia, Katibu wa Shirikisho la Amani kwa Wote Tanzania (UPF_Tanzania), Bw Stylos Simbamwene,

IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU,

S. L. P. 980,

41193 – DODOMA.

ALHAMISI, JUNI 28, 2018.

 

 


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Zimbabwe Kuendelea kuimarisha uhusiano  na Tanzania

Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa akikagua gwaride la heshima mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku mbili.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amesimama pamoja na mgeni wake Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa wakati nyimbo za mataifa mawili ya Tanzania na Zimbabwe zikipigwa katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere mara baada ya Rais huyo wa Zimbabwe kuwasili nchini.

Na. Immaculate Makilika –MAELEZO

Rais wa Jamhuri ya Zimbabwe Emmerson Mnangangwa  amesema serikali yake itaendelea kushirikiana  na kuimarisha uhusiano wake na Tanzania  ili kuimarisha uchumi wa nchi hizo mbili.

Akizungumza na waandishi wa habari Ikulu jijini Dar es salaam leo, Rais Mnangagwa  amesema kuwa Tanzania imesaidia kwa kiasi kikubwa katika harakati za ukombozi wa nchi za Zimbabwe, Afrika  Kusini, Namibia na Msumbiji na hivyo ni jukumu lao kuimarisha uhusiano huo mzuri.

“Sisi kizazi cha zamani ni jukumu letu kuhakikisha kuwa tunakieleza kizazi cha sasa kuhusu  jitihada za Tanzania katika harakati za ukombozi  wa nchi za kusini mwa Afrika”

“Tulikuwa tunakuja hapa, jengo hili na Mwalimu Nyerere alikuwa Rais wakati huo, ambapo aliweza kusuluhisha migogoro iliyokuwepo kati ya chama cha ZANU na ZAPU” aliongeza Rais Mnangangwa.

Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

​​​​​BAKWATA, EAGT Sikonge Wamaliza Mgogoro wa Miaka Kumi

Na Tiganya Vincent – RS Tabora

HATIMAYE mgogoro wa muda mrefu wa kugombania eneo lililopo Mwanamkola mjini Sikonge ambalo lilikuwa likileta mvutano kati ya Waislamu na Kanisa la EAGT uliodumu toka mwaka 2000 umemalizika rasmi baada ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora kuzikutanisha pande zote.

Hatua hiyo imefikiwa jana Wilayani Sikonge na  Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Sikonge, Peres Magiri baada ya kuongoza kikao cha usuluhishi kati ya viongozi wa BAKWATA wilayani Sikonge na Mchungaji wa Kanisa la EAGT Sikonge.

Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

 

Afisa Matekelezo wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya  mkoani Tanga, Sophia Kaku
akizungumza wakati wa mkutano wa Jukwaa la wadau wa maendeleo ya ushirika mkoani Tanga uliofanyika
kwenye ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga na kufunguliwa na Katibu
Tawala wa Mkoa huo Mhandisi Zena Saidi.

Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya mkoani Tanga (NHIF) umewahamasisha wanaushirika mkoani Tanga
kujiunga na mpango wa Ushirika Afya ili waweze kupata kadi za matibabu
ambazo wanaweza kunufaika na huduma ya matibabu nchini nzima kwani bila
afya imara mipango wanayopanga inaweza kushindwa kufanyika kwa ufanisi
mkubwa.

Uhamaishaji huo ulifanywa na Afisa Matekelezo wa Mfuko
huo mkoani Tanga, Sophia Kaku wakati wa mkutano wa Jukwaa la wadau wa
maendeleo ya ushirika mkoani humo uliofanyika kwenye ukumbi wa ofisi ya
Mkuu wa Mkoa wa Tanga na kufunguliwa na Katibu Tawala wa Mkoa huo
Mhandisi Zena Saidi.

Alisema bila wana ushirika hao kuwa na afya
imara mipango yao wanayopanga itashindwa kufanikiwa kwa sababu
wanapokuwa wakiungua wanaweza kutumia kiasi kikubwa cha fedha nyingi
kuweza kujitibu lakini wanapokuwa kwenye mpango huo wataweza kupata
matibabu kwa gharama nafuu.

“Lakini niwaambie kuwa mkijiunga na
mpango wa ushirika mnaweza kunufaika na huduma za matibabu nchi nzima
lakini pia utawawezesha kuweza kuwa na uhakika wa matibabu wakati wote
bila kujali kama utakuwa na fedha wakati unapougua “Alisema.

Alisema mpango wa ushirika afya ni mpango maalumu unaomuwezesha wana ushirika
kwa umoja wao kuchangia huduma za matibabu kabla ya mwanachama kupata
majanga yakiwemo maradhi, kuunguliwa au magonjwa mbalimbali wakati
wakiendelea na shughuli zao.

Hata hivyo aliwataka wanaushirika
hao kuona umuhimu wa kuwekeza kwenye mpango huo ili kuweza kupata huduma
za matibabu wakati wanapokuwa wakikumbana na maradhi mbalimbali ambayo
yanaweza kuwapelekea kushindwa kutekeleza wajibu wao kama ilivyokuwa
awali.

“Ndugu zangu niwaambieni bima ya afya ndio mambo yote
bila kuwa na afya imara mipango tunayopanga haiwezi kukamilika hivyo
niwaase tujiunge na mpango huo wa Ushirika Afya ambao ni mpango maalumu
unaowawezesha kuchangia huduma za matibabu kabla ya kupata
majanga”Alisema.

 


FacebooktwittermailFacebooktwittermail