Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Viongozi wa Mahakama Wakumbushwa Kusimamia Utendaji wa Madalali

Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Majaji wakati wa sherehe za kuwakabidhi hati Mahakimu 24 pamoja na kuwaapisha Naibu Wasajili 9. Sherehe hizo zimefanyika leo jijini Dodoma.Kushoto kwake ni Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi.

Na Jacquiline Mrisho.

Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma amewakumbusha viongozi wa Mahakama kusimamia kwa makini upangaji na utendaji wa madalali ili kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za wadaawa.

Read more

Lukuvi Azindua Baraza la Taifa la Ushauri wa Ardhi

Na Jonas Kamaleki – Dodoma

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendelo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi amezindua Baraza la Taifa la Ushauri wa Ardhi leo jijini Dodoma na kuwataka wajumbe wa baraza hilo kufanya kazi kwa kujitolea badala ya kusubiri vikao.

Akizindua Baraza hilo, Waziri Lukuvi amewataka wajumbe waishauri Serikali juu ya matumizi bora ya ardhi ikiwemo upimaji na upangaji kila kipande cha ardhi kwa matumizi bora na endelevu.

“Natoa rai kwenu mtushauri namna ya kupunguza gharama za upatikanaji wa hati na kwa uharaka ili hata mtu wa kipato cha chini aweze kumiliki ardhi salama”, alisema Waziri Lukuvi.

Waziri Lukuvi amesema anampongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kwa kubadili muundo wa usimamizi wa ardhi ambao una lengo la kuondoa urasimu katika kushughulikia masuala ya ardhi kwani hayo yote yatakuwa chini ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, tofauti na ilivyo kuwa awali.

Read more

Muhogo Sasa Rasmi Kwenye Mazao ya Biashara – Majaliwa

Ni baada ya kupata soko kubwa nchini China

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali ya China imetoa fursa ya kufungua soko la muhogo mkavu kutoka Tanzania, tukio ambalo  linafungua ukurasa mpya wa zao la muhogo kuwa miongoni mwa mazao ya biashara.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Ijumaa, Juni 29, 2018) bungeni jijini Dodomakatika hotuba yake aliyoitoa wakati wakuahirisha Mkutano wa 11 wa Bunge.

Amesema ili kuwezesha wakulima na wafanyabiashara wa Tanzania kunufaika na fursa hiyo, Mei, 2018 ulisainiwa mkataba kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya China kuruhusu bidhaa za muhogo mkavu kutoka Tanzania kuingia katika soko la China.

Read more

RC Tabora Kuwasaka Wanaochoma Moto Misitu na Miti Iliyopandwa

Na Tiganya Vincent – Rs Tabora

Watendaji wa ngazi mbalimbali mkoani Tabora wameagiza kuanza zoezi la kuwasaka na kuwakamata watu ambao wamekuwa na tabia ya kuchoma moto ovyo wakati wa maandalizi ya mashamba na wengine kwa ajili ya kutaka nyasi ziote upya kwa ajili ya mifugo.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri alitoa kauli hiyo jana wilayani Uyui wakati wa ziara yake katika Kijiji cha Kakola na Msimba akiwa katika kampeni ya kuhimiza wananchi kujiunga na ushirika, kupinga vita utoro na mimba za utotoni.

Read more

Jumuiya za Watumia Maji Zaaswa Kufanya Kazi kwa Uadilifu

Mwakilishi kutoka Wizara ya Maji na Umwagiliaji Mhaidrolojia Mkuu, Bernad Chikarabani akizungumza na washiriki katika warsha ya Jumuiya ya Watumia Maji.

Jumuiya za Watumia Maji nchini zimeaswa kufanya kazi kwa uadilifu ili kuweza kulinda na kuhifadhi rasilimali za maji kwa ajili ya manufaa ya taifa katika warsha ya siku mbili iliyoshirikisha Jumuiya za Watumia Maji zinazotoka kwenye mabonde matano ya Pangani, Wami-Ruvu, Rukwa, Ruvuma na Rufiji iliyoandaliwa na Wizara ya Maji na Umwagiliaji kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo wakiwemo IWaSP-GIZ, UNDP, WWF, IUCN, 2030 WRG, SNV, Shahidi wa Maji, Waridi na mashirika mengine.

Read more

Tanzania ni Kimbilio kwa Waliokosa Amani – Majaliwa

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema kuvumiliana na kustahamiliana ndiko kunakolifanya Taifa la Tanzania kuwa mfano wa kuigwa na kimbilio la wale waliovurugikiwa na amani katika nchi zao.

Kadhalika, uwepo wa amani nchini si tu unatoa fursa ya kutekeleza majukumu ya kiuchumi na kijamii bila hofu bali pia ni sababu muhimu ya wenzetu wengine kutoka nje kuona fursa ya kuwekeza na kushirikiana nasi katika kujenga maendeleo ya nchini.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Alhamisi, Juni 28, 2018) wakati akizindua Umoja wa Kimataifa wa  Wabunge Wapenda Amani tawi la Tanzania (IAPP), kwenye mkutano uliyofanyika katika ukumbi wa Msekwa Bungeni, jijini Dodoma.

Read more

Tanzania Yaongoza kwa Wanyama Pori Afrika

*Ni baada ya Serikali na wananchi kulinda rasilimali za nchi  

IMEELEZWA kuwa jitihada za Serikali za kulinda rasilimali za nchi na ushirikiano kutoka kwa wananchi zimesababisha ongezeko kubwa la idadi ya wanyama pori, hivyo kuifanya Tanzania kuwa nchi yenye wanyama wengi barani Afrika.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameyasema hayo leo (Ijumaa, Juni 29, 2018) katika hotuba yake aliyoitoa bungeni wakati wakuahirisha Mkutano wa 11 wa Bunge jijini Dodoma.

Read more

Serikali Yawataka Watendaji Kuwajibika

*Ni katika ukusanyaji wa mapato na nidhamu ya matumizi

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka watendaji wa Serikali katika ngazi zote wawajibike ipasavyo kwenye ukusanyaji wa mapato na kuwa na nidhamu katika matumizi ya fedha na rasilimali za Taifa.

Pia, Waziri Mkuu amesema Serikali itaimarisha ukaguzi katika ngazi zote na ufuatiliaji wa karibu wa miradi ya maendeleo na kufanya tathmini za mara kwa mara ili kuhakikisha kwamba miradi na kazi zitakazofanyika zinawiana na thamani ya fedha (Value for money) za umma zinazotolewa na Serikali.

Read more

Rais Mnangagwa Akabidhi Dola Elfu Kumi kwa Chuo cha Wazazi Kaole.

 

Na. Immaculate Makilika-  Bagamoyo

Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnganagwa amekabidhi dola za kimarekani elfu 10, kwa Chuo cha Wazazi Kaole ikiwa ni mchango wake katika chuo hicho, ambacho aliwahi kupatiwa mafunzo ya ufundi wakati wa harakati za ukombozi za kusini mwa Afrika.

Akizungumza  wakati alipotembelea Chuo hicho leo mjini Bagamoyo, Rais Mnangagwa alisema kuwa amefurahia kuona chuo hicho kikiendelea ambapo hapo zamani mwaka 1963 walitumia kama kambi ya kijeshi  katika harakati za kupigania uhuru.

“Naishukuru serikali ya Tanzania na Msumbiji kwa kuendelea kutunza sehemu hii, pia na mimi ninapenda kuchangia kiasi cha fedha dola elfu 10 za kimarekani. Alisema Rais Mnangagwa”. Read more