Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Matukio Katika Picha Bungeni June 30, 2018

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Kangi Lugola akijibu swali kuhusu utaratibu unaotumika kutoa ajira kwa wananchi katika sekta za Muungano leo Bungeni Jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Madini Mhe. Stanslaus Nyongo akisisitiza jambo kwa Waziri wa Madini Mhe. Angellah Kairuki  na Naibu Waziri Mhe. Dotto Biteko leo Bungeni  Jijini Dodoma wakati wa kipindi cha maswali  na majibu.

Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe. Tate Ole Nasha akieleza mikakati ya Serikali kuhakikisha kuwa inajenga vyuo vya ufundi stadi kila Wilaya hapa nchini leo  Bungeni  Jijini Dodoma.

Sehemu ya wageni waliofika Bungeni kwa ziara ya mafunzo wakifuatilia kipindi cha maswali na majibu leo Bungeni Jijini Dodoma.

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa  (JKT) Dkt. Hussein Mwinyi ( kulia) akisisitiza jambo kwa Waziri wa  Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu  Sera,  Bunge, Uratibu,   Kazi,  Vijana,  Ajira na Wenye Ulemavu Mhe.   Jenista Mhagama wakati wa kipindi cha maswali na majibu leo Bungeni  Jijini Dodoma.

Mbunge wa Welezo  Mhe. Saada Salum  Mkuya akiuliza swali kuhusu utaratibu unaotumika katika kutoa ajira katika sekta za Muungano.

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa  (JKT) Dkt. Hussein   Mwinyi akieleza hatua zinazochukuliwa na Serikali  katika kutatua migogoro ya mipaka kati ya wananchi na Jeshi  la Ulinzi  la Wananachi wa Tanzania ( JWTZ) wakati wa kipindi cha maswali na majibu  leo Bungeni Jijini Dodoma.

Wanafunzi wa Shule ya Tusiime ya Jijini Dar es Salaam wakiwa Bungeni kwa ziara ya mafunzo  wakati wa kipindi cha maswali na majibu, leo Jjijini Dodoma.

 

(Picha na Frank Mvungi)


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Matukio Katika Picha Uzinduzi wa Tume ya Madini

Waziri wa Madini Mhe. Angellah Kairuki  (Mb) akihutubia washiriki wa hafla ya uzinduzi wa Tume ya Madini  Jijini Dodoma ambapo alikuwa mgeni rasmi .

Mwenyekiti wa Tume ya Madini Prof. Idrissa   Kikula  akihutubia  washiriki wa wa hafla ya uzinduzi wa Tume ya Madini  Jijini Dodoma ambapo Waziri wa Madini Mhe. Angellah Kairuki  (Mb)   alikuwa mgeni rasmi .

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge  akisisitiza kuhusu fursa zilizopo Mkoani Dodoma wakati  wa  wa hafla ya uzinduzi wa Tume ya Madini  Jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa  Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Mhe. Dustan Kitandula akizungumzia  manufaa ya kuanzishwa kwa Tume ya Madini wakati wa  hafla ya uzinduzi wa Tume hiyo  Jijini Dodoma

Katibu Mkuu Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila  akitoa hotuba ya kumkaribisha Waziri wa Madini Mhe. Anjellah Kairuki Kuzindua Tume ya Madini leo Jijini Dodoma.

Waziri wa Madini Mhe. Angellah Kairuki  (Mb) akifurahia jambo na   Mwenyekiti wa Tume ya Madini Prof. Idrissa   Kikula wakati akimkabidhi vitendea kazi mara baada ya Kuzindua Tume hiyo leo Jijini Dodoma.

Waziri wa Madini Mhe. Angellah Kairuki  (Mb) akimkabidhi vitendea kazi  Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume hiyo Prof.   Shukrani Manya  mara baada  ya Kuzindua Tume hiyo leo Jijini Dodoma.

Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Prof. Florens  Luoga   ( kushoto) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali  Dkt. Aderladus Kilangi(  kulia)  Wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Madini  ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa  hafla ya uzinduzi wa Tume ya madini  leo Jijini Dodoma.

Makamishana wa Tume hiyo wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Madini Mhe. Angellah Kairuki  (Mb) ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa hafla ya kuzindua Tume hiyo leo Jijini Dodoma.

Waziri wa Madini Mhe. Angellah Kairuki  (Mb) akimkabidhi  Vitendea kazi  mmoja wa Makamishna wa Tume hiyo Dkt. Florence  Turuka ambaye pia ni  Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa wakati wa hafla ya uzinduzi wa Tume ya Madini leo Jijini Dodoma.

Waziri wa Madini Mhe. Angellah Kairuki  (Mb) akiwa kwenye picha ya pamoja na Makamishna wa Tume ya Madini mara baada ya Kuzindua Tume hiyo leo Jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Madini Mhe. Dotto Biteko (kushoto) akiteta jambo na Waziri wa Madini Mhe. Anjellah Kairuki wakati wa hafla ya kuzindua  Tume hiyo iliyofanyika leo Jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt. Anjelina Mabula  akiteta jambo na Naibu Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Elias Kuandikwa wakati wa hafla ya uzinduzi wa Tume ya Madini leo Jijini Dodoma.

 ( Picha zote na Frank Mvungi )FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Tume ya Madini Kutekeleza Majukumu Yake Kwa Maslahi ya Taifa

 

 Frank Mvungi-  Dodoma

Tume ya Madini imetakiwa  kuhakikisha inatekeleza kikamilifu jukumu la usimamizi, Udhibiti, Ukaguzi, Ufuatiliaji, Ukusanyaji wa taarifa na kuweka kumbukumbu kwa kusimamia sekta hiyo kwa uadilifu  hali itakayosaidia Taifa kunufaika na uwepo wa rasilimali  madini.

Akizungumza wakati akizindua Tume hiyo Jijini Dodoma, Waziri wa Madini Mhe. Angellah Kairuki amesema kuwa kuzinduliwa kwa Tume hiyo  kunaashiria kuanza kwa ukurasa mpya katika sekta ya madini nchini kwa kuwa uamuzi huo ni mapinduzi makubwa  hali itakayosaidia  wananchi  kunufaika na sekta hiyo.

“Ni imani yangu, na pia ni imani ya Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli na imani ya Watanzania wote kuwa mtatubadilishia simulizi za sekta ya madini kutoka kuwa za kukatisha tamaa na kuwa za matumaini, kuibadili historia ya sekta ya madini kutoka kuwa ya miguno na manunguniko na kuwa yakujivunia” Alisisitiza Mhe. Kairuki

Akifafanua Mhe. Kairuki amesema kuwa, si kwamba Tume hiyo imepewa mamlaka makubwa bali pia imepewa imani kubwa kwa kuwa mamlaka makubwa yanakuja na wajibu mkubwa mikononi mwa watendaji wa Tume hiyo. Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Dkt. Abbasi Awataka Wanahabari Kutumia Kalamu Zao Kupunguza Ajali

Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi akiongea wakati wa ufunguzi rasmi wa mafunzo maalum kuhusu uandishi wa habari za usalama barabarani leo jijini Dar es Salaam (Picha na MAELEZO)

Na Mwandishi wetu, MAELEZO

Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi amewataka waandishiwa habari nchini kutumia taaluma ya habari kuielemisha jamii juu ya usalama barabarini ili kupunguza ajali ambazo zimeendelea kusababisha vifo visivyo vya lazima na ulemavu wa maisha.

Dkt. Abbasi ametoa wito huo leo jijini Dar es Salaam wakati akifungua rasmi mafunzo maalumu ya miezi sita juu ya uandishi bora wa habari zinazohusu usalama barabarani, kwa waandishi wa habari 17 kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini.

Ameeleza kuwa ajali za barabarani zitapungua kwa kiwango kikubwa endapo waandishi wa habari watatumia taaluma yao kuielemisha jamii juu ya usalama barababrani, kupaza sauti za wananchi pale palipo na changamoto zinazohitaji usimamizi wa Serikali na pia kuwa sehemu ya mageuzi yanayofanywa na Serikali kuwaondolea wananchi changamoto za ajali. Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Wizara ya Ardhi Yaimarisha Alama za Mpaka wa Tanzania, Kenya Mkoani Mara

Bw. Nairoti Kenanda kutoka kijiji cha Njoroi katika tarafa ya Loliondo wilayani Ngorongoro mkoani Arusha, akishiriki kuchimba shimo lenye urefu wa mita moja kwa ajili ya kuwekwa alama ndogo ya mpaka wa kimataifa kati ya Tanzania na Kenya unaopita katika kijiji hiko.

Na Rehema Isango, Arusha

Jumla ya kilomita 91 za mpaka wa kimataifa kati ya Tanzania na Kenya mkoani Mara zenye alama kuu zimeimarishwa na zingine kuwekwa upya baada ya zile za awali kung’olewa na sasa timu za wataalam wa upimaji ardhi na ramani zimeanza kazi hiyo wilayani Ngorongoro katika mkoa wa Arusha.

Kiongozi wa timu ya wataalam kutoka Tanzania, Isaack Marwa amefafanua kuwa jumla ya alama kuu 66 zenye umbile la pembetatu zimeimarishwa ambapo kati ya hizo, 47 zimejengwa upya baada ya kung’olewa na 19 zimekarabatiwa baada ya kuchakaa katika maeneo ya mbalimbali ya wilaya za Rorya na Tarime mkoani Mara.

Amesema kuwa wamefanikiwa kuweka alama mpya ndogo takriban 900 zenye umbile la pembe nne ambazo zinaonana na kwamba sasa zinawezesha eneo la lote la mpaka wa kimataifa mkoani Mara kuonekana kwa urahisi ambapo kazi hiyo imetumia muda wa mwezi moja na majuma mawili. Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Matukio Katika Picha Warsha ya Wadau wa Sekta ya Fedha

Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Prof. Florens   Luoga akitoa hotuba ya ufunguzi wa warsha ya siku moja  ya wadau wa sekta ya fedha nchini kujadili mchango wa sekta hiyo kwenye maendeleo ya uchumi wa Viwanda kwa niaba ya Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango (Mb) leo Jijini Dodoma.

Naibu Katibu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatib  Kazungu akizungumza katika warsha ya siku moja  ya wadau wa sekta ya fedha nchini kujadili mchango wa sekta ya fedha kwenye maendeleo ya uchumi wa Viwanda kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango  Bw. Dotto James leo Jijini Dodoma.

Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Prof. Florens   Luoga akiteta jambo na Naibu Katibu  Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatib  Kazungu warsha ya siku moja  ya wadau wa sekta ya fedha nchini kujadili mchango wa sekta ya fedha kwenye maendeleo ya uchumi wa Viwanda .

Mbunge  wa  Viti maalum  Mhe. Maria Kangole akiteta jambo na Mbunge wa  Muheza Balozi Adadi Rajabu wakati wa warsha ya siku moja  ya wadau wa sekta ya fedha nchini kujadili mchango wa sekta ya fedha kwenye maendeleo ya uchumi wa Viwanda .

Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda Biashara na Uwekezaji Prof. Elisante  Ole Gabriel  akiteta jambo na  Naibu Katibu  Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatib  Kazungu wakati wa warsha ya siku moja  ya wadau wa sekta ya fedha nchini kujadili mchango wa sekta hiyo  kwenye maendeleo ya uchumi wa Viwanda.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu  Sera  na  Uratibu Prof. Faustine Kamuzora akizungumza wakati wa warsha ya siku moja  ya wadau wa sekta ya fedha nchini kujadili mchango wa sekta ya fedha kwenye maendeleo ya uchumi wa Viwanda

Sehemu ya washiriki wa warsha   ya siku moja  ya wadau wa sekta ya fedha nchini iliyolenga kujadili  mchango wa sekta ya fedha kwenye maendeleo ya uchumi wa Viwanda wakifiatilia hotuba ya mgeni rasmi leo Jijini Dodoma .

Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda Biashara na Uwekezaji  Prof. Elisante  Ole  Gabriel  akitaeta jambo na  mbunge wa viti maalum  Mhe. Maria Kangole wakati wa warsha  ya siku moja  ya  wadau wa sekta ya fedha nchini iliyolenga kujadili  mchango wa sekta ya fedha kwenye maendeleo ya uchumi wa Viwanda.

 


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

NBS Kukusanya Takwimu Kwa Njia ya  Satelaiti  na Vishikwambi.

 

Na Beatrice Lyimo

 

Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) imeanzisha mfumo wa ukusanyaji wa taarifa kwa kutumia teknolojia mpya na ya kisasa ya kielektroniki kwa njia ya satelaiti  na Vishikwambi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo mkoani Dodoma mrasimu ramani mwandamizi na msimamizi wa Sehemu ya mfumo wa Ukusanyaji na Usambazaji wa taarifa za Kijiografia (GIS) Benedict Mgambi amesema kuwa lengo la mfumo huo ni kuboresha ukusanyaji wa  taarifa na tafiti mbalimbali   kwa ajili ya maendeleo ya nchi.

Mgambi amesema kuwa teknolojia hii mpya imerahisisha kwa kiasi kikubwa ufanyaji kazi ikilinganishwa na taratibu zilizokuwa zikitumika awali.

“Awali tulikuwa tunatumia teknolojia ya duni ambapo mchakato wake ulihusisha watu wengi, gharama kubwa ila kwa sasa hivi kila kitu kinafanyika eneo husika la tafiti na kutumwa moja kwa moja makao makuu” amesema Mgambi Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Matukio Katika Picha Ziara ya NBS Wilayani Chamwino

Mrasimu ramani Mwandamizi   kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Benedict Mgambi akieleza kwa waandishi wa habari  faida za kutumia mfumo wa ukusanyaji na usambazaji wa taarifa za kijiografia  wakati wa ziara yao iliyonga kujionea jinsi Ofisi ya hiyo inavyotekeleza majukumu yake katika ukusanyaji wa taarifa mbalimbali ikiwemo  tafiti zinazofanywa kwa kutumia mfumo huo wa kisasa.

 Mtaalamu wa masuala ya Jiografia kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bi Matha Macha  akitoa maelezo kuhusu namna mfumo huo unavyofanya kazi.

Mrasimu ramani msaidizi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Rahim  Mussa  akisisitiza kuhusu namna mfumo huo unavyochochea maendeleo na kusaidia Serikali kuokoa gharama kubwa zilizokuwa zikitumika awali katika kukusanya takwimu na taarifa mbalimbali.

Mrasimu ramani Mwandamizi   kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Benedict Mgambi (wapili kutoka kushoto) akiongoza ujumbe kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu kutembelea  kijiji cha  Sasa Wilaya ya Chamwino ambapo  ujumbe huo umeambatana na waandishi wa habari kujionea mfumo wa ukusanyaji na usambazaji wa taarifa za kijiografia  wakati wa ziara yao iliyonga kujionea jinsi Ofisi ya hiyo inavyotekeleza majukumu yake katika ukusanyaji wa taarifa mbalimbali ikiwemo sense na tafiti zinazofanywa kwa kutumia mfumo huo wa kisasa.

Mwenyekiti   wa  kijiji cha  Sasa Wilaya ya Chamwino ambapo ni ujumbe wa NBS  na waandishi wa habari walitembelea  kujionea jinsi  mfumo wa ukusanyaji na usambazaji wa taarifa za kijiografia   unavyofanya kazi  na jinsi ulivyounganishwa na Makao Makuu ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu ,  hiyo ilikuwa wakati wa ziara yao iliyonga kujionea jinsi Ofisi  hiyo inavyotekeleza majukumu yake katika ukusanyaji wa taarifa mbalimbali ikiwemo  za  tafiti zinazofanywa kwa kutumia mfumo huo wa kisasa.

(Picha zote na Frank Mvungi)


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Kikao cha kuwajengea uwezo konga za watu wanaoishi na virusi vya ukimwi na utekelezaji wa Sheria chafanyika Jijini Dodoma

Kaimu Mkurugenzi-TACAIDS Bw.Jumanne Isango akifungua kikao cha kuzijengea uwezo konga za watu wanaoishi na virusi va ukimwi na utekelezaji wa sheria katika ukumbi wa maktaba Jijini Dodoma.Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Ufuatiliaji na Tathmini Dkt.Jerome Kamwela na Kulia kwake ni Mratibu wa Kanda ya Dar es Salaam baraza la watu wanaoishi na VVU Tanzania Bi Edna Edson.

Kaimu Mkurugenzi-TACAIDS Bw.Jumanne Isango akifungua kikao cha kuzijengea uwezo konga za watu wanaoishi na virusi va ukimwi na utekelezaji wa sheria katika ukumbi wa maktaba Jijini Dodoma.

 

Mkurugenzi wa Ufuatiliaji na Tathmini Dkt.Jerome Kamwela akielezea historia ya UKIMWI na taarifa kuhusu matokeo ya utafiti wa kitaifa wa viashiria na Matokeo ya UKIMWI wa mwaka 2016/2017 katika ukumbi wa maktaba Jijini Dodoma.

 

 

Mkurugenzi Idara ya Sera,Mipango na Utafiti-TACAIDS Bw.Richard Nywira akielezea mkakati wa nne wa taifa wa udhibiti wa UKIMWI nchini na Mfuko wa udhamini wa kudhibiti UKIMWI katika ukumbi wa maktaba Jijini Dodoma.

Mmoja wa Washiriki wa kikao cha kuzijengea uwezo konga za watu wanaoishi na virusi va ukimwi na utekelezaji wa sheria akiuliza swali wakati wa kikao hicho kilichofanyika leo Jijini Dodoma.

 

Washiriki wa kikao cha kuzijengea uwezo konga za watu wanaoishi na virusi va ukimwi na utekelezaji wa sheria wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa na wataalam kutoka Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania(TACAIDS) leo Jijini Dodoma.

Washiriki wa kikao cha kuzijengea uwezo konga za watu wanaoishi na virusi va ukimwi na utekelezaji wa sheria wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa na wataalam kutoka Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania(TACAIDS) leo Jijini Dodoma.

Washiriki wa kikao cha kuzijengea uwezo konga za watu wanaoishi na virusi va ukimwi na utekelezaji wa sheria wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa na wataalam kutoka Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania(TACAIDS) leo Jijini Dodoma.

 


FacebooktwittermailFacebooktwittermail