Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Rais Dkt. Magufuli Aitangaza Dodoma kuwa Jiji.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi wakati wa maadhimisho ya sherehe za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mapema leo mkoani Dodoma katika uwanja wa Jamhuri ikiwa ni miaka 54 tangu kuasisiwa kwa muungano huo .

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akikagua gwaride la heshima lililoandaliwa na vikosi vya ulinzi na Usalama wakati wa maadhimisho ya sherehe za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mapema leo mkoani Dodoma katika uwanja wa Jamhuri ikiwa ni miaka 54 tangu kuasisiwa kwa muungano .

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akielekea jukwaa kuu mara baada ya kukagua gwaride la heshima lililoandaliwa na vikosi vya ulinzi na Usalama wakati wa maadhimisho ya sherehe za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mapema leo mkoani Dodoma ikiwa ni miaka 54 tangu kuasisiwa kwa muungano .

Na Beatrice Lyimo-MAELEZO, Dodoma

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametangaza rasmi kwa mamlaka aliyonayo kuipandisha hadhi Manispaa ya Dodoma kuwa Jiji.

Dkt. Magufuli ameyasema hayo leo Mkoani Dodoma wakati wa Maadhimisho ya Miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yaliyoadhimishwa Uwanja wa Jamhuri mkoani humo.

“Tuliona Dar es Salaam ilivyokuwa makao makuu kipindi hicho na ilikuwa inaitwa Jiji, nikaona niangalie katika nchi yetu kuna Majiji mangapi, tuna Manispaa ngapi, Halmashauri ngapi na mimi nina mamlaka gani katika kutengeneza Majiji au Manispaa, nikakuta Dar es Salaam ni Jiji, Tanga ni Jiji, Arusha ni Jiji, Mwanza ni Jiji, Mbeya ni Jiji nikaambiwa Dodoma ni Manispaa nikasema hili haliwezekani kwa hiyo kuanzia leo kwa mamlaka waliyonipa Watanzania Dodoma ni Jiji”

Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Israel Yaahidi Kupanua Wigo wa Miradi Yao Iliyopo Nchini

Serikali ya Israel imeahidi kuendelea kupanua wigo katika miradi yake mbalimbali iliyopo hapa nchini ikiwemo miradi ya afya ili  iweze kuwafikia wananchi wengi zaidi.

Ahadi hiyo imetolewa jana na  Waziri wa Sheria wa nchi hiyo Mhe. Aleyet Shaked alipotembelea Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ili kuona ushirikiano uliopo kati ya Taasisi hiyo na Taasisi ya  Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child’s Heart – SACH) ya nchini humo.

Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

UCSAF Yagawa Kompyuta 25 Shule za Sekondari Wilayani Kibondo

Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye akisalimiana na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Boni Consilii alipowasili kuzungumza nao wakati wa ziara yake jimboni kwake Muhambwe, Kibondo mkoani Kigoma

Na Mwandishi Wetu

Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye amepokea kompyuta 25 zenye thamani ya shilingi milioni 45 kutoka kwa Mkuu wa Uendeshaji  kutoka Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) Mhandisi Albert Richard kwa ajili ya shule za Sekondari zilizopo Wilayani Kibondo mkoani Kigoma ili ziwawezeshe wanafunzi na walimu kujifunza, kufundisha na kwenda sambamba na ulimwengu wa kisasa wa sayansi na teknolojia.

Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

RC Wangabo Aonya Mimba Mashuleni na Saratani Mlango wa Kizazi

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo akimhoji mwanafunzi aliyepata chanjo Gift Ndenje wakati wa uzinduzi wa chanjo hiyo uliofanyika katika shule ya sekondari Mazwi 24/4/2018.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amewatahadharisha wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kuwa makini na kushiriki katika tendo la ndoa katika umri mdogo kwani kufanya hivyo wanajiweka katika hatari ya kupata saratani ya mlango wa kizazi.

Amesema kuwa miongoni mwa sababu zinazochangia kupata saratani ya mlango wa kizazi ni pamoja na kushiriki katika tendo la ndoa na wapenzi wengi, kuzaa watoto wengi, ndoa za mitala pamoja na uvutaji wa sigara.

Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Waziri wa Sheria wa Israel Atembelea JKCI

Waziri wa Sheria wa Israel Mhe. Aleyet Shaked akiagana na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi mara baada ya kumaliza ziara yake ya kikazi jana ya kuona ushirikiano uliopo wa matibabu ya moyo kwa watoto kati ya JKCI na Taasisi ya Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child’s Heart – SACH) ya nchini Israel. Kulia ni Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Mohammed Kambi.

Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

TLS – Chama cha Umma Kifanye Kazi kwa Mujibu wa Sheria

Na Lydia Churi, Magreth Kinabo – Mahakama

Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma amesema Chama cha Wanasheria cha Tanganyika (TLS) ni taasisi ya Umma na siyo binafsi hivyo amekitaka kutekeleza majukumu yake ya msingi ya kisheria kwa kushirikiana na Mahakama na kuacha kujiingiza kwenye masuala ya uanaharakati na siasa.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo jijini Dar es salaam Jaji Mkuu amesema TLS ni chama huru cha kitaaluma kwa kuwa kilianzishwa kwa mujibu wa sheria kufanya kazi kwa manufaa mapana ya Umma.

Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Dkt. Magufuli: EAC Tunaweza Kujitegemea

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Martin Ngoga,alipohutubia Bunge hilo leo Mjini Dodoma.

Na Lilian Lundo – MAELEZO,Dodoma

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewataka Wanaafrika Mashariki kujiamini kuwa wanaweza kutekeleza miradi ya maendeleo bila kutegemea mataifa mengine.

Rais Dkt. Magufuli ameyasema hayo leo Mjini Dodoma alipokuwa  akihutubia Bunge la Nne la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalofanyika mkoani humo kwa mara kwanza  tangu kuanza kwa Bunge hilo.

“Ninazungumza hili si kwamba hatuhitaji msaada au hatuhitaji ushirikiano, lakini ni lazima tuliweke hili wazi, kwamba tukiamua tunaweza na mifano ipo mingi ikiwemo Tanzania”. Alisisitiza Mhe. Rais Dkt. Magufuli.

“Tanzania tunajenga reli ya kisasa yenye urefu wa kilometa 700.26 kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma kwa thamani ya shilingi Trilioni 7.6, tumeweza kununua ndege sita na pia tumejenga meli kubwa katika Ziwa Victoria bila kuomba mkopo popote,” amesema Rais Magufuli.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia Bunge la Afrika Mashariki (EALA) Leo Mjini Dodoma

Aidha, Rais Magufuli ameongeza kuwa wabunge wa Afrika Mashariki wanaowajibu wa kuhakikisha wanalinda na kuendeleza mafanikio yaliyopatikana ndani ya Jumuiya hiyo.

Akitaja baadhi ya mafanikio yaliyopatikana na Jumuiya hiyo Rais Magufuli amesema kuwa kabla ya kuanza kwa umoja wa forodha mwaka 2005 biashara kati ya nchi wanachama ilikuwa na thamani ya dola za kimarekani bilioni 1.8 lakini baada ya kuanzishwa kwa umoja wa forodha imeongezeka hadi kufikia zaidi ya dola za kimarekani bilioni 5.

Mbali na hayo Rais,  Magufuli ameshukuru uamuzi wa bunge hilo kufanyika mjini Dodoma ambapo kwa sasa Serikali imehamishia shughuli zake zote katika mkoa huo, na tayari watumishi wa serikali zaidi ya 3000 wameshahamia huku Rais Magufuli akitarajiwa kuhamia muda wowote mwaka huu.

Kwa upande wake Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Dkt. Martin Ngoga amesema Bunge hilo linasubiri marekebisho ya mkataba wa kuanzishwa kwa jumuiya hiyo ili  lugha ya Kiswahili ianze kutumika kama lugha rasmi katika vikao vya bunge hilo na katika jumuiya hiyo kwa kuzingatia azimio lililokwishapitishwa.

“Hatuoni sababu ya kutumia lugha za wageni wakati kuna lugha yetu ambayo tunazungumza ambayo ni kiswahili,” alisema Dkt. Ngoga.

Bunge la Afrika Mashariki linaendelea na vikao vyake mkoani Dodoma katika ukumbi mdogo wa Bunge wa Pius Msekwa. Bunge hilo limefanyika kwa mara ya kwanza mkoani humo.


FacebooktwittermailFacebooktwittermail