Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

TEWW Kuendelea Kushirikiana na Wadau Kukuza Elimu Nchini

Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW) , Dkt. Kassimu A.Nihuka akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa Habari (hawapo pichani) juu ya dhana ya Elimu ya Sekondari nje ya mfumo rasmi, kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Karibu Tanzania Organization (KTO) Bw.Maggid Mjengwa.

Na Mwandishi wetu

Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW) kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo imeandaa mafunzo ya siku tano ili kuwajengea uwezo walimu 30 kutoka vyuo vya Maendeleo ya Wananchi hapa nchini.

Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa leo na  TEWW Jijini Dar es Salaam, Programu hii ijulikanayo kama “ Elimu Haina Mwisho- Skills Development Program For Young Women Through Folk Development Colleges ” inalenga kukuza kiwango cha elimu hapa nchini.

Sehemu ya taarifa hiyo imeeleza kuwa programu hiyo imegawanyika katika awamu mbili na inalenga  Wanawake na Vijana ambao wamekatishwa masomo kwasababu mbalimbali ikiwamo mimba za utotoni.

“ Mafunzo haya yanaandaliwa na Karibu Tanzania Organization (KTO) kwa kushirikiana na Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW) pamoja na Taasisi ya Aflatoun International ya Uholanzi na Wakfu wa Mastercard(Mastercard Foundation) “ Imesisitiza sehemu ya taarifa hiyo.

Mafunzo yanayotolewa ni ya miaka miwili ikiwamo elimu ya sekondari nje ya mfumo rasmi, ujasiriamali, stadi za maisha na ufundi.

Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Matukio Katika Picha Bungeni leo

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson akijibu miongozo ya wabunge mapema leo Bungeni mjini Dodoma mara baada ya kipindi cha maswali na majibu.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Hamad Masauni akisisitiza kuhusu mikakati ya Jeshi la Polisi kuendelea kuhakikisha usalama wa wananchi na mali zao kote nchini leo Bungeni mjini Dodoma wakati wa kipindi cha maswali na majibu.

Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

SERIKALI YASISITIZA HAKUNA UPOTEVU WA SHILINGI TRILIONI 1.5

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji akitoa taarifa ya Serikali kuhusu hoja ya kutoonekana kwenye matumizi ya Serikali shilingi trilioni 1.51 leo Bungeni mjini Dodoma.

TAARIFA KWA UMMA

Dodoma, April 20, 2018:

Serikali leo imelithibitishia Bunge na umma kwa ujumla kuwa kufuatia maneno ya baadhi ya watu yaliyosheheni upotofu, siasa na yenye nia ya kuchafua taswira ya nchi kwamba kuna Shilingi trilioni 1.5 zimepotea, ukweli ni kwamba hakuna upotevu huo na mchanganuo wa matumizi uko wazi.

Akitoa taarifa hiyo ya kina Bungeni leo, huku akiainisha mchanganuo wa matumizi ya fedha hizo, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, amesisitiza kuwa chini ya Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Dkt. John Pombe Magufuli, fedha za umma ziko salama na wanaojaribu kufanya ufujaji hatua kali zinachukuliwa. Taarifa kamili yenye aya 12 ni kama ifuatavyo:  

  • Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Kanuni ya 49 ya Kanuni za Bunge Toleo la Januari 2016, naomba kuwasilisha mbele ya Bunge lako Tukufu Kauli ya Serikali juu ya madai ya kutoonekana kwa matumizi ya shilingi trilioni 1.51 kwenye matumizi ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2016/2017.

Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Mafuriko Jangwani Kupatiwa Ufumbuzi

Baadhi ya Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika(SADC) wakiwa kwenye majadiliano ya pamoja ambapo walizungumzia vipaumbele vinne, ikiwemo kuendeleza sekta ya viwanda pamoja na kukuza umoja wa kikanda katika sekta ya fedha na uwekezaji, mjini Washington DC Marekani.

Na. WFM- Washington D.C

Benki ya Dunia (WB) imekubali kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kukabiliana na athari za mafuriko zinazosababishwa na mvua kubwa zinazonyesha kila mwaka katika Jiji la Dar es Salaam na kuleta madhara makubwa hususan katika eneo la Jangwani jijini humo.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) wakati akizungumza na ujumbe wa Benki ya Dunia ulioongozwa na Mkurugenzi wa Benki hiyo kwa nchi za Tanzania, Somalia, Burundi na Malawi Bi. Bella Bird, katika mikutano ya kipupwe inayoendelea mjini Washngton DC.

Dkt. Mpango amesema kuwa Benki ya Dunia imekubali kusaidia kukabiliana na mafuriko katika bonde la mto Msimbazi hasa katika eneo la  kutoka Magomeni Mapipa kwenda Faya  na tayari Benki hiyo imeanza  zoezi la kutafiti eneo la Jangwani ili kuweza kuangalia namna nzuri ya kugharamia uboreshaji wa  mifereji katika bonde la mto Msimbazi ili kumaliza kero hiyo kwa wananchi wa Dar es Salaam.

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) akisikiliza majadiliano katika mkutano wa SADC, ambapo alishauri katika utaratibu wa uandaaji wa bajeti ni vyema Mawaziri wa Fedha wakashirikishwa. Kushoto kwake ni Gavava wa Benki Kuu ya Tanzania Prof. Florens Luoga, mjini Washington DC Marekani.

“Tumewaeleza Benki ya Dunia  changamoto hii ambayo imekuwa inajirudia kila mara na kusababisha upotevu wa maisha ya watu, kusababisha kufungwa kwa barabara , watu kushindwa kwenda kazini na wanafunzi kushindwa kwenda shule, hivyo wameonesha nia ya kumaliza kero hii kwa wananchi “ Alisema Dkt. Mpango.

Amesema kuwa baada ya timu ya Benki ya Dunia kumaliza kufanya kazi yao kwa kushirikiana na Manispaa ya jiji la Dar es Salaam, Serikali inaamini njia ya kudumu itapatikana na kuondokana na tatizo hilo la mafuriko ya mara kwa mara katika eneo la Jangwani.

Ujumbe wa Tanzania ukifuatilia kwa makini majadiliano kati yake na Benki ya Dunia ya namna yakumaliza tatizo la mafuriko eneo la Jangwani jijini Dar es Salaam. Wapili kulia ni Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), kushoto kwake ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Zanzibar Bw. Khamis Mussa Omar na wa kwanza kulia kwake ni Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Prof. Florens Luoga na wa pili kulia kwake ni Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Bw. Charles Kichere mjini, Washington DC Marekani.

Ujumbe wa Benki ya Dunia ukiongozwa na Mkurugenzi wa Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania, Somalia, Burundi na Malawi Bi. Bella Bird. (upande wa kulia mwenye scarf shingoni) wakijadiliana na ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto) namna ya kutatua changamoto za mafuriko eneo la Jangwani, mjini Washington DC Marekani. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha na Mipango)


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Benki ya Kilimo Tanzania Kufungua Ofisi za Kikanda Kwa Awamu

Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma

Serikali imeeleza kuwa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) inatekeleza Mpango wa Miaka Mitano (2017- 2021), wa kusogeza huduma karibu na wateja kwa kuanzisha ofisi za Kikanda katika Kanda ya Kaskazini, Kusini, Kati, Ziwa, Nyanda za Juu Kusini na Zanzibar kwa awamu.

Hayo yameelezwa Bungeni Mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), wakati akijibu maswali ya msingi ya Mbunge wa Viti Maalumu Mhe.  Jacqueline Msongozi (CCM), aliyetaka kujua lini Serikali itapeleka Benki ya Kilimo katika Mkoa wa Ruvuma ili wananchi waweze kukopeshwa.

Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Rais Magufuli Afanya Mazungumzo na Wageni Kutoka AU na Misri

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Kamishna wa Amani na Usalama wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika Balozi Smail Chergui Ikulu jijini Dar es Salaam.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu wa Misri ambaye kwasasa ni Mshauri wa Rais wa Misri Injinia Ibrahim Mahlab kabla ya kuanza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.

Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail