Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Hakikisheni Wafanyakazi Wanashiriki Michezo-Mhe. Samia Suluhu

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Shirikisho la Michezo la Mashirika ya Umma na Makampuni Binafsi Tanzania (SHIMMUTA) uliofanyika Chuo Kikuu Dodoma (UDOM) Machi 27, 2018 mjini Dodoma.

Na: Lilian Lundo – MAELEZO, Dodoma.

Waajiri ambao ni wanachama wa SHIMMUTU wametakiwa kuhakikisha wanahamasisha wafanyakazi wao wanashiriki kikamilifu kwenye michezo mahala pa kazi ili waweze kuongeza tija na ufanisi katika kazi zao..

Hayo yameelezwa leo, Mjini Dodoma na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mhe. Samia Suluhu Hassan alipokuwa akifungua mkutano wa Halmashauri Kuu ya SHIMMUTA.

“Ili tuweze kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa uchumi wa viwanda ni lazima kwanza tuwe na afya njema. Ikumbukwe kuwa Serikali ilianzisha mashirikisho ya michezo ya wafanyakazi kwa lengo la kuimarisha afya ili waweze kuongeza tija na ufanisi katika kazi zao,” alisema Mhe. Samia.

Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Wawekezaji Wazawa Wapewa Rai Kujenga Viwanda vya Dawa

17. Rais Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza wakati wa hafla ya magari 181 yatakayokuwa yatayosafirisha vifaa tiba na vitendanishi katika Mikoa na Halmashauri mbalimbali nchini. Hafla hiyo ilifanyika leo Jumatatu Machi 26, 2018 katika Ofisi za MSD Keko Mwanga Jijini Dar es Salaam.

Na Mwandushi Wetu, MAELEZO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametoa rai kwa wawekezaji wazawa na wafanyabiashara nchini kujenga viwanda vya dawa na vifaa vya tiba hapa nchini ili kuongeza kasi ya ujenzi wa uchumi wa viwanda na kukuza ajira.

Rais Magufuli ametoa rai hiyo leo Jijini Dar es Salaam, kwenye hafla ya uzinduzi wa magari 181 yenye thamani ya shilingi bilioni 20.7 ya kusambaza dawa na vifaa vya tiba yaliyotolewa msaada na Shirika la Global Fund kwa Serikali ya Tanzania kupitia Bohari ya Dawa (MSD).

“Asilimia 94 ya dawa zinanunuliwa nje ya nchi, hivyo wawekezaji wazawa watumie changamoto hii kama fursa ya kuanzisha viwanda vya dawa na vifaa tiba hapa hapa nchini kwetu,” alisema Rais Magufuli. Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Serikali, Wadau Kuendelea Kuzuia Maambukizi Mapya ya Virusi vya Ukimwi

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akizungumzia mikakati ya Serikali kupambana na janga la Ukimwi hapa nchini wakati wa warsha kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ukimwi na Madawa ya Kulevya mapema leo Bungeni mjini Dodoma. kushoto ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana na Ajira Mhe. Antony Mavunde.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ukimwi na Madawa yakulevya Mhe. Osca Mukasa (Mb) akisisitiza jambo wakati wa warsha kwa wabunge wa Kamati hiyo kuhusu hali ya Ukimwi hapa nchini iliyofanyika mapema leo mjini Dodoma.kulia ni Katibu wa Kamati hiyo Bi Happiness Ndalu.

Frank Mvungi- MAELEZO, Dodoma

Serikali imesema itaendeleza mapambano ya Vita dhidi ya ugonjwa wa Ukimwi kwa kuongeza kasi katika kuzuia maambukizi  mapya ikiwemo kutoa elimu kwa umma.

Akizungumza leo mjini Dodoma wakati wa warsha kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge inayoshugulikia Ukimwi na Madawa yakulevya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu mhe. Jenista Mhagama amesema kuwa dhamira ya Serikali baada ya kuanzisha mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti Ukimwi (ATF) ni kuhakikisha kuwa mfuko huo unajengewa uwezo ili lengo la kuanzishwa kwake litimie.

Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Rais Dkt Magufuli Ashiriki Ibada ya Jumapili ya Matawi Kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay Jijini Dar es Salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, mkewe Mama Janeth Magufuli na mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakiwa wamejumuika na waumini wengine katika Ibada ya Jumapili ya Matawi katika kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es Salaam leo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, mkewe Mama Janeth Magufuli na mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakipeana amani na Masista wa Kanisa Katoliki walipojumuika na waumini wengine katika Ibada ya Jumapili ya Matawi katika kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es Salaam leo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwa na mkewe Mama Janeth Magufuli akishukuru baada ya kupokea Sakramenti takatifu wakati wa Ibada ya Jumapili ya Matawi katika kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es Salaam leo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na wananchi baada ya kushiriki Ibada ya Jumapili ya Matawi katika kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es Salaam leo .


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Dkt. Mpango na Balozi wa Kuwait Wazungumza Kuhusu Ujenzi Barabara ya Morogoro- Dodoma

Msaidizi wa Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), Bw. Edwin Makamba na Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bw. Hangi Laban, wakifuatilia mazungumzo kati ya Waziri huyo na Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Jassem Al-Najem (hawapo pichani), Mjini Dodoma.

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia) akifurahia jambo na Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Jassem Al-Najem alipomtembelea Ofisini kwake Mjini Dodoma.

Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Jassem Al-Najem (kulia) akimkabidhi zawadi Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto) alipomtembelea kwa mazungumzo Mjini Dodoma.

Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Jassem Al-Najem (kulia) akiagana na mwenyeji wake Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto) alipomtembelea Mjini Dodoma.

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia) akizungumza jambo na Kamishna wa Fedha za Nje wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. John Rubuga (katikati) baada ya kuagana na Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Jassem Al-Najem (hayupo pichani) alipomtembelea Ofisini kwake Mjini Dodoma.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Selikarini Wizara ya Fedha na Mipango)


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Biteko Atoa Wito kwa Wadau Kuzingatia Sheria Mpya ya Madini

Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko, akizungumza na wananchi wa Nholi wilayani Bahi, kulipo na machimbo ya madini ya dhahabu, alipowatembelea Machi 22 mwaka huu, kujionea shughuli wanazofanya.

Na Veronica Simba – Dodoma

Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko ametoa wito kwa wadau wote wa sekta ya madini nchini, kuzingatia sheria mpya ya madini ambayo inaelekeza namna bora ya usimamizi wa sekta hiyo.

Alitoa wito huo jana, Machi 22 mwaka huu kwa nyakati tofauti, alipokuwa katika ziara ya Mkoa wa Dodoma, kukagua shughuli mbalimbali za madini.

 “Moja ya mambo muhimu ambayo sheria mpya ya madini inaelekeza ni kutunza rekodi za uzalishaji wa madini ili Serikali iweze kujua ni kitu gani kinazalishwa na hatimaye tuweze kujua kodi gani zinalipwa na wenye leseni husika,” alifafanua. Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Mkoa wa Mbeya Wadhamiria Kuongeza thamani Mazao Yanayozalishwa ili Kukuza Viwanda.

Frank Mvungi- MAELEZO, Dodoma

Mkoa wa Mbeya wadhamiria kuongeza thamani mazao yanayozalishwa katika Mkoa huo ili kutekeleza azma ya Serikali ya kujenga Uchumi wa Viwanda utakaosaidia kukuza uchumi wan chi na kutoa ajira kwa wananchi

Akizungumza katika kipindi cha TUNATEKELEZA kinachorushwa na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) na kuratibiwa na Idara ya Habari MAELEZO Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Amos Makala amesema kuwa  dhamira ya Serikali ni kuhakikisha kuwa dhana ya ujenzi wa Viwanda inatekelezwa kwa Vitendo .

“Mwishoni mwa mwaka huu tunatarajia kuwa na moja ya viwanda vikubwa vyakuongeza thamani mazao yetu yakiwemo mahindi kwa kuzalisha unga na kitaanza uzalishaji katika Mkoa wetu. Kwa sasa kinachofanyika ni kukamilisha ujenzi na ufungaji wa mitambo,” alisisitiza Makala.

Akifafanua Mhe. Makala amesema kuwa mkoa huo umepiga hatua katika kutoa huduma bora kwa wananchi ambapo asilimia zaidi ya 80 wanapata maji safi na salama katika mkoa huo.

Akizungumzia mikakati ya mkoa huo katika kukuza uchumi, Makala amesema ni pamoja na ujenzi wa bandari kavu, barabara kwa kiwango cha lami ambapo Wilaya zote katika mkoa huo zimeunganishwa na barabara za lami hali inayochochea shughuli za uzalishaji mali.

Aliongeza kuwa, tayari Serikali imekamilisha ujenzi wa meli mbili zenye uwezo wa kubeba tani 1000 na zimeanza kutoa huduma katika ziwa Nyasa hali itakayokuza bishara kati ya Tanzania na nchi jirani na kuwanufaisha Wananchi wa pande zote. Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail