Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Serikali Yaelekeza Dhana ya Ukosoaji kwa Kuzingatia Misingi na Maadili

Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi akizungumza na wadau mbalimbali wa habari wakati wa mkutano ulioandaliwa na taasisi ya Twaweza kuhusiana na hali ya upatikanaji wa taarifa na dhana ya uhuru wa habari nchini. Mkutano huo ulifanyika leo.

Serikali imesema haijazuia vyombo vya habari kukosoa utekelezaji wa sera, mikakati na programu zake na badala yake imesisitiza kuzingatia miiko na maadili ya taaluma hiyo yaliyoanishwa sheria za kimataifa.

Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi wakati wa uzinduzi wa Awamu ya 25 ya utafiti wa sauti ya wananchi iliyotolewa na taasisi ya Twaweza. Read more

CAG: Deni la Taifa ni Himilivu

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG ) Prof. Mussa Assad akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu kauli yake aliyoitoa wakati akiwasilisha ripoti za Ukaguzi wa fedha kwa mwaka unaoishia June 30, 2017 kwa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.Kulia ni Naibu mkaguzi mkuu wa hesabu za Taifa Bw. Athumani Mbuttuka na kushoto ni Naibu mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali anayeshughulia Mamlaka za Serikali za Mitaa Bw. Jasper Mero.

Baadhi ya Waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG ) Prof. Mussa Assad uliofanyika leo mjini Dodoma.

Frank Mvungi- MAELEZO, Dodoma.

Serikali imesema kuwa Deni la Taifa ni stahimilivu hali inayoonyesha kuendelea kuimarika kwa uchumi wa Taifa letu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo mjini Dodoma  Mdhibiti na Mkaguzi  Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG ) Prof. Mussa Juma  Assad amesema kuwa hadi kufikia tarehe 30 June 2017 deni la taifa lilikuwa trilioni 46.08 ambapo deni  la ndani ni shilingi trilioni 13.34 sawa na asilimia 29.

Read more

Idadi ya Watalii Nchini Yazidi Kuongezeka

Waziri wa Mali Asili na Utalii Mhe. Dkt. Hamis Kigwangala akihutubia Wafanyakazi wa Wizara hiyo wakati wa Kikao cha Baraza la Wafanyakazi kilichofanyika mjini Dodoma.

Katibu Mkuu Wizara ya Mali Asili na Utalii Meje Jenerali Gaudensi Milanzi akizungumza na Wafanyakazi wa Wizara hiyo wakati wa Kikao cha Baraza la Wafanyakazi kilichofanyika mjini Dodoma.

Frank Mvungi- MAELEZO, Dodoma.

Tanzania imefanikiwa kuongeza idadi ya watalii kutoka 1,284,279 mwaka 2016 hadi kufikia 1,327,143  mwaka 2017 hali iliyopelekea  kuongezeka kwa mapato ya Serikali.

Akizungumza wakati wa Kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mali Asili na Utalii Dkt. Hamis Kigwangala amesema Wizara hiyo itaendelea kuvutia watalii zaidi ili kukuza utalii na kuongeza pato la Taifa.

“Mapato yanayotokana na utalii yameongezeka kutoka Dola za Kimarekani Bilioni 2.1 mwaka 2016 hadi Dola za Kimarekani Bilioni 2.2 mwaka 2017” Alisisitiza Kigwangala

Read more

MOI Wafanya Upasuaji Mwingine Mkubwa na Wa Kihistoria

Madaktari Bingwa wa MOI kwa kushirikiana na daktari kutoka India wakifanya upasuaji mkubwa wa kubadilisha kiungo cha nyonga kilichochakaa kwa kuweka kiungo bandia ,kama asingefanyiwa upasuaji huu hapa MOI Mgonjwa huyu angelazimika kwenda nje ya nchi kwa gharama kubwa

Na Mwandishi Wetu

Madaktari Bingwa wa Taasisi ya Mifupa Muhimbili kwa kushirikiana na daktari bingwa wa Mifupa kutoka hospitali ya Prashanth Chenai ya nchini India leo wamefanya upasuaji mkubwa na mgumu wa kibingwa wa kubadilisha kiungo cha nyonga (Complicated Total Hip Surgery) cha mgonjwa ambacho kimeharibika na hivyo kumsababishia mgonjwa kushindwa kutembea  na kupata maumivu makali.

Upasuaji huo umefanywa na jopo la madaktari bingwa wanne ambao wameongozwa na Dkt Mani Ramesh Kutoka India na Dkt Samweli Kitugi Nungu wa MOI ambapo upasuaji huo umefanyika kwa ufanisi na  kwa masaa matatu.

Read more

Maandalizi ya Mfumo wa Pamoja wa Kielektroniki wa Uondoshaji Shehena Yaanza

: Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Charles Kichere akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wa Wakuu wa Taasisi za Serikali wanaohusika na udhibiti wa mizigo Bandarini, Viwanja vya Ndege vya Kimataifa na Mipakani pamoja na wadau mbalimbali wa sekta binafsi kwa lengo la kuboresha utendaji kazi na ufanisi. Pamoja nae ni Kaimu Mkurugenzi wa TEHAMA kutoka Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) Mussa Shilla.

Na Veronica Kazimoto,TRA

Serikali imeanza maadalizi ya kutengeneza Mfumo wa Pamoja wa Kielektroniki wa Uondoshaji Shehena Bandarini, Viwanja vya Ndege vya Kimataifa na Mipakani kwa lengo la kuboresha utendaji kazi na ufanisi.

Akizungumza leo Jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wa Wakuu wa Taasisi za Serikali wanaohusika na udhibiti wa mizigo katika maeneo hayo na wadau mbalimbali wa sekta binafsi, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Charles Kichere amesema lengo la kuwashirikisha wakuu hao ni kujenga uelewa wa pamoja wa utekelezaji wa mfumo huo.

“Uwepo wenu katika mkutano huu ni muhimu sana kwasababu mtaweza kupitia mahitaji yote ya mfumo yaliyoandaliwa na watalaamu wetu ikiwa ni pamoja na maeneo ya kisheria, kiufundi na kibiashara ili muweze kuuboresha zaidi”, alisema Kichere. Read more

Wafanyabiashara Kutoka China Waridhishwa na Mazingira ya Uwekezaji Nchini

Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Prof. Elisante Ole Gabriel akifafanua jambo mbele ya waandishi wa Habari wakati wa mkutano wake na ujumbe wa Wafanyabiashara kutoka China leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Rais wa Chama cha Maendeleo ya Uchumi China – Asia (CAEDA), Huang Zhaojin na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uwekezaji (EPZA), Kanali Mstaafu Joseph Simbakali.

Read more