Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

FIFA Yakunwa na Utendaji wa Rais Magufuli

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimkabidhi zawadi ya Kinyango Rais wa Shirikisho la Mpira Duniani(FIFA)Bwana Gianni Infantino katika mkutano na waandishi wa Habari uliofanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu February 22/2017Jijini Dar es salaam Tanzania

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipokea Bandera ya FIFA kutoka kwa Rais wa Shirikisho la Mpira Duniani(FIFA)Bwana Gianni Infantino katika mkutano na waandishi wa Habari uliofanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu February 22/2017Jijini Dar es salaam Tanzania

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Rais wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), Gianni Infantino ameondoka nchini huku akionesha kufurahishwa na juhudi za Mhe. Rais John Pombe Magufuli katika kupambana na rushwa na ufisadi katika kujenga uchumi wa Tanzania.

Rais huyo wa FIFA alionyesha kuukubali utendaji wa Rais Magufuli wakati akiongea na jopo la wahariri wa habari za michezo nchini baada ya Mkutano wa Mkuu wa FIFA uliofanyika hapa nchini siku ya Alhamisi.

Infantino amesema moja ya mambo aliyokabiliana nayo alipoingia tu katika uongozi wake ni kupambana  na rushwa na ufisadi katika shirikisho hilo na hivyo juhudi zinazofanywa na Serikali ya Tanzania chini ya Rais Magufuli katika kupambana na rushwa zinamvutia sana.

Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Tanzania, Rwanda Zang’ara EAC Vita ya Rushwa

Na Mwandishi Wetu

MISIMAMO thabiti ya Rais John Pombe Magufuli katika masuala mbalimbali ya maendeleo ya Taifa imezidi kuleta mafanikio ambapo ripoti mpya katika mapambano dhidi ya rushwa imeonesha Rwanda na Tanzania kuongoza katika ukanda wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) katika mapambano dhidi ya rushwa kwa mwaka 2017.

Kwa mujibu wa Ripoti ya Tathmini ya Hali ya Rushwa (Corruption Perception Index) iliyotolewa jana Februari 21, 2018 na Taasisi ya Transparency International, juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano Tanzania chini ya Dkt. John Pombe Magufuli katika kupambana na rushwa zimezidi kuzaa matunda katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita.

Taarifa hiyo iliyokusanya takwimu za mwaka mzima wa 2017 zinaonesha kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi chache zilizopanda kwa kiasi kikubwa katika kupambana na rushwa huku nyingi nyingi zikishuka au kubaki pale pale.

Wakati mwaka 2016 Tanzania ilikuwa ya 116 duniani, katika ripoti hiyo mpya Tanzania imepanda kwa nafasi 13 na kuwa ya 103 huku ikizizidi kwa mbali nchi kadhaa kubwa duniani katika utafiti huo uliohusisha mataifa 180.

Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Makamu wa Rais Autaka Mkoa wa Simiyu Kuendeleza Mpango wa EQUIP-Tanzania

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongea na wadau wa Elimu Mkoani Simiyu, leo wakati wa Kongamano kubwa la Elimu ya Juu lililoandaliwa na Chuo Kikuu Huria Tanzania kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo.

 

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka akimuelezea Makamu wa Rais (hayupo pichani) namna utekelezaji wa mpango wa EQUIP-Tanzania unavyofanyika mkoani humo katika kongamano la Elimu ya Juu lililofanyika leo, mkoani humo.

Na: Mwandishi Wetu.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amewaagiza watalaamu wa elimu na viongozi wa Mkoa wa Simiyu kuhakikisha wanaendeleza Mpango wa Kuinua Ubora wa Elimu Tanzania (EQUIP-Tanzania) unaotekelezwa na Serikali kwa ushirikiano na Shirika la Maendeleo la nchini Uingereza (DFID).

Makamu wa Rais ametoa agizo hilo leo Mkoani Simiyu alipokuwa akiongea na viongozi na watumishi wa Serikali wa Mkoa huo  katika kikao cha majumuisho ya ziara yake ya siku tano mkoani humo.

“Mpango huu umekuwa na mafanikio makubwa kwa Mkoa wa Simiyu, kutokana na kuongezeka kwa kiwango cha ufaulu wa wanafunzi katika mitihani ya kitaifa ya darasa la Saba ambapo Mkoa umetoka kushika nafasi za mwisho Kitaifa hadi kufikia nafasi ya 11 mwaka 2017.

Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Tanzania Yaiunga Mkono FIFA Mapambano Dhidi ya Rushwa Michezoni

Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa akiongea na Waandishi wa Habari mara baada ya kukutana na mgeni wake, Rais wa Shirikisho la Soka Duniani, Gianni Infantino ambaye alimtembelea ofisini kwake jana Februari 22, 2018 (Picha na Anitha Jonas-WHUSM).

Na Mwandishi Wetu.

Katika juhudi za kuhakikisha kuwa mchezo wa soka unaendelea na kuheshimika duniani, Serikali ya Tanzania imesema itaendelea kuliunga mkono Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) katika mapambano yake dhidi ya rushwa na ubadhirifu katika sekta ya michezo.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa ameeleza hay oleo Februari 22, 2017 mara baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na Rais wa FIFA, Gianni Infantino ambaye alimtembelea Waziri Mkuu ofisini kwake jijini Dar es Salaam. Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Serikali Yaagiza Viwanda Nchini Kutumia Barcodes za GS1

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa akifungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Sita wa GS 1 Tanzania wa Watumiaji wa Barcodes nchini na Mkutano wa Saba wa Wadau uliofanyika Dar es Salaam, LEO Februar 22/2018.(PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

Na Mwandishi Wetu-Ofisi ya Waziri Mkuu

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameagiza kila kiwanda kilichopo nchini kihakikishe kinatumia alama za utambuzi za GS1 Tanzania simbomilia (barcodes).

Ametoa agizo hilo leo (Alhamisi, Februari 22, 2018) wakati akifungua Mkutano wa Sita wa Wamiliki wa Viwanda na Watumiaji wa simbomilia (barcodes). Hadi sasa GS1 ina wanachama 2000.

“Natoa wito kwa wenye viwanda kutumia GS1 Tanzania kutangaza na kuuza bidhaa zenye ubora katika maduka ya kimataifa, ambapo pia bidhaa zao zitachangia katika ulipaji wa kodi kwa usahihi”.

Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Rais Dkt. Magufuli Ametoa Wito kwa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Musimamia Vizuri Rasilimali

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia katika Mkutano huo Maalum wa Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) unaofanyika Kampala nchini Uganda.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta wakati wakielekea kwenye ukumbi wa Mkutano Maalum wa Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC unaojadili masuala mbalimbali ikiwemo Maendeleo ya Sekta ya Miundombinu na Afya.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amekaa pamoja na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais wa Uganda Yoweri Museveni wanne kutoka kulia, Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta pamoja na Rais wa Sudani ya Kusini Salva Kiir wakati wa mkutano huo Maalumu wa Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki unao endelea jijini Kampala.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ametoa wito kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kusimamia vizuri rasilimali walizonazo na kukusanya kodi vizuriili waweze kutekeleza miradi mikubwa ya ujenzi wa miundombinu na kuimarisha huduma za afya kwa wananchi.

Mhe. Rais Magufuli ametoa wito huo leo tarehe 22 Februari, 2018 mjini Kampala nchini Uganda wakati akichangia katika mkutano wa wakuu wa nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki unaojadili maendeleo na upatikanaji wa fedha kwa ajili ya miradi ya sekta ya miundombinu na afya.

Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Rais wa FIFA Awasili Nchi Leo Alfajiri

Waziri Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) akiwa na Rais wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) Gianni Infantino mara baada ya Rais huyo kuwasili nchini leo alfajiri kuhudhiria Mkutano wa FIFA. Infatino pia anatarajia kukutana na Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa.

Waziri Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akimtambulisha Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia kwa Rais wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) Gianni Infantino mara baada ya Rais huyo kuwasili nchini leo alfajiri kuhudhiria Mkutano wa FIFA. Infatino pia anatarajia kukutana na Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa.


FacebooktwittermailFacebooktwittermail