Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Upasuaji wa Kihistoria Wafanyika MOI Kwa Mafanikio.

Na Mwandishi wetu

Madaktari Bingwa wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa  Muhimbili  (MOI) kwa kushirikiana na Madaktari wa Hosipitali ya BLK  India leo wamefanya upasuaji maalum wa mgongo kwa kutumia matundu (Minimal Invasive Spine Surgery) kwa mgonjwa aliyedhoofika uti wa mgongo.

Kwa Mujibu wa Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa leo na Taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam, Upasuaji  huo umefanywa kwa mafanikio makubwa ukiwashirikisha Madakatari Bingwa wanne wakiongozwa na Profesa Joseph Kahamba wa MOI  na Dkt. Puneet Girdhan kutoka hosipitali ya BLK.

Taarifa hiyo imebainisha kuwa upasuaji huo umefanyika kwa mafanikio makubwa kwa muda wa masaa manne ambapo pamoja na upasuaji huo,  MOI imeanzisha huduma za upasuaji wa magoti kwa njia ya matundu ( Athroscopy ).

Read more

Wawekezaji Watakiwa Kuchangamkia Fursa Mkoani Kigoma.

Frank Mvungi- Maelezo, Dodoma

Serikali imetoa rai kwa wawekezaji kujitokeza kuwekeza katika  viwanda vya kuchakata samaki, madini ya chokaa na michikichi ili kuchochea ukuaji wa uchumi na Ustawi wa Wananchi na Taifa kwa Ujumla.

Akizungumza katika Kipindi cha TUNATEKELEZA kinachorushwa na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Mkuu wa Mkoa  huo Brigedia Jenerali (Mstaafu) Emmanuel Maganga amesema kuwa Mkoa huo una  mkakati wa kuanzisha viwanda vitatu (3) mpaka vitano (5) vya kuchambua pamba na katika kipindi cha miaka miwili kutakuwa na viwanda  vya kutengeneza bidhaa za pamba.

 

“Kichocheo Kikubwa cha maendeleo ni kuwepo kwa miundombinu ya barabara za lami,Reli na Bandari ambapo kwasasa Serikali inajenga barabara kutoka Nyakanazi hadi Kigoma, Kigoma hadi Tabora, Kigoma hadi Mpanda”

Read more

Nyongo Awataka Wachimbaji Wadogo Kuwajibika

Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo, akizungumza na wananchi na wachimbaji madini wadogo katika Mgodi wa Musasa uliopo Chato, akiwa katika ziara ya kazi inayoendelea Kanda ya Ziwa

Afisa Madini Mkazi wa Geita, Ally Maganga akitambulisha msafara wa Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (katikati), alipofika katika Machimbo ya Nyakafuru wilayani Mbogwe Mkoa wa Geita, akiwa katika ziara ya kazi inayoendelea Kanda ya Ziwa. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe, Martha Mkupasi.

Na Veronica Simba – Geita

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo amewataka wachimbaji wadogo wa madini nchini, kufahamu wajibu wao na kuutekeleza kikamilifu ili waendeshe shughuli zao kwa amani na tija.

Aliyasema hayo Februari 26 mwaka huu, alipotembelea na kuzungumza na wachimbaji wadogo wa Lwamgasa, Bingwa, Musasa na Nyakafuru katika Wilaya za Mbogwe na Chato, Mkoa wa Geita, akiwa katika ziara ya kazi inayoendelea Kanda ya Ziwa.

“Msiishie kulalamika tu. Jifunzeni kuwajibika kikamilifu katika nafasi zenu ili kazi zenu zilete tija na kuwanufaisha ninyi wenyewe, jamii na Taifa kwa ujumla.”

Read more

Waziri Mkuu Atembelea Mradi wa Ujenzi wa Chuo cha Walimu Kitangali

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipewa maelezo ya mradi wa ujenzi wa chuo cha walimu Kitangali na Mshauri wa mradi, Benson Mwemezi, wakati akikagua mradi huo uliopo katika Kata ya Maputi, Wilayani Newala, Februari 27, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Dkt Leonard Akwilapo, wakati alipo kagua mradi wa ujenzi wa chuo cha walimu Kitangali, uliopo katika Kata ya Maputi, Wilayani Newala, Februari 27, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Mgalu aonya matapeli miradi ya REA

Sehemu ya wakazi wa kata Zogoali katika wilaya ya Ilala wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (hayupo pichani).

Mmoja wa wakazi wa kata ya Bomba Mbili iliyopo Ilala jijini Dar es Salaam, Dkt. Isaya Madama akitoa kero yake mbele ya Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (hayupo pichani).

Na Greyson Mwase, Dar es Salaam

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu ametoa onyo kwa matapeli wanaojitokeza kwa kujifanya maafisa wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na kuwatoza wananchi fedha kama malipo ya kuunganishiwa huduma ya umeme.

Mgalu aliyasema hayo mwishoni mwa wiki  katika  mikutano aliyoifanya wakati wa ziara  yake katika  katika kata za Bomba Mbili, Mbondole,  Kiboga, Zogoali,  Kigezi Buyuni na Chanika zilizopo katika wilaya ya  Ilala nje kidogo ya Jiji la  Dar es Salaam.

Lengo la ziara yake lilikuwa ni kutembelea maeneo  ambayo hayajafikiwa  na miundombinu ya umeme, kuzungumza na wananchi na kuweka mikakati ya  namna ya kumaliza changamoto hizo kwa kushirikiana na REA na  Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO)

Read more

Makamu wa Rais amsaidia mkazi wa Salasala Kiti cha Magurudumu

Msaidizi wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Nehemia Mandia (kulia)akizungumza na Bi. Sidonia Ntibashigwa mkazi wa Machimbo ya Zamani Salasala kabla ya kumkabidhi Kiti cha Magurudumu kilichotolewa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Bi. Sidonia Ntibashigwa mkazi wa Livingstone , Machimbo ya Zamani akikabidhiwa kiti cha magurudumu alichosaidiwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Asilimia 95 ya Wananchi Kufikiwa na Huduma ya Maji Safi Ifikapo 2020.

Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Juma Aweso (Wapili kutoka kushoto) akiangalia maji yakiingia ndani ya tenki la kibamba lenye ujazo wa lita milioni 10 wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya Maji safi na Majitaka katika Wilaya ya Ubungo Jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Juma Aweso akinywa maji katika chanzo cha maji ya Kisima Hondogo wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya Maji safi na Majitaka inayoteklelezwa katika Wilaya ya Ubungo Jijini Dar es Salaam.

Na Mwandishi Wetu

Serikali imesema kuwa ifikapo mwaka 2020 itahakikisha asilimia 95 ya wakazi wote wanapata huduma ya majisafi mijini ili kuchochea ukuaji wa uchumi na ujenzi wa Viwanda hapa nchini.

Akizungumza wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya majisafi na majitaka inayotekelezwa na kusimamiwa na Serikali katika Wilaya ya Ubungo Jijini Dar es Salaam Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso amesema kuwa  Wizara yake itahakikisha kuwa lengo la kuwafikisahia wananchi wote huduma ya maji linafikiwa kwa wakati.

“Kama kuna madai yoyote ya wakandarasi na mna uhakika kuwa kazi imefanyika kwa mujibu wa mkataba yaleteni Wizarani nasi hatutakawia kuyalipa”  Alisisitiza Mhe. Aweso

Akifafanua Mhe Aweso alisema  kuwa Wizara ya Maji kamwe haiwezi kuwa kikwazo cha utekelezaji wa miradi ya maji hivyo imejipanga vyema kuendana na kasi ya Serikali ya Awamu ya Tano katika utekelezaji wa miradi ya maji.

Read more

Asilimia 95 ya Wananchi Kufikiwa na Huduma ya Maji Safi Ifikapo 2020.

Na Mwandishi Wetu

Serikali imesema kuwa ifikapo mwaka 2020 itahakikisha asilimia 95 ya wakazi wote wanapata huduma ya majisafi mijini ili kuchochea ukuaji wa uchumi na ujenzi wa Viwanda hapa nchini.

Akizungumza wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya majisafi na majitaka inayotekelezwa na kusimamiwa na Serikali katika Wilaya ya Ubungo Jijini Dar es Salaam Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso amesema kuwa  Wizara yake itahakikisha kuwa lengo la kuwafikisahia wananchi wote huduma ya maji linafikiwa kwa wakati.

“Kama kuna madai yoyote ya wakandarasi na mna uhakika kuwa kazi imefanyika kwa mujibu wa mkataba yaleteni Wizarani nasi hatutakawia kuyalipa”  Alisisitiza Mhe. Aweso

Akifafanua Mhe Aweso alisema  kuwa Wizara ya Maji kamwe haiwezi kuwa kikwazo cha utekelezaji wa miradi ya maji hivyo imejipanga vyema kuendana na kasi ya Serikali ya Awamu ya Tano katika utekelezaji wa miradi ya maji.

Read more

Dodoma Yatekeleza kwa Vitendo Dhana Ujenzi wa Uchumi wa Viwanda

Frank     Mvungi- Maelezo, Dodoma

Mkoa wa Dodoma umefanikiwa kujenga viwanda 892 vingi kati ya hivyo vikiwa ni Vidogo na vya Kati ambavyo vinachochea ukuaji wa uchumi  ikiwa ni sehemu ya mkakati wa Serikali kutekeleza dhana ya ujenzi wa uchumi wa viwanda.

Akizungumza katika Kipindi maalum cha TUNATEKELEZA kinachorushwa na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC)  Mkuu wa Mkoa wa Dodoma  Mhe. Dkt. Binilith  Mahenge amesema kuwa Mkoa huo umejipanga vyema kama Makao Makuu ya Nchi kuhakikisha kuwa dhana ya Ujenzi wa Uchumi wa Viwanda inatekelezwa na wananchi wote kwa vitendo .

 Akifafanua zaidi Dkt. Mahenge amesema kuwa Dodoma ni mahali salama na kuna maeneo yakutosha kwa ajili ya uwekezaji hivyo wawekezaji wote wa ndani na nje ya nchi wanakaribishwa kuja kuwekeza.

Read more