Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Serikali Yaazimia Kuboresha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji Nchini

Na: Mwandishi Wetu

Serikali imeazimia kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini kwa kuweka mifumo ya kielektroniki katika utoaji wa huduma ili kuongeza ufanisi katika utendaji wa kazi na kuondoa urasimu usio wa lazima .

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa mapangokazi baina ya Sekta ya Umma na Sekta binafsi Prof. Faustin Kamuzora alisema leo tarehe 30 Januari, 2018 katika Ukumbi wa Mikutano wa JNICC Dar es Salaam, mkutano huu ni ushahidi kwamba Serikali na Sekta Binafsi ni wadau muhimu katika kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii na kwamba mazingira wezeshi ya biashara ni kichocheo muhimu katika jitihada za Serikali kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi. Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Umri wa Kustaafu Kwa Madaktari Bingwa, Wahadhiri Waandamizi na Maprofesa Sasa miaka 65.

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Tulia Ackson akisoma dua ya kuliombea Bunge katika kikao cha kwanza cha Mkutano wa kumi wa Bunge hilo leo Mjini Dodoma.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi,Ajira,Vijana na Wenye ulemavu Mhe.Jenista Mhagama akizungumza jambo na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.Dkt.Suzan Kolimba na Naibu Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi Mhe.Angeline Mabula wakati wa kikao cha kwanza cha Mkutano wa kumi wa Bunge hilo leo Mjini Dodoma.

Frank Mvungi- Maelezo, Dodoma.

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepitisha muswaada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria mbalimbali ikiwemo sheria ya Utumishi wa Umma, Sura ya 298  (The Public Service Act) itakayowezesha muda wa kustaafu kwa  Wahadhiri waandamizi, Maprofesa na Madaktari Bingwa kuwa miaka 60 kwa hiari na lazima miaka 65.

Akizungumza wakati akiwasilisha muswaada huo  Mwanasheria  Mkuu wa Serikali Mhe. George Masaju amesema kuwa marekebisho katika jedwali yanapendekeza kuongezwa kwa kifungu kipya cha 25A ambacho kinaainisha kuhusu umri wa kustaafu ambapo kwa sasa sheria ilivyo  haina masharti hayo isipokuwa umri wa kustaafu umetajwa katika sheria zinazoanzisha mifuko ya hifadhi za jamii.

Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Matukio Katika Picha Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Akiwa Addis Ababa

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia Mhe Naimi Aziz, nje ya ukumbi wa Nelson Mandela mjini Addis Ababa, Waziri Mkuu yupo Nchini Ethiopia, kumwakilisha Rais John Pombe Magufuli kwenye Mkutano wa Viongozi Wakuu wa Nchi za Umoja wa Afrika AU.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri Mkuu Mstaafu Salim Ahmed Salim, wakati alipo mtembelea kwenye Hoteli ya Radisson Blue, mjini Addis Ababa Ethiopia. Januari 30, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Utoaji wa takwimu bora, chanzo cha matokeo chanya ya maendeleo.

Na: Mwandishi Wetu

Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) imekanusha tetesi kwamba sheria ya takwimu ya mwaka 2015 inazuia takwimu zinazofanywa na wanafunzi wa vyuo vikuu hapa nchini na kusema kuwa sheria hiyo haihusiki kabisa kwani vyuo vikuu wana sheria zao zinazowasimamia na kuwaongoza katika utoaji wa takwimu.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt Albina Chuwa alipokuwa akizungumza leo na wadau mbalimbali wa takwimu jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wa  semina ya siku moja kuhusiana na uelewa wa matumizi wa sheria ya takwimu namba 9 ya mwaka 2015 iliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Mwalimu Julius Nyerere.

Akiendelea kuzungumza na wadau hao wa takwimu Dkt chuwa amesema kuwa ofisi ya takwimu ni tasnia kama zilivyo tasnia nyingine za kiserikali hivyo utoaji wa takwimu siyo suala jepesi kwani ni jambo linalohitaji kufuata na kuzingatia sheria katika utoaji wa takwimu hizo.

“Ofisi ya takwimu ni tasnia kama zilivyo tasnia nyingine za kiserikali kama vile asasi za kiraia na nyinginezo, hivyo utoaji wa takwimu siyo suala jepesi kwani ni jambo linalohitaji kufuata na kuzingatia sheria katika utoaji wa takwimu hizo” amesema Dkt Chuwa.

Pia amesema kuwa matumizi ya takwimu zilizo rasmi wigo wake umekuwa mpana zaidi na utoaji wa takwimu bora kunasaidia na kuleta matamanio ya kuondokana na wimbi la umaskini na kuongeza kuwa serikali inayotaka matokeo chanya katika safari ya maendeleo ni lazima kufuata takwimu zilizo bora na rasmi.

“utoaji wa takwimu bora kunasaidia na kuleta matamanio ya kuondokana na wimbi la umaskini na kuongeza kuwa serikali inayotaka matokeo chanya katika safari ya maendeleo ni lazima kufuata takwimu zilizo bora na rasmi” amesema Dkt Chuwa.

Aidha amebainisha kuwa kutokana na changamoto mbalimbali ambazo zimejitokeza baada ya kupitishwa kwa sheria ya takwimu ya mwaka 2015 sasa jukumu kubwa la ofisi ya takwimu ni kuratibu na kusimamia mfumo mzima wa ukusanyaji na utoaji wa takwimu zilizo bora na rasmi.

 

 

 

 

 

 

 


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Bodi ya Filamu Yamaliza Mzozo Malipo Filamu ya Utu Wangu

Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania (KBF) Bibi. Joyce Fissoo akipitia nyaraka za makubaliano ya mauziano ya Filamu ya Utu Wangu baina ya Mtayarishaji wa Filamu hiyo Bi. Sikujua Mbwembwe (hayupo pichani) na Kampuni ya Steps Entertainment wakati wa kikao cha usuluhishi leo jijini Dar es Salaam. Kikao hicho kimefanyika katika Ofisi za Bodi ya Filamu kufuatia mlalamikaji ambaye ni mtayarishaji wa filamu hiyo kufikisha malalamiko ya kutolipwa haki yake tangu mwaka 2015.

Na: Mwandishi Wetu

Hatimaye Bodi ya Filamu nchini imerejesha furaha kwa msanii na mtayarishaji wa filamu ya Utu Wangu kufuatia kuongoza kikao cha usuluhishi kilichofikia muafaka  kwa msanii huyo kulipwa stahiki zake.

Hayo yamejitokeza leo wakati wa kikao cha usuluhishi wa madai ya Msanii  Sikujua Mbwembe mtayarishaji wa Filamu ya Utu Wangu dhidi ya Kampuni ya Steps Entertainment  kilichofanyika katika ofisi za Bodi hiyo leo jijini Dar es Salaam. Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Prof. Mbarawa Afungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi Shirika la Posta

Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania (TPC), Dk. Haruni Kondo (wa pili kulia), akibadilishana mawazo na Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa TPC, Joseph Ngowi (kulia), wakati wakimsubiri mgeni rasmi, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa. Katikati ni Kaimu Postamasta Mkuu, Hassan Mwang’ombe.Wengine kushoto ni Maofisa waandamizi kutoka wizarani.

Kaimu Postamasta Mkuu, Hassan Mwang’ombe akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Shirika la Posta, ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, jijini Dar es Salaam leo. Wa pili kulia ni mgeni rasmi, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa.

Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Rais Magufuli Akutana na Dkt. Slaa, Awaaga Maafisa wa JWTZ

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Balozi Mteule Dkt. Wilbrod Slaa kabla ya kuanza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Balozi Mteule Dkt. Wilbrod Slaa Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na mgeni wake Balozi Mteule Dkt. Wilbrod Slaa kabla ya kuzungumza na wanahabaari Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Balozi Mteule Dkt. Wilbrod Slaa mara baada ya kuzungumza na wanahabari Ikulu jijini Dar es Salaam.

 

Balozi Mteule Dkt. Wilbrod Slaa akizungumza na Wanahabari mara baada ya kuzungumza na wanahabari Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wanahabari mara baada ya kufanya mazungumzo na Balozi Mteule Dkt. Wilbrod Slaa Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Balozi Mteule Dkt. Wilbrod Slaa mara baada ya kuzungumza na wanahabari Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini (CDF) Jenerali Venance Mabeyo kabla hajaanza kuwatambulisha Maafisa Wakuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (hawaonekani pichani) ambao wanatarajia kustaafu.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini (CDF) Jenerali Venance Mabeyo ambaye aliambatana na Maafisa Wakuu (sita) wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania ambao wanatarajiwa kustaafu.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini (CDF) Jenerali Venance Mabeyo pamoja na Maafisa Wakuu (sita) wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania wanaotarajiwa kustaafu ambao ni Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi wa Tanzania Luteni Jenerali James Mwakibolwa wanne kutoka (kulia), Meja Jenerali Michael Isamuhyo watatu kutoka (kulia) Brigedia Jenerali Aron Robert Lukyaa wapili kutoka (kulia), Kanali Peter Samuel Sameji wa kwanza (kulia). Wengine katika picha ni Brigedia Jenerali William Ephraim Kivuyo wapili kutoka kushoto na Brigedia Jenerali Elizaphani Lutende Marembo.(Picha na Ikulu)


FacebooktwittermailFacebooktwittermail