Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Wafanyakazi wa JKCI Wapewa Mafunzo na Kampuni ya Medtronic ya Mfumo wa Umeme wa Moyo

Madaktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwtete (JKCI) Peter Kisenge na Prof. Ahmed Osman wa Broward General Medical Centre ya nchini Marekani wakimfanyia mgonjwa upasuaji wa Moyo wa bila kufungua kifua na kumuwekea kifaa maalum cha kuusaidia moyo kufanya kazi vizuri (pace maker) ikiwa ni sehemu ya mafunzo kwa vitendo yaliyoandaliwa na kampuni ya Medtronic tawi la Kenya ambao ni watengenezaji wa vifaa tiba vya magonjwa ya Moyo.

Read more

Rais Dkt Magufuli Amjulia Hali Msanii Mkonge King Majuto Hospitalini Dar es Salaam Leo

Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akimjulia hali msanii mkongwe Amri Athumani maarufu kama King Majuto aliyelazwa katika hospitali ya Tumaini jijini Dar es salaam leo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimjulia hali msanii mkongwe Amri Athumani maarufu kama King Majuto aliyelazwa katika hospitali ya Tumaini jijini Dar es salaam leo

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mkewe Mama Janeth Magufuli wakimjulia hali msanii mkongwe King Amri Athumani maarufu kama Majuto aliyelazwa katika hospitali ya Tumaini jijini Dar es salaam leo. (Picha na Ikulu)

Basata Yazindua Chama cha Wanamitindo Tanzania

Mwanzilishi wa Chama cha Wanamitindo Tanzania (FAT) Mustafa Hassanali (kulia) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa chama hicho mapema hii leo jijini Dar es Salaam, katikati ni Katibu Mtendaji toka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Godfrey Mngereza na kushoto ni Mwanamitindo mkongwe nchini Bi. Asia Idarous.

Na: Nyakongo Manyama

BARAZA la Sanaa la Taifa (BASATA) kwa kushirikiana na wabunifu wa Tanzania wamezindua Chama cha Mitindo Tanzania (FAT) kitakachowaunganisha wabunifu wote hatua inayolenga kuinua na kuiongezea hadhi sekta ya mitindo nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam Katibu  Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa  (BASATA) Bw. Godfrey Mngereza  amesema sekta ya mitindo nchini ikiimarishwa itaweza kuleta mapinduzi makubwa kwa kuzalisha ajira kwa vijana.

“Katika kuunga mkono juhudi za Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika kujenga Tanzania ya viwanda, tasnia ya ubunifu wa mavazi, tumeamua kulima pamba ambayo ndiyo itakayozalisha mavazi, hivyo kusingekuwa na wabunifu hatungekuwa na mavazi yenye utamaduni wa Tanzania” alisema Mungereza Read more

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Aongoza Kikao cha Baraza la Usimamizi wa Maafa Tanzania

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Prof. Fautin Kamuzora akifungua Kikao cha Baraza la Usimamizi wa maafa Tanzania kilichofanyika mapema leo mjini Dodoma, kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Maafa Bw. Bashiri Taratibu, na kushoto ni Muwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Kanali Jimmy Said.

Na. Mwandishi Wetu

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera na Uratibu Profesa Faustin Kamuzora ameongoa kikao cha Siku moja cha Baraza la Usimamizi wa Maafa nchini kinacholenga kujadili masuala ya Menejimenti ya Maafa.

Akifungua kikao hicho alisema kuwa Serikali imejipanga kuhakikisha inadhibiti na kuweka miundombinu rafiki ili kukabili maafa yanayotokea nchini.

Akifafanua Profesa Kamuzora amebainisha kuwa moja ya hatua zilizochukuliwa na Serikali ni kuunda Kikosi kazi cha Taifa kitakachoshughulikia tatizo la sumukuvu, uwepo wa panya wanaoharibu mazao, viwavi jeshi na kwelea kwelea wanao haribu mazao. Read more

Rais Dkt Magufuli Azindua Pasipoti Mpya ya Tanzania ya Kielektronikia

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akionesha kwa furaha passipoti yake mpya ya kielektronikia baada ya kuipokea kutoka kwa Waziri wa mambo ya Ndani Dkt. Mwigulu Nchemba makao makuu ya Idara ya Uhamiaji Kurasini jijini Dar es salaam leo Januari 31, 2018. Kushoto ni Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein na kushoto kwa Waziri ni Kamishna Mkuu wa Uhamiaji Dkt. Anna Peter Makakala.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akionesha kwa furaha passipoti yake mpya ya kielektronikia baada ya kuipokea kutoka kwa Waziri wa mambo ya Ndani Dkt. Mwigulu Nchemba makao makuu ya Idara ya Uhamiaji Kurasini jijini Dar es salaam leo.

Read more