Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Wakulima Wataka Pamba Yao Inunuliwe kwa Fedha Taslimu.

Na Tiganya Vincent, RS-Tabora

Baadhi ya wakulima wa Pamba wilayani Nzega wameiomba Serikali kudhibiti mtindo wa Kampuni ambazo zimekuwa na tabia ya kukopa mazao ya wakulima kwani vitendo hivyo vimekuwa vikiwakatisha tamaa.

Kauli hiyo ilitolewa jana Wilayani Nzega na baadhi ya wakulima wakati wa Mkutano na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri alipokuwa katika ziara ya kukagua mashamba ya pamba katika kwenye maeneo ili kujionea kama wamezingatia kanuni za kilimo cha zao hilo.

Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Taarifa kwa Umma.

WAZIRI MKUU AWAPOKEA WANACHAMA 60 WA CUF.

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amepokea wanachama wapya 60 kutoka Chama cha Wananchi (CUF) ambao wameamua kurejea Chama cha Mapinduzi (CCM).

Wanachama hao wamepokelewa leo mchana (Ijumaa, Desemba 29, 2017) kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kijiji cha Nkowe kata ya Nkowe, wilayani Ruangwa mkoani Lindi.

Kabla ya kuwakabidhi kadi za CCM, Waziri Mkuu alipokea kadi za CUF kutoka kwa vijana saba kwa niaba ya wenzao 60. Vijana hao ni Hamisi Juma, Fatuma Abdallah, Mwajuma Mohammed, Thomas Moto, Zainab Nachiluku, Samia Said na Juma Said.

Vijana hao saba waliokabidhiwa kadi mpya za CCM pamoja na wenzao 53, walikula kiapo cha uaminifu.

Kwa mujibu wa Katibu wa CCM wa wilaya hiyo, Bw. Barnabas Essau wanachama wote ni vijana ambao wanajishughulisha na shughuli mbalimbali na wameridhishwa na utendaji wa Serikali ya awamu ya tano.

Bw. Essau alisema wanachama hao wote wametoka vijiji vya Kipindimbi, Nkowe na Mpumbe.

Novemba 5, mwaka huu, Waziri Mkuu alipokea wanachama 37 kutoka vyama vya CUF na CHADEMA kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kijiji cha Mbekenyera, wilayani Ruangwa.

 

IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU, 

IJUMAA, DESEMBA 29, 2017.

 

 


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Deni la Taifa Liko Chini ya Ukomo wa Hatari – Dkt. Mpango

Waziri wa Fedha na Mipango wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Phillip Mpango akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu hali ya uchumi kwa mwaka 2017 leo Jijini Dar es Salaam.

Na. Paschal Dotto.

Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango imewatoa hofu wananchi kuhusu uvumi wa kuongezeka kwa deni la Taifa kwamba deni hilo ni himilivu na liko chini ya ukomo wa hatari.

Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam  na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philipo Mpango wakati akitoa mwenendo wa  hali ya uchumi na utekelezaji wa bajeti  ya Serikali kwa mwaka 2017/2018 .

Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Serikali Yasikia Kilio cha Wadau wa Sekta ya Uwindaji wa Kitalii Nchini,

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na
wadau wa sekta ya uwindaji wa kitalii katika mkutano uliondaliwa na Wizara yake
mjini Dodoma jana kwa ajili ya kujadili mikakati mbalimbali ya kuimarisha sekta
hiyo ikiwemo utekelezaji wa azma ya Serikali ya kuanzisha utaratibu mpya wa
utoaji wa leseni za vitalu vya uwindaji wa kitalii kwa njia ya mnada. Kushoto
ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mej. Jen. Gaudence Milanzi na Naibu Katibu Mkuu,
Dk. Aloyce Nzuki (kulia).
 
Na Hamza Temba, Dodoma
Serikali imesikia kilio cha wadau wa sekta ya uwindaji wa
kitalii nchini na kuamua kuongeza muda wa miaka miwili ya umiliki wa leseni za vitalu
95 vya uwindaji wa kitalii ambazo zilikuwa ziishe muda wake tarehe 31 Desemba
mwaka huu (2017).
 
Uamuzi huo umetolewa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk.
Hamisi Kigwangalla wakati wa kikao cha majumuisho na watendaji wa Wizara hiyo
muda mfupi baada ya kumalizika kwa mkuano wa wadau wa sekta hiyo ulioandaliwa
na Wizara hiyo mjini Dodoma jana.
 
Akizungumzia uamuzi huo Dk. Kigwangalla alisema, lengo ni kuwapa
muda wawekezaji hao ili waweze kujiandaa na mabadiliko ya mfumo mpya wa utowaji
wa leseni za vitalu vya uwindaji wa kitalii kwa njia ya mnada ikiwemo kurudisha
baadhi ya gharama za uwekezaji walizoweka katika vitalu hivyo.
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali
Gaudence Milanzi (kushoto) akizungumza katika mkutano huo. Kulia ni Waziri wa
Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla.
Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Kampuni za Uwindaji wa Kitalii nchini,
Michael Mantheakis (kulia) akiwasilisha mapendekezo yake katika mkutano wa wadau
wa sekta ya uwindaji wa kitalii katika mkutano uliondaliwa na Wizara ya
Maliasili na Utalii mjini Dodoma jana kwa ajili ya kujadili mikakati mbalimbali
ya kuimarisha sekta hiyo ikiwemo utekelezaji wa azma ya Serikali ya kuanzisha
utaratibu mpya wa utoaji wa leseni za vitalu vya uwindaji wa kitalii kwa njia ya
mnada.

Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Mgodi wa ZEM Wapewa Siku Saba Kutoa Vifaa vya Kujikinga

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (wa pili kushoto) akitembelea Mgodi wa Dhahabu wa ZEM Tanzania Company Limited alipofanya ziara mgodini hapo kujionea shughuli ziazoendelea. wa pili kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Butiama Annarose Nyamubi.

Serikali imetoa siku Saba kwa Mgodi wa Dhahabu wa ZEM (T) Company Ltd wa Nyasirori Wilayani Butiama kuwapatia vifaa vya kujikinga kazini wafanyakazi wa mgodi huo vinginevyo mgodi utafungwa.

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo ametoa agizo hilo Desemba 27, 2017 alipofanya ziara kwenye mgodi huo kujionea shughuli zinazoendelea mgodini hapo na kuzungumza na wafanyakazi na wananchi wanaozunguka maeneo jirani na mgodi huo.

Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Taarifa kwa Umma.

VIPAUMBELE VYA SEKTA YA ELIMU KAMA ILIVYOAINISHWA KATIKA ILANI YA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) 2015/20 NA MPANGO WA MAENDELEO WA MIAKA MITANO 2015/2020

 

Ilani ya CCM inaipa kipaumbele Sekta ya Elimu umuhimu wa kipekee ili kuiendeleza sekta hii. Katika kipindi cha miaka mitano ijayo (2015-2020), CCM itahakikisha Serikali inasimamia Utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 kwa kutekeleza yafuatayo:-

  1. Kuandaa mfumo, muundo na taratibu nyumbufu za kutoa Elimu ya Awali na Elimumsingi (1+6+4) bila malipo ili kuhakikisha kwamba:-

 

  • Uandikishwaji rika lengwa la watoto wa darasa la Elimu ya Awali unaongezeka kutoka asilimia 45 mwaka 2015 hadi asilimia 100 mwaka 2020
  • (ii) Uandikishwaji rika lengwa la watoto wa Darasa la Kwanza unaongezeka kutoka asilimia 95 mwaka 2015 hadi asilimia 100 mwaka 2020; na
  • (iii) Uandikishwaji rika lengwa la Wanafunzi wa Kidato cha Kwanza unaongezeka kutoka asilimia 60 mwaka 2015 hadi asilimia 80 mwaka 2020.
  1. Kuhuisha taratibu za kujiunga na taasisi zinazotoa Elimu na Mafunzo katika ngazi mbalimbali kwa kutambua sifa zinazopatikana katika mifumo na Taasisi tofauti ili kuhakikisha kwamba:-

Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa Ziarani Ruangwa

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Lindi Godfrey Zambi, alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Nachingwea, kwa ajili ya mapumziko ya mwisho wa mwaka ambapo aliamua kukagua miradi ya maendeleo jimboni kwake wilayani Ruangwa, mkoani Lindi leo.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na mwananchi wa kijiji cha Mibure, Mzee Menrad Kilian, baada ya kukagua ujenzi wa zahanati kijijini hapo, wilayani Ruangwa mkoani Lindi leo.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mibure, wakati alipoenda kukagua ujenzi wa zahanati ya kijiji hicho Desemba 28, 2017. Waziri Mkuu yupo jimboni kwake kwa mapumziko ya mwisho wa mwaka.

Mkurugenzi Mtendaji wa KALIF Construction, Ally Mohamed Libaba akitoa maelezo kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (katikati) wakati wakijaribu kuvuta maji kutoka kwenye pampu ya mradi wa maji wa kijiji cha Namakuku, Desemba 28, 2017. Wa kwanza kulia ni msimamizi wa mradi huo, Bw. Fadhil Ally Libaba. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


FacebooktwittermailFacebooktwittermail