Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Sekretarieti ya Maadili ya Umma Yapongezwa kwa Kuwajali Wateja Wake

Afisa wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma akikagua fomu ya tamko la rasilimali na madeni iliyowasilishwa na mmoja wa viongozi wa umma katika ofisi za Sekretarieti hiyo Jijini Dar es Salaam leo. . Leo ndiyo siku ya mwisho ya kuwasilisha fomu hizo ambapo kila kiongozi aliyetajwa katika sheria husika analazimika kuwa amewasilisha fomu yake.

Afisa wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma akimuelekeza jambo mmoja wa viongozi wa umma aliyefika katika ofisi za Sekretarieti hiyo kwa ajili ya kuwasilisha fomu yake ya tamko la rasilimali na madeni leo Jijini Dar es Salaam. . Leo ndiyo siku ya mwisho ya kuwasilisha fomu hizo ambapo kila kiongozi aliyetajwa katika sheria husika analazimika kuwa amewasilisha fomu yake.

Afisa wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma akikagua fomu ya tamko la rasilimali na madeni iliyowasilishwa na Mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki Mhe. Omary Mkumba katika ofisi za Sekretarieti hiyo Jijini Dar es Salaam leo. . Leo ndiyo siku ya mwisho ya kuwasilisha fomu hizo ambapo kila kiongozi aliyetajwa katika sheria husika analazimika kuwa amewasilisha fomu yake.

Mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki Mhe. Omary Mkumba akisaini fomu yake ya tamko la rasilimali na madeni mara baada ya kuwasilisha na kukaguliwa na Afisa wa Sektretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma leo Jijini Dar es Salaam. Leo ndiyo siku ya mwisho ya kuwasilisha fomu hizo ambapo kila kiongozi aliyetajwa katika sheria husika analazimika kuwa amewasilisha fomu yake. (Picha na: MAELEZO)

Rais Dkt. Magufuli Asali Ibada ya Familia Takatifu Katika Kanisa la Mtakatifu Petro Jijini Dar Es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akishukuru mara baada ya kushiriki Sakramenti Takatifu katika Ibada ya Jumapili ya Familia Takatifu iliyofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitakiana Heri na Masista walioshiriki katika Ibada ya jumapili ya Familia Takatifu katika Kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Paroko Msaidizi wa Kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay Fr. Asis Mendokta mara baada ya Ibada ya jumapili ya Familia Takatifu katika Kanisa hilo jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na waumini wa Kanisa la Katoliki la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es Salaam mara baada ya Ibada ya jumapili ya Familia Takatifu katika Kanisa hilo jijini Dar es Salaam. (Picha na Ikulu)

 

Mke wa Mwanri Ataka Wananchi Kuunga Mkono Juhudi za Viongozi

Na. Tiganya Vicent, RS TABORA

Wakazi wa Mkoa wa Tabora wametakiwa kuhakikisha wanaunga mkono juhudi za viongozi mbalimbali mkoani humo katika kampeni za upandaji miti badala ya kuwakatisha tamaa kwa kuichoma moto na kuing’oa miti hiyo.

Kauli hiyo ilitolewa jana mjini Tabora na Mke wa Mkuu wa Mkoa huo ,Bibi Grace Mwanri wakati wa zoezi la upandaji miti maji 500 iliyotolewa na Kampuni ya Usambazaji wa Gesi ya Manji’s kwa ajili ya kuungana na uongozi wa Mkoa wa Tabora katika kampeni ya kuifanya Tabora iwe ya kijana katika kipindi kifupi.

Alisema vitendo vya kuhujumu miti vinavyofanywa na baadhi ya wakazi wa Tabora kwa kuichoma na kuing’oa na wengine kuikanyaga na magari  vinaweza kuvunja moyo jitihada za viongozi wa mkoa huo. Read more

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Azuru Hifadhi ya Saadani

1. Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (katikati) akioneshwa ramani ya Hifadhi ya Taifa ya Saadani na Mwakilishi wa Mkuu wa Hifadhi za Taifa, Vitalis Kuluka huku akishirikiana kuonesha eneo hilo na Katibu Tawala wa Wilaya ya Bagamoyo,Erica Yigella ( wa pili kulia) mahali kilipo Kitongoji cha Uvinje ambapo wakazi wa eneo hilo wamegoma kuhama ndani ya hifadhi hiyo na wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea hifadhi hiyo jana. Wa kwanza kulia ni Afisa Wanyamapori, Godfrey Maro na Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Saadani, Stephano Msumi na pande wa kulia nyuma ya Katibu Tawala ni Msaidizi wa Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi za Taifa, Fredrick Mofulu

1. Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (katikati) akioneshwa ramani ya Hifadhi ya Taifa ya Saadani na Mwakilishi wa Mkuu wa Hifadhi za Taifa, Vitalis Kuluka huku akishirikiana kuonesha eneo hilo na Katibu Tawala wa Wilaya ya Bagamoyo,Erica Yigella ( wa pili kulia) mahali kilipo Kitongoji cha Uvinje ambapo wakazi wa eneo hilo wamegoma kuhama ndani ya hifadhi hiyo na wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea hifadhi hiyo jana. Wa kwanza kulia ni Afisa Wanyamapori, Godfrey Maro na Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Saadani, Stephano Msumi na pande wa kulia nyuma ya Katibu Tawala ni Msaidizi wa Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi za Taifa, Fredrick Mofulu

Read more