Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Mhe. Samia Suluhu Hassan Amjulia Hali Tundu Lissu

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 28 Novemba, 2017 amemjulia hali Mbunge wa Singida Mashariki Mhe. Tundu Lissu anayepata matibabu katika hospitali ya Nairobi nchini Kenya.
Mhe. Samia Suluhu Hassan amemfikishia salamu za pole kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ambaye amemtakia matibabu mema na kupona haraka ili arejee nyumbani na kuendelea na majukumu yake.
Mhe. Tundu Lissu amemshukuru Mhe. Rais Magufuli na Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kumjulia hali na amewatakia heri katika majukumu yao.
“Msalimu Mhe. Rais mwambie namshukuru sana kwa salamu zake na kunijulia hali” amesema Mhe. Tundu Lissu.


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Tutawashughulikia Wote Wanaotumia Vibaya Fedha Ukimwi-Majaliwa

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akihutubia alipokuwa akifungua kongamano la Kitaifa la Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani, lililofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) leo jijini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akihutubia alipokuwa akifungua kongamano la Kitaifa la Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani, lililofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) leo jijini Dar es Salaam.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Mama Samia Suluhu Hassan Amwakilisha Rais Dkt. Magufuli Sherehe za Uapisho wa Rais Kenyatta

Makamu wa Rais akimpongeza Rais Kenyatta kwa kuapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya kenya katika uwanja wa Moi Kasarani Mjini Nairobi. Mhe. Samia Suluhu Hassan amemwakilisha Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan (wa tatu kulia) akiwa pamoja na viongozi wengine wa nchi mbalimbali waliohudhulia katika Sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Jamhuri ya Kenya, Rais Uhuru Kenyatta iliyofanyika leo kwenye uwanja wa Moi Kasarani Mjini Nairobi, Kenya. Mhe. Samia Suluhu Hassan amehudhulia sherehe hizo akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli. Picha na Ikulu.

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan akimpongeza Rais Uhuru Kenyatta kwa kuapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Kenya kwa awamu ya pili, katika Sherehe zilizofanyika leo kwenye uwanja wa Moi Kasarani Mjini Nairobi, Kenya. Mhe. Samia Suluhu Hassan amehudhulia sherehe hizo akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Masauni, Dk. Makakala Wazungumza na Wavuvi Mkoani Mara

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na wananchi wanaoishi na kufanya shughuli zao za uvuvi Ziwa Victoria, katika kijiji cha Nyang’ombe kilichopo wilayani Rorya, Mkoani Mara.Katika ziara hiyo Naibu Waziri aliambatana na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dk. Anna Makakala ikiwa na lengo la udhibiti uhalifu na uingiaji wa kinyume na sheria kwa raia kutoka nchi jirani.

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dk. Anna Makakala , akizungumza na wananchi wanaoishi na kufanya shughuli zao za uvuvi Ziwa Victoria katika kijiji cha Nyang’ombe kilichopo wilayani Rorya, mkoani Mara. Lengo la ziara hiyo ni kudhibiti uhalifu na kudhibiti uingiaji wa kinyume na sheria kwa raia kutoka nchi jirani.

Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima, akizungumza na wananchi wanaoishi na kufanya shughuli zao za uvuvi Ziwa Victoria katika kijiji cha Nyangombe, kilichopo wilayani Rorya, mkoani Mara. Lengo la ziara hiyo ni kudhibiti uhalifu na kudhibiti uingiaji wa kinyume na sheria kwa raia kutoka nchi jirani.

Mwananchi wa kijiji cha Nyang’ombe akiuliza maswali kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni, wakati wa ziara ya kikazi ambapo naibu waziri aliongozana na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dk. Anna Makakala, lengo la ziara hiyo ni kukagua udhibiti uhalifu na uingiaji wa kinyume na sheria kwa raia kutoka nchi jirani.

Wananchi wakishangilia jambo wakati Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni (hayupo pichani), akizungumza katika mkutano uliofanyika kijiji cha Nyang’ombe ,wilayani Rorya. Naibu Waziri yupo katika ziara ya kikazi ikiwa na lengo la kukagua udhibiti uhalifu na uingiaji wa kinyume na sheria kwa raia kutoka nchi jirani.(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Kituo cha Umeme Kigamboni Chakamilika

Msimamizi wa Ujenzi wa Kituo cha Kupoza Umeme cha Kigamboni kilichopo jijini Dar es Salaam, Sylvester Sikare (kulia) akielezea maendeleo ya ukamilishaji wa kituo kwa Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (katikati) mara alipofanya ziara katika kituo hicho jana.

Na: Greyson Mwase, Dar es Salaam

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu amesema kuwa kata za Kigamboni, Vijibweni, Tungi zinatarajiwa kupata umeme wa uhakika  kufuatia kukamilika kwa mradi wa upanuzi wa kituo cha kupoza umeme cha Kigamboni kilichopo jijini Dar es Salaam.

Waziri Mgalu aliyasema hayo  tarehe 27 Novemba, 2017 kwenye ziara yake katika kituo cha kupoza umeme Kigamboni na katika mikutano ya hadhara aliyoifanya katika kata za Kisiju na Mkamba zilizopo wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani.

Alisema kituo hicho kitakuwa na uwezo wa kuhudumia wateja kutoka 6,000 hadi 12,000 na kuongeza kuwa Serikali kupitia  Wizara ya Nishati  itahakikisha  vituo vingine vya kuboresha  hali ya umeme ndani ya jiji la  Dar es Salaam  vinakamilika mapema Desemba 15, 2017 na kuondoa  tatizo la  kukatika kwa umeme mara kwa mara lililokuwa linajitokeza. Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Masauni Atembelea Mradi wa Ujenzi Nyumba Mpya za Askari Polisi Mkoani Mara

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kulia),akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Mara,Adam Malima (watatu kulia) na viongozi wengine, baada ya kukagua mradi wa Ujenzi wa Nyumba zinazooenekana pichani za askari polisi na familia zao ulioko kata ya Mukonde, Mkoani Mara, kulia ni Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Tarime/Rorya, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Henry Mwaibambe. Nyumba hizo ziko katika hatua ya mwisho kukamilika ili ziweze kumaliza changamoto za makazi kwa askari hao.

Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail