Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Vyombo Vya Habari Vyaaswa Kuripoti Miradi na Programu Zinazotekelezwa na SADC

Na: Frank Mvungi – Botswana

Waratibu wa vyombo vya Habari wa nchi Wanachama  wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC)  wametakiwa  kuhamasisha vyombo vya habari katika  nchi wanachama kuripoti habari za miradi na progamu zinazotekelezwa na umoja huo kwa manufaa ya wananchi wa nchi wanachama.

 Akizungumza katika  hafla ya ufunguzi  kwa niaba ya Katibu Mtendaji wa Jumuiya hiyo Dkt. Stergomena Tax , inayofanyika  Makao Makuu ya Umoja huo mjini Gaborone nchini Botswana , Mkuu wa  mawasiliano wa Jumuiya hiyo Bi Barbara  Lopi amesema Warsha hiyo itawajengea uwezo waratibu hao ili waweze kutekeleza jukumu la kuhamasisha vyombo vya habari kutangaza umuhimu wananchi kutumia fursa zilizopo katika nchi wanachama kuchochea maendeleo na Ustawi wa umoja huo. Read more

Majaliwa Awasili Singida

Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akisalimiana na Mwenuyekiti wa CCM wa Mkoa wa Singida, Martha Mlata baada ya kuwasili Ikulu Ndogo ya Singida Novemba 29, 2017. Kesho Mheshimiwa Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Mahafali ya Chuo Kikuu Huria chaTanzania yatakayofanyika mjini Singida.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary (kuila) wakimsikiliza mwimbaji wa Kwaya ya Africa Inland Church Tanzania, Loice Jonathan (kushoto) baada ya kuwasili kwenye Ikulu ndogo ya Singida Novemba 29, 2017. Kesho anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Mahafali ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania yatakayofaanyika mini Dodoma. Watatu kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Mwanri: Bodi ya Pamba Waongezeeni Wakulima Mbegu za Pamba

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akihamasisha ulimaji wa zao la Pamba kwa wakulima wa Wilaya ya Urambo Mkoani humo wakati wa ziara yake ya kikazi kuhamishisha shughuli za maendeleo.

Na: Tiganya Vincent; RS-TABORA

BODI  ya Pamba Tanzania imetakiwa kuongeza mbegu za pamba kufuatia wakazi wengi wa maeneo mbalimbali ya mkoa wa Tabora kujitokeza kwa wingi kutaka kulima zao hilo katika msimu wa kilimo ulianza hivi karibuni.

Kauli hiyo ilitolewa jana Novemba 28, 2017 na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakati wa mkutano wake na wanavijiji wa Wilaya ya Urambo waliojitokeza na kumweleza kero mbalimbali ikiwemo uhaba wa kuwa mbegu za pamba kufuatia wengi wao kuonesha nia ya kulima zao hilo.

Alisema kuwa baada wakulima wengi kupatiwa elimu ya uhamasishaji juu ya kilimo cha kisasa cha zao hilo ikiwemo uzingatiaji wa sheria na kanuni za ulimaji wa pamba kumekuwepo na mwitikio mkubwa wa wanakijiji kutaka kulima zao hilo. Read more

TAMISEMI Waziagiza Halmashauri Kutumia Mafundi Wazawa.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Joseph Kakunda akipima kiasi cha saruji kilichowekwa kwenye mchanga katika ujenzi shule ya Sekondari Iguguni Wilayani Mkalama katika ziara yake ya Siku moja kufuatilia utoaji huduma mbalimbali kwa jamii.

Na Mwandishi wetu –  Singida

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Joseph Kakunda ameziagiza Halmashauri zote nchini kutumia mafundi wa kawaida wazawa waliopo katika maeneo yao katika miradi yote midogo kupitia utaratibu unaojulika kama ‘force account’.

Naibu Waziri Kakunda ametoa agizo hilo jana mara baada ya kufanya ziara Wilayani Mkalama kufuatilia utoaji wa huduma mbalimbali kwa jamii huku akijikita zaidi katika sekta ya maji na elimu ambapo ametembelea mradi wa maji Iguguno na Shule ya Sekondari Iguguno.

Read more

Serikali Yasisitiza Mwisho Desemba 31 Uwekaji Vigingi vya Mpaka Hifadhini.

 

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (kushoto) akioneshwa ramani ya Hifadhi ya Msitu wa Isalalo na Meneja wa Wakala wa Huduma za Misitu Wilaya ya Mbozi, Fred Mgeni (kulia) wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua hifadhi hiyo kwa ajili ya kuimarisha uhifadhi mkoani Songwe jana.

Na Hamza Temba – Wizara ya Maliasili

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga amesisitiza agizo la Serikali lililotolewa

hivi karibuni na Waziri Mkuu kuhusu kukamilisha zoezi la uwekagi wa vigingi vya

mpaka kwenye maeneo ya hifadhi nchini ifikapo Desemba 31 mwaka huu. 

Amesema lengo la kukamilisha zoezi hilo ni kuiwezesha Serikali kufanya uamuzi wa mwisho wa kumaliza migogoro ya ardhi iliyodumu kwa muda mrefu baina ya vijiji na maeneo ya hifadhi nchini. 

 

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (kulia) akiongozana na Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, John Palingo wakati wa kukagua Hifadhi ya Msitu wa Isalalo Mkoani Songwe kwenye ziara yake ya kikazi ya kuimarisha uhifadhi mkoani humo jana.

Mhe. Hasunga ametoa kauli hiyo jana wakati wa ziara yake ya kikazi katika hifadhi ya msitu wa

Isalalo Wilaya ya Mbozi mkoani Songwe ambapo aliziagiza taasisi zilizo chini ya

Wizara yake kukamilisha zoezi hilo kabla ya tarehe hiyo ili kuiwezesha Serikali

kubaini maeneo yenye mapungufu na kuyatolea uamuzi.

 

“Ifikapo tarehe 31 tuwe tumemaliza kuweka hizo beacon (vigingi) za mipaka, baada ya hapo hatua

itakayofuata, Serikali tutakaa na kuangaliza ni vijiji vingapi au maeneo gani

yameingia ndani ya hifadhi, tuangalie je tuwaachie hayo maeneo wananchi au

tuwahamishe tuwapeleke maeneo mengine, maamuzi hayo yatakuja baada ya kufanya

tathmini na kubaini penye mapungufu.

 

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (kulia) akizungumza na Mkuu wa Wilaya Mbozi, John Palingo (kushoto) wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua Hifadhi ya Msitu wa Isalalo uliopo wilaya ya Mbozi mkoani Songwe jana kwa ajili ya kuimarisha uhifadhi mkoani humo.

 

“Sasa ikitokea kwamba imefika tarehe 31 hatujatekeleza hili mimi kama Naibu Waziri nitakuwa sina

kazi, maana sijatekeleza agizo la Serikali, kwahiyo lazima tulisimamie, na mimi

sasa kabla halijanipasukia nitakupasukia bwana Meneja (Meneja TFS Wilaya ya

Mbozi), nitakuja kukagua mipaka, na kabla ya tarehe 31 nitakuja kukagua tena,”alisema

Naibu Waziri Hasunga.

 

Wakati huo huo amekemea vitendo vya baadhi ya wananchi wanaoingiza mifugo kwenye maeneo ya

hifadhi nchini na kuwataka kufugia majumbani kwao au maeneo yaliyotengwa kwa

ajili hiyo, amewatahadharisha pia juu ya ukali wa sheria za uhifadhi na kwamba

endapo mifugo itakamatwa hifadhini sheria zilizopo zinaruhusu utaifishaji.

 

Aidha aliwataka wananchi wanaozunguka hifadhi hiyo ya msitu wa Isalalo kuacha vitendo vya

uharibifu wa mazingira ikiwemo ukataji wa miti hovyo kwa ajili ya mkaa na

uanzishaji wa maeneo ya kilimo. Pia alitoa wito kwa wananchi kulinda vyanzo vya

maji na kuacha vitendo vya uchomaji moto misitu.

 

 

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (wa pili kulia) akimsikiliza Meneja wa Wakala wa Huduma za Misitu Wilaya ya Mbozi, Fred Mgeni (kulia) wakati akikagua Hifadhi ya Msitu wa Isalalo uliopo wilaya ya Mbozi mkoani Songwe wakati wa ziara yake ya kikazi ya kuimarisha uhifadhi mkoani humo jana. Wa tatu kulia ni Mkuu wa Wilaya hiyo, John Palingo.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (kulia) akizungumza na wananchi wa kijiji cha Malolo wilaya ya Mbozi Mkoani Songwe wakati wa ziara yake ya kikazi ya kuimarisha uhifadhi mkoani humo jana, alikagua Hifadhi ya Msitu wa Isalalo na kuagiza zoezi la uwekaji vigingi vya mpaka likamilike ifikapo Desemba 3l.

Katika hatua nyingine ameuagiza uongozi wa Wakala wa Huduma za Misitu Nyanda za Juu Kusini kuwashirikisha wananchi wanaoishi jirani na hifadhi hiyo ya msitu kwenye ulinzi wa hifadhi ikiwa ni pamoja na

kuwawezesha miche ya miti ya kutosha kwa ajili ya kupanda  kwenye maeneo

yao yanayozunguka hifadhi hiyo.

Aidha ameuagiza uongozi wa halmashauri ya wilaya ya Mbozi kupima maeneo yao na kuweka mpango bora wa matumizi ya ardhi

kwa kuanisha maeneo kwa ajili ya kilimo, ufugaji na maeneo ya hifadhi ili

kuepusha migogoro isiyo ya lazima ya wananchi

 

Kwa upande wake Meneja wa Wakala wa Huduma za Misitu Wilaya ya Mbozi, Fred Mgeni alisema katika kuimarisha mpaka wa

hifadhi ya msitu huo wa Isalalo ambao una ukubwa wa hekta 11,552, jumla ya

vigingi 30 vimewekwa kuzunguka hifadhi hiyo.

Alizitaja baadhi ya  changamoto katika hifadhi hiyo kuwa ni uvamizi wa wakulima na wafugaji, uvunaji haramu wa

miti, uchomaji mkaa na moto, na ung’oaji wa vigingi vya mpaka na mabango.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, John Palingo alisema ili kuimarisha uhifadhi wa msitu wa Isalalo ni vema wananchi

wakashirikishwa ikiwemo kuanzishwa kwa vikundi vya vijana ambao watawezeshwa

bodaboda zitakazowanufaisha kiuchumi na wakati huo huo zikatumika kwenye ulinzi

wa hifadhi.

 

 

 

 

Waziri Mkuu Abaini Semi Trela 44 Zikitaka Kutolewa Bandarini Bila Utaratibu

Waziri Mkuu. Kassim Majaliwa (mwenye Tai nyekundu) amefanya ziara ya kushitukiza katika Bandari ya Dar es salaam leo November 29, 2017 nakubaini Kampuni ya NAS ikitaka kutuo Semi Tela Arobaini na nne bilayakufuata utaratibu.

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemtaka Inspekta Jenerali wa Polisi, Simon Sirro kuwakamata, Bw. Bahman wa kampuni ya NAS na Wakala wa Kampuni ya Wallmark Bw. Samwel kwa kutaka kutoa bandarini magari makubwa aina ya semi tela 44 bila ya kulipa kodi kwa kutumia jina la Waziri Mkuu.

Pia Waziri Mkuu ameitaka Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kufanya kazi kwa mujibu wa sheria na kutowasikiliza wafanyabiashara wanaotaka kukwepa kodi kwa madai ya kupewa vibali vya msamaha wa kodi kutoka kwa viongozi wa juu Serikalini.

Read more

Hatutakuwa Kikwazo cha Utekelezaji wa Miradi ya Maji.

                                                                                                                                                                                                                                              
 Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso (wa kwanza kulia) akikagua sehemu ya mtambo wa kutibu wa kutibu na kusafisha maji wa Matogoro, pamoja na Meneja Ufundi wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira mjini Songea (SOUWASA), Mhandisi John Kapinga.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso amesisitiza kuwa wizara yake haitakuwa kikwazo cha utekelezaji wa ahadi ya Rais, Dkt. John Magufuli ya kuwapatia wananchi majisafi na salama, bali itasimimamia utekelezaji wa miradi hiyo ipasavyo ili ikamilike kwa wakati na kuleta tija.
Aweso alizungumza hayo katika ziara yake ya kikazi aliyoianza katika mkoa wa Ruvuma, ambapo anakagua utekelezaji wa miradi ya maji katika wilaya zote mkoani humo.

Read more

Makamu wa Rais Mama Samia Arejea Nchini Akitokea Nairobi Kenya

Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akisindikizwa na Balozi wa Tanzania nchini Kenya Mhe. Dkt. Pindi Chana katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta Jijini Nairobi.

Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokelewa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokelewa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.