Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Rais Magufuli Afungua Kiwanda cha Sayona Mwanza

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amefungua kiwanda cha vinywaji baridi cha Sayona kilichopo Nyakato Mjini Mwanza kilichojengwa na kampuni ya Kitanzania ya Motisan kwa gharama ya takribani Shilingi Bilioni 11 na Milioni 800.TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Kiwanda hiki cha kisasa ambacho kimejengwa kwa muda wa mwaka mmoja na nusu kina uwezo wa kuzalisha chupa 1,200 kwa dakika moja katika mitambo yake minne ya kuzalisha vinywaji baridi pamoja na chupa 100 za maji, kimezalisha ajira za watu 200 na kinaungana na kiwanda kingine cha vinywaji baridi cha Sayona kilichopo Mboga Mkoani Pwani kusindika matunda ya wakulima na kuinua hali zao za maisha.

Akizungumza baada ya Mhe. Rais kufungua kiwanda cha Sayona Mwanza, Mkurugenzi Mkuu wa Motisan Group Bw. Subhash Patel amesema kampuni yake imedhamiria kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano za kujikita katika uchumi wa viwanda na ameahidi kuwa mwaka ujao wa 2018 kampuni hiyo itajenga viwanda vingine vitano.

Mhe. Rais Magufuli amempongeza Bw. Subhash Patel kwa uwekezaji mkubwa anaoufanya katika viwanda na amemtaka yeye pamoja na wafanyabiashara wengine kutumia muda huu kuwekeza zaidi katika viwanda na kwamba Serikali yake itawaunga mkono.

“Bw. Subhash nakupongeza sana, wewe jenga viwanda Serikali itakuunga mkono, na nataka niwaambie wafanyabiashara na wawekezaji, huu ndio wakati wa kuwekeza na mimi nawapenda wafanyabiashara na wawekezaji, hapa kusingekuwa na kiwanda hiki, vijana hawa 200 wasingepata ajira, nataka kukupongeza sana hata kwa mpango wako wa kujenga viwanda vingine vitano mwakani, hii ni safi sana” amesema Mhe. Rais Magufuli.

Mhe. Dkt. Magufuli amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Bw. John Mongella kwa juhudi anazofanya kusimamia utekelezaji wa sera ya viwanda kwa kuhakikisha viwanda vinaanzishwa na ametaka juhudi hizo ziendelee ili Mwanza irejeshe historia yake ya kuwa na viwanda vingi vinavyozalisha ajira na kukuza uchumi wa mkoa.

Wakizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika eneo la Nyakato Mwatex Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa Mnyaa na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Anjelina Mabula wamewahakikishia wananchi wa Mwanza kuwa Serikali ya Awamu ya Tano inaendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuuendeleza Mkoa wa Mwanza kwa kuhakikisha viwanda zaidi vinajengwa, miundombinu inaimarishwa na migogoro ya ardhi inamalizwa na wamewataka wananchi wajielekeze zaidi katika uzalishaji mali.

Katika mkutano huo, Mbunge wa Nyamagana Mhe. Stanslaus Mabula, Umoja wa Wamachinga na Umoja wa Wanawake wajasiriamali Mkoa wa Mwanza wamemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa juhudi kubwa anazofanya kuwajali wananchi hasa wa hali ya chini na kupigania maendeleo ya Taifa zima.

Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amezungumzia utekelezaji wa ahadi ya kutoa Shilingi Milioni 50 kwa kila Kijiji ama Mtaa kwa kueleza kuwa Serikali imeona njia bora ni kuelekeza fedha hizo katika miradi mikubwa yenye manufaa na matokeo mapana kwa wananchi na amesisitiza kuwa utekelezaji wa dhamira hiyo umeanza.

Amebainisha kuwa pamoja na hatua hizo Serikali inaendelea kukabiliana na wote waliojihusisha na ufisadi wa mali za umma na kwamba haitasita kuchukua hatua za kisheria hata kama wahusika watakimbia, kujificha ama kutetewa mahali popote.

Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Mwanza

30 Oktoba, 2017


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Taasisi za Fedha Punguzeni Riba ya Mikopo-Makamu wa Rais.

Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizundua rasmi Sera ya Taifa ya Huduma Ndogo ya Fedha ya mwaka 2017 na Mkakati wa Utekelezaji wake katika kipindi cha miaka 10 kuanzia 2017/2018 hadi mwaka 2027/2028, mjini Dodoma.

 

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), akizungumzia mapinduzi makubwa yaliyofanywa na Serikali kwa kuja na Sera ya kuhudumia Sekta Ndogo ya Fedha nchini ijulikanayo kama Sera ya Taifa ya Huduma Ndogo ya Fedha ya mwaka 2017 na Mkakati wa Utekelezaji wake katika kipindi cha miaka 10 kuanzia 2017/2018 hadi mwaka 2027/2028, iliyozinduliwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango mjini Dodoma.

Na Benny Mwaipaja, Dodoma

 MAKAMU wa Rais Mhe. SAMIA SULUHU HASSAN, amezinduzi  Sera ya Taifa ya Huduma Ndogo ya Fedha ya mwaka 2017 na Mkakati wa Utekelezaji wake katika kipindi cha miaka 10 kuanzia 2017/2018 hadi mwaka 2027/2028, tukio litakalofanyika Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango mjini Dodoma.

Makamu wa Rais ametoa wito kwa watoa huduma ndogo za fedha kupunguza riba za mikopo na tozo mbalimbali ili kufanikisha  lengo la Sera hiyo ambalo ni  kuimarisha huduma jumuishi za fedha kwa kujenga mazingira wezeshi yatakayoleta ufanisi wa utoaji wa huduma ndogo za fedha nchini kwa wananchi wenye kipato cha chini.

Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

RC Tabora: Madiwani Toeni Elimu Wananchi Waondokane na Kilimo cha Kizamani.

Na: Tiganya Vincent; RS-TABORA

MADIWANI Mkoani Tabora wameombwa kusaidia kutoa elimu kwa wananchi juu ya kilimo cha kisasa cha mazao mbalimbali ili waweze  kuongeza uzalishaji ambao utaweka mazingira yanayovutia wawekezaji katika sekta ya viwanda vikiwemo vya mafuta ya alizeti.

Kauli hiyo imetolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakati akifunga mafunzo ya siku tatu ya Madiwani na Watendaji wa Halmashauri ya Wilaya wa Kaliua yalikuwa yakiendeshwa na Chuo cha Serikali za Mitaa –Hombolo. Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Naibu Waziri Kwandikwa: Zingatieni Vipaumbele Ujenzi Miradi Ya Barabara

Makamu wa Rais wa Chama cha wataalamu wa magonjwa ya Figo Tanzania (NESOT), Dkt. Paschal Ruggajjo akiongea dhima kubwa ya mkutano huo ni teknolojia ya upandikizaji wa viungo nchini ili kuweza kuhudumia wagonjwa takribani milioni 23.

Baadhi ya Wataalamu wa magonjwa ya figo waliohudhuria mkutano huo. Mkutano huo ni wa siku mbili ambapo watajadili dhana mbalimbali ya ugonjwa wa figo ikiwemo kutoa elimu kwa umma ili kuweza kukabiliana na magonjwa ya figo pamoja na upandikizaji. Tanzania imekua ikipeleka wastani wa wagonjwa thelathini na tano(35) kwa mwaka nje ya nchi kwa ajili ya kupandikiza figo na gharama ya kupandikiza nje ya nchi ikiwemo India ni shilingi milioni 75 hadi 77 kwa mtu mmoja ikiwemo kupandikiza,nauli pamoja na malazi

Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Naibu Waziri Kwandikwa: Zingatieni Vipaumbele Ujenzi Miradi Ya Barabara

Mitambo ya ujenzi ikiwa eneo la kazi kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Kaliua-Urambo KM 28, mkoani Tabora.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mheshimiwa Elias Kwandikwa (Mb), ametoa wito kwa madiwani nchini kuanisha barabara zote zenye kipaumbele katika maeneo yao ili ziweze kuingizwa kwa urahisi kwenye mpango wa matengenezo.

Kwandikwa ametoa wito huo mkoani Tabora wakati akikagua ujenzi wa barabara ya Kaliua-Urambo yenye urefu wa KM 28 ambapo pamoja na mambo mengine amesema mapendekezo yao yawasilishwe katika kamati za maendeleo za wilaya, mikoa na bodi za barabara.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Mhe. Elias Kwandikwa, akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Aggrey Mwamri, wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa barabara ya Kaliua-Urambo KM 28 kwa kiwango cha lami, mkoani humo.

“Unakuta diwani analalamika kwamba barabara haijatengenezwa ama haifikiliwi kutengenezwa lakini ukija kufuatilia unakuta hakuna mahali popote ambapo taariza za barabara hiyo kutengenezwa zimewasilishwa”,    amesema Mhe. Kwandikwa.

Amesisitiza kuwa umuhimu wa kupeleka mapendekezo hayo kutasaidia barabara hizo kutambulika na kuondoa malalamiko kwa wananchi na baadhi ya viongozi kwa kuwa zitaingizwa katika mipango ya ujenzi kwa wakati.

Kuhusu barabara hiyo ya Kaliua-Urambo inayojengwa kufuatia agizo la Rais Dkt John Magufuli, Mhe. Kwandikwa amemtaka mkandarasi kuhakikisha ujenzi huo unafanyika kwa kuzingatia viwango vya ubora uliopangwa kwa mujibu wa mkataba wake.

Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Tabora Eng. Damian Ndibalinze akitoa taarifa ya mradi kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Mhe. Elias Kwandikwa, alipokagua ujenzi wa barabara ya Kaliua-Urambo KM 28 kwa kiwango cha lami, mkoani humo. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Aggrey Mwamri.

Lengo la mheshimiwa rais ni kurahisha huduma ya usafiri na usafirishaji kwa wananchi hivyo mkandarasi huna budi kufanya kazi hii haraka na kw kuzingatia makubaliano ya mkataba wako.Amesema waziri kwandika.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwamnri, amemuhakikishia Naibu Waziri Kwandikwa kuwa serikali ya mkoa huo imejipanga kushirikiana na mkandarasi ili barabara hiyo ikamilike ndani ya muda uliopangwa.

 

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Mhe. Elias Kwandikwa, akitoa maelekezo kwa Mhandisi Mshauri anayesimamia ujenzi wa barabara ya Kaliua-Urambo KM 28 kwa kiwango cha lami. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Aggrey Mwamri.

Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Tabora Eng. Damian Ndibalinze akifurahi jambo na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Aggrey Mwamri, wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa barabara ya Kaliua-Urambo KM 28 kwa kiwango cha lami, mkoani humo.

“Kwanza sisi kama mkoa tunamshukuru Mheshimiwa Rais kwa kuona umuhimu wa kutuwekea lami katika barabara hii kwa sababu itaongeza ufanisi kwa wananchi kufanya shughuli zao kiurahisi”, amesema Mwanri.

Naye Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Tabora Eng. Damian Ndibalinze amesema kuwa Wakala utawasimamia makandarasi wazawa Samota Construction, Anam Roads Works na Jossam Contractor (JV) ili kuhakikisha wanamaliza ujenzi huo kwa wakati baada ya changamoto ya tatizo la maji kupatiwa ufumbuzi.

Naibu Waziri Mhe. Elias Kwandikwa, yupo katika ziara ya kikazi ya kukagua ujenzi wa barabara na madaraja katika mikoa ya Singida, Tabora na Kigoma.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

 

 


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

DED Kaliua : Tumeanza Kulima Korosho Kama Zao Jingine La Biashara

Na: Tiganya Vincent

Halmashauri  ya Wilaya ya Kaliua imesema imeanza ulimaji wa zao la Korosho ili kuongeza katika mazao ya biashara litakaloungana na pamba na tumbaku ikiwa ni hatua ya kuandaa malighafi kwa ajili ya viwanda na kuongeza mapato yake.

Kauli hiyo imetolewa jana mjini hapa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua John Pima wakati wa ufungaji wa mafunzo ya Madiwani yaliyokuwa yakiendeshwa na Chuo cha Serikali za MItaa Hombolo ili kuwajengea uwezo viongozi hao ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi zaidi.

Alisema kuwa tayari washapanda miche zaidi ya 1350 katika vijiji 10 vya Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua ikiwa ni sehemu ya mashamba darasa kwa ajili ya wananchi kujifunza kwa wale wanaohitaji kulima zao hilo. Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Lugola: Wananchi Epukeni Uchafuzi wa Mazingira.

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Kangi Lugola akizungumza na waandishi wa habari na wakazi wa eneo la Tande kwa Mtogole wakati wa ziara ya waziri huyo ya kuzindua operesheni ya miezi miwili ya kusafisha mito nchi nzima.

Na:Paschal Dotto

SERIKALI imewataka Wananchi kuzingatia usafi kuwa kusafisha mitaro na kuzibua maji yaliyopo katika mito ili kuepukana na adha ya mafuriko inayosababishwa kuwepo na taka ngumu zinazozuia utiririkaji wa maji kwa urahisi.

Akizungumuza katika uzinduzi wa Operesheni ‘Tudhibiti Uchafuzi wa Mazingira Tusalimike’ Jijini Dar es Salaam,  itakayoanza nchini kote tarehe Novemba Mosi 1 hadi Desemba 30, mwaka huu, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Kangi Lugola alisema ili jamii ibaki salama katika mazingira yao ni wajibu wao kuzingatia dhana ya usafi. Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Rais Mhe. Dkt. Magufuli Afungua Daraja la Waenda Kwa Miguu la Furahisha Jijini Mwanza

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella pamoja na viongozi mbalimbali akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Daraja la Waenda kwa miguu la Furahisha liliopo jijini Mwanza.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaMhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa pamoja na viongozi mbalimbali akivuta utepe kwenye jiwe la ufunguzi kuashiria ufunguzi wa wa Daraja la Waenda kwa miguu la Furahisha liliopo jijini Mwanza.

Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Serikali Yamshukia Zitto kwa Upotoshaji.

Meneja wa Takwimu za Pato la Taifa toka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Daniel Masolwa (kulia) akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) wakati akikanusha taarifa za upotoshaji kuhusu takwimu za Pato la Taifa mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kushoto ni Mkurugenzi wa Sera na Tafiti toka Benki Kuu ya Tanzania, Johnson Nyella.

Na.Jacquiline Mrisho..

Serikali imetoa onyo kali kwa Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini, Mh. Zitto Kabwe juu ya taarifa za upotoshaji wa takwimu za Pato la Taifa alizozitoa hivi karibuni.

Taarifa hizo za Mh. Zitto zimeripoti kuwa ukuaji wa Pato la Taifa kwa robo ya pili ya mwaka 2017 kuwa ni asilimia 5.7 badala ya asilimia 7.8. Kasi ya ukuaji ya asilimia 5.7 ilikuwa ni kwa robo ya kwanza ya Januari hadi Machi 2017.

Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail