Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Dkt Nchimbi Atoa Mwezi Mmoja kwa Halmashauri ya Iramba Kujenga Vyoo Mnada wa Malendi.

Na Mwandishi wetu – Singida.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi amempa mwezi mmoja Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Linno Mwageni kujenga vyoo bora katika Mnada uliopo Kijiji cha Malendi, Kata ya Mgongo Wilayani humo..

Dkt Nchimbi ametoa agizo hilo mara baada ya kutembelea mnada huo ambapo wananchi wamelalamika kukosa huduma za vyoo na maji kwa kipindi kirefu huku halmashauri hiyo ikiendelea kukusanya ushuru bila kuwaboreshea miundombinu.

Read more

Ziara ya Naibu Waziri Maliasili na Utalii katika Shamba la Miti Sao Hill na Kituo cha Malikale cha Ismila na Kalenga Mkoani Iringa

 

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet
Hasunga (kulia) akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, 
Mhe. Amina Masenza
alipotembelea shamba la miti Sao Hill kukagua shughuli mbalimbali zinazofanyika shambani hapo. Aliagiza uongozi wa shamba hilo
kuongeza juhudi za upandaji miti ili kukidhi mahitaji makubwa yaliyopo nchini
na hivyo kusisimua ukuaji wa uchumi wa viwanda.

Read more

Makandarasi Kujadili Maendeleo ya Ukuaji wa Viwanda.

Mwenyekiti wa Chama cha Makandarasi (CATA) Mhandisi Lawrence Mwakyambiki (katikati) akieleza jambo kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) katika utambulisho wa mkutano wa chama hicho utakaofanyika Novemba 17, 2017 Diamondi Jubilee Jijini Dar es Salaam,kulia ni Meneja Mauzo wa Benki ya Biashara ya Afrika (CBA) Bi.Kunenguda Dedede na kushoto ni Mkuu wa Masoko kutoka NMB Bi.Linda Teggisa.

Na: Paschal Dotto

Chama cha Makandarasi (CATA) kinachounganisha wakandarasi wote nchini kinatarajia kukutana Novemba 17, 2017 kujadili kuhusu ukuaji wa viwanda nchini mkutano utakaofanyika katika ukumbi wa Diamondi Jubilee Jijini Dar es Salaam.

Akizungumuza na Waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam, Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Mhandisi Lawrence Mwakyambiki alisema kuwa  Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi wa Rais John Pombe Magufuli iko kwenye njia ya ujenzi wa viwanda kwa hiyo sekta ya ujenzi inahitajika kwa kiasi kikubwa kwenye sera hii ya viwanda.

“Lengo la mkutano huu kwa wakandarasi hawa ni kutaka kuleta mchango wao katika ujenzi wa uchumi wa Tanzania na wameona kwamba kama wazawa wanaowajibu wa kutoa mchango katika katika ujenzi wa viwanda nchini”, alisema Mhandisi Mwakyambiki. Read more

Rais Mhe. Dkt. Magufuli Afungua Viwanda Viwili Jijini Mwanza

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi katika eneo la kona ya Butimba wakati akitokea Igogo jijini Mwanza.

Wananchi wa Butimba na Mkuyuni wakifurahi wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipokuwa akizungumza nao katika eneo la kona ya Butimba wakati akitokea Igogo jijini Mwanza.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi katika eneo la kona ya Butimba wakati akitokea Igogo jijini Mwanza.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Waziri wa Viwanda na Biashara Charles Mwijage mara baada ya kufungua kiwanda cha Victoria Molders and Polybags kilichopo Igogo jijini Mwanza.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono mafundi wa Kiwanda cha Victoria Molders and Polybags mara baada ya kutengeneza Tanki la kuhifadhia maji.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia utengenezaji wa viti vya plastiki katika kiwanda cha Victoria Molders and Polybags katika eneo la Igogo jijini Mwanza.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia mfuniko uliotengenezwa katika kiwanda hicho cha Victoria Molders and Polybags Igogo jijini Mwanza.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Meya ya jiji la Mwanza James Bwire mara baada ya kufungua kiwanda cha Victoria Molders and Polybags Igogo jijini Mwanza.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifungua kiwanda cha madawa cha Prince Pharmaceuticals kilichopo Buhongwa nje kidogo jijini Mwanza. PICHA NA IKULU

Benki ya kilimo kusaidia mageuzi ya Kilimo Njombe

Na Mwandishi Wetu, Njombe

Benki ya Maendeleo ya Kilimo ya Tanzania (TADB) imesema imejipanga katika kusaidia kuchagiza kusaidia Mapinduzi ya Kilimo kutoka kilimo cha kujikimu kwenda cha kibiashara ili kuchangia kwenye ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini kwa wakulima mkoani Njombe na Tanzania kwa ujumla.

Ahadi imetolewa na Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya TADB, Bibi Rehema Twalib wakati alipouongoza ujumbe wa Benki walipomtembelea na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Christopher Ole Sendeka mkoani Njombe.

Bibi Twalib alisema kuwa TADB ilianzishwa mahsusi kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za kuinua ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini nchini Tanzania ili kuisaidia Serikali kuharakisha maendeleo ya sekta ya kilimo ambayo inaajiri zaidi ya asilimia 75 ya watu wenye uwezo wa kufanya kazi nchini na pia kutoa kiasi cha zaidi ya  asilimia 65 cha mali ghafi kwa ajili ya viwanda vya nchi.

Read more

Kiswahili Ndio Utambulisho Wetu Watanzania Lazima Tukitumie kwa Usahihi:Dkt. Mwakyembe.

Na Shamimu Nyaki-WHUSM.

Serikali imesema Lugha ya Kiswahili ndio lugha ambayo inatambulisha Watanzania hivyo ni wajibu kwa Wananchi kutumia Lugha hiyo kwa usahihi katika shughuli zao za ndani na nje ya Taifa ili kukikuza na kukiendeleza .

Hayo yamesemwa  jana na Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo  Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe alipokua akizungumza katika kipindi cha TUNATEKELEZA kinachorushwa na Luninga ya Taifa  ambapo ameliagiza Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) kuandaa na kuwasilisha kwake orodha ya wahitimu wa lugha hiyo ili Serikali iwatambue.

“Lugha ya Kiswahili ni lugha ya 10 kati ya 6000 hapa Duniani, ni lazima Watanzania waone umuhimu wa kutumia lugha hii kwakua inatoa fursa mbalimbali ikiwemo ajira kwa nchi ambazo zinahitaji wataalamu wa lugha hiyo,” alisema Mhe. Mwakyembe.

Read more