Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Serikali Yapongezwa Sheria Upatikanaji wa Taarifa.

Na: Thobias Robert

Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli imepongezwa kwa kupitisha Sheria ya haki ya upatikanaji wa habari kutoka katika taasisi na mashirika ya umma pamoja na binafsi hapa nchini.

Pongezi hizo zimetolewa Jijini Dar es Salaam jana na Jaji Mstaafu Amiri Manento ambaye pia aliwahi kuwa Mwenyekiti wa  Tume ya Haki za Binadamu na Utawala bora, alipokuwa katika  maadhimisho ya siku ya  Kimataifa ya Upatikanaji wa Taarifa iliyofanyika katika ukumbi wa   Millenium Tower.

“Kwa mujibu wa Katiba kila Mtanzania anayo haki ya kupewa taarifa wakati wowote kuhusu matukio mbalimbali na muhimu kwa maisha ya wananchi kuhusu masuala ya kijamii na kimaendeleo, hivyo mwaka 2016, Sheria ya kupata taarifa ilipitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuidhinishwa na Rais John Pombe Magufuli ili kuwezesha wananchi kupata taarifa,” alifafanua Jaji Manento. Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Serikali: Kasi ya Mendeleo ya Teknolojia Inatulazimu Kufanya Maboresho ya Kanuni Zetu

 

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akipokelewa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Mhandisi. James Kilaba alipowasili kwa ajili ya kukutana na wadau wa sekta ya habari ili kujadili kanuni za maudhui ya utangazaji katika redio na tevelisheni, na kanuni za maudhui mtandaoni leo Jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari(MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbassi. (Picha na: Frank Shija) 

Na: Pascal Dotto

Serikali imesema kasi kubwa ya maendeleo ya teknolojia ya habari na mawasiliano ambayo imeikumba sekta ya habari inalazimu jamii kufanya maboresho ya mara kwa mara ya Sera na Kanuni ili kuepusha matumizi mabaya ya vyombo vya habari.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel amesema kuwa katika kufanya hivyo ni wajibu wa wadau wote kushirikiana kutumia vyema maendeleo hayo ya tekinolojia kwa ajili ya ustawi wa jamii na maendeleo ya taifa.   Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Dkt: Shein: Jitihada za Kuimarisha Mazingira ya Mahakama Ziende Sambamba na Ufanisi Katika Utoaji wa Huduma

Waziri wa Katiba, Sheria na Utawala Bora toka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) Haruna Ali Suleiman akizungumza kwa niaba ya Rais wa Zanzibar Dkt. Mohamed Ali Shein katika hafla ya kufunga mkutano Mkuu wa mwaka wa Chama cha Majaji na Mahakimu toka nchi wananchama wa Jumiya ya Madola (CMJA) leo Jijini Dar es Salaam. (Picha na: Frank Shija)

Na. Paschal Dotto

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amesema jitihada zinazochukuliwa na serikali za nchi za Jumuiya ya Madola kuimarisha mazingira ya kazi katika Mahakama hazina budi kwenda sambamba na kuimarika kwa utendaji wa mahakama hizo katika kutoa huduma kwa wananchi.

Katika hotuba yake kufunga mkutano wa siku tatu wa Chama cha Majaji na Mahakimu cha nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola leo, Dk. Shein amesema ni kweli kuwa Serikali ina wajibu mkubwa katika kuimarisha mazingira ya kazi katika mahakama lakini pia mahakama zinapaswa kutimiza wajibu wake ipasavyo. Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Rais Dkt Magufuli Aendesha Kikao Cha Kamati Kuu ya CCM

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Philip Mangula akikaribishwa ukumbini katika kikao cha Kamati Kuu ya Chama hicho kilichoanza leo Jumatano ya Sept 27, 2017 Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt John Pombe Magufuli akiwasili ukumbini kuongoza kikao cha Kamati Kuu ya CCM kilichoanza leo Jumatano ya Sept 27, 2017 Ikulu Jijini Dar Es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt John Pombe Magufuli akiongoza kikao cha Kamati Kuu ya CCM kilichoanza leo Ikulu Jijini Dar es Salaam. Kikao hicho kimehudhuriwa na wajumbe wote wa Halmashauri Kuu, wakiwemo Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Alli Mohamed Shein, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa na Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Alli Idd

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi akisalimiana na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan kabla ya kuanza kwa kikao cha Kamati Kuu ya CCM kilichoanza leo Jumatano ya Sept 27, 2017 Ikulu Jijini Dar Es Salaam

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi akisalimiana na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kabla ya kuanza kwa kikao cha Kamati Kuu ya CCM kilichoanza leo Jumatano ya Sept 27, 2017 Ikulu Jijini Dar Es Salaam.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Rodrick Mpogolo kabla ya kuanza kwa kikao cha Kamati Kuu ya CCM kilichoanza leo Jumatano ya Sept 27, 2017 Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt John Pombe Magufuli akiongoza kikao cha Kamati Kuu ya CCM kilichoanza leo Ikulu Jijini Dar es Salaam. Kikao hicho kimehudhuriwa na wajumbe wote wa Halmashauri Kuu, wakiwemo Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Alli Mohamed Shein, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa na Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Alli Idd


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

UCSAF Yatoa Ruzuku ya Tsh. Bilioni 93.3 Kwa Makampuni ya Simu.

Na: Mwandishi Wetu

SERIKALI kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote imetoa ruzuku ya Tsh Bilioni 93.3 kwa makampuni ya simu za mkononi kwa ajili ya kujenga minara ya mawasiliano ili kufikisha huduma za mawasiliano katika kata 518 nchini hatua inayolenga kuchochea ukuaji wa uchumi na utoaji wa huduma za kijamii kwa wananchi.

Hayo yameelezwa hivi karibuni na Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) Mhandisi Peter Ulanga wakati wa ziara iliyoandaliwa na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kupitia UCSAF ya kuwapeleka wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu kukagua maendeleo ya ujenzi wa minara ya simu za mkononi, hali ya upatikanaji wa huduma za mawasiliano kwa wananchi pamoja na changamoto zilizopo.

Mhandisi Ulanga aliongeza kuwa Serikali kupitia UCSAF inaendelea kutoa ruzuku kwa kampuni za simu za mkononi  ili ziweze kufikisha mawasiliano kwenye vijiji vyote nchini, ambapo hadi sasa jumla ya kata 391 kati ya kata 518 zimefikishiwa huduma ya mawasiliano katika kipindi cha miaka minne kuanzia mwezi Machi 2013 mpaka mwezi Agosti 2017 mwaka huu. Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Milambo Waomba Radhi Kwa Utovu wa Nidhamu Uliofanywa na Wenzao.

Na: Tiganya Vincent, RS – TABORA

WANAFUNZI wa Shule ya Sekondari Milambo wameiomba radhi Serikali kwa vitendo vya utovu wa nidhamu vilivyosababisha baadhi wamefikishwe Mahakamani na wengine kulazimishwa kuhamishwa shule hiyo kwa makosa ya kutoroka shuleni nyakati za usiku.

Kauli hiyo imetolewa hivi karibuni na Mwanafunzi wa Kidato cha Sita katika Masomo ya Fizikia, Kemia na Hisabati (PCM) ambaye pia ni Makamu Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Shule hiyo Baraka Fundo kwa niaba ya wanafunzi wenzake waliobaki shuleni hapo wakati Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri alipopita kukagua miradi mbalimbali ya shule.

Alisema kuwa matukio mawili yaliyofanywa na wenzao yamechafua jina zuri la Shule hiyo ya Milambo ambayo ina historia ya kutoa vijana wengi wanaojiunga na vyuo vikuu hapa nchini na kutoa mchango mkubwa kwa Taifa.

Fundo alisema kuwa wanafunzi waliobaki shuleni ni safi na wako pale kwa ajili ya kusoma na kuendelea mbele zaidi ili waweze kutoa mchango wao kuliendeleza Taifa hilo katika sekta mbalimbali na kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano ya kujenga Tanzania ya viwanda. Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Ahmadiyya Kufanya Mkutano Mkuu wa 48 Jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu Msaidizi wa Jumuiya ya Waislam ya Ahmadiyya Tanzania Sheikh Abdurahman Muhamed Ame (kushoto) akielezea juu ya Mkutano wa 48 wa Jumuiya hiyo mbele ya waandishi wa habari unaotarajiwa kufanyika tarehe 30 September hadi 1 Oktoba leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Amir na Mbashiri Mkuu wa Jumuiya hiyo Tahir Mahmood Chandhry.

Na: Neema Mathias na Thobias Robert

Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya   inatarajia kufanya mkutano  mkuu wa mwaka wa  48 ut kuanzia tarehe 29 Septemba hadi 1 Oktoba mwaka huu katika viwanja vya Kitonga Manispaa ya Ilala, lengo likiwa ni kuhamasisha amani, upendo ushirikiano na kutii sheria kwa waumini wa dini zote duniani.

Hayo yameelezwa jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Msaidizi wa Jumuiya hiyo Sheikh Abdurahman Ame alipokuwa  akizungumza na waandishi wa habari ambapo alisema kauli mbiu ya mkutano huo ni, “Muislam wa kweli ni yule ambaye watu wengine wote wako salama dhidi ya shari ya ulimi wake na mikono yake.” Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail