Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Mafunzo ya PlanRep yaendelea Mjini Dodoma

Meneja wa Mradi wa PS3 Mkoa wa Dodoma Bw. Gideon Muganda akizungumza wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo watumiaji wa Mfumo wa Kielektroniki wa Kuandaa Bajeti, Mipango na Kutoa Ripoti (PlanRep) yanayoendelea mjini Dodoma kwa siku nane.

Mmoja wa Wawezeshaji wa Mafunzo kwa watumiaji wa mfumo wa kuandaa Bajeti, Mipango na Kutoa Ripoti (PlanRep) Bw. Ismail Juma akiwasilisha mada kwa washiriki (hawapo pichani) wakati wa mafunzo hayo yanayoendelea mjini Dodoma.

Sehemu ya washiriki wakifuatilia mada wakati wa mafunzo hayo

Mmoja wa Washiriki wa mafunzo hayo akisisitiza jambo wakati wa mafunzo hayo. (Picha zote na Frank Mvungi-Dodoma)


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Mkemia Mkuu wa Serikali: Huduma Zetu Zinapatikana Kote Nchini

Kaimu Meneja Masoko, Mawasiliano na Huduma kwa Wateja wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemi Mkuu wa Serikali Bw.Cletus Mnzava akiwasomea Waandishi wa Habari (hawapo pichani) baadhi ya mikakati ya mamlaka ya hiyo kuhusu uimarishwaji wa ofisi zao hapa nchini, kulia ni Afisa Mawasiliano wa Mamlaka hiyo Bw. Silvester Omary katika mkutano uliofanyika katika ukumbI wa Idara ya Habari (MAELEZO) Jijini Dar es Salaam leo.

Na: Georgina Misama

Serikali kupitia Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali inafanya maboresho katika maabara zake za kanda zilizopo kote nchini ili kusogeza huduma hiyo kwa wananchi.

Akiongea na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam, Kaimu Meneja Masoko, Mawasiliano na Huduma kwa Wateja kutoka Mamlaka hiyo  Cletus Mnzava alisema kwamba Mamlaka inafanya maboresho katika Ofisi zake za kanda kwa kuboresha miundombinu na kuzipatia vifaa vya maabara vya kisasa.

“Lengo kuu la kuimarisha Maabara zetu za kanda ni kusogeza huduma karibu na wananchi kote nchini ili kuwaondolea ulazima wa kuja kufuata baadhi ya huduma kwenye ofisi zetu za Dar es salaam”. Alisema Mnzava Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Ulinzi wa Kimtandao Kuimarishwa Nchini Ili Kulinda Mifumo

Na: Jonas Kamaleki

Serikali  kushirikiana na sekta binafsi wanaweza kujenga msingi wa kitaifa katika kuimarisha Usalama katika ulimwengu mzima kwa ujumla na kudondokana na uhalifu wa kimitandao.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Naibu Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Mhe. Matt Sutherland wakati wa ufunguzi wa Warsha ya masuala muhimu katika kuweka miondombinu ya kiusalama katika mitandao.

Sutherland amesema kuwa uhalifu wa kimitandao haungalii mipaka ya nchi bali unaweza kutokea mahali popote na wakati wowote. Alisisitiza hilo amesema kuwa mwezi Mei mwaka huu shambulio la kimtandao lilipiga mifumo karibu nchi 100 Duniani.. Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Home Affairs Minister to Chair Tripartite Meeting On Burundi Refugees Tomorrow

By Staff Writer-Tanzania Information Services-MAELEZO

Tanzania, Burundi and United Nations High Commission for Refugees (UNHCR) are expected to meet tomorrow for a one-day meeting to discuss preparations for the repatriation exercise of the Burundian refugees.

According to sources at the Ministry of Home Affairs, Minister Mwigulu Nchemba will chair the tripartite meeting which will be held at Mwalimu Nyerere International Convention Centre in the city.

The meeting which will be attended by UNHCR country Representative, ministers in charge of refugees of both countries as well as regional commissioners of refugees hosting regions of Kigoma and Kagera and returnees home regions. Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Mafunzo ya PS3 Yaendeleo Mkoani Dodoma

Mwezeshaji kutoka Mradi wa Uimarishaji Sekta za Umma (PS3) Christopher Masaaka ambaye pia ni Afisa Uchumi kutoka Halmashauri ya Wangingómbe Mkoa wa Njombe akitoa mafunzo kwa moja ya kundi la washiriki wa mafunzo ya Mfumo wa Kielektroniki (PlanRep) iliyoboreshwa wa kuandaa Mipango, Bajeti na Ripoti za Mamlaka ya Serikali za Mitaa leo Mjini Dodoma. Kushoto ni Wagisha Ronald na Hussein Kiranga (Katikati) kutoka Taasisi ya GIZ-TGPSH.

Baadhi ya Maafisa Uchumi, Mipango na Makatibu Afya kutoka Manispaa ya Singida wakijadili jambo wakati wa mafunzo ya Mfumo wa kielektroniki (PlanRep) iliyoboreshwa wa kuandaa Mipango, Bajeti na Ripoti za Mamlaka ya Serikali za Mitaa leo Mjini Dodoma.

Baadhi ya Watumishi mbalimbali wakiwemo Maafisa Uchumi, Mipango na Makatibu Afya kutoka Halmashauri za Mkoa wa Manyara wakifuatilia mafunzo ya Mfumo wa kielektroniki (PlanRep) iliyoboreshwa wa kuandaa Mipango, Bajeti na Ripoti za Mamlaka ya Serikali za Mitaa yanayoratibiwa na Mradi wa Uimarishaji Sekta za Umma (PS3) kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID) leo Mjini Dodoma. (Picha na Beatrice Lyimo)


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Nipashe, Mwananchi Wapewa Onyo na Serikali.

Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi (katikati) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akitoa onyo kwa magazeti ya Mwananchi na Nipashe kwa kuandika vichwa vya habari vinavyohukumu, kulia ni Mkurugenzi Msaidizi kitengo cha Habari, Rodney Thadeus na kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi kitengo cha Usajili, Patrick Kipangula.

Na:  Neema Mathias

Serikali imevionya vyombo vya habari nchini hususan baadhi ya magazeti ambayo yamekuwa na mtindo wa kuandika habari pasi na kuzingatia maadili na weledi wa kitaaluma.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa Idara ya Habari-MAELEZO jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu, Idara ya Habari –MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi alitahadharisha kuwa aina hiyo ya uandishi unaweza kuleta madhara kwa jamii. Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail