Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Majaliwa Akutana na Mkuu wa Majeshi wa India

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mkuu wa Majeshi wa India, Admiral Sunil Lanba Ofisini kwake Jijini Dar es salaam Julai 28, 2017. Kulia ni Mkuu wa Majeshi, Jeneral Venance Mabeyo.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mkuu wa Majeshi wa India, Admiral Sunil Lanba Ofisini kwake Jijini Dar es salaam Julai 28, 2017. Kulia ni Mkuu wa Majeshi, Jeneral Venance Mabeyo.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mkuu wa Majeshi wa India , Admiral Sunil Lanba (kulia kwake) pamoja na ujumbe wake, Ofisini kwake jijini Dar es salaam Julai 28, 2017. Kushoto kwake ni Mkuu wa Majeshi, Jeneral Venance Mabeyo

6042 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akijadili jambo na Mkuu wa Majeshi wa India, Admiral Sunil Lanba (kulia) baada ya mazungumzo yao Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Julai 28, 2017 . Wapili kulia ni Mkuu wa Majeshi Nchini, Jeneral Venance Mabeyo na kushoto ni Balozi wa India Nchini, Sandeep Arya.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Majeshi wa India Admiral Sunil Lanba (wapili Kushoto) na Mkuu wa Majeshi nchini, Jeneral Venance Mabeyo (kushoto) baada ya mazungumzo yao, Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Julai 28, 2017. Kushoto ni Balozi wa India Nchini, Sandeep Arya.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Majeshi wa India Admiral Sunil Lanba (kulia kwake ) na Mkuu wa Majeshi nchini, Jeneral Venance Mabeyo (kushoto kwake ) baada ya mazungumzo yao, Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Julai 28, 2017. Kushoto ni Balozi wa India Nchini, Sandeep Arya.


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Tanzania Kuendeleza Ushirikiano na India-Majaliwa

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali ya Tanzania itaendeleza ushirikiano na Serikali ya India katika nyanja mbalimbali ikiwemo ya ulinzi.

Ametoa kauli leo (Ijumaa, Julai 28 , 2017) alipokutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Majeshi wa India, Bw. Admiral Sunil Lanba jijini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu amesema Tanzania na India ni nchini ambazo zina uhusiano mzuri na wa muda mrefu, ambapo ameahidi kwamba Serikali itaendelea kuudumisha. Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Profesa Mbarawa Asaini Mkataba wa Ushirikiano wa Pamoja wa Usafirshaji

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akipitia mkataba wa makubaliano katika mkutano wa kwanza wa Mawaziri wa usafirishaji na uchukuzi mkoani Kigoma,kuhusu kushirikiana katika miradi ya maendeleo ya pamoja kati ya nchi ya Tanzania, Burundi, Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amesaini mkataba wa ushirikiano katika miradi ya pamoja inayohusu masuala ya usafirishaji na uchukuzi, lengo likiwa ni kuleta maendeleo na kukuza uchumi katika nchi wanachama.

Akizungumza mara baada ya kusaini mkataba huo mkoani Kigoma, Waziri Mbarawa amesema kuwa mkataba huo ambao unahusisha nchi ya Tanzania, Uganda, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), unalenga kuhuisha fursa za kiuchumi katika Ukanda wa Ziwa Tanganyika.

Amesema pamoja na mambo mengine, Mawaziri wa Muungano wa Uchukuzi na Usafirishaji wa Nchi za Ukanda wa Ziwa Tanganyika (LTITS), wamepokea ripoti ya wataalam inayooelekeza utekelezaji wa miradi kwa nchi wananchama ili kufikia malengo yanayotarajiwa. Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Kamati ya Kuzuia Usafirishaji Haramu ya Binadamu Wakutana na Wadau Kujadili Namna ya Kupambana ya Biashara Hiyo

Katibu wa Kamati ya Kuzuia Usafirishaji Haramu wa Binadamu , Seperatus Fella, akizungumza na wadau kutoka Taasisi zinazojihusisha na kupambana na biashara hiyo waliokutana ili kujadili mikakati ya kutokomeza biashaara hiyo nchini leo Jijini Dar es Salam.

Afisa Uchunguzi Sekretarieti ya Kuzuia na Kupambana na Biashara Haramu ya Usafirishaji Binadamu, Ahmed Mwendadi akifafanua jambo kwa wadau kutoka Taasisi zinazopambana na biashara hiyo waliokutana ili kujadili mikakati ya kutokomeza biashaara hiyo leo Jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa ANPPCAN Tanzania, Wilbert Muchunguzi, akieleza jambo juu ya shughuli wanazofanya katika kupambana na Biashara Haramu ya Kuzuia Usafirishaji Binadamu nchini. Kushoto ni Katibu wa Kamati ya Kuzuia Usafirishaji Haramu wa Binadamu, Seperatus Fella.

Mkurugenzi wa kituo cha C-sema, Michael Kehongoh, akieleza jambo juu ya shughuli wanazofanya katika kituo hicho kuunga mkono harakati za kupambana na Biashara Haramu ya Kuzuia Usafirishaji Binadamu nchini. Kushoto ni Katibu wa Kamati ya Kuzuia Usafirishaji Haramu wa Binadamu , Seperatus Fella. (Picha na: Wizara ya Mambo ya Ndani)


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Serikali Haitavumili Kuona Taasisi Zinajiendesha kwa Hasara

Msajili wa Hazina Dkt. Oswaid J. Mashindano akifafanua jambo katika kikao kazi cha uhamasishaji wa sheria mbalimbali za Ofisi ya Msajili wa Hazina, wajibu na majukumu mbele ya Wenyeviti wa Bodi, Watendaji Wakuu wa Taasisi na Mashirika ya Umma pamoja na Makatibu Wakuu wa Wizara leo Jijini Dar es Salaam.Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma za Kimenejimenti kutoka Ofisi ya Msajili wa Hazina Bw. Mihale Mwakabinga na Mkurugenzi wa Uwekezaji wa Umma wa OMH, Bw. Maftah Bunini.

Mkurugenzi wa Huduma za Kimenejimenti wa Ofisi ya Msajili wa Hazina Bw. Mihale Mwakabinga akiwasilisha mada kuhusu majukumu ya Msajili wa Hazina, Bodi na Wizara Mama katika usimamzi wa Mashirika na Taasisi za Umma katika kikao kazi kikao kazi cha uhamasishaji wa sheria mbalimbali za Ofisi ya Msajili wa Hazina, wajibu na majukumu kilichowakutanisha na Wenyeviti wa Bodi za Wakurugenzi,Watendaji Wakuu wa Mashirika na Taasisi za Umma pamoja na Makatibu Wakuu wa Wizara leo Jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Uwekezaji wa Umma kutoka Ofisi ya Msajili wa Hazina akielezea jambo wakati akiwasilisha mada kuhusu maana ya Mashirika ya Umma katika kikao kazi kikao kazi cha uhamasishaji wa sheria mbalimbali za Ofisi ya Msajili wa Hazina, wajibu na majukumu kilichowakutanisha Wenyeviti wa Bodi za Wakurugenzi, Watendaji Wakuu wa Mashirika na Taasisi za Umma pamoja na Makatibu Wakuu wa Wizara leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Msajili wa Hazina Dkt. Oswaid J. Mashindano na Mkurugenzi wa Huduma za Kimenejimenti wa Ofisi ya Msajili wa Hazina Bw. Mihale Mwakabinga.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC), Samwel Mwita Nyantahe akichangia hoja wakati wa kikao kazi baina ya Ofisi ya Msajili wa Hazina na Wenyeviti wa Bodi za Wakurugenzi, Watendaji Wakuu wa Mashirika na Taasisi za Umma pamoja na Makatibu Wakuu wa Wizara leo Jijini Dar es Salaam. Kikao hicho kimefanyika kwa lengo la kuhamasisha sheria mbalimbali za Ofisi ya Msajili wa Hazina, wajibu na majukumu yao.

Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) akichangia mada wakati wa kikao kazi baina ya Ofisi ya Msajili wa Hazina na Wenyeviti wa Bodi za Wakurugenzi, Watendaji Wakuu wa Mashirika na Taasisi za Umma pamoja na Makatibu Wakuu wa Wizara leo Jijini Dar es Salaam. Kikao hicho kimefanyika kwa lengo la kuhamasisha sheria mbalimbali za Ofisi ya Msajili wa Hazina, wajibu na majukumu yao.

Baadhi ya washiriki wa kikao kazi cha uhamasishaji wa sheria mbalimbali za Ofisi ya Msajili wa Hazina, wajibu na majukumu mbele ya Wenyeviti wa Bodi, Watendaji Wakuu wa Taasisi na Mashirika ya Umma pamoja na Makatibu Wakuu wa Wizara leo Jijini Dar es Salaam.

Msajili wa Hazina Dkt. Oswald J. Mashindano akifurahia jambo na Kaimu Mkurugenzi wa Bima ya Maisha na Mafao kutoka Shirika la Taifa la Bima (NIC) Bw. Michael Mowo walipokutana katika kikao kazi cha uhamasishaji wa sheria mbalimbali za Ofisi ya Msajili wa Hazina, wajibu na majukumu kilichowakutanisha Wenyeviti wa Bodi za Wakurugenzi, Watendaji Wakuu wa Taasisi na Mashirika ya Umma pamoja na Makatibu Wakuu wa Wizara leo Jijini Dar es Salaam.

Msajili wa Hazina Dkt. Oswald J. Mashindano akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wenyeviti wa Bodi za Wakurugenzi wa Taasisi na Mashirika ya Umma mara baada ya kumaliza kikao kazi cha uhamasishaji wa sheria mbalimbali za Ofisi ya Msajili wa Hazina, wajibu na majukumu yao leo Jijini Dar es Salaam. Kikao hicho kimewakutanisha Wenyeviti wa Bodi za Wakurugenzi, Watendaji Wakuu wa Taasisi na Mashirika ya Umma pamoja na Makatibu Wakuu wa Wizara. (Picha na: Frank Shija)


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Chanjo ya Homa ya Ini Kupungua Bei Nchini

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika kilele cha Maazimisho ya Siku ya Homa ya Ini Duniani yaliyofanyika leo katika Ofisi ndogo za Wizara ya Afya Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Muhamad Bakari Kambi na Kulia ni Afisa kutoka kitengo cha magonjwa ya Mlipuko Dkt. Azma Simba.

Na: Agness Moshi

Bohari Kuu ya Dawa (MSD) imepunguza gharama ya chanjo ya ugonjwa wa homa ya ini kutoka shilingi 22,000 kufikia shilingi 5,300 ili kusaidia upatikanaji wa chanjo hiyo katika vituo vingi vya tiba hapa nchini hususani vituo vya Umma.

Hayo yamesemwa leo  Jijini Dar es Salaam  na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee  na Watoto Ummy Mwalimu  katika maadhimisho ya siku ya homa ini Duniani  yanayoadhimishwa kila mwaka Julai 28 kama ilivyopendekezwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) Kwa lengo la kuelimisha jamii  na kutambua athari za ugonjwa huo. Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Watoto wa Kike Waaswa Kusoma Masomo ya Sayansi.

Mgeni Rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, anayeshughulukia Muungano na Mazingira January Makamba akizungumza na wahandisi wanawake nchini wakati akizindua kongamano la tatu la wahandisi wanawake nchini mapema hii leo jijini Dar es Salaam.

 

Mgeni Rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, anayeshughulukia Muungano na Mazingira January Makamba (kulia) akimsikiliza Mwenyekiti wa Chama cha Wahandisi Wanawake nchini Mhandisi Alice Isibike akielezea changamoto wanazokutana nazo wahandisi wanawake mapema hii leo wakati wa uzinduzi wa kongamano la tatu la wahandisi wanawake nchini mapema hii leo jijini Dar es Salaam. (PICHA NA ELIPHACE MARWA)

Na. Paschal Dotto

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano Mhe. Janauary Makamba amewaasa watoto wa kike kusoma masomo ya sayansi ambayo yatawawezesha kupata utaalamu katika fani ya uhandisi.

Akizungumza kwa niaba ya Makamu wa Rais katika Tamasha la Wahandisi wanawake(TAWECE) lililofanyika katika ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es salamu Mhe. Makamba amesema kuwa katika juhudi za kujenga taifa la viwanda fani ya uhandisi ni muhimu hivyo watoto wakike hawana budi kuweka kipaumbele katika masomo ya sayansi.

Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Serikali Yapongezwa kwa Kupunguza Ukatili Dhidi ya Watu Wenye Ulemavu wa Ngozi Nchini

Mtaalamu wa Kujitegemea kuhusu kunufaika na haki za binadamu kwa watu wenye ulemavu wa ngozi, Bi. Ikponwosa Ero akiwasilisha taarifa ya utafiti unaoonyesha Tanzania imepiga hatua katika kukabiliana na changamoto zinazowakabili watu wenye Ualbinism mbele ya waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkaazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini Alvaro Rodriguez

Na: Bushiri Matenda

Serikali ya Tanzania imepongezwa kwa jitihada zake za kukabiliana na mashambulizi dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albinism) ambazo zimepelekea kupungua kwa kiasi kikubwa cha vitendo hivyo vya kikatili dhidi yao.

Akiwasilisha Taarifa ya Utafiti wake, Mtaalamu wa Kujitegemea kuhusu kunufaika na haki za binadamu kwa watu wenye ulemavu wa ngozi, Mtaalamu wa kujitegemea Bi. Ikponwosa Ero amesema kuwa Tanzania imepiga hatua kubwa katika kushughulikia kadhia inayowapata watu wenye ulemavu wa ngozi.

“nimefurahishwa na taarifa ya kupungua kwa idadi ya mashambulizi yaliyoripotiwa na naipongeza Serikali ya Tanzania kutokana na juhudi zake  kushughulikia tatizo hilo” alieleza Mataalamu huyo. Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Rais Magufuli Azidi Kupongezwa

Na: Thobias Robert

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amepongezwa na Shirika lisilo la kiserikali la ‘We are all needed’ (WAN) kwa agizo lake la kukataza wanafunzi wenye ujauzito kuendelea na masomo katika shule za Serikali.

Pongezi hizo zimetolewa leo Jijijni Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Shirika hilo, Bi Salome Lwena alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kuunga mkono agizo hilo.

Bi. Lwena amesema kuwa shirika lake liko tayari kumuunga mkono Rais Magufuli katika harakati za kukuza na kuendeleza maadili nchini ikiwemo suala la kupunguza mimba za utotoni. Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail