Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Waziri Mkuu Awaasa Watumishi Wanaofanyakazi Viwandani

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewasihi Watanzania wanaofanya kazi katika viwanda mbalimbali nchini kufanya kazi kwa bidii na kuwa waaminifu.

Amesema Tanzania imedhamiria kukuza uchumi wake kupitia sekta ya viwanda hivyo ni vema watakaopata fursa ya ajira katika viwanda hivyo kuwa waadilifu.

Ameyasema hayo leo (Jumapili, Julai 30, 2017) wakati akizungumza na wafanyakazi wa kiwanda cha gesi cha Ikama kilichoko wilayani Rungwe.

Waziri Mkuu amesema wakati Serikali ikiendelea kuwakaribisha wawekezaji nchini, wananchi walioajiriwa kwenye maeneo hayo wawe waaminifu. Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Ziara ya Waziri Mkuu Wilayani Rungwe

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa umma wa wilaya ya Rungwe Julai 30, 2017. Kulia ni Naibu Spika, Dkt. Tulia Ackson na kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana viongozi wa kiwanda cha chai cha Katumba wilayani Rung wakati alipowasili kiwandani hapo kukagua shuguli za kiwanda hicho Julai 30, 2017.

Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Melela Yapitisha Mpango wa Matumizi ya Ardhi

Na Jacquiline Mrisho 

Kijiji cha Melela kilichopo wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro kimepitisha mpango wa matumizi ya Ardhi chini ya mradi wa Ushiriki wa Wananchi katika Kusimamia Sekta ya Kilimo unaoratibiwa na Shirika lisilo la kiserikali la PELUM.

Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya ya Mvomero, Rugembe Maiga alisema hivi karibuni kuwa mpango huo utasaidia kupunguza migogoro ya ardhi wilayani Mvomero na kulishukuru shirika la PELUM kwa jitihada zao za kupima vipande vya ardhi na kuwakabidhi hatimiliki makundi ya wananchi yasiyojiweza.

“Sisi kama Serikali tunalipongeza sana shirika hili hasa kwa kugusa kundi la watu wasiojiweza ambalo linajumuisha wazee kuanzia miaka 60, wajane, walemavu na watu wenye kipato kidogo kwenye jamii lakini rai yetu kwenu ni kuwaomba kuendelea kutafuta miradi mingine ambayo itahakikisha wanamfikia mwananchi mmoja mmoja wa kijiji hiki ili kila mtu aweze kumiliki hatimiliki ya ardhi yake na hata ikiwezekana kumalizia kupima vijiji 52 vilivyobaki katika Wilaya yetu”, alieleza Maiga. Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Ziara ya Waziri Mkuu Majaliwa Wilayani Kyela

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akivuka lango kuu linalotenganisha Malawi na Tanzania katika mpaka wa nchi hizo katika eneo la Kasumulu Wilayani Kyela Julai 29, 2017. Kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa kwenye eneo la mpaka wa Tanzania na Malawi katika eneo la Kasumulu Wilayani Kyela Julai 29, 2017. Kushoto ni Naibu Spika, Dkt Tulia Ackson Mwansasu na kulia kwa Waziri Mkuu ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi wa Kata ya Njisi Wilayani Kyela wakati alipowasili kwenye uwanja wa michezo kuhutubia mkutano wa hadhara Julai 29, 2017.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia mkutano wa hadhara kwenye Uwanja wa Kata ya Njisi katiak eneo la Kasumulu lililopo kwenye mpaka wa Tanzania na Malawi ktika wilaya ya Kyela Julai 29, 2017.


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Tanzania Siyo Lango la Kupitishia Dawa za Kulevya – Majaliwa

*Aagiza Kuimarishwa kwa Ukaguzi wa Watu, Magari na Mizigo Mipakani

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Tanzania siyo lango la kupitishia dawa za kulevya kwenda nchi za nje hivyo ameagiza ulinzi uimarishwe katika mipaka yote.

Amesema kunatabia ya baadhi ya watu wasiokuwa waaminifu kutumia Tanzania kama njia ya kupitisha dawa za kulevya kwa ajili ya kupeleka nchi za  Afrika ya Kusini, Malawi na Zambia.

Alitoa kauli hiyo jana jioni (Jumamosi, Julai 29, 2017) alipozungumza na watumishi wa kituo cha forodha cha Kasumulu kilicho katika mpaka wa Tanzania na Malawi wilayani Kyela.

Waziri Mkuu alisema ili kuhakikisha jambo hilo linadhibitiwa ni vema ukaguzi wa watu wanaopita kwenye maeneo hayo pamoja na mizigo ukaimarishwa.

“Endeleeni kufanya upekuzi wa kina wa magari, watu na mizigo yote yote katika mipaka yetu. Tanzania siyo lango la kupitishia dawa za kulevya na Serikali haitakubaliana na jambo hilo.” Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Uhamiaji Wafafanua Kuhusu Wafanyakazi wa Acacia kuhojiwa Uwanja wa Ndege

Idara ya Uhamiaji   imesema jukumu la Udhibiti  wa Uingiaji na Utokaji  wa raia  wa kigeni nchini, linatekelezwa kwa mujibu wa Sheria ya Uhamiaji  Sura ya 54 (Rejeo la 2016) na wala  haiwalengi  wafanyakazi  wa  Kampuni ya Madini ya Acacia  peke yake.

 Ni hitajio la kisheria  kwa kila raia wa kigeni  anayeingia na kutoka nchini  kukaguliwa  ili kujiridhisha  iwapo  hakuna  dosari zozote za Uhamiaji, Ulinzi na Usalama.

Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Mhe. Anastazia Wambura autaka Uongozi Wilaya ya Geita kushirikiana na Wasanii Filamu ya Magwangala katika kuiboresha.

Naibu Waziri, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Anastazi J. Wambura (aliyekaa mbele) akiongoza Kikao kilichowakutanisha Waandaaji wa Filamu ya ‘Magwangala’ (hawapo pichani) pamoja na baadhi ya Viongozi wa Mkoa wa Geita kwa ajili ya kutafuta namna ya kuiboresha filamu hiyo ili iweze kuvutiwa zaidi na Watanzania hivi karibuni alipotembelea Mkoani hapo.

Mbunge wa Geita Mjini, Mhe. Constantine J. Kanyasu (aliyesimama) akijibu baadhi ya hoja na kuchangia mada katika Kikao kwa ajili ya kuiboresha filamu ya Magwangala iliyoandaliwa na Wasanii wa Geita 28 Julai, 2017 Mjini Geita.

Mkuu wa Wilaya ya Geita Bw. Herman Kapuf (aliyesimama) akichangia mada katika Kikao kwa ajili ya kuiboresha filamu ya Magwangala iliyoandaliwa na Wasanii wa Geita 28 Julai, 2017 Mjini Geita.

Mfanyabiashara na Mbunge wa Geita vijijini Joseph Musukuma (aliyesimama) akichangia mada kuhusu filamu ya Magwangala ambayo Mhe. Naibu Waziri Anastazia Wambura ameutaka Uongozi wa Wilaya kushirikiana na Waandaaji wa filamu hiyo kwa ajili ya kuioboresha zaidi.

(PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-WHUSM)


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Waziri Mkuu Azindua Meli Mbili Zilizotengenezwa na Kampuni ya Kitanzania

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe kuzindua meli mbili zilizonunuliwa na serikali ili zihudumie wananchi katika ziwa Nyasa . Uzinduzi huo ulifanyika kwenye bandari ya Kiwira wilayani Kyela Julai 29, 2017. Meli hizo zimejengwa na Kampuni ya Kizalendo ya Songoro Marine Transport Limited. Wapili kushoto kwake ni Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson Mwansasu na Kulia kwa Waziri Mkuu ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla.

Moja kati ya meli mbili zilizonunuliwa na serikali na kujengwa na Kampuni ya Songoro Marine Transport Limited ikiondoka kwenye gati la bandari Kiwira wilayani Kyela baada ya kuzinduliwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Julai 29, 2017 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Na Mwandishi Wetu

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amezindua meli mbili za mizigo za Mv Njombe na Mv Ruvuma zitakazotumika katika kusafirishia mizigo kwenye ziwa Nyasa na kuonya kwamba zisitumike kama eneo la kuvushia wahamiaji haramu na dawa za kulevya.

Amesema kukamilika kwa ujenzi wa meli hizo zilizogharimu sh. bilioni 11.253 ni utekelezaji wa ahadi ya Rais Dkt. John Magufuli alizozitoa katika ilani ya uchaguzi ya CCM ya  mwaka 2015-2020 kwa lengo la kutatua changamoto ya usafiri wa abiria na mizigo katika ziwa Nyasa.

Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Waziri Mkuu Atoa Siku Mbili kwa Madiwani Kyela Kumaliza Tofauti Zao

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Songwe kuanza ziara ya mkoa wa Mbeya Julai 28, 2017.

 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Songwe kuanza ziara ya mkoa wa Mbeya julai 28, 2017.

Na Mwandishi Wetu

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa amewapa siku mbili Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela Mkoani Mbeya kumaliza tofauti zao zinazokwamisha utendaji wa Halmashauri hiyo na kuendelea kufanya kazi walizotumwa na wananchi.

Tofauti hizo ambazo zimedumu kwa takriban mwaka mmoja zmesababisha Madiwani hao kushindwa kufanya vikao jambo linalokwamisha shughuli za maendeleo ya wananchi katika Halmashauri hiyo.

Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail