Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Meya Mstaafu Mbeya Matatani

*Ni baada ya kulisababishia Jiji la Mbeya hasara ya sh. bilioni 63

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amemuagiza Kamanda wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Mbeya Bw. Emanuel Kiabo kumkamata na kumuhoji Mheshimiwa Atanas Kapunga aliyekuwa Meya wa Jiji la Mbeya na wenzake 11 kwa tuhuma za kuisababishia Serikali hasara ya sh. bilioni 63.448.

“Serikali hii haiwezi ikawaacha watu hawa ambao wameisababishia hasara kubwa kiasi hiki tena kwa halmashauri moja. Kama wako humu ndani nagiza wakamatwe na waanze kuhojiwa na ambao wamestaafu au kuhamishwa kituo cha kazi wasakwe popote walipo ili nao waje kuhojiwa.”

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Jumatatu, Julai 31, 2017) alipozungumza na watumishi wa Halmashauri za wilaya ya Mbeya na Halmashauri ya Jiji la Mbeya katika mkutano uliofanyika ukumbi wa Benjamin Mkapa. Read more

Dk. Shein Akutana na Wasafirishaji Baharini

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein (katikati) akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji pamoja na Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Usafirishaji Baharini na Uongozi wa Mamlaka ya Usafirishaji Baharini katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein (katikati) akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji pamoja na Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Bandari na Uongozi wa Shirika la Bandari katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akisisitiza jambo wakati alipokuwa akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji pamoja na Uongozi wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Bandari na Uongozi wa Shirika la Bandari katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) alipokuwa akizungumza na Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Meli, Uongozi wa Shirika la Meli pamoja na Uongozi wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo.(Picha na Ikulu, Zanzibar)

Baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la meli wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza na Bodi hiyo na Uongozi wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo.

 

Majaliwa Zungumza na Watumishi wa Manispaa ya Mbeya

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa Umma, Viongozi wa Dini na Viongozi wa Taasisi Binafisi wa Manispaa ya Mbeya kwenye ukumbi wa Benjamin Mkapa jijini Mbeya Julai 31, 2017. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla na Kulia ni Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson.

Baadhi ya Watumishi wa Umma, Viongozi wa Dini na Viongozi wa Taasisi Binafsi wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao kwenye ukumbi wa Benjamin Mkapa jijini Mbeya julai 31, 2017.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Mkuu wa TAKUKURU wa Mkokoa wa Mbeya, Mhandisi Emmanuel Kyabo taarifa zinaoonyesha ubadhirifu uliofanywa na baadhi ya watendaji katika ujenzi wa soko la Mwanjelwa jijini Mbeya ili afanye uchunguzi wa kina na kumshauri Waziri Mkuu hatua zinazostahili kuchukuliwa kwa wanatakaobainika kuwa wamefanya makokosa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Tanzania, Uganda Kushirikiana Kupeleka Umeme Vijiji Vya Mpakani

Mawaziri mbalimbali kutoka Serikali za Tanzania na Uganda wakiwa katika picha ya pamoja baada ya Mkutano wao kuhusu ushirikiano kwenye masuala ya mpakani, uliofanyika mjini Bukoba, Mkoa wa Kagera hivi karibuni.

Na:  Veronica Simba – Kagera

Serikali za Tanzania na Uganda zimetiliana saini Mkataba wa Makubaliano ya Awali (MoU) wa kupeleka umeme kwenye Vijiji vya Mpakani mwa nchi hizo.

Hati ya Makubaliano hayo ilisainiwa mwishoni mwa wiki na Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dk. Augustine Mahiga akiwakilisha Wizara ya Nishati na Madini (Tanzania) na Waziri wa Nishati wa Uganda, Dk. Simon D’Ujanga, wakati wa Mkutano wa Mawaziri wa nchi hizo kuhusu ushirikiano kwenye masuala ya mpakani, uliofanyika mjini Bukoba, Mkoani Kagera.

Makubaliano ya msingi katika Hati iliyosainiwa ni utekelezaji wa Mradi wa kupeleka umeme kwenye vijiji vya Nangoma, katika eneo lililopo mpakani mwa Tanzania na Uganda na vijiji vingine vya maeneo hayo kwa kutokea upande wa Tanzania. Read more

Kamati ya Makinikia ya Tanzania Yaanza Mazungumzo na Barrick Gold Corporation

Waziri wa Sheria na Katiba Profesa Palamagamba Kabudi ambaye pia ni mwenyekiti wa Kamati Maalum iliyoundwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kufanya mazungumzo na uongozi wa Barrick Gold Corporation juu ya biashara ya madini yanayochimbwa na migodi ya kampuni hiyo hapa nchini akiulaki ujumbe wa kampuni hiyo kabla ya kuanza kwa mazungumzo hayo leo tarehe 31 Julai, 2017 Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Sheria na Katiba Profesa Palamagamba Kabudi ambaye pia ni mwenyekiti wa Kamati Maalum iliyoundwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kufanya mazungumzo na uongozi wa Barrick Gold Corporation juu ya biashara ya madini yanayochimbwa na migodi ya kampuni hiyo hapa nchini akizungumza akiwa na Afisa Mwendeshaji Mkuu wa kampuni hiyo Bw. Richard Williams kabla ya kuanza kwa mazungumzo hayo leo tarehe 31 Julai, 2017 Jijini Dar es Salaam. (Picha na: Ikulu)

Waziri wa Sheria na Katiba Profesa Palamagamba Kabudi ambaye pia ni mwenyekiti wa Kamati Maalum iliyoundwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akifanya mazungumzo na uongozi wa Barrick Gold Corporation juu ya biashara ya madini yanayochimbwa na migodi ya kampuni hiyo hapa nchini akipata picha ya pamoja na ujumbe wa kampuni hiyo kabla ya kuanza kwa mazungumzo hayo leo tarehe 31 Julai, 2017 Jijini Dar es Salaam

Tanzania Excels in Statistical Capacity among Sub-Saharan African Nations, WB Report Shows.

A graph showing Tanzania as a second country among  Sub – Saharan countries in better statistical capacity. According to the World Bank report, Tanzania scored 90 percent for periodicity, 80 percent for source data and 50 percent for methodology which contributed to an overall of 73.3 percent.

By Veronica Kazimoto-NBS.

Tanzania has been ranked second, behind South Africa in statistical capacity among Sub-Saharan African nations.

This is according to the World Bank (WB) 2016 Statistical Capacity Indicator (SCI).

WB has been assessing national statistical capacity in developing countries since 2004 and has produced overall SCI score as well as scores for three categories, Methodology, Source Data and Periodicity. Regional overall and specific category SCI are also produced to allow for comparison.

For every dimension, a country is scored against specific criteria, using information available from the WB, IMF, UN, UNESCO, and WHO.
A composite score for each dimension and an overall score combining all three dimensions are derived for each country on a scale of 0 – 100. A score of 100 indicates that the country meets all the criteria.

The statistical methodology aspect measures a country’s ability to adhere to internationally recommended standards and methods, by assessing guidelines and procedures used to compile macroeconomic statistics and social data reporting and estimation practices by looking at an updated national accounts base year, use of the latest Balance of payment, external debt reporting and IMF’s Special Data Dissemination Standard and enrollment data reporting to UNESCO.

On source data, this measures data collection activities in line with internationally recommended periodicity, and whether data from administrative systems are available and reliable for statistical estimation purposes and periodicity of population and agricultural censuses, the periodicity of poverty and health related surveys, and completeness of vital registration system coverage.

The third aspect concerned with the periodicity and timeliness looks at the availability and periodicity of key socio-economic indicators of which nine are MDG indicators.

Tanzania scored 90 percent for periodicity, 80 percent for source data and 50 percent for methodology which, contributed to an overall SCI of 73.3 percent. Although this overall score ranks Tanzania as second behind South Africa (82.2%) there is still room for improvements, especially in methodology.

The National Bureau of Statistics (NBS) is committed to continuing strengthening of the National Statistical System.

Wanariadha 8 Kuiwakilisha Tanzania Nchini Uingereza.

Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akiwahutubia Wanariadha (hawapo pichani) watakaoiwakilisha Tanzania katika Mashindano ya Mbio nchini Uingereza.

Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akiwahutubia Wanariadha (hawapo pichani) watakaoiwakilisha Tanzania katika Mashindano ya Mbio nchini Uingereza.

Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania (DSTV) Bw. Maharage Chande akiwahutubia Wanariadha (hawapo pichani) watakaoiwakilisha Tanzania katika Mashindano ya Mbio nchini Uingereza.

Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akiwakabidhi Bendera ya Taifa Wanariadha watakaoiwakilisha Tanzania katika Mashindano ya Mbio nchini Uingereza.

Hawa ni baadhi ya Wanariadha wakiwa pamoja na Makocha wao ambapo jumla ya Wanariadha watakaoiwakilisha Tanzania katika mbio nchini Uingereza ni nane (8) na wanatarajia kuanza safari yao hapo kesho 1 Agosti, 2017.

(Picha zote na Anitha Jonas)