Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

TIC Yawafunda Wajasiriamali

Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Uwekezaji Bw. John Mnali akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mafunzo hayo leo Jijini Dar es Salaam.

Na: Frank Mvungi

Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimewataka Wajasiriamali nchini kujiamini na kutumia fursa zilizopo ili kukuza biashara zao na kuchochea ukuaji wa uchumi.

Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Uwekezaji wa TIC, Bw. John Mnali AMETOA WITO HUO wakAti wa mafunzo ya siku moja kwa wajasiriamali yaliyolenga kuwajengea uwezo wa kuzalisha bidhaa zinazokidhi mahitaji ya soko kwa kuzingatia ubora.

Akifafanua Mnali amesema mafunzo hayo ni fursa kwa wajasiriamali wakati na wadogo kukutana na wajasiriamali wakubwa waliowekeza hapa nchini hali itakayochochea kuongeza ubora wa bidhaa na huduma wanazotoa. Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Serikali Yajipanga Kukuza Lugha ya Kiswahili

 

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe akiongea wakati wa sherehe za kuadhimisha miaka 60 ya Idhaa hiyo hapa nchini. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Kiswahili kutoka Chuo Kikuu cha Nairobi, Profesa Riyah Timamy. Maadhimisho hayo yalifanyika jana Jijini Dar es Salaam.

Na: Zawadi Msalla

Serikali imeahidi kuweka misingi madhubuti ya kukuza lugha ya Kiswahili kwa kuhakikisha lugha hiyo inatumika katika ngazi mbalimbali ikiwemo kufundishia katika taasisi za kielimu, Mahakamani na Bunge.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe wakati wa maadhimisho ya miaka 60 ya kuanzishwa kwa Idhaa ya Kiswahili ya Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC)jana Jijini Dar es Salaam. Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Zaidi ya Nchi 30 Kushiriki Sabasaba

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) Bw.Edwin Rutageruka akiongea na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam. (Picha na: Frank Shija)

Na: Frank Mvungi

Wananchi wametakiwa kujitokeza kwa wingi kushiriki maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam yaliyoanza mapema leo jijini Dar es salaam yakihusisha zaidi ya makampuni 2500 ya ndani na jumla ya nchi 30 zikishiriki.

Kauli hiyo imetolewa Leo na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa  Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tan Trade)  Bw. Edwin Rutageruka wakati wa mahojiano maalum kuhusu maonesho hayo. Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Jeshi la Zimamoto Lafanikiwa Kuzima Moto Jijini Dar es Salaam

Watanzania wenye asili ya kihindi wakiwa kwenye kifaa kinachotumika na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, baada ya jengo lililopo Mtaa wa Indira Ghandhi,jijini Dar es Salaam, kushika moto ambao ulifanikiwa kuzimwa na askari wa jeshi hilo kabla haujaleta madhara.Chanzo cha moto huo bado hakijajulikana.

Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, wakiwa katika shughuli za uzimaji moto baada ya jengo lililopo Mtaa wa Indira Ghandhi,jijini Dar es Salaam,kushika moto ambao ulifanikiwa kuzimwa na askari wa jeshi hilo kabla haujaleta madhara.Chanzo cha moto huo bado hakijajulikana. 

Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Makamu wa Rais Awaasa Waendesha Mashtaka, Wapelelezi Kuepuka Rushwa

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa Uzinduzi wa Mwongozo kwa Wapelelezi na Waendesha Mashitaka wa Kesi za Wanyamapori na Misitu kwenye ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. (Picha na: OMR)

Na: Mwandishi Wetu

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amewaagiza wapelelezi na waendesha mashtaka nchini kuepuka vitendo vya rushwa na badala yake wafanye kazi kwa bidii kwa kuweka mbele maslahi ya taifa.

Makamu wa Rais ametoa agizo hilo wakati akizindua  mwongozo kwa wapelelezi na waendesha mashtaka wa kesi za wanyamapori na misitu. Uzinduzi huo umefanyika leo katika Lituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius kilichopo Jijini Dar es Salaam amabpo amewataka wapelelezi na waendesha mashtaka kuchukua hatua stahiki dhidi ya watu wanaoiba rasilimali za taifa.

Amesema mwongozo aliouzindua utasaidia kwa kiwango kikubwa Kuboresha shughuli za upelelezi na uendeshaji wa kesi zinazohusu wanyapori na misitu nchini. Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Dawasa Yapongezwa Kwa Utendaji

Meneja wa Kituo cha uzalishaji maji Ruvu Juu Bw. Emmanuel Makusa (katikati) akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof. Kitila Mkumbo (kushoto) wakati wa ziara yake ya kukagua miradi inayotekelezwa na DAWASA katika Mikoa ya Pwani na Dar es Salaam mapema jana.

Na: Frank Mvungi

Serikali imesema imeridhishwa na Utendaji kazi wa Mamalaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA)  katika kutekeleza miradi mikubwa ya maji kwa kuzingatia Sheria na Kanuni hali inayoongeza tija katika mamlaka hiyo.

Akizungumza wakati wa ziara ya kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa na DAWASA  katika Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani  Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof. Kitila Mkumbo amesema moja ya miradi hiyo ni ule wa kupanua na kusambaza maji katika mji wa Chalinze utakaonufaisha wakazi zaidi ya laki mbili.

“Kwa ujumla naridhishwa na kazi inayofanywa na DAWASA  katika kutekeleza miradi  ya maji nawatia moyo muendelee kufanya kazi hii  kwa bidii ili azma ya Serikali kuwafikishia wananchi huduma ya maji kwa wakati itimie” Alisisitiza Prof. Mkumbo. Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Serikali Kushirikiana na Halmashauri Kuboresha Barabara

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani, akitazama taarifa ya makadirio ya gharama za ujenzi wa sehemu ya barabara ya Mboga kuelekea kiwanda cha Matunda cha Sayona, wilayani Bagamoyo, leo. Kulia ni Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), Mkoa wa Pwani Eng. Rehana Yahya.

Na: Mwandishi Wetu

Serikali imesema kuwa itashirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo katika kutoa wataalam, kuandaa michoro na kusimamia ujenzi wa barabara zote zinazoingia katika viwanda vinavyojengwa mkoani Pwani.

Akizungumza leo mkoani humo, Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani, amesema kuwa hatua hiyo imefikiwa baada ya uongozi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo kuandika barua kwa Wizara kuomba msaada wa kujengewa barabara ya Kilometa moja inayoingia kwenye kiwanda kipya cha Matunda cha Sayona kutoka kwenye barabara kuu ya Chalinze – Arusha na ile iliyopo katika kiwanda cha Twyford kinacho tengeneza marumaru na masinki. Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Rais Dkt Magufuli Akutana na Wataalamu wa Nishati Kutoka Ethiopia na Tanzania, Akutana Pia na Kamati za Uchunguzi wa Mchanga wa Madini (Makinikia)

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi (kulia) akiongea na Waziri wa Maji, Umwagiliaji na Umeme wa Ethiopia Dkt. Ing Seleshi Bekele anayaongoza ujumbe kutoka kwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo iliyopo nchini kusaidia mchakato wa ujenzi wa Dam (bwawa la kuzalisha umeme) la Steigler’s Gorge kabla ya kukutana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 28, 2017

Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Rais Magufuli Kufungua Maonesho ya Biashara Sabasaba

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage akizungumza katika moja ya matuki ya wizara hiyo.(Picha ya Maktaba)

Na: Mwandishi Wetu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, anatarajiwa kufungua Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam maarufu kama Sababsaba Julai Mosi mwaka huu.

Kwa mujibu wa taarifa kwa Vyombo vya Habari iliyotolewa na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage, Rais atafanya ufunguzi huo katika Uwanja wa Maonesho wa Mwalimu Julius Nyerere, Barabara ya Kilwa Jijini Dar es Slaam. Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail