Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari

Majaliwa: Biashara ya Dawa za Kulevya Kuwa Historia

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imeadhimia kupambana vilivyo dhidi ya biashara haramu ya dawa za kulevya na kuhakikisha inakuwa historia nchini.

Pia ametoa wito kwa wazazi wote nchini waendelee kufuatilia nyendo za watoto ili wasijiingize kwenye mtego wa dawa za kulevya na wala wasisubiri vijana wao waanze kutumia.

Ametoa kauli hiyo leo (Alhamisi, Juni 29, 2017) kwenye maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya Duniani, iliyoadhimishwa mjini Dodoma.

Kufuatia hali hiyo Waziri Mkuu amesema Serikali imejidhatiti kuhakikisha kuwa uzalishaji, usambazaji na matumizi ya dawa za kulevya unadhibitiwa kikamilifu nchini.

Amesema katika kutimiza azma hiyo, ambayo pia inaelekezwa na Ilani ya Uchaguzi ya CCM, Serikali ilifanya mabadiliko ya Sheria ya Dawa za Kulevya kwa kuanzisha chombo cha kisheria cha kupambana na biashara hiyo, ambayo imeongeza adhabu kwa wanaoshiriki.

Waziri Mkuu amesema Serikali itaendelea kuimarisha chombo hicho kinachoongoza mapambano ya dawa za kulevya ili kiendelee kufanya kazi kwa weledi na kwa kutumia mbinu za kisayansi.

“Tunaponadi uchumi wa viwanda lazima tuwe na nguvu kazi yenye siha njema kuweza kushiriki kwenye kazi halali za kujenga Taifa letu na yeyote anayetaka kudhohofisha nguvu kazi ya Taifa letu au kuhujumu jitihada za uchumi wa viwanda atashughulikiwa bila huruma,” amesema.

Aidha, kauli mbiu ya maadhimisho hayo kitaifa ni ‘Tuwasikilize na Kuwashauri Vijana na Watoto ili Kuwaepusha na Dawa za kulevya.’

Waziri Mkuu amesema kauli mbiu hiyo imetokana nan a takwimu za waathirika wakubwa wa dawa za kulevya ambao ni vijana wenye umri kati ya miaka 15-35.

“Hili ndilo kundi kubwa kwenye jamii jetu na ndilo tegemeo kubwa kwa ustawi wa nchi yetu. Hili ndilo kundi litakalotoa askari wa kulinda Nchi yetu, wanasiasa wa kuongoza Taifa letu na wataalamu mbalimbali wa kuisaidia Tanzania,” amesema.

Awali Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu), Mheshimiwa Jenista Mhagama alisema matumizi ya dawa za kulevya yamelisababishia Taifa madhara makubwa ya kiafya na  kiuchumi hivyo kila mwananchi ashiriki katika mapambano hayo.

Mapema Waziri Mkuu aliweka jiwe la msingi la Kituo cha Kutoa Huduma ya Tiba kwa Waathirika wa Dawa za Kulevya katika eneo la Itega mkoani Dodoma na kuwashauri wakazi wa mkoa huo kutojihusisha na biashara hiyo.

IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU,

S. L. P. 980,

DODOMA.

ALHAMISI, JUNI 29, 2017

 


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Wananchi Waendelea Kumiminika Sabasaba

Baadhi ya wananchi wakiingia katika viwanja vya maonesho ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayoendela katika viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere Jijini Dar es Salaam. Maonesho hayo ni 41 yameanza jana tarehe 28 Juni na yanatarajia kufikia kilele tarehe 8 Julai 2017ni ya 41 ambapo yanahusisha wafanyabiashara kutoka nchi mbalimbali duniani.

Baadhi ya samani zinazotengenezwa ndani ya nchi. (Picha na: Frank Mvungi)


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Wataalam wa Afya Watakiwa Kufanya Tafiti za Kisasa

 

Na: Fatma Salum 

Serikali imetoa rai kwa wataalamu wa sekta ya afya nchini kufanya tafiti nyingi za kisasa ili kuboresha huduma za afya na kuliwezesha taifa kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu.

Rai hiyo imetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla kwa niaba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Tano la Wanasayansi lililoandaliwa na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS).

Kigwangalla alisema kuwa ili kufanikisha upatikanaji wa huduma bora za afya kwa watu wote nchini, ni muhimu wataalamu waka kaa pamoja na kujadili namna bora ya kufanya tafiti zenye tija, ambazo zitasaidia kupata ufumbuzi wa changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya afya. Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Wanafunzi Wanaopata Mimba Watafutiwe Programu Nyingine za Masomo

Na: Lilian Lundo

Taasisi isiyo ya Kiserikali inayojihusisha na utafiti wa maadili ya wanafunzi  Shule za Msingi na Sekondari hapa nchini, “Maadili Centre” imeshauri Wanafunzi wanaopata mimba kutorudi shuleni badala yake watafutiwe program nyingine za masomo kama vile masomo ya ufundi katika vyuo vya VETA.

Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Florentina Senya ameyasema hayo leo, Jijini Dar es Salaam alipokuwa akiongea na waandishi wa habari juu ya maoni mbalimbali yaliyokusanywa na taasisi hiyo kuhusu mtoto akipata mimba, mara anapojifungua aruhusiwe aendelee na masomo au la?

“Msimamo wa Maadili Centre ni kwamba haiwezekani wanafunzi wanaopata mimba wakiwa shuleni kuendelea na masomo,” amesema Senya. Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Mawakili Watakiwa Kujikita Vijijini

Mgeni Rasmi Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Hamis Juma (wanne toka kushoto waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Majaji na Mawakili wapya mara baada ya kuwaapisha mapema hii leo katika viwanja vya Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam.(Picha na: Eliphace Marwa)

Na. Eliphace Marwa

Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Hamis Juma amewataka Mawakili wapya kufanya kazi kwa kuzingatia maadili ya taaluma ya uwakili na kutumia taaluma zao kwa kutoa msaada wa kisheria kwa jamii.

Aliyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam wakati wa Sherehe za 56 ya kuwapokea na kuwaapisha Mawakili wapya 248 iliyofanyika katika viwanja vya Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam.

Mgeni Rasmi Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Hamis Juma (katikati) akifuatilia jambo wakati wa sherehe za 56 za kuwakubali na kuwasajiri, Mawakili wapya 248 mapema hii leo katika viwanja vya Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam.

Aidha Kaimu Jaji Mkuu amewahimiza Mawakili wapya kujiendeleza kitaaluma kwa sababu kuwa wakili sio mwisho wa taaluma kwani wanahitajika kusoma sheria za nchi mbalimbali Duniani ili kuweza kuingia mikataba ya kimataifa.

Alisema mawakili wapya wanatakiwa washiriki katika kutoa haki, wawe waaminifu kwa mahakama na wateja kwani wakienda kinyume haki itapotea.

“Mawakili wote wanatakiwa kuwa waaminifu kwa wateja wanaowahudumia na kushirikiana na mahakama katika kutoa haki na wasiwe mawakala wa rushwa bali wawe mawakala wa kutenda haki,” alisema Kaimu Jaji Mkuu Prof. Ibrahim.

Baadhi ya ndugu wa Mawakili wapya wakisubiri zoezi la kuapishwa kwa ndugu zao mapema hii leo katika viwanja vya Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam.

Aidha Kaimu Jaji Mkuu aliwataka mawakili hao kufika maeneo ya nje ya mji ili wasaidie upatikanaji wa haki kwani kumekuwa na changamoto kubwa ya mawakili katika maeneo ya nje ya miji.

Naye Rais wa Chama cha Wanasheria cha Tanganyika (TLS) Tundu Lissu amewataka Mawakili hao kutumia taaluma hiyo katika kuisaidia jamii kujua haki zao na utawala wa sheria japo kuna changamoto mbalimbali zinazoikabili tasnia ya sheria nchini.

Baadhi ya Mawakili wapya wakisubiri zoezi la kuapishwa mapema hii leo katika viwanja vya Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam.

“Napenda kuwatakia kila la kheri mawakili hawa wapya ila niwaombe watumie taaluma hii kwa kuisaidia jamii kujua haki zao pamoja na utawala wa sheria,” alisema Mh. Tundu Lissu.

 Idadi ya mawakili walioapishwa leo imepelekea Tanzania kuwa na idadi ya zaidi ya mawakili 6300.


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Atembea Kilometa 500 Kumuunga Mkono Magufuli

Na: Jonas Kamaleki

Mkazi wa Mkoa wa Iringa, Thomas Lubinza ametembea zaidi ya kilometa 502 kutoka Iringa mpaka Dar es Salaam kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kwa jitihada zote anazozifanya katika kulinda na kusimamia raslimali za watanzania.

Akizungumza na waandishi wa habari, Lubinza amasema kuwa Rais Magufuli kwa kipindi kifupi cha uongozi wake ameweza kufanya mambo makubwa ikiwemo kudhibiti na kupambana na vitendo vya rushwa, kurudisha nidhamu serikalini na kuboresha miundombinu.

Licha ya juhudi hizi zinazofanywa na Mhe. Magufuli,wapo ambao wanabeza jitihada hizi na wengine kukejeli, alisema Lubinza na kuongeza kuwa yeye ameona ni vyema ajitokeze kumpongeza. Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

UWASA Wapongeza Jitihada za JPM Katika Sekta Ya Misitu

: Mwenyekiti wa Umoja wa Wavunaji Sao Hill(Uwasa) Chritian Ahia akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Naibu Katibu wa umoja huo Bw. Alex Crispin Ngogo na Katibu Mkuu wa umoja huo Dkt. Brazil Tweve.

Na. Immaculate Makilika

Umoja wa Wavunaji Sao Hill (UWASA) pamoja na Wadau wa mazao ya miti wamepongeza jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli za ugawaji wa malighafi za misitu  kwa wenye viwanda vya mbao.

 Akizungumza na waandishi wa habari  leo jijini Dar es salaam, Mwenyekiti wa UWASA, Christian Ahia pamoja na wadau wa mazao ya miti  wamesema kuwa hatua hiyo itawasaidia katika  kuboresha na kupanua soko la mbao hapa nchini.

 “Tunaipongeza  serikali kwa hatua nzuri iliyofikia ambapo imetoa vibali 421  kwa wawekezaji wa viwanda vya kuchakata mbao huko Mafindi mkoani Iringa, ukilinganisha na    vibali 1,000  vilivyokuwa vimetolewa awali kwa watu ambao hawakuwa na wawekezaji halali wa mbao” alisema Ahia. Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Majaliwa: Zuio la Usafirishaji Chakula Nje Liko Pale Pale

Taarifa Kwa Umma

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema msimamo wa Serikali wa kuzuia usafirishaji wa chakula kwenda nje ya nchi uko pale pale.

Pia amesema mahindi iliyokamatwa mkoani Kilimanjaro yakisafirishwa kwenda nje ya nchi yataingizwa kwenye Hifadhi ya Taifa ya Chakula (NFRA) na magari yatabaki polisi.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo ( Alhamisi Juni 29, 2017) Bungeni mjini Dodoma wakati wa kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri  Mkuu wakati akijibu swali la Mheshimiwa Ritha Kabati  (Viti Maalumu) aliyetaka ufafanuzi kuhusu zuio la kusafirisha mazao nje ya nchi kwa mikoa yenye chakula cha ziada.

“Tumedhibiti na kuzuia usafirishaji wa chakula hasa mahindi kwenda nje ya nchi ili kuliepusha Taifa kukumbwa na baa la njaa kutokana na baadhi ya mikoa kutopata mavuno ya kutosha,” Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail