Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Wabunge Kuingia Darasani Somo la Maadili

Afisa Uhusiano wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu JK Nyerere Bi Evelyn Mpasha (kushoto) akifurahia Jambo na baadhi ya wananchi waliotembelea banda la Chuo hicho katika maonesho ya Sabasaba yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julias.K Nyerere,barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam.

Na: Lilian Lundo

Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kinatarajia kufundisha programu ya uongozi maadili na utawala bora kwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo watasoma kwa awamu, mara baada ya kumalizika kwa Bunge la Bajeti.

Hayo yamesemwa na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Chuo hicho, Evelyne Mpasha leo jijini Dar es Salaam katika maonesho ya saba saba  ya 41 yanayoendelea Jijini humo.

Alisema Chuo hicho kimejizatiti kurejesha maadili kwa viongozi na Watanzania kupitia programu ya uongozi ya maadili na utawala bora inayotolewa chuoni hapo. Read more

Matukio Katika Picha Ndani ya Sabasaba

Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage akisisitiza jambo wakati wa mkutano na waadishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam kuhusu ufunguzi wa maonesho ya 41 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (Sabasaba).yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu J.K Nyerere,barabara ya Kilwa.

Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage akikagua moja ya mabanda katika maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba).

Naibu Balozi waUjerumani nchini Mhe. John Reyels akiongea na waandishi wa habarikuhusu dhamira ya nchi yake kuwekeza katika Viwanda hapa nchini ili kuunga mkono juhudi za Serikali kujenga uchumi wa Viwanda. Kushoto ni Mkurugenzi mkazi wa ujumbe wa wafanyabiashara kutoka Ujerumani waliowekeza Kanda ya AfrikaMashariki, kulia ni Mkuu wa Masoko na Mawasilia no wa Kampuni ya GMBH ya Ujerumani.

Mkurugenzi Mkazi wa ujumbe wa wafanyabiashara kutoka Ujerumani waliowekeza Kanda ya Afrika Mashariki Bi MarenDiale –Schellschmidt akizungumzia ufunguzi wa Ofisi zaTaasisi hiyo hapa nchini ili kuchochea uwekezaji kutoka Ujerumani. (Picha zote na: Frank Mvungi-MAELEZO)

Serikali Yazungumzia Mauaji Kibiti

Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani), baada ya kufanya kikao na viongozi wa ngazi za juu wa Jeshi la Polisi kuhusiana na uhalifu katika maeneo ya Kibiti,Mkuranga na Ikwiriri,mkoani Pwani.Mkutano huo umefanyika katika Ukumbi wa polisi makao makuu,jijini Dar es Salaam.

Na. Eliphace Marwa

Naibu Waziri Mambo ya Ndani ya Nchi Masauni  Hamad Masauni amekutana na vingozi waandamizi wa Jeshi la Polisi katika kikao cha kujadili hali ya ulinzi na usalama nchini  mara baada ya kufanya ziara hapo jana katika Mkoa wa Pwani.

Akizungumza na waandishi wa habari  mara baada ya kikao hicho Naibu Waziri Masauni Hamad Masauni amewataka wananchi kuwa na amani kwani vyombo vya ulinzi na usalama vinafanya kazi kubwa ya kupambana na uhalifu nchini. Read more

Tanzania Kupata Umeme wa Megawati 5000 Ifikapo 2021

Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dk. Medard Kalemani ( wa pili kulia kutoka kulia) akimwongoza Waziri wa Maji, Nishati na Umwagiliaji kutoka Ethiopia, Dk. Seleshi Bekele kwenye ziara ya kukagua eneo la ujenzi wa mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia nguvu za maji la Stiegler’s Gorge, Rufiji mkoani Pwani.

Na Greyson Mwase, Rufiji.

Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dk. Medard Kalemani amesema Tanzania inatarajia kupata umeme wa uhakika wa Megawati 5000 ifikapo mwaka 2021, mara baada ya kukamilika kwa mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia  nguvu za maji katika maporomoko ya maji ya Mto Rufiji.

Dk. Kalemani aliyasema hayo katika ziara ya Waziri wa Maji, Nishati na Umwagiliaji kutoka  Ethiopia, Dk. Seleshi Bekele aliyeambatana na wataalam wa masuala ya ujenzi wa mitambo  ya kuzalisha umeme kwa kutumia maji kutoka  Ethiopia kwenye eneo  la mradi uliopo  Rufiji mkoani Pwani. Read more

Prof. Mbarawa Aridhishwa na Ujenzi wa Jengo la 3 la Abiria JNIA

Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania Prof. Ninatubu Lema, (aliyenyoosha mikono) akimweleza jambo Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (wa tatu kutoka kulia), leo wakati akianza ziara ya kutembelea jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA_TBIII).

Na: Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Ujenzi

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amekagua ujenzi wa jengo la Tatu la Abiria la uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), na kuelezea kuridhishwa kwake kwa hatua ya ujenzi iliyofikiwa.

Akizungumza mara baada ya kukagua ujenzi huo Waziri Profesa Mbarawa amemhakikishia mkandarasi BAM International anayejenga jengo hilo kuwa Serikali italipa madai yake kwa wakati kwa kadri atakavyoyawasilisha.

Meneja wa Mradi wa Jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA-TBIII), Bw. Ray Blumrick (kushoto) akitoa ufafanuzi wa kuhusu ujenzi wa jengo hilo, kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof Makame Mbarawa (wa tatu kutoka kushoto).

“Nia yetu ujenzi huu ukamilike ifikapo Septemba mwakani, hivyo tunamtaka mkandarasi kuongeza kasi ya ujenzi na wasimamizi kumsimamia kikamilifu ili vifaa vinavyofungwa katika jengo hilo viwe na ubora uliokusudiwa na vidumu kwa muda mrefu”, amesisitiza Profesa Mbarawa.

Prof. Mbarawa amesema kukamilika kwa jengo la tatu la abiria la uwanja wa ndege wa Julius Nyerere kutawezesha uwanja huo kuweza kuhudumia abiria wapatao milioni nane na  nusu kwa mwaka na hivyo kukuza uchumi wa nchi kwa kuwezesha watalii na wageni wengi zaidi kufika nchini.

Mhandisi Simba Charles (aliyenyoosha mkono) akionesha eneo la maegesho ya magari kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (katikati), leo alipofanya ziara ya kutembelea ujenzi wa jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere.

Meneja Mradi wa jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA-TBIII) Bw. Ray Blumrick akimwelekeza namna paa lilivyo imara, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa wakati wa ziara yake kwenye jengo hilo leo.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Profesa Ninatubu Lema amemhakikishia Waziri Prof. Mbarawa kuwa ujenzi huo unasimamiwa kikamilifu na utamalizika kwa wakati.

“Kama wasimamizi tumejipanga kuhakikisha zoezi la ufungaji vifaa katika jengo hili, linakamilika kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa,” amesisitiza Prof. Lema.

Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri (MAB) ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Prof Ninatubu Lema akifafanua jambo mbele ya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Prof. Makame Mbarawa (wa pili kutoka kushoto) leo alipofanya ziara ya kutembelea jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere. Kulia ni Mkurugenzi wa Fedha wa TAA, Bw. Richard Malulu.

Naye Meneja ujenzi wa BAM International, Bw. Rey Blumrick amesema kazi iko katika hatua nzuri na itakamilika kwa wakati.

Mradi wa ujenzi wa jengo la tatu la abiria ni sehemu ya uboreshaji wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere lengo likiwa ni kuwezesha ndege na abiria wengi kutumia uwanja huu na kuhuisha sekta ya usafiri wa anga hapa nchini.

Maegesho ya Kivuko Lindi Kukamilika Mwezi Novemba Mwaka Huu

Meneja wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS). Mkoa wa Lindi,Eng. Issack Mwanawima (mwenye koti la draft), akimweleza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kushoto), hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa maegesho hayo, Mkoani humo, wakati Waziri huyo alipotembelea mradi huo hivi karibuni.

Serikali imesema ujenzi wa maegesho ya kivuko Mkoani Lindi utakamilika mwezi Novemba mwaka huu ili kurahisisha usafirishaji wa abiria na mizigo kwa wakazi wa eneo la Kitunda Mkoani Lindi.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa alipokagua maendeleo ya ujenzi  wa maegesho hayo na kusema ujenzi huo umegharimu kiasi cha Tsh, bilioni 1.8 ambazo zitahusisha maegesho ya Kivuko na kujenga barabara ya kiwango cha lami mita 150 upande wa Kitunda Mkoani Lindi. Read more

Rais Dkt. Magufuli Akutana na Kufanya Mazungumzo na Waziri na Mambo na Nje na Norway Borge Brende Ikulu Jijini Dar Es Salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway Borge Brende aliyeambatana na ujumbe wake Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway Borge Brende wanne kutoka (kushoto), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Augustine Mahiga wanne kutoka (kulia)pamoja na vingozi wengine wa Tanzania na Norway mara baada ya mazungumzo Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway Borge Brende mara baada ya mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwatazama Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway Borge Brende wakati akizungumza jambo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Augustine Mahiga Ikulu jijini Dar es Salaam.
Picha na: Ikulu

Prof. Mbarawa Aridhishwa na Ujenzi wa Jengo la 3 la Abiria JNIA

Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania Prof. Ninatubu Lema, (aliyenyoosha mikono) akimweleza jambo Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa  (wa tatu kutoka kulia), leo wakati akianza ziara ya kutembelea jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA_TBIII).

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amekagua ujenzi wa jengo la Tatu la Abiria la uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), na kuelezea kuridhishwa kwake kwa hatua ya ujenzi iliyofikiwa.

Akizungumza mara baada ya kukagua ujenzi huo Waziri Profesa Mbarawa amemhakikishia mkandarasi BAM International anayejenga jengo hilo kuwa Serikali italipa madai yake kwa wakati kwa kadri atakavyoyawasilisha.

Read more

Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Yapongezwa kwa Kufungua Kituo cha Urithi wa Ubunifu Majengo na Utalii

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi. Nuru Millao akitoa hotuba kwa niaba ya Waziri wa Wizara hiyo Mhe.Dkt. Harrison Mwakyembe katika hafla ya kufungua kituo cha Urithi wa Ubunifu Majengo  na Utalii kilichopo katika jengo la Old Boma leo Jijini Dar es Salaam.

Na Lorietha Laurence- WHUSM.

NAIBU Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi. Nuru Millao  ameupongeza Uongozi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa kulifanya jengo la Old Boma kuwa Kituo cha Urithi wa Ubunifu wa Majengo na Utalii (DARCHI).

Akizungumza katika hafla ya kufungua  kituo  hicho leo Jijini Dar es Salaam kwa niaba ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt.Harrison Mwakyembe, Millao alisema hatua hiyo inadhihirisha dhamira ya Serikali ya kuhakikisha kuwa utamaduni wa Mtanzania unadumishwa na kukuzwa.

Read more