Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Serikali Yatoa Bilioni 13 Kumalizia Ujenzi MOI

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu (MOI), Dkt. Respicious Boniface akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku nne kwa madaktari kutoka nchi mbali mbali za Afrika, Kushoto ni Daktari bingwa wa MOI, Dkt. Edmund Ndalama.Ufunguzi huo umefanyika leo Jijini Dar es Salaam.

Na Jacquiline Mrisho.

Serikali imetoa jumla ya shilingi bilioni 13.5 kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa awamu ya tatu wa jengo jipya la Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu (MOI) linalotegemewa kukamilika na kuanza kutumika kwa asilimia mia moja mwaka huu.

Hayo yamebainishwa leo Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Dkt. Respicious Boniface alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku nne ya madaktari kutoka nchi mbali mbali za Afrika.

Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

WCF yawataka Waajiri Kutii Sheria Bila Shuruti

Makamu Mwenyekiti kutoka Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Radhimina Mbilinyi akifungua Semina ya uelimishaji kwa Waajiri kuhusu haki na wajibu wa mwajiri na mfanyakazi jijini Dar es Salaam jana.

 Na Benjamin Sawe.                    

Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), umeendesha semina ya siku moja kwa waajiri nchini ili kutoa elimu juu ya shughuli za Mfuko na wajibu wa waajiri kwa wafanyakazi wao katika kujisajili na kuwalipa michango kwa niaba ya waajiriwa wao.

Akizungumza katika semina hiyo Mjumbe wa Bodi ya Mfuko huo Richard Wambali amesema kuanzishwa kwa mfuko huo kumekuja wakati muafaka ambapo Tanzania inaelekea katika uchumi wa viwanda hivyo kupelekea ongezeko la wafanyakazi ambapo chombo hicho ndio mkombozi wa majanga yatokanayo na kazi.

Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Polisi Tabora Yamkamata Kijana kwa Kutumia Sare za JWTZ Kutapeli

Na Tiganya Vincent – RS Tabora

Mkulima mmoja Kitangili mkoani Shinyanga Francis Martin Kilalo  (31) anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani Tabora kwa kukutwa na sare na vifaa vingine vya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ambavyo anatuhumiwa kuvitumia kupateli na kuwadanganya kwa kuchukua fedha kutoka kwa vijana wanaotafuta nafasi ya kujiunga na Jeshi hilo.

Taarifa hiyo imetolewa jana na Kamanda wa Polisi wa wa Mkoa wa Tabora, Wilbroad Mtafungwa alipokuwa anaongea na waandishi wa habari Ofisi kwake jana juu ya hatua mbalimbali walizochukua katika kupambana na uhalifu mkoani humo.

Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Singida Wafundishwa Kutambua Noti Bandia

Na Mwandishi Wetu

Benki Kuu ya Tanzania (BOT) imetoa mafunzo kwa watumishi wote wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida, juu ya alama zinazopatikana katika noti halali za fedha za Tanzania.

Akitoa mafunzo hayo leo kwa wafanyakazi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida, Afisa Kutoka Benki Kuu ya Tanzania, Rehema Zongo amewafafanulia watumishi hao namna ya kutambua noti halali kwa vitendo huku akisisitiza alama muhimu zinazopatikana katika noti halali ili waweze kutofautisha na zile bandia.

Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Watanzania Watakiwa Kuisaidia Serikali

Mdau wa Maendeleo Bw. Boniface Myala akizungumza na wanafunzi alipotembelea shule ya Msingi Kunguru Goba na kugawa madaftari kwa wanafunzi 300 wa darasa la kwanza leo jijini Dar es Salaam.

Na: Mwandishi Wetu

Watanzania wametakiwa kuisaidia serikali katika kutatua changamoto katika sekta mbalimbali ili kujiletea maendeleo kwa haraka badala ya kusubiri kila jambo lifanywe na serikali.

Kauli hiyo imetolewa na Mdau wa Maendeleo Bw. Boniface Myalla wakati alipotembelea shule ya Msingi Kunguru iliyopo Goba na kugawa Daftari kwa wanafunzi 300 wa darasa la kwanza. Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

NBS Yaanza Maandalizi Utafiti wa Matumizi ya Tumbaku Nchini

Mtaalam wa Utafiti wa Matumizi ya Tumbaku kwa Watu wazima Bw. David Plotner (kushoto) kutoka shirika la CDC Marekani akijadiliana na maafisa wa TEHAMA wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Bw. Munir Mdee (katikati) na Abdullah Othman (kulia) wakati wa mafunzo ya awali ya utafiti huo yaliyofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam. Utafiti wa Matumizi ya Tumbaku kwa Watu wazima unatarajia kufanyika nchini mwezi Agosti, 2017.

Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Manispaa ya Tabora Yatakiwa Kuwaondoa Wauza Miti

Na Tiganya Vincent-RS Tabora

Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Dkt .Thea Ntara ameuagiza uongozi wa Manispaa ya Tabora na Maafisa Biashara kuhakikisha wanawaondoa haraka wafanyabiashara wote waliotundika nguo za mitumba katika miti kwa ajili ya kuuza na kufanya mji kuonekana mchafu.

Dkt. Ntara alitoa agizo hilo jana mjini Tabora wakati wa kikao na Wakuu wa Idara  wa Ofisi yake.

Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Waziri Magembe Apiga Marufuku Minada ya Ng’ombe Hifadhini.

Na Tiganya Vincent – RS Tabora

Waziri wa Maliasili na Utalii Profesa Jumanne Maghembe amepiga marufuku minada ya ng’ombe wanaokamatwa katika Misitu ya Hifadhi kufanyika katika maeneo hayo badala yake ifanyike katika maeneo ya wazi ili kutoa  nafasi kwa wananchi kushiriki kwa uwazi.

Waziri Magembe alisema hayo juzi mjini Kahama katika ziara yake wilayani kahama kufuatia oparesheni za kuondoa mifugo kwenye Misitu ya Hifadhi ambapo mifugo hiyo imekuwa ikipigwa mnada ndani ya hifadhi badala ya maeneo ya wazi.

Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail