Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Majaliwa Atembelea Maonyesho ya Ujenzi wa Nyumba

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama picha za nyumba wakati alipotembelea Maonyesho ya Mpango wa ujenzi wa Nyumba za Gharama Nafuu kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Mei 30, 2017. Maonyesho hayo yameandaliwa na Muungano wa Vikundi Vya Vicoba Tanzania (VIGUTA) .Kushoto ni Mwenyekiti wa Taifa wa VIGUTA, Dkt. Salmin Ibrahim Dauda.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WCF Tells Employers: Pay Contributions as Per the Law.

The member of Workers Compensation Fund (WCF) Board of Trustees, Felix Kagisa (Center) officiating at the Sensitisation Seminar for Employers on the Rights and Obligations of employers and employees, held today (yesterday) in Dar es Salaam, On the Right side is The Director of Operation of WCF Ansilim Peter and on the left side is the member of Workers Compensation Fund (WCF) Board of Trustees Jaicy Kayera.

By Benjamin Sawe

Employers have been argued to promptly pay, to Workers Compensation Fund (WCF), contributions of their workers to enable the Fund to adequately and timely provide compensation benefits to effected workers.

Speaking at the opening of a one-day sensitisation seminar to employers, Mr. Felix Kagisa, Board Member of the Fund, reminded employers that, according to the law establishing the fund, it was their responsibility to contribute to the fund for their employees.

Read more

Taarifa Kwa Umma.

“Kwa masikitiko nimepokea taarifa za kifo cha Mbunge Mstaafu wa Jimbo la Moshi Mjini, Mzee wangu Philemon Ndesamburo kilichotokea leo tarehe 31 Mei, 2017 katika hospitali ya rufaa ya KCMC iliyopo Moshi Mkoani Kilimanjaro, Namkumbuka Mzee Ndesamburo kwa hekima zake na uongozi wake uliozingatia siasa za kistaarabu”

Hii ni kauli ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli aliyoitoa katika salamu zake za rambirambi kwa familia ya Marehemu Philemon Ndesamburo, Viongozi na wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) pamoja na ndugu, jamaa na marafiki wote walioguswa na kifo hicho.

Read more

Hali ya Usalama Nchini ni Shwari – IGP Sirro

Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania – IGP Simon Sirro akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Jijini Dar es Salaam leo.

Na Eliphace Marwa.

Jeshi la Polisi limewahakikishia watanzania kuwa hali ya usalama nchini iko vizuri pamoja na kuwepo na matukio machache ya uhalifu katika baadhi ya maeneo ambayo yamekuwa yakijitokeza.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini,IGP Simon Sirro wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam.

Read more

Tabora yakusanya Milioni 180 Makosa ya Barabarani.

Na Tiganya Vincent – RS Tabora

Jumla ya Shilingi Milioni 180 zimekusanywa na Jeshi la Polisi mkoani Tabora katika kipindi cha Mwezi Mei kutokana na makosa mbalimbali yaliyofanywa na waendeshaji wa vyombo vya moto.

Takwimu hizo zilitolewa jana mjini Tabora na Kamanda wa Mkoa wa Tabora Wilbroad Mtafungwa wakati wa mkutano na waandishi wa habari ofisini kwake wakati akitoa ufafanuzi juu ya jitihada mbalimbali wanazozifanya katika kukabiliana na vitendo vya uhalifu mkoani humo.

Read more

Kamishna Ustawi wa Jamii Atembelea Kituo cha Wazee Kibirizi.

Afisa Mfawidhi wa kituo cha kulea Wazee cha Kibirizi Bw. Heradius Mushi (kulia) akifafanua mambo mbalimbali yanayohusu kituo hicho kwa Kamishna wa Ustawi wa Jamii Bw. Rabikira Mushi (katikati) wakati Kamishna huyo alipokitembelea kituo hicho mapema wiki hii Mkoani Kigoma.

Kamishna wa Ustawi wa Jamii, Bw. Rabikira Mushi (katikati) akiwa na Mwenyekiti wa wazee waishio katika Kituo cha Kulea Wazee cha Kibirizi mkoani Kigoma, Bw. Said Lekegwa (kulia) na Bi.  Veronika Ramadhani (kushoto) mara baada ya kuwakabidhi zawadi ya sabuni. Read more

Taarifa kwa Umma

Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo ambayo ni msimamizi wa sekta ya Sanaa na Utamaduni inawajulisha wadau wake kushiriki katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki (JAMAFEST) linalotarajia kufanyika kuanzia tarehe 7 hadi 15 Septemba mwaka huu nchini Uganda.

Tamasha hilo lenye kauli mbiu “TASNIA YA UBUNIFU NA UTAMADUNI NI INJINI YA KUJENGA UMOJA NA KUZALISHA AJIRA” litahusisha nchi wanachama ambapo kila nchi itapaswa kupeleka washiriki wasiopungua mia mbili (200) ambao watahusika katika maonesho mbalimbali yakiwemo burudani mbalimbali, maonesho ya kazi za ubunifu, warsha, mikutano,midahalo,maonesho mbalimbali ya Utamaduni na Sanaa, maonesho ya biashara, michezo ya watoto katika fani mbalimbali, michezo ya jadi, maonesho ya filamu, maonesho ya mavazi na urembo pamoja na maonesho ya vyakula vya asili.

Read more

Waajiri na Mamlaka za Ajira watakiwa kuzingatia Sheria na Miongozo ya Utumishi wa Umma

Katibu Ofisi ya Rais Tume ya Utumishi wa Umma Bw. Nyakimura Muhoji akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu majukumu mbalimbali yaliyotekelezwa na Tume hiyo katika mwaka wa fedha 2016/17 kwa ajili ya kuboresha utendaji katika utumishi wa umma. Kushoto ni Katibu Msaidizi wa Tume hiyo Bw. Peleleja Masesa.

Katibu Msaidizi Idara ya Afya kutoka Ofisi ya Rais Tume ya Utumishi wa Umma Bw. Peleleja Masesa akifafanua kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu Sheria ya Utumishi wa Umma Na.8 inayoelezea majukumu ya Tume hiyo. Kulia ni Katibu Msaidizi Idara ya Utumishi Serikalini kutoka Tume hiyo Bw. John Mbisso.

Na Fatma Salum

Serikali imewataka Waajiri na Mamlaka za Ajira na Nidhamu kote nchini kuzingatia Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo inayosimamia Utumishi wa Umma ili kuleta ufanisi katika usimamizi na uendeshaji wa masuala ya Rasilimali Watu kwenye Utumishi wa Umma.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu Ofisi ya Rais Tume ya Utumishi wa Umma Bw.Nyakimura Muhoji wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.

Read more