Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Makamu wa Rais Mgeni Rasmi Kongamano la Kimataifa la Jinsia

Afisa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE), Lila Mandu akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu Kongamano la Kimataifa la Jinsia na Usawa Katika Jamii leo Jijini Dar es Salaam. Kongamano hilo linatarajiwa kufanyika Aprili 27 mpaka 28 mwaka huu Chuoni hapo. Kutoka kulia kulia ni Mhadhri wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE), Dorothea Fumpuni na Mratibu Kitengo cha Jinsia DUCE Dkt, Fatma Hamad.

Na Husna Saidi-MAELEZO

Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Kongamano la Kimataifa la Jinsia na Usawa Katika Jamii  lililoandaliwa na Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) Aprili 27 mpaka 28 mwaka huu  chuoni hapo.

Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na  Afisa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Chuo hicho Lila Mandu  alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuhusu lengo la kongamano hilo.

Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Serikali Yasikitishwa Kushambuliwa kwa Wanahabari

Na Nuru Juma

Serikali imepokea kwa masikitiko taarifa za kushambuliwa na kujeruhiwa baadhi ya waandishi wa habari katika mvutano uliotokea juzi jijini Dar es Salaam kati ya wafuasi wa pande mbili zinazokinzana za Chama cha Wananchi (CUF).

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi, idara ya Habari- MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi katika taarifa yake aliyoitoa leo tarehe 24 Aprili, 2017 kwa vyombo vya habari.

 “Tumechukua muda kidogo kulifuatilia suala hili na kubaini licha ya baadhi ya waandishi kujeruhiwa na kuripoti polisi, wapo ambao vifaa vyao vya kazi vililengwa katika shambulizi hilo”. Alisema Dkt. Abbasi

Aliongeza kuwa Serikali imelaani kitendo cha kuumizwa kwa wanahabari hao ambao walikuwa wamealikwa kuhudhuria mkutano huo.

“Ifahamike kuwa uandishi wa habari ni taaluma adhimu na nadhifu inayopaswa kuheshimiwa, kuenziwa, kulindwa na kutoingizwa katika migogoro ya pande zinazofarakana katika jamii”. Alisisitiza Dkt. Abbasi.

Pia Dkt. Abbasi aliaanisha baadhi ya vifungu vya Sheria vinavyomlinda mwanahabari katika kazi yake ambapo kifungu cha 7 (1) (a) cha Sheria ya Huduma za Habari Na. 12 ya mwaka 2016 kinaainisha uhuru wa wanahabari katika kukusanya habari kwa muktadha wa kuwepo katika maeneo ya matukio kama hakuna sababu nyingine za kuzuiwa.

Aliongeza kuwa misingi ya uhuru huo wa kitaaluma umesisitizwa pia  katika Ibara za 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 na  Ibara ya 19 ya Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kiraia na Kisiasa wa mwaka 1966 ambao nchi yetu imeuridhia hivyo wananchi wanatakiwa kuheshimu hilo.

Dkt. Abbasi aliwatakia nafuu ya haraka wanahabari waliojeruhiwa na wengine waliopatwa na jakamoyo katika tukio hilo na kuwaomba wadau wote wa habari na wanasiasa kutulia na kuviachia vyombo husika vifanye kazi yake ili hatua stahiki za kisheria zichukuliwe.


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Idara ya Habari (MAELEZO) yafanya Mahojiano na Makamu wa Rais.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika mahojiano maalumu na Mkurugenzi Idara ya Habari (MAELEZO) Dkt. Hassan Abbasi kuhusu masuala ya Muungano kwa ujumla kuelekea maadhimisho ya Miaka 53 ya Muungano.

Mkurugenzi Idara ya Habari (MAELEZO) Dkt. Hassan Abbasi akimkabidhi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan Jarida la Nchi yetu linalotolewa na Idara ya Habari ( MAELEZO). Jarida hilo liliandaliwa kwa ajili ya maadhimisho ya Miaka 55 ya Uhuru wa Tanganyika.

Mkurugenzi Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akifurahia jambo na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan walipofanya mahojiano kuelekea maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (katikati) katika picha ya pamoja na watumishi wa Idara ya Habari (MAELEZO) mara baada ya mahojiano maalumu kuelekea Maadhimisho ya Miaka 53 ya Muungano( kutoka kushoto ni Beatrice Lyimo, Dkt. Hassan Abbasi, Jonas Kamaleki na Hassan Silayo. (PIicha na Mpigapicha wetu)


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Rais Magufuli, Makomandoo Kupamba Sherehe za Muungano Dodoma.

Na: Lilian Lundo

Maonesho ya ukakamavu na mbinu za medani katika kupambana na adui hasa kulinda amani ya nchi yetu kutoka Kikosi Maalum cha Makomandoo wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), itakuwa ni sehemu ya shamrasha zitakazopamba maadhimisho ya  miaka 53 ya Muungano yatakayofanyika kwa mara ya kwanza mjini Dodoma Aprili 26 mwaka huu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira, Kazi, Vijana na Watu Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama  maadhimisho hayo yanatarajiwa kuhudhuriwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli, pia yatapambwa na burudani nyingine kutoka vikundi mbalimbali.

Taarifa ya  Waziri Mhagama ametaja shughuli  nyingine zinazotarajiwa kufanyika siku ya Muungano  kuwa ni gwaride la heshima lililoandaliwa na vikosi vya ulinzi na usalama (JWTZ,JKT, Polisi na Magereza) na onesho la mbwa na farasi waliofunzwa.

Aidha, Waziri Mhagama aliongeza kuwa mambo mengine yatakayofanyika ni gwaride la uzalendo la wanafunzi wa shule za sekondari za Dodoma,  burudani za vikundi vya ngoma za asili kutoka Dodoma na Zanzibar, Yamoto Band, vikundi vya muziki wa kizazi kipya kutoka kwa wasanii Mchungaji Zayumba, Jacob Beats, Mwenge Jazz Band na Mgosi Maturumbeta.

“Kauli mbiu ya sherehe za kutimiza miaka  53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni Miaka 53 ya Muungano; Tuulinde na Kuumarisha, Tupige Vita Dawa za Kulevya na Kufanya Kazi kwa Bidii,” alifafanua Waziri Jenista Mhagama.

Ametoa wito kwa wananchi wote nchini kusherehekea siku hiyo muhimu kwa kudumisha amani, upendo, umoja na mshikamano kwa maendeleo ya nchi.

“Ninaomba kuchukua nafasi ya pekee kuwaomba wananchi wote waliopo Dodoma kujitokeza kwa wingi  uwanja wa  Jamhuri siku hiyo ya Jumatano  tarehe  26 Aprili  2017 kuanzia saa 12:00 asubuhi ili kusherehekea kwa pamoja maadhimisho hayo muhimu kwa nchi yetu,” alisema Jenista Mhagama.

Maadhimisho ya Muungano yanafanyika kwa mara ya kwanza Dodoma ikiwa ni siku kadhaa tangu Serikali ya Awamu ya Tano iabnze kutumiza azma ya kuhamia katika makao makuu hayo mapya.


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Former Israel Prime Minister Ehud Barak praises the government of Tanzania

Deputy Minister of Natural Resources and Tourism, Mr Ramo Makani shakes hands with the former Prime Minister of the nation of Israel, Ehud Barak as they met in ​​Olduvai Gorge

By Staff Writer,

Tanzania Information Services,

Dar es Salaam, Sunday 16 April, 2017. Former Israel Prime Minister Ehud Barak has praised the government of Tanzania for the way it preserves the country’s tourist attractions.

Mr. Barak who was leading a group of over hundred Israeli tourists including his family arrived in the country early this week for a tourist mission.

Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

Tanzania to be the first country in Africa to have long distance electrical powered train

President of the United Republic of Tanzania, Dr. Joseph Pombe Magufuli listerning details from the Chief Executive of RAHCO Masanja Kadogosa about the project for the construction of the Standard Gauge Railway during placement of the foundation stone for in Dar es Salaam

By Staff Writer

Tanzania Information Services.

Wednesday, 12 April, 2017.

 Tanzania is set to become the first country in Africa to have fast modern long distance train using both electricity and diesel power.

Speaking during the official ceremony to lay the foundation stone for the construction of the new standard gauge railway line at Pugu in the outskirts of Dar es Salaam today, President of Tanzania Dr. John Pombe Magufuli said that the new train will be travelling at a speed of 160 per hour.

“The new state of the art train will be the first in the continent and expected to contribute in the economic growth as well as stimulate trade within and outside the country” President Magufuli said.

Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail

TANZANIA NCHI YA KWANZA KUWA NA RELI YA KISASA YA MASAFA MAREFU AFRIKA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Joseph Pombe Magufuli akiwasili katika viwanja vya Pugu Stesheni kwa ajili ya hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa Reli ya kisasa kwa Kiwango cha Kimataifa (Standard Gauge) kutoka Dar hadi Morogoro yenye urefu wa Kilomita 300 katika hafla iliyofanyika Pugu nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam leo. Kushoto kwake ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Joseph Pombe Magufuli akizungumza wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa Reli ya kisasa kwa Kiwango cha Kimataifa (Standard Gauge) kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro yenye urefu wa Kilomita 300 katika hafla iliyofanyika Pugu nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam leo.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akizungumza wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa Reli ya kisasa kwa Kiwango cha Kimataifa (Standard Gauge) kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro yenye urefu wa Kilomita 300 katika hafla iliyofanyika Pugu nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam leo.

Read more


FacebooktwittermailFacebooktwittermail