Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

MAKAMU WA RAIS AZINDUA MRADI WA MAJI WA BILIONI 29 MKOANI TABORA.

Na Tiganya Vincent-RS-Tabora

Serikali imezindua mradi wa ujenzi na usambazaji maji vijijini wenye thamani ya shilingi bilioni 29 katika Halmashauri saba za mkoani Tabora.

Mradi huo umezinduliwa leo na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katika Kijiji cha Mabama Wilayani Uyui mkoani Tabora.

Ujenzi wa Mradi huo umefadhiliwa na Japan kupitia  Shirika la Maendeleo la Japan (JICA) ambao umewezesha uchimbaji wa visima 111 na ujenzi wa mitandao minne ya bomba.

Akizungumza na wananchi wa Mabama mkoani Tabora wakati wa sherehe za uzinduzi wa mradi huo Makamu wa Rais huyo alisema kuwa ujenzi wa mradi huo ni sehemu ya mpango wa Serikali wa kuhakikisha wananchi wengi hapa nchini na wale wa mkoa huo wanakuwa na uhakika wa huduma ya maji safi na salama. Read more

RAIS DKT.MAGUFULI AONDOKA MKOANI DODOMA NA KUELEKEA MKOANI KILIMANJARO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Dodoma tayari kwa kuondoka na kuelekea mkoani Kilimanjaro.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mkuu wa mkoa wa Dodoma Jordan Rugimbana wakati akielekea kwenye ndege tayari kwa safari yake ya kuelekea mkoani Kilimanjaro.

Read more

WATANZANIA WATAKIWA KUENDELEA KUISAIDIA TIMU YA SERENGETI BOYS

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya MUUNGANO WA Tanzania Kassim Majaliwa akizungumza wakati wa hafla ya kuchangia timu ya Taifa ya Vijana chini ya miaka 17 Serengeti Boys jana Jijini Dar es Salaam. Hafla hiyo iliandaliwa na TFF kupitia Kamati ya Hamasa ya Serengeti Boys kwa lengo la kuchangia fedha za kugharamia mahitaji ya timu hiyo inayoshiriki Kombe la AFCON U17 nchini Gabon. Kutoka kushoto ni Rais wa TFF Jamal Malinzi, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe na Mwenyekiti wa Kamati ya Hamasa ya Serengeti Boys Charles Hillary.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza wakati wa hafla ya kuchangia timu ya Taifa ya Vijana chini ya miaka 17 Serengeti Boys jana Jijini Dar es Salaam. Hafla hiyo iliandaliwa na TFF kupitia Kamati ya Hamasa ya Serengeti Boys kwa lengo la kuchangia fedha za kugharamia mahitaji ya timu hiyo inayoshiriki Kombe la AFCON U17 nchini Gabon. Kutoka kulia ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya MUUNGANO WA Tanzania Kassim Majaliwa na Rais wa TFF Jamal Malinzi, na Mwenyekiti wa Kamati ya Hamasa ya Serengeti Boys Charles Hillary.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya MUUNGANO WA Tanzania Kassim Majaliwa akipokea zawadi ya Mpira wa miguu kutoka kwa Rais wa TFF Jamal Malinzi wakati wa hafla ya kuchangia timu ya Taifa ya Vijana chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) jana Jijini Dar es Salaam. Hafla hiyo iliandaliwa na TFF kupitia Kamati ya Hamasa ya Serengeti Boys kwa lengo la kuchangia fedha za kugharamia mahitaji ya timu hiyo inayoshiriki Kombe la AFCON U17 nchini Gabon.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya MUUNGANO WA Tanzania Kassim Majaliwa akimpongeza Makamu wa Rais wa Simba SC Geofrey Nyange Kaburu mara baada ya kununua picha ya Timu ya Serengeti Boys, wakati wa hafla ya kuchangia timu ya hiyo jana Jijini Dar es Salaam. Hafla hiyo iliandaliwa na TFF kupitia Kamati ya Hamasa ya Serengeti Boys kwa lengo la kuchangia fedha za kugharamia mahitaji ya timu hiyo inayoshiriki Kombe la AFCON U17 nchini Gabon. Kutoka kushoto ni Rais wa TFF Jamal Malinzi, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe, Mwenyekiti wa Kamati ya Hamasa ya Serengeti Boys Charles Hillary na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Omary Singo.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya MUUNGANO WA Tanzania Kassim Majaliwa akipeana mkono na Balozi Mdogo wa Mauritius Syed Abbas Rizvi wakati wa hafla ya kuchangia timu ya hiyo jana Jijini Dar es Salaam. Hafla hiyo iliandaliwa na TFF kupitia Kamati ya Hamasa ya Serengeti Boys kwa lengo la kuchangia fedha za kugharamia mahitaji ya timu hiyo inayoshiriki Kombe la AFCON U17 nchini Gabon. Kutoka kushoto ni Rais wa TFF Jamal Malinzi, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe, Mwenyekiti wa Kamati ya Hamasa ya Serengeti Boys Charles Hillary na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Omary Singo.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa akimpongeza Mkurugenzi wa Mtandao wa Fullshangwe Blog, John Bukuku mara baada ya kuchangia shilingi laki mbili wakati wa hafla ya kuchangia timu ya hiyo jana Jijini Dar es Salaam. Hafla hiyo iliandaliwa kwa lengo la kuchangia fedha za kugharamia mahitaji ya timu hiyo inayoshiriki Kombe la AFCON U17 nchini Gabon. Kutoka kushoto ni Rais wa TFF Jamal Malinzi, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe, Mwenyekiti wa Kamati ya Hamasa ya Serengeti Boys Charles Hillary na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Omary Singo.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa akiweka saini katika mpira amabo umenunuliwa na aliyewahi kuwa Miss Tanzania ambaye pia ni mjumbe wa Kamati ya Hamasa ya Serengeti Boys, Bi. Hoyce Temu wakati wa hafla ya kuchangia timu ya Serengeti Boys jana Jijini Dar es Salaam. Hafla hiyo iliandaliwa na kwa lengo la kuchangia fedha za kugharamia mahitaji ya timu hiyo inayoshiriki Kombe la AFCON U17 nchini Gabon. Kutoka kushoto ni Rais wa TFF Jamal Malinzi, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe, Mwenyekiti wa Kamati ya Hamasa ya Serengeti Boys Charles Hillary.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa akimpongeza aliyewahi kuwa Miss Tanzania ambaye pia ni mjumbe wa Kamati ya Hamasa ya Serengeti Boys, Bi. Hoyce Temu mara baada ya kumkabidhi mpira alioununua wakati wa hafla ya kuchangia timu ya Serengeti Boys jana Jijini Dar es Salaam. Hafla hiyo iliandaliwa na kwa lengo la kuchangia fedha za kugharamia mahitaji ya timu hiyo inayoshiriki Kombe la AFCON U17 nchini Gabon. Kutoka kushoto ni Rais wa TFF Jamal Malinzi, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe, Mwenyekiti wa Kamati ya Hamasa ya Serengeti Boys Charles Hillary.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa akimpongeza Afisa Masoko wa Benki ya DTB, Baguma Ambary baada ya kuchangia Serengeti Boys wakati wa hafla ya kuchangia timu hiyo jana Jijini Dar es Salaam. DTB benki ndiyo benki rasmi ya TFF ambapo pia Akaunti maalum ya kuchangia Serengeti Boys imefunguliwa.Kutoka kushoto ni Rais wa TFF Jamal Malinzi, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe, Mwenyekiti wa Kamati ya Hamasa ya Serengeti Boys Charles Hillary.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa akisalimiana na Mchezaji wa zamani wa Timu ya taifa, Mzee Manara wakati wa hafla ya kuchangia timu ya Serengeti Boys jana Jijini Dar es Salaam. Hafla hiyo iliandaliwa na kwa lengo la kuchangia fedha za kugharamia mahitaji ya timu hiyo inayoshiriki Kombe la AFCON U17 nchini Gabon.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa akifurahia jambo na Mwenyekiti wa Kamati ya Hamasa ya Serengeti Boys Charles Hillary (kushoto) wakati wa hafla ya kuchangia timu ya Serengeti Boys jana Jijini Dar es Salaam. Hafla hiyo iliandaliwa na kwa lengo la kuchangia fedha za kugharamia mahitaji ya timu hiyo inayoshiriki Kombe la AFCON U17 nchini Gabon.Kulia ni Rais wa TFF Jamal Malinzi.
Picha zote na: Frank Shija

ELIMU BURE YASAIDIA KUONGEZA IDADI YA UDAHILI WA WANAFUNZI WA KIKE.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiteta jambo na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Profesa Rwekaza Mukandala (kulia) mara baada ya kuwasili katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) alipomwakilisha Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan katika ufunguzi wa Kongamano la Kimataifa kuhusu Usawa wa Kijinsia lililoandaliwa na Chuo hicho leo Jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Mkuu wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) Profesa William Anganisya.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Kimataifa kuhusu Usawa wa Kijinsia lililoandaliwa na Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam(DUCE) leo Jijini Dar es Salaam. Waziri Ummy alimwakilisha Makamu wa Rais katika ufunguzi wa Kongamano hilo.

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Profesa Rwekaza Mukandala akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Kimataifa kuhusu Usawa wa Kijinsia lililoandaliwa na Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) leo Jijini Dar es Salaam.

Read more

MAADHIMISHO YA SHEREHE ZA MIAKA 53 YA MUUNGANO WA TANZANIA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Johna Pombe Magufuli akiwa katika Gari maalum na kuwapungia mkono Wananchi mbali mbali wa Mji wa Dodoma wakati wa sherehe za miaka 53 ya Muungano wa Tanzania zilizofanyika leo katika Uwanja wa Jamhuri

Baadhi ya Wananchi waliohudhuria katika sherehe za maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano wa Tanzania katika Uwanja wa Uhuru zilizofanyika leo,ambapo Mgeni rasmi akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Johna Pombe Magufuli.

Vikosi vya Jeshi la Wananchi wa TRanzania JWTZ,pamoja na Wananchi mbali mbali wa Mji wa Dodoma wakiwa katika Uwanja wa Jamhuri,wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano wa Tanzania zilizofanyika leo,Mgeni rasmi akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Johna Pombe Magufuli [Picha na Ikulu.]

Read more

VIJANA WAHAMASISHWA KUJIUNGA NA KILIMO CHA MBOGAMBOGA,MATUNDA NA NAFAKA.

Mwenyekiti wa Umoja wa Kilimo cha Mbogamboga Wilaya ya Temeke, Joseph Kunguru (katikati) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Kampeni ya kuwahamasisha Vijana kujihusisha na kilimo cha kisasa cha Mbogamboga na Matunda leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Diwani wa Kata ya Buza, Manispaa ya Temeke, James Raphael Mkude na Makamu Mwenyekiti wa Umoja huo Waziri Pembe Waziri.

Diwani wa Kata ya Buza Manispaa ya Temeke James Raphael Mkude akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari kuhusiana Kampeni ya kuwahamasisha vijana kujihusisha na kilimo cha kisasa cha Mbogamboga na Matunda leo Jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya waandishi wa habari wakifatilia kwa umakini mkutano baina yao na viongozi wa Umoja wa Kilimo cha Mbogamboga na Matunda leo Jijini Dar es Salaam.
Picha na: Husna Saidi

Na Nuru Juma na Husna Saidi-MAELEZO

Umoja wa Kilimo cha Mbogamboga, Matunda na Nafaka umeanzisha Kampeni ya Kijana Inuka na Kilimo cha Mbogamboga na Matunda kwa lengo la kuepukana na kilimo cha mvua na vijana waweze kujiajiri wenyewe.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Umoja huo Wilaya ya Temeke Joseph Kunguru alipokutana na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam.

Kunguru alisema kuwa kilimo hicho ni kilimo biashara  na kinahitaji maji na miundombinu ya uhakika ili kuwafanya wananchi kulima kilimo chenye tija badala ya kulima kwa kutegemea mvua.

“Kilimo hiki kinaonekana ni kilimo ghari sana kwani ujenzi wa Green House unaonekana ni kilimo cha watu wenye pesa lakini ukweli ni kwamba wananchi wakiungana pamoja katika kilimo hiki wanaweza kufanikiwa badala ya kulima kwa kutegemea mvua,” alisema Kunguru.

Aidha alisema kuwa vijana wengi mtaani hawana ajira hivyo viongozi kupitia kampeni hii watumie fursa hiyo kuwaelimisha kuhusiana na kilimo hiki cha umwagiliaji ili waweze kujiajiri wenyewe.

Umoja huo wa kilimo cha Mbogamboga na Matunda na Nafaka umesajiliwa kisheria na ulianza na wanachama 17 mpaka sasa wapo 100 ila wanachama hai wapo 74 hivyo wanawasihi wananchi waendelee kujitokeza kujiunga.

Kwa upande wake mmoja wa wanakikundi hicho Sifa Karuka alisema alihamasika kujiunga na kikundi hicho baada ya kupata taarifa kuhusu kilimo hicho cha kisasa  licha ya kuwa na shughuli zake binafsi hivyo anawasihi wakinamama na wasichana wajitokeze kwa wingi ili waweze kujiendeleza kiuchumi.

Nae Diwani wa Kata ya Buza James Raphael Mkude aliwahamasisha madiwani wenzie kuweza kuunda vikundi kama hivyo katika kata zao ili wananchi wao hasa vijana wasiokuwa na ajira waweze kujikwamua kiuchumi.

Kikundi hicho kimeiomba Serikali kupitia Maofisa Ugani kutoa mafunzo kwa vijana ambao hawana ajira kuhusiana nakilimo hicho ili kupunguza ukosefu wa ajira kwa kujitegemea wao wenyewe.

TRA Yaja na Mikakati Mipya Ya Ukusanyaji Kodi

Na Husna Saidi na Nuru Juma- MAELEZO

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imekusanya Trilioni 10.87 mpaka kufikia Machi mwaka huu kwa mwaka wa fedha 2016/2017.

Hayo yamesemwa na Kamishna Mkuu wa Mamlaka hiyo Charles Edward Kichere wakati wa  mahojiano na mtangazaji wa TBC1 Rashid Salum katika kipindi cha Tunatekeleza kinachorushwa  kila siku za Jumatatu saa moja kamili jioni na Alhamisi saa tatu na nusu usiku.

Kichere alisema, mwaka huu wa fedha 2016/2017 TRA inatakiwa kukusanya Trilioni 15.105 na hadi kufikia Machi mwaka huu TRA  imefanikiwa kukusanya Shilingi Trilioni 10.87.

Aliendelea kwa kusema kuwa mpaka kufikia Juni mwaka huu TRA  itahakikisha inatimiza lengo la kukusanya Shilingi Trilioni 15.105 ili kusaidia  Serikali kuleta maendeleo kwa wananchi wake.

Alisema kuwa TRA ina waajiriwa wapya ambao wamepewa mafuzo ya miezi sita katika  chuo cha kodi juu ya mifumo mbalimbali ya ukusanyaji kodi ambao waliajiriwa moja kwa moja na mamlaka hiyo  kwaajili ya kutekeleza majukumu ya ukusanyaji kodi ndani ya nchi.

“Tunatumia mfumo wa Tehama kukusanya kodi na mifumo mingine mbalimbasli  kama  vile Tigo Pesa , Airtel Money na MPesa ili kurahisishia watu kulipa kodi wakiwa nyumbani na kuepuka usumbufu,” alisema Kichere.

Kichere aliongeza kuwa kwa mwaka huu wa fedha mapato yameongezeka mpaka kufikia asilimia 9.9 hadi 10 licha ya kuwa kuna baadhi ya maeneo hawakuweza kukusanya.

Aidha Kichere alisema Mamlaka kwa sasa imejipanga kuwa na mahusiano mazuri na wafanyabiashara ili kuhakikisha wafanyabiashara wanalipa kodi stahiki na kwa mujibu wa sheria bila kutumia nguvu au uonevu wowote.

Hata hivyo mamlaka hiyo imekuwa ikitoa  elimu kwa walipa kodi kwa kupitia vyombo mbalimbali vya habari, kutoa semina kwa watumishi wa umma , kuandaa makongamano ambayo yanatoa elimu, kupitia mitandao ya kijamii na ziara mbalimbali ambazo wamekuwa wakizifanya ili kuhakikisha wafanyabiashara wanapata elimu pamoja na kujua wajibu wao katika kulipa kodi ili kuleat maendeleo nchini.